Kinga kwa Rais aliyeko madarakani na wastaafu ni kichocheo cha uvunjaji haki, Iangaliwe upya

Mkimshtaki Mkapa mtapata nini? Je ndo ita-solve solution ya wizi wa mali za umma? Tatizo sio Mkapa, tatizo ni system ya utendaji Tanzania. Wafanyakazi wa Umma ni waoga. Kwa nini waoga? Ni kwa sababu nchi yetu haina msingi mzuri wa sheria.

Kuna watu kibao wanaojua haya maovu yanayoendelea kila siku. Bila kuwapa hawa watu sauti za kuongea ni bure tu!

Mtapelekana mahakamani na kulana pesa! Narudia tena, Nchi inahitaji misingi bora ya sheria kwa kusudi la kuendelea. Bila misingi ya sheria, wakubwa wataendelea kunyonya wanyonge. Ivi Tanzania kuna Legal Aid?
 
Mkimshtaki Mkapa mtapata nini? Je ndo ita-solve solution ya wizi wa mali za umma? Tatizo sio Mkapa, tatizo ni system ya utendaji Tanzania. Wafanyakazi wa Umma ni waoga. Kwa nini waoga? Ni kwa sababu nchi yetu haina msingi mzuri wa sheria. Kuna watu kibao wanaojua haya maovu yanayoendelea kila siku. Bila kuwapa hawa watu sauti za kuongea ni bure tu! Mtapelekana mahakamani na kulana pesa! Narudia tena, Nchi inahitaji misingi bora ya sheria kwa kusudi la kuendelea. Bila misingi ya sheria, wakubwa wataendelea kunyonya wanyonge. Ivi Tanzania kuna Legal Aid?
Well said,

Hakuna haja ya kumshitaki mkapa wala hatutapata chochote..kumbuka mkapa yeye mwenyewe ameshajutia baadhi ya maamuzi yake mimi naona inatosha sana kwa binadamu yeyote..humiliation aliyokwisha pata is more than enough

tusonge mbele, tuwe na uwezo wa ki-taasisi ambao rais hatakuwa na madaraka na mamlaka makubwa ya kufanya kila uchafu...ni bora zaidi kuliko kutafuta na kupoteza muda for head hunting..what waste of time and resources??

mkapa ana makosa mengi lakini ana mazuri mengi pia...hivi kuna mtu ana makosa kama Bush wa merakani angalia wamerakani hawana muda na jamaa wanasonga mbele na mambo yao

sisi lazima tunajadili yaliyopita muda mrefu kuliko kujadili yajayo muda mrefu..wa type of people we are??? stupid, tumjadili na tumsaidie JK alete maedeleo aliyoahidi finito..

akishindwa tutafute namna ya kumweka pembeni nchi akabidhiwe mtanzania makini..na chama makini..OK
 
Mkimshtaki Mkapa mtapata nini? Je ndo ita-solve solution ya wizi wa mali za umma? Tatizo sio Mkapa, tatizo ni system ya utendaji Tanzania. Wafanyakazi wa Umma ni waoga. Kwa nini waoga? Ni kwa sababu nchi yetu haina msingi mzuri wa sheria. Kuna watu kibao wanaojua haya maovu yanayoendelea kila siku. Bila kuwapa hawa watu sauti za kuongea ni bure tu! Mtapelekana mahakamani na kulana pesa! Narudia tena, Nchi inahitaji misingi bora ya sheria kwa kusudi la kuendelea. Bila misingi ya sheria, wakubwa wataendelea kunyonya wanyonge. Ivi Tanzania kuna Legal Aid?

Mwizi wa kuku anapokamatwa na kushtakiwa tunapata nini? Je, hiyo inasolve solution ya wizi wa kuku nchini? Jibu ni hapana. Lakini sheria inasema ukiiba unakamatwa na kuswekwa lupango. Vivyo hivyo na Mkapa.

Akikamatwa utakuwa ni mwazo wa kubadilisha system ya utendaji Tanzania. Marais watakaofuata watakuwa waadilifu zaidi wakizingatia kanuni za kisheria.

