Elections 2010 Kinana kukutana na waandishi wa Habari kesho

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,474
39,987
Subject: YAH: MWALIKO WA MKUTANO NA WAANDISHI WA HABARI KESHO IJUMAA-08.10.2010

Habari za leo ndugu zangu,
Napenda kuwaalika katika mkutano na Waandishi wa habari kukutana na Mwenyekiti wa Kampeni za Urais kupitia CCM, Mheshimiwa Abdulrahman Kinana. Mkutano huu utafanyika kesho, Ijumaa tarehe 08.10.2010 saa nane (8) kamili mchana katika ofisi ndogo ya Chama cha Mapinduzi, Lumumba.
Waandishi wote wa habari na wapiga picha mnakaribishwa...
Natanguliza Shukrani..

--
Campaign Communications Team
Kikwete 2010
 
Hallo halo. Redet imekuvivia nguvu za giza za mnajimu Yahya. Njoo utuambie nyara zetu ulizotorosha na Wasomali uliowaleta hapa . Eti Paradise. Ulipata wapi hela za kumiliki meli kama ww sio ja,bazi
 
Sasa utakuwa mkutano wa kukanusha au kuunga mkono hoja? Maana tangu Kinana aje na risiti sijamsikia tena. Lakini bora atupe cha kujadili kama REDET
 
Subject: YAH: MWALIKO WA MKUTANO NA WAANDISHI WA HABARI KESHO IJUMAA-08.10.2010

Habari za leo ndugu zangu,
Napenda kuwaalika katika mkutano na Waandishi wa habari kukutana na Mwenyekiti wa Kampeni za Urais kupitia CCM, Mheshimiwa Abdulrahman Kinana. Mkutano huu utafanyika kesho, Ijumaa tarehe 08.10.2010 saa nane (8) kamili mchana katika ofisi ndogo ya Chama cha Mapinduzi, Lumumba.
Waandishi wote wa habari na wapiga picha mnakaribishwa...
Natanguliza Shukrani..

--
Campaign Communications Team
Kikwete 2010

Naomba wale waandishi wenye ujasiri -- kama vile Kubenea wasisahau kumuuliza Kinana kwa nini aliwafanya Watz wote mafala kwa kuleta 'risiti' feki kuhusu malipo ya ndege ya serikali aliyokodi Salma.

Pili akizungumzia kuhusu REDET wamkumbushe composition ya taasisi hiyo tata kama vile:

* Prof Mukandala,aliwahi kuwa mwenyekiti, sasa ni makamu mkuu wa udsm na swahiba mkuu wa JK
* Dr Ndumbaro, alikuwa mwenyekiti wa REDETsasa ni mshauri wa rais JK mambo ya siasa
* Dr Bana, swahiba mkuu wa Prof Mukandala na sasa ndiye mwenyekiti mwenza wa REDET

* Dr Killian Bernadetha, makamu mwenyekiti wa redet na mtu wa karibu sana wa prof mukandara

Kwa muundo huu REDET si taasisi huru na yenye tija kwa taifa.
 
Natumaini hatojibu maswali mnayotaka; atakuja kuzungumzia suala la Jeshi na vyombo vya usalama.
 
Ni lazima ajibu maswali ya waandishi wa habari na mengine pia kuhusu yakwake binafsi kwani anatajwa sana katika tuhuma kadha za ufisadi pia, hasa kusafirisha nyara za serikali. Maana kama siyo mtu msafi kwa nini alikubali kuwa msemaji mkuu wa kampeni za CCM

Natamka hivyo kwa sababu hivi kweli CCM hawana mtu yoyote mwingine msafi wa kuwa msemaji wa chama hicho bila ya kuibua maswali ya kashfa yanayohusu yeye mwenyewe binafsi?
 
Huyu jamaa ikibidi alipuliwa zaidi ili aache kutufanya wajinga. Anyway, nchi tulishaiuza kwa JK. Naye JK keshaiuza kwa wamarekani na waaarabu sasa ni juu yetu kusuka au kunyoa. Maana kama tunakubali kumwacha tena, basi gharama yake tusilaumu mtu hapa. Wapenzi na mashabiki wote jitoeni saizi ni muda wa lala salama hakuna kurudi nyuma bado wiki tatu tu tumnyoe kipara JK.
 
Hiyu Kinana, Mbona ametuhumiwa kujihusisha na Biashara haramu na hajibu..! au ni kweli ?
 
