Kinga kwa Rais aliyeko madarakani na wastaafu ni kichocheo cha uvunjaji haki, Iangaliwe upya

Kama rais aliyepo madarakani anaweza kutafutiwa asilimia 20% ya wabunge kuunga mkono hoja ya kumshitaki (impeachment proceeding) halafu kupelekwa mahakamani kushtakiwa baada ya hoja kuungwa mkono na theluthi mbili ya wabunge, itakuwaje rais mstaafu asiweze kushtakiwa?
 
Kama rais aliyepo madarakani anaweza kutafutiwa asilimia 20% ya wabunge kuunga mkono hoja ya kumshitaki (impeachment proceeding) halafu kupelekwa mahakamani kushtakiwa baada ya hoja kuungwa mkono na theluthi mbili ya wabunge, itakuwaje rais mstaafu asiweze kushtakiwa?
Nijuavyo mimi ni kuwa raisi hawezi shitakiwa ila bunge lina uwezo wa kumuondoa madarakani kwa kura ya kutokuwa na imani na raisi.

Mwenye kujua zaidi atusaidie hapa.
 
Hivi huyu Laki si pesa jamani yuko sawasawa kichwani kweli?mashaka makubwa.Jambo la maana kama hili unavulumishia wenzio mitusi mmmh.Haingii akili hata kama ni mapenzi huu ni ukichaa na upofu
 
Nijuavyo mimi ni kuwa raisi hawezi shitakiwa ila bunge lina uwezo wa kumuondoa madarakani kwa kura ya kutokuwa na imani na raisi.

Mwenye kujua zaidi atusaidie hapa.

Bunge linaweza kumpigia kura ya kutokuwa na imani Waziri Mkuu. Bunge haliwezi kumpigia kura ya kutokuwa na imani rais kwa sababu rais ni mkuu wa mhimili kama bunge, wa utawala.

Kama bunge halina imani na rais, linaweza kupiga kura ya kuwezesha rais kushtakiwa (impeachment) kama nilivyoeleza hapo juu.

Kura ikipata theluthi mbili ya wabunge, rais anafunguliwa mashitaka katika "Special Committee of Inquiry" itakayoongozwa na Jaji Mkuu.

Rais akikutwa ana makosa ya kumuondoa madarakani na mahakama, anaondolewa mahakamani kwa mujibu wa katiba.

Soma Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ibara za 46 na 46A.

Kifungu cha 46 (3) kinaonyesha kwamba bakuna jinsi ya kunshtaki rais mstaafu kwa makosa aliyoyafanya akiwa rais kama makosa hayo hayajawekwa kwenye mchakato wa impeachment awali. Which is odd. It's like your only chance of prosecuring a Tanzanian president is during his/her tenure through impeachment. A retired president is untouchable as far as the weongs done during his/her presidency are concerned, according to these articles.
 
Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inampa kinga Rais kutokushitakiwa kwa makosa aliyotenda akiwa madarakani.

Aidha katiba hiyo hiyo inalipa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mamlaka ya kuanzisha mchakato wa kumwondoa Rais madarakani ikiwa ni pamoja na kupiga kura ya kutokuwa na imani na Rais.

Hoja yangu ni kwamba tangu Rais alipotoa tangazo la kuvunjwa kwa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania alitakiwa kulivunja Baraza lake la Mawaziri baada ya siku 14 tangu kutolewa kwa tangazo la kuvunjwa Bunge.

Muda huo uliotajwa ktk sheria umepita na Baraza la Mawaziri halijavunjwa na wataalam wa maswala ya sheria na katiba nchini wakiwemo wana siasa, wanaharakati na watetezi wa haki za binadamu wamekaa kimya wakati katiba ambayo ndiyo sheria mama inakiukwa.

Mawaziri wanapoendelea na nyadhifa zao huku wengine wakifanya kampeni kwa kujitanabaisha kama mawaziri hivi watakaposhinda uchaguzi wapinzani wao kisiasa hawawezi kuwakatia rufaa mahakamani?.

Najua Mwanasheria mkuu wa serikali anapitia humu, naomba ufafanuzi tafadhali kwani huko nyuma uzoefu umeonyesha kuwa baraza la mawaziri linapovunjwa, majumu yaliyokuwa yakitendwa na mawaziri hufanywa na makatibu wakuu wa wizara husika kwa ushirikiano na wataalam.
 