Kama kweli tunataka kubadilkisha mindset na kuweka misingi bora ya sheria ni lazima tuanze na wale waliopewa dhamana ya kulinda sheria zetu.

Tena kwa hao lazima tuwe wakali zaidi ili wananchi wa kawaida waweze kurejesha imani kuwa tunaishi chini ya utawala wa kisheria, ebo!
 
Mwizi wa kuku anapokamatwa na kushtakiwa tunapata nini? Je, hiyo inasolve solution ya wizi wa kuku nchini? Jibu ni hapana. Lakini sheria inasema ukiiba unakamatwa na kuswekwa lupango. Vivyo hivyo na Mkapa. Akikamatwa utakuwa ni mwazo wa kubadilisha system ya utendaji Tanzania. Marais watakaofuata watakuwa waadilifu zaidi wakizingatia kanuni za kisheria. Kama kweli tunataka kubadilkisha mindset na kuweka misingi bora ya sheria ni lazima tuanze na wale waliopewa dhamana ya kulinda sheria zetu. Tena kwa hao lazima tuwe wakali zaidi ili wananchi wa kawaida waweze kurejesha imani kuwa tunaishi chini ya utawala wa kisheria, ebo!
I don't think so! na mfano wako siyo sahihi,
tukimshtaki rais mstaafu ni precedent ambayo haisaidii nchi wala rais atakayechaguliwa

itasaidia kupunguza ufanisi na kutafuta namna nzuri ya kuiba na kujilinda

achaneni na mkapa he the past let talk the present and future.
 
Tina,
samahani sana kwa kutokubaliana nawe kwani makosa ya mtu hayapimwi kwa muda ulopita..Mkapa asamehewe kwa sababu nyinginezo lakini sii hizi za kupita wakati ama Katiba.

Nitaandika kitu kimoja kinyume cha Ubinadam na mjue kwamba Katiba yetu ina tobo kibao za kijinga sana. majuzi tu kuna watu walihukumiwa KIFO kwa kuua Albino jambo ambalo kikatiba linaweza pingana..Huu ni mtazamo wangu mimi Mkandara.

Katiba inaturuhusu sote sisi kuabudu dini zetu... Hii ruksa kikatiba ni risk kubwa sana kisheria.. Je, ikiwa waumini wa dini za Asili ni moja ya waruhusiwa, iweje watu hawa wahukumiwe kifo kwa ibada yao ili hali imani za Kichawi (kuua) ni moja ya ibada zao?

Katiba imewapa Uhuru wa kuabudu, na hata kama sheria yetu inakataza kuua, ruksa kama hizi huondoa ama kupingana na sheria inayokataza kuua kwa Makusudi. Kwani waumini wa dini za Asili wanafanya Ibada kwa imani ya dini yao (kuua0 na sii kwamba wanaua kwa MAKUSUDI..

Hivyo, tunaweza bishana hadi kesho achilia mbali kabisa haki ya Kuishi ambayo kikatiba pia inapingana na adhabu kama hizi, wakati mimi naelewa vizuri kwamba watu hawa wamefanya makosa makubwa na hakuna hukumu iliyo na haki mbele ya sheria zaidi ya watu wahusika hawa kupewa hukumu ya Kifo.

Na siwezi kufikiria kabisa kwamba hata tukiwaua haitasaidia kitu maadam Albino wameisha kufa, hivyo tugange yajayo.

Noo sheria ipo kukomesha vitendo kama hivyo na kama ni Ibada yao basi wafikirie Upya kuandika sura za Agano jipya..
 
Mwizi wa kuku anapokamatwa na kushtakiwa tunapata nini? Je, hiyo inasolve solution ya wizi wa kuku nchini? Jibu ni hapana. Lakini sheria inasema ukiiba unakamatwa na kuswekwa lupango. Vivyo hivyo na Mkapa. Akikamatwa utakuwa ni mwazo wa kubadilisha system ya utendaji Tanzania. Marais watakaofuata watakuwa waadilifu zaidi wakizingatia kanuni za kisheria. Kama kweli tunataka kubadilkisha mindset na kuweka misingi bora ya sheria ni lazima tuanze na wale waliopewa dhamana ya kulinda sheria zetu. Tena kwa hao lazima tuwe wakali zaidi ili wananchi wa kawaida waweze kurejesha imani kuwa tunaishi chini ya utawala wa kisheria, ebo!