Natumaini hatojibu maswali mnayotaka; atakuja kuzungumzia suala la Jeshi na vyombo vya usalama.

Aulizwe kuhusu 'chain of command' ya vyombo hivyo vya usalama ili tupate jibu nani alimtuma Shimbo. Pia je, wizara ya ulinzi na JKT imekuwa wizara ya ulinzi, JKT na kilimo? Je, nini hasa dhumuni la ibara ya 41 (7) ya katiba ya jamhuri ya muungano wa Tanzania? Je, kiti cha Rais kiko wazi au la? Kwa nini Urais ni suala la kifamilia?
 
Subject: YAH: MWALIKO WA MKUTANO NA WAANDISHI WA HABARI KESHO IJUMAA-08.10.2010

Habari za leo ndugu zangu,
Napenda kuwaalika katika mkutano na Waandishi wa habari kukutana na Mwenyekiti wa Kampeni za Urais kupitia CCM, Mheshimiwa Abdulrahman Kinana. Mkutano huu utafanyika kesho, Ijumaa tarehe 08.10.2010 saa nane (8) kamili mchana katika ofisi ndogo ya Chama cha Mapinduzi, Lumumba.
Waandishi wote wa habari na wapiga picha mnakaribishwa...
Natanguliza Shukrani..

--
Campaign Communications Team
Kikwete 2010

Iam sure haitakuwa address ya ONE-WAY!
Wanahabari kuweni active, ulizeni maswali yenye utata kwa huyu mtu!
Isije ikawa wanaohudhuria ni wale wenye Jackets za "KIKWETE 2010" peke yao!
Naungana na wengine, kama angekuwemo Saeed Kubenea tungepata ladha ya ukweli wa PC hiyo!
 
Wakao kuwa huko wamwulize hivi ni kwanini CCM inawatumia REDET vibaya? Hivi wanafikiri hatujui ni nani kipenzi cha wapigakura?
 
Huyu jamaa ikibidi alipuliwa zaidi ili aache kutufanya wajinga. Anyway, nchi tulishaiuza kwa JK. Naye JK keshaiuza kwa wamarekani na waaarabu sasa ni juu yetu kusuka au kunyoa. Maana kama tunakubali kumwacha tena, basi gharama yake tusilaumu mtu hapa. Wapenzi na mashabiki wote jitoeni saizi ni muda wa lala salama hakuna kurudi nyuma bado wiki tatu tu tumnyoe kipara JK.

Wewe ni mjinga tu. Asipokufanya mjinga Kinana, basi atakufanya Mbowe na Slaa. Mtu yeyote anayewaamini wanasiasa ni mjinga tu! :tonguez:
 
Wakao kuwa huko wamwulize hivi ni kwanini CCM inawatumia REDET vibaya? Hivi wanafikiri hatujui ni nani kipenzi cha wapigakura?

Teh teh teh! Huko nyuma mlikuwa mnalia kwanini REDET haitoi matokeo ya utafiti wao. Sasa wametoa mnalia vilio vya aina nyingine!

Mlijitayarisha "kisaikolojia" kwa kura za JF kujipa moyo, wenzenu wanajitayarisha "kibaiolojia" kwa kura za maoni ya REDET!

Dalili za maumivu hayo! Teh teh teh :tonguez: :tonguez: :tonguez:
 
ni lazima ajibu maswali ya waandishi wa habari na mengine pia kuhusu yakwake binafsi kwani anatajwa sana katika tuhuma kadha za ufisadi pia, hasa kusafirisha nyara za serikali. Maana kama siyo mtu msafi kwa nini alikubali kuwa msemaji mkuu wa kampeni za ccm

natamka hivyo kwa sababu hivi kweli ccm hawana mtu yoyote mwingine msafi wa kuwa msemaji wa chama hicho bila ya kuibua maswali ya kashfa yanayohusu yeye mwenyewe binafsi?

ccm wooooooooooote wameoza
 
Kinana atuambie kwanini CCM hawataki kuulizwa maswali na watanzania (midahalo) na ikiwa haoni kama hiyo ni kutotutendea haki wapiga kura?
 
Wewe ni mjinga tu. Asipokufanya mjinga Kinana, basi atakufanya Mbowe na Slaa. Mtu yeyote anayewaamini wanasiasa ni mjinga tu! :tonguez:

Umwamini au usimwamini, mwanasiasa atakuwa kiongozi wako tu, kwa hiyo wote tu wajinga basi!
 
Back
Top Bottom