Kama Magufuli ni muadilifu afanye mambo haya :
1 Aondoe kinga ya rais

2 Arudishe kipengele cha maadili kama kilivyo kwenye katiba ya Warioba .

3 Aunde tume huru ya kupambana na rushwa na madawa ya kulevya .

4 Uhuru wa mahakama.

Lile genge la mpigadili anaejiandaa kuwa waziri mkuu litafyata kazi.
 
Wakuu habari....

Kwa jinsi serikali ya awamu ya nne ilivyovurunda hasa kwenye matumizi mabovu ya fedha na rasilimali za wananchi, natamani Rais kama mkuu wa nchi, kiongozi mkuu wa serikali ashitakiwe mahakamani.

Lakini nimesoma katiba yetu ibara ya 46 kifungu cha kwanza hadi cha tatu vinasema nimarufuku kumshitaki rais akiwa madarakani na hata baada ya kustaafu kutokana na makosa aliyotenda akiwa madarakani.

vifungu vyenyewe ni kama kama vifuatavyo...

46.-(1) Wakati wote Rais atakapokuwa bado ameshika madaraka yake kwa mujibu wa Katiba hii, itakuwa ni marufuku kumshitaki au kuendesha mashataka ya aina yoyote juu yake mahakamani kwa ajili ya kosa lolote la jinai.

(2) Wakati wote Rais atakapokuwa bado ameshika madaraka yake kwa mujibu wa Katiba hii, haitaruhusiwa kufungua mahakamani shauri kuhusu jambo lolote alilolitenda au alilokosa kulitenda yeye binafsi kama raia wa kawaida ama kabla au baada ya kushika madaraka ya Rais, ila tu kama angalau siku thelathini kabla ya shauri kufunguliwa mahakamani, Rais atapewa au ametumiwa kwamba taarifa ya madai kwa maandishi kwa kufuata utaratibu uliowekwa kwa mujibu wa sheria iliyotungwa na Bunge, na taarifa hiyo ikiwa inatoa maelezo kuhusu chanzo cha shauri hilo, kiini cha madai yenyewe, jina lake na anwani ya mahali anapoishi huyo mdai na jambo hasa analodai.

(3) Isipokuwa kama ataacha kushika madaraka ya Rais kutokana na masharti ya ibara ya 46A(10), itakuwa ni marufuku kumshtaki au kufungua mahakamani shauri lolote la jinai au la kumdai mtu aliyekuwa anashika madaraka ya Rais baada ya kuacha madaraka hayo kutokana na jambo lolote alilofanya yeye kama Rais wakati alipokuwa bado anashika madaraka ya Rais kwa mujibu wa Katiba hii.


Sasa nauliza je bunge linaweza muondolea Rais mstaafu kinga ya kutokushtakiwa mahakamani??

Naomba ufafanuzi wa kisheria tafadhali....
 
Mkapa Ni zaidi ya shetani.asilimia kubwa watz tunateseka kwa sababu yake,huyu jamaa ana Roho mbaya sana.
 
Mimi siku zote huwa nasema Nyerere alipaswa kubadili katiba kabla hajaakabidhi Ikulu kwa watu wengne.

Bunge lina mamlaka hayo lakini si hili lililotawalia na ma-CCM.

Nchi tajiri zinazotupa misaada maraisi wanashtakwa,alafu sisi nchi masikini tena omba omba,raisi ni marufuku kushitakiwa! Nani alituloga?
 
Mimi siku zote huwa nasema Nyerere alipaswa kubadili katiba kabla hajaakabidhi Ikulu kwa watu wengne.

Bunge lina mamlaka hayo lakini si hili lililotawalia na ma-CCM.

mkuu kwa uchumi tulionao, wabunge wa sasa hawata mtetea mtu, km mtu fisadi atakatwa tu, tena magufuli anahasira nao sanaa
 
mkuu kwa uchumi tulionao, wabunge wa sasa hawata mtetea mtu, km mtu fisadi atakatwa tu, tena magufuli anahasira nao sanaa
Mkuu mara hii ushaanza kumsifia Magufuli , ashalisahau lile kapi lenu mlokuwa mkilidekia barabara! wala hatukuhitaji CCM usijipendekeze
 
Muweweseko wa deraya 700 na mita 200 kwa vijana wa BAVICHA hautokuja kukaa uwaishe, kila siku JK JK! andamameni barabarani kama hamjipendi
 
Back
Top Bottom