Ahsante sana Mkuu Jasusi.. Tanzania hakuna yeyote yule ambaye yuko above the law. Kama kuna mambo ambayo ameyafanya yamekiuka sheria za nchi basi ni lazima sheria ziachwe zichukue mkondo wake na siyo kuuliza maswali eti mkishtaki Mkapa mtapata nini!!! :confused:

Kama Mkapa atashtakiwa basi Viongozi mbali mbali wa sasa na wa baadaye akiwemo Rais watakuwa wanafikiria mara mbili mbili kufanya ufisadi wanapokuwa madarakani lakini kwa hali ilivyo sasa Kiongozi anaweza kusema mbona Mkapa hakushtakiwa kwa ufisadi wake, mbona Mzee wa Vijisenti, Idrissa Rashid, Rostam na wengi wengine hawakushtakiwa.

Hivyo na Kiongozi huyo kuamua kufanya ufisadi akiwa madarakani bila woga wowote.

Duh! mtu anathubutu kuuliza mtapata nini mkishtaki Mkapa!!! Kazi kweli kweli!
 
15897.jpg

Makerere University Chancellor Mond Kogonyera confers an hononary Doctor of low degree on former Tanzania president Benjamin Mkapa at the university in Kampala yesterday. Mr. Mkapa was honoured for his good democratic governance credentials, Looking in is Vice-Chancellor Venansius

Mkapa mmachinga mfisadi aliyeingizwa mjini na Mchaga Anna
 
Kwa kufupisha stori MKAPA ni Mwizi na Mlarushwa. Ndani ya hayo mawili kuna mlolongo wa tuhuma za ubadhirifu na coraption ukianzia Manunuzi ya Ndege ya Raisi , Rada, Kujiuzia Kiwira na mengineyo the list is long enough.
Mwizi ni wewe, Kama angelikuwa ni mwizi si angeondoka na Ndege ile au akaiuza na kupata 10%? Tumshukuru mtu huyu badala ya kumtukana kwani hata hiyo ndege aliinunua na kwa ajili ya Rais (Ajaye) wa sasa, tena kutokana na fedha zetu siyo za kukopa!!!
 
Anachosema Semenya - pamoja na hisia za wananchi kama inavyoonerkana katika post hiyo hapo juu, je was there wilful wrong doing by Mkapa personally that would make him liable in court with concrete evidence? What about his immunity? Watu wasidhani kufikiria na moyo, na kushikwa na hasira au hata kuhisi, ni ushahidi tosha wa makosa ya Mkapa na wengineo.Mnasahau kinga ya kikatiba aliyo nayo?

JAMANI - TRUTH BE TOLD.... KUDHANI KUNA SIKU MKAPA ATABURUTWA MAHAKAMANI - IS JUST A WISHFUL THINKING. HAKUNA KITU KAMA HICHO. TULIZENI MUNKARI, TUJIFUNZE KUTOKANA NA MAKOSA NA TUJISAHIHISHE.

Najua wengi watachukizwa na mchango huu lakini habari ndio hiyo.
 
Hawezi kuondolewa kinga hata iweje, hawa jamaa hawawezi kuchomana labda kama walikua maadui, hapa hashtakiwi wala nini hata kama ushahidi upo wa kwamba alijiuzia Kiwira na mengine, cha msingi na kuacha kupiga kelele na kusonga mbele kwa ajili ya kufikiria maswala ya maendeleo, lakini tukipiga kelele, jueni kuwa hakuna lolote linaloweza kumfanya huyu jamaa akaozea jela, ni ndoto jamani kwa hii nchi
 
Mwizi ni wewe, Kama angelikuwa ni mwizi si angeondoka na Ndege ile au akaiuza na kupata 10%? Tumshukuru mtu huyu badala ya kumtukana kwani hata hiyo ndege aliinunua na kwa ajili ya Rais (Ajaye) wa sasa, tena kutokana na fedha zetu siyo za kukopa!!!

Usiwe na jazba! Mkapa anastahili kuchukuliwa hatua kwa madudu yote aliyoyafanya akiwa Ikulu ambayo yamekuwa yakiorodheshwa kila siku humu na kwenye magazeti pia. Tumemshauri awaombe radhi wananchi ili wamsamehe yaishe lakini kwa kiburi chake bado hajafanya hivyo. Asulubiwe!!
 
Anachosema Semenya - pamoja na hisia za wananchi kama inavyoonerkana katika post hiyo hapo juu, je was there wilful wrong doing by Mkapa personally that would make him liable in court with concrete evidence? What about his immunity? Watu wasidhani kufikiria na moyo, na kushikwa na hasira au hata kuhisi, ni ushahidi tosha wa makosa ya Mkapa na wengineo.Mnasahau kinga ya kikatiba aliyo nayo?
JAMANI - TRUTH BE TOLD.... KUDHANI KUNA SIKU MKAPA ATABURUTWA MAHAKAMANI - IS JUST A WISHFUL THINKING.HAKUNA KITU KAMA HICHO.TULIZENI MUNKARI, TUJIFUNZE KUTOKANA NA MAKOSA NA TUJISAHIHISHE.Najua wengi watachukizwa na mchango huu lakini habari ndio hiyo.

J, Habari za nanihii? naona ulikuwa umepotea kwa siku tele. Mzima wewe? Hata crib yako ilikuwa imenuna..kizaa kinene. ;)

Kuhusu immunity ya Mkapa inahusu maamuzi aliyoyafanya kama Rais wa Tanzania lakini immunity hiyo haimkingi kwenye ufisadi wake wa kufanya biashara akiwa Ikulu au kuiba Mgodi wa Kiwira. Sidhani kama madhumuni ya immunity ya Rais wetu ilikuwa ni kumkingia kifua pale anapofanya madhambi dhidi ya Wananchi wake waliomuweka madarakani.

Kwa hiyo fisadi Mkapa haka immunity yoyote kwa kufanya biashara akiwa Ikulu au kwa wizi wa kuiba Kiwira kwa kutumia nafasi aliyonayo wakati ule.

Kutofikishwa Mkapa mahakamani kwa ufisadi wake haina maana sheria za nchi zinafuatwa bali ni kutokana na walio madarakani pia kuwa mafisadi.

Kuna ushahidi wa kutosha kuhusu ufisadi wa Rostam, Mzee wa Vijisenti, Idrissa Rashid na wengineo, dalili zinaonyesha kwamba hawa pia hawataburutwa mahakamani kujibu tuhuma dhidi yao na hili siyo kwamba sheria za nchi zinafuatwa bali ni kwa sababu mafisadi wamewawaka Viongozi wa nchi mifukoni mwao.
 
Semenya,
Umeuliza Mkapa ashtakiwe kwa kosa gani. Kosa kubwa alilofanya Mkapa ni kula rushwa akiwa rais wa TZ. Aliuza NBC kwa rushwa. Alileta Net Problems kwa rushwa. Alijiuzia Kiwira kwa kukiuka taratibu za nchi. Hii inaweza kuangukia chini ya sheria za uhujumu uchumi. Na ushahidi upo.
Basi nikawa natafuta Net Problems... Ndo Net Group Solutions?

Anachosema Semenya - pamoja na hisia za wananchi kama inavyoonerkana katika post hiyo hapo juu, je was there wilful wrong doing by Mkapa personally that would make him liable in court with concrete evidence? What about his immunity? Watu wasidhani kufikiria na moyo, na kushikwa na hasira au hata kuhisi, ni ushahidi tosha wa makosa ya Mkapa na wengineo.Mnasahau kinga ya kikatiba aliyo nayo?

JAMANI - TRUTH BE TOLD.... KUDHANI KUNA SIKU MKAPA ATABURUTWA MAHAKAMANI - IS JUST A WISHFUL THINKING. HAKUNA KITU KAMA HICHO. TULIZENI MUNKARI, TUJIFUNZE KUTOKANA NA MAKOSA NA TUJISAHIHISHE.

Najua wengi watachukizwa na mchango huu lakini habari ndio hiyo.
The truth hurts :(
 
Wale wote wenye uchungu naamini ni wengi sana waanzishe pressure group wawe wawazi tu wasiogope chochote waje na ushahido wote wa wizi halafu wapeleke suala hilo katika vyombo wa sheria waone kama halitofanyiwa kazi -- kwa mtindo huu wa kuongea vimaneno vya vijiweni , majungu , mipasho na aina nyingine ya tabia tatutafika watanzania wengi halafu wengi hawa ni vijana kazi yao mipasho tu kwa majina bandia
 
Mwizi wa kuku anapokamatwa na kushtakiwa tunapata nini? Je, hiyo inasolve solution ya wizi wa kuku nchini? Jibu ni hapana. Lakini sheria inasema ukiiba unakamatwa na kuswekwa lupango. Vivyo hivyo na Mkapa. Akikamatwa utakuwa ni mwazo wa kubadilisha system ya utendaji Tanzania. Marais watakaofuata watakuwa waadilifu zaidi wakizingatia kanuni za kisheria. Kama kweli tunataka kubadilkisha mindset na kuweka misingi bora ya sheria ni lazima tuanze na wale waliopewa dhamana ya kulinda sheria zetu. Tena kwa hao lazima tuwe wakali zaidi ili wananchi wa kawaida waweze kurejesha imani kuwa tunaishi chini ya utawala wa kisheria, ebo!

Ahsante sana Mkuu Jasusi.. Tanzania hakuna yeyote yule ambaye yuko above the law. Kama kuna mambo ambayo ameyafanya yamekiuka sheria za nchi basi ni lazima sheria ziachwe zichukue mkondo wake na siyo kuuliza maswali eti mkishtaki Mkapa mtapata nini!!! :confused:
Kama Mkapa atashtakiwa basi Viongozi mbali mbali wa sasa na wa baadaye akiwemo Rais watakuwa wanafikiria mara mbili mbili kufanya ufisadi wanapokuwa madarakani lakini kwa hali ilivyo sasa Kiongozi anaweza kusema mbona Mkapa hakushtakiwa kwa ufisadi wake, mbona Mzee wa Vijisenti, Idrissa Rashid, Rostam na wengi wengine hawakushtakiwa. Hivyo na Kiongozi huyo kuamua kufanya ufisadi akiwa madarakani bila woga wowote.

Duh! mtu anathubutu kuuliza mtapata nini mkishtaki Mkapa!!! Kazi kweli kweli!

Waheshimiwa....I seriously think you guys have missed the point and dont see the big picture. Makosa ya Mkapa sio kama wizi wa kuku. Wizi/makosa ya Mkapa yanawekwa katika kundi lijulikanalo kama 'White Collar Crime".

Kwa nini kundi hili? Makosa kama haya yanahitaji sheria na mfumo mzima wa sheria ulio sophisticated kuweza ku-deal nayo.

Kwa stage yetu ya sheria, HATUNA UWEZO WA KU-PROSECUTE SUCH CRIMES. Angalia mfano wa Chiluba kule Zambia na pesa iliyotumika na bado akatoka huru. (kwa info zaidi search thread ya Zitto).

Mtatumia pesa nyingi, maana yeye atatumia kila trick katika kitabu ku-delay justice.

Ukitaka kujua hizi njia, uliza wana-sheria wanaofanya kazi kwenye makampuni ya insurance.

Pili, system yetu ya sheria iko very much inter-twined with politics. Hivi kweli utategemea AG (mwenye kadi ya chama) anyanyuke na kumshtaki mwana-chama mwenzake. Kumbuka, na yeye amekula hizo pesa pia.

Twende kwa DPP, huyu anachaguliwa na nani? Sio AG? Twende kwa ma-judge? Na ni nani aliyewachagua? Sio Rais? (Tena utakuta ni huyo huyo Mkapa)hahahaha.

Tatu, Ivi wana-sheria waliobobea watakaoweza ku-deal na hii Tanzania ni kina nani? Kina Alex Stuart?Sio nao wanasemekana wako linked na hayo ma-deal!! Who else? Mwakembye? Huyu anakula posho mara mbili na wana-kadi ya chama kimoja?

Kwanza yule wa Utamu mwenyewe, imishindikana ku-deal naye...hahaha! Sembuse Mkapa!!! Be serious guys!

At this stage, we can not deal with such crimes. We need to develop our judicial system. Na hii ndo njia pekee ya kuendelea.

Hivyo basi, solution ni nini? Change and improvement of the judicial system. From here, we can then have a serious discussion on helping the country badala ya blah blah za kila siku!!

am out...
 
Waheshimiwa....I seriously think you guys have missed the point and dont see the big picture. Makosa ya Mkapa sio kama wizi wa kuku. Wizi/makosa ya Mkapa yanawekwa katika ***** lijulikanalo kama 'White Collar Crime". Kwa nini kundi hili? Makosa kama haya yanahitaji sheria na mfumo mzima wa sheria ulio sophisticated kuweza ku-deal nayo. Kwa stage yetu ya sheria, HATUNA UWEZO WA KU-PROSECUTE SUCH CRIMES. Angalia mfano wa Chiluba kule Zambia na pesa iliyotumika na bado akatoka huru. (kwa info zaidi search thread ya Zitto). Mtatumia pesa nyingi, maana yeye atatumia kila trick katika kitabu ku-delay justice. Ukitaka kujua hizi njia, uliza wana-sheria wanaofanya kazi kwenye makampuni ya insurance. Pili, system yetu ya sheria iko very much inter-twined with politics. Hivi kweli utategemea AG (mwenye kadi ya chama) anyanyuke na kumshtaki mwana-chama mwenzake. Kumbuka, na yeye amekula hizo pesa pia. Twende kwa DPP, huyu anachaguliwa na nani? Sio AG? Twende kwa ma-judge? Na ni nani aliyewachagua? Sio Rais? (Tena utakuta ni huyo huyo Mkapa)hahahaha
Tatu, Ivi wana-sheria waliobobea watakaoweza ku-deal na hii Tanzania ni kina nani? Kina Alex Stuart?Sio nao wanasemekana wako linked na hayo ma-deal!! Who else? Mwakembye? Huyu anakula posho mara mbili na wana-kadi ya chama kimoja?
Kwanza yule wa Utamu mwenyewe, imishindikana ku-deal naye...hahaha! Sembuse Mkapa!!! Be serious guys!
At this stage, we can not deal with such crimes. We need to develop our judicial system. Na hii ndo njia pekee ya kuendelea.
Hivyo basi, solution ni nini? Change and improvement of the judicial system. From here, we can then have a serious discussion on helping the country badala ya blah blah za kila siku!!

am out...

Mkuu tuko pamoja kwa hili.Natamani sana Mkapa ashitakiwe,apande karandinga lakini sheria zetu, mahakama zetu, waendesha nashitaka wetu na siasa zetu hazituwezeshi kufanya hivyo labda tusubiri siku Tanzania ikimpata rais mwenye uwezo tutaweza kufanya haya tunayotaka kufanya lakini si sasa.
 
Hata nyinyi wote hapa ni wezi wa aina yake kwa kuwa mnatumia muda vibaya badala ya kuchapa kazi mnabwata! Kipimo ni number of posts. Jipime ni mwizi grade gani mwenyewe kisha uone kama mkapa anastahili kufunguliwa mashitaka. Mkapa alifanya yaliyomhusu. Wewe je?
Tunaheshimu sana maoni yako kama mwana JF mwenza lakini kiasi unatukwaza kwa kuenda nje ya mada na kutuita wenzako wezi, kwa niaba ya waliokerwa na hili nakupongeza kwa matumizi huru ya uhuru uliopo bila kujali uchokozi dhidi ya utulivu.

Tukirudi kwenye suala la msingi ni kwamba, watu waungwana hawaogopi kutuhumiwa bali huogopa KUHUKUMIWA kwa sababu kutuhumiwa ni dhana ambayo hudhihirika baada ya process ya kisheria (MAHAKAMA).

Watu safi hupenda kufikishwa mahakamani ili kujisafisha, ingawa kuna tatizo jingine huko mahakamani kutokana na mifumo mibovu ya mtu mmoja kuhodhi haki za watu bila kuhojiwa, lakini bado ina ubora fulani kwamba angalau taratibu zimefuatwa.
 
Manung'uniko na mijadala mingi imeonekana ikisema Mheshimiwa Rais Mstaafu angefaa kupelekwa mahakamani, na wengine hudiriki kusema 'angestahili kuozea jela'.

Jambo ambalo najiuliza hata akiondolewa kinga,je katiba inaruhusu rais mstaaf kushtakiwa?

na kama inaruhusu, DPP atamshtaki kwa kosa gani na lililopo katika sheria ipi?, Je ushaidi upo wakutosha?

Adhabu ya makosa au kosa hilo ni ipi?, kifungo au fine?

je na kama kinga yakatiba ikitolewa itakua applied retrospectively?yani namaanisha itamgusa Mpaka Rais mwinyi au ni kwa marais wanaofuatia?

Dhumuni lakuuliza maswali haya ni kwasababu inaonekana kama jamii ya Kitanzania tunashabikia tu kwakusema Mkapa apelekwe mahakamani bila ya kusema kwa kosa lipi na lililokatika sheria ipi, na kujua ugum wa kikatiba unaomlinda. Si maanishi kusema tu Kiwira, la hasha hiyo haitoshi. Si maanishi kufungua kampuni ikulu, tunaweza kusema hayo yote, lakini cha muhimu sheria zetu zinasemaje kuhusu mambo kama hayo? na process yake ikoje ya kikatiba?kama nilivyouliza hapo juu.

Naomba tujadili bila matusi au shutuma.
Asanteni.

kwanza alitakiwa kuondolewa madarakani na Bunge siku alipovunja sheria ya maadili ya 1998. Lakini zaidi kwa kutumia madaraka yake vibaya na kulisababishia taifa hasara.
 
[h=2]30 DECEMBER 2011[/h][h=3][/h]

Na Yusuph Mussa, Korogwe

BAADHI ya wananchi katika Wilaya ya Korogwe, mkoani Tanga, wamesema kama Katiba Mpya itaendelea kumlinda rais asishtakiwe akiwa madarakani na baada ya
kumaliza utumishi wake serikalini, upo uwezekano wa kutokea kiongozi ambaye atatumia fursa hiyo kufanya maamuzi yanayoweza kusababisha machafuko nchini.

Wananchi hao walishauri hoja ya mgombea binafsi ni vyema ikaruhusiwa ili kuwalinda viongozi wanaochaguliwa na wananchi ambao vyama vyao vinatishia kuwavua uanachama na kupoteza nafasi zao kutokana na migondano inayotokea ndani ya chama.

Wakazi hao waliyasema hayo juzi mjini Korogwe, katika mdahalo wa kujadili katiba iliyopo, kasoro zake na kutoa maoni yao ambayo wangependa yaingizwe katika Katiba Mpya.

Walisema umefika wakati wa rais kushtakiwa kama itabainika ameshindwa kuwajibika kwa kuhudumia wananchi wake.

“Kinga ya rais iondolewe kama itabainika amefanya makosa ili aweze kuwajibika kwa wananchi na kuifanya Ikulu yetu kuwa sehemu takatifu.

“Enzi ya uhai wake, Baba wa Taifa Hayati Mwalimu Julius Nyerere aliwahi kusema kuwa, Ikulu si mahali pa mchezo lakini katiba iliyopo inamlinda rais asiwajibishwe hata aanapofanya kosa,” alisema Bw. Renatus Mchau.

Naye Bw. Omar Chagogwe, alisema udikteta ulioingia katika vyama vya siasa dhidi ya viongozi waliochaguliwa na wananchi, hauwezi kukoma kama suala la mgombea binafsi halitaingizwa kwenye Katiba Mpya.

“Mgombea binafsi ni jambo la msingi sana kwani katika vyama vya siasa kuna fitina nyingi zinazowafanya wawakilishi wa wananchi washindwe kufanya kazi zao ipasavyo, kama mwanachama hawezi majungu, hawezi kupitishwa na chama chake kugombea uongozi.

“Kama tutakuwa na mgombea binafsi ambaye anakubalika na wananchi, watamchagua ili awatumikie, tunaomba Katiba Mpya izingatia jambo hili,” alisema Bw. Chagogwe.

Kwa upande wake, Mchumi wa Halmashauri ya Wilaya hiyo, Bw. Lameck Kajala, alisema kitendo cha serikali kuteua wabunge kuwa mawaziri, kinapunguza uwajibikaji hivyo Katiba Mpya ione umuhimu wa kutenganisha mfumo huo.

Mchumi wa Halmashauri ya Mji wa Korogwe Bi. Grace Mbarouk, alisema Serikali imegawa madaraka kwa wananchi kinadharia lakini bado haizisaidii halmashauri kujiendesha kwani bado inachukua kodi zote na kuzipeleka Serikali Kuu.

Mshiriki mwingine katika mdahalo huo, Bw. Abdillah Ibrahim, alisema wakuu wa mikoa na wilaya wanapochaguliwa na rais ni vyema wakapigiwa kura, kuthibitishwa na wabunge kama ilivyo kwa Waziri Mkuu ili kuondoa watendaji wasio na sifa.

Akitoa mada katika mdahalo huo, Hakimu Mkazi wa Wilaya ya Handeni, Bw. Jonathan Mgongoro, alisema Azimio la Arusha bado halijafa bali limeboreshwa ili kuwafanya watumishi wa Serikali wasipate shida baaada ya kustaafu na kuwawezesha wafanyabiashara kujiunga na siasa.

Muongozaji wa mdahalo huo na mjumbe wa Kamati ya Jukwaa la Katiba nchini, Bw. Esrael Ilunde, alisema kuna mipaka kwa wananchi kutoa maoni yao juu ya Katiba Mpya na wale ambao watavuka mipaka hiyo watashtakiwa na kufungwa jela.

“Ukifika wakati wa Tume ya Rais kukusanya maoni ya wananchi, alafu mtu akajifanya ni mjumbe wa tume hiyo au kufanya kosa lolote, atalipa faini kati ya sh. milioni tano hadi 15, kwenda jela miaka mitatu hadi saba au vyote kwa pamoja,” alisema.

Mwenyekiti wa Mtandao wa Asasi za Kiraia wilayani Korogwe (KOCISCO), ambao ndio waratibu wa mdahalo huo, Mchungaji Hebert Mwaimu, alisema lengo la mdahalo huo ni kuwaandaa wananchi kujua Katiba ya sasa na kujiandaa kuipokea tume hiyo.

Wakuu,
Nafahamu yamekuwepo mapendekezo mengi kuhusu mabadiliko ya Katiba ya JMT. Hata hivyo, mapendekezo yangu (ambayo naamini yamekwishatolewa mara kadhaa) ni kwamba, kipengele kinachompa kinga Rais asishtakiwe akiwa madarakani (au baada ya kutoka) kifutwe kwa sababu zifuatazo:
* Kuanzia utawala wa Ben Mkapa, tumeshuhudia ufisadi mkubwa wa kuiuza nchi yetu kwa wawekezaji.
* Mashirika mengi ya umma yameuzwa wakati wa uatawala wake kwa kisingizio cha ubinafsishaji, hata yale yaliyokuwa yana uwezo wa kuzalisha.
* Viongozi wengi, akiwemo mwenyewe, walijiuzia mashirika hayo kwa bei chee na kuwadhulumu wananchi haki yao.
* Tangu utawala wa ****** JK, madudu mengi yamejionyesha huku mwenyewe akitabasamu na kucheka cheka tu.
* Mafisadi sugu wameshindwa kufikishwa mahakamani kwa misingi ya kuwalinda washkaji zake.
* Ni katika utawala wake tumeshuhudia akiwaamuru wezi (wa EPA) warejeshe fedha halafu bila kushtakiwa.
* Kwa kutumia kisingizio cha kuvutia wawekezaji, ameiuza ardhi ya tanzania kwa wageni ambao wanadai wanaendesha kilimo wakati si kweli.
na kadhalika na kadhalika.....

Naanzisha mjadala huu wadau, tafadhali tuchangie kwa maslahi ya taifa letu linaloangamia. miaka minne iliyobaki ni mingi, hata barabara inaweza kuuzwa kwa wawekezaji....

lol
 
Back
Top Bottom