Elections 2010 Kinana aomba wasilaumiwe sana - "Tusiwachanganye wananchi"

Leo nimejikuta nacheka sanaaa.. Mwenyekiti wa Kampeni ya Urais ya Kikwete Bw. Kinana akihojiwa mapema leo asubuhi na ITV amevisihi vyama vingine visiwaeleze sana mambo mabaya na yenye kubebesha lawama serikali ya Kikwete kwani kwa kufanya hivyo wanawachanganya wananchi.

Politics is a zero sum game. You win by making your opponent lose. And you do so by hitting hard on his/her achilles' heel.

Him (Kinana) pleading for the opposition not to tell the people about CCM's wrongs is hilarious and something I have never heard of since I started following poltics.
 
Japo siungani na msomali moja kwa moja, lakini hoja ya msingi ina mantiki tuu tusibakie kulaumu, kulalamika na kulalama tuu, bali kampeni ziseme tutafanya nini.
Yaani zisibakie kampeni za fault finding mission, bali trend setting mission, hayo mabaya ya nyjuma/CCM yatumike kama sababu, cause ya kutufikisha hapa tulipo, na isiwe ndio the only finger pointing CCM, CCM, tunawapa free publicity hawa CCM kwenye kampeni zetu.
Aaaaah mkuu wangu Pasco sikutegemea kama wewe utaweza kusema hivi. Yaani kweli unaweza kwenda mbele pasipo kujua fault zilizowakwamisha ni zipi ili kuzirekebisha ili ku set hizo trend za kwenda mbele. I mean mkuu wangu hata sikuelewi kabisa hapa.

Siku zote watu tunajifunza kwamba ni lazima ujue unakotoka ili upate kusonga mbele laa sivyo hutaweza kuona tofauti baina ya kule ulikotoka, ulipo na unakotaka kwenda. Soote Watanzania tunajua fika kwamba Tuna matatizo makubwa ya afya, elimu, maji, miundombinu toka tumepata Uhuru na sii kutokana na maafa au vita wala kitu kinachoweza kuzungumziwa kisayansi kwa nini tumeshindwa.
Hivyo ili twende mbele ni lazima tufahamu kilichotukwamisha mkuu wangu.

Hata ktk usafiri mkikwama njiani, ni vizuri kujua hata kama ilikuwa pancha tu ya tairi, mnasimamam kuziba hilo pancha halafu ndio safari ipangwe kwa sera mpya kwa kuzingatia muda tulopoteza kuziba pancha. Na wala sii vibaya kujua hiyo pancha imesababishwa na kitu gani yaweza kuwa rimu ndio mbaya au lolote lile.

Swali la wananchi ni moja tu Kwa nini tumeshindwa kuondoa matatizo yetu kwa miaka 50 iliyopita hali Utajiri wote tunao?..Ndipo hawa viongozi wanaanza kutupa Ukweli, moja wapo ni UFISADI na kibaya zaidi CCM badala ya kukubali kuwepo kwa tatizo la UFISADI wanataka tujifunge mikanda kwa ahadi zile zile tulizokuwa tukipewa for the last 50 Yrs huku mali yetu ikifisadiwa..

Mkuu wangu yawezekana sisi Wajinga lakini siii wajinga hivyo. Kwanza tujue kwanini gari letu limesimama, limekwama hapa tulipofikia na sii kudanganywa tu kwamba kila kitu ni safi tutafika huko tuendako tusizungumzie mabaya, huu ni ushenzi wa tabia na mila za kizamani kwamba usitake kuhoji wakubwa zako.. wee fuata tu hata kama anakosea..Ndio malezi wanayotaka hawa kina Makamba.
 
Leo nimejikuta nacheka sanaaa.. Mwenyekiti wa Kampeni ya Urais ya Kikwete Bw. Kinana akihojiwa mapema leo asubuhi na ITV amevisihi vyama vingine visiwaeleze sana mambo mabaya na yenye kubebesha lawama serikali ya Kikwete kwani kwa kufanya hivyo wanawachanganya wananchi. "Tuna matatizo mengi ya afya, elimu, maji, miundombinu hivyo tuzungumzie sera zaidi tutafanya nini" amesema Kinana.

Je vyama vingine vitamsikiliza na kuacha kuzungumzia mambo ya kashfa au ubovu na kuanza kueneza sera tu? Je kuna umuhimu wa kuwajulisha wananchi mambo yaliyokwenda kombo miaka mitano iliyopita?
Ni sawa na kuhubiri pasopo kutaja ubaya wa shetani na dhambi.
Ubaya au ubovu haujileti bali hupangwa na kustawishwa na wenye dhamira.
hivyo kuwabebesha lawama CCM ndo mwake kwani hawakusaidiwa na mtu kuimong'onyoa Tanzania hadi kufikia hapa tulipo.
Lazima tuseme na kama si hivyo mawe yatapiga kelele
 
Ni sawa na kuhubiri pasopo kutaja ubaya wa shetani na dhambi.
Ubaya au ubovu haujileti bali hupangwa na kustawishwa na wenye dhamira.
hivyo kuwabebesha lawama CCM ndo mwake kwani hawakusaidiwa na mtu kuimong'onyoa Tanzania hadi kufikia hapa tulipo.
Lazima tuseme na kama si hivyo mawe yatapiga kelele

Naomba nimwombe rasmi Mwanakijiji aiweke hapa ile article yake ya "Jambo(kama si ukweli) ambao CCM hawataki uujue". halafu aunganishe na mada hii.

Mzee mwanakijiji, article hiyo uliitoa katika gazeti la Tanzania daima.
 
Kama kumuanika Mwizi Hadharani kutawachanganya Wanannchi, basi Acha Wachanganyikiwe tu lakini Ukweli ni Lazima waufahamu
 
Wananchi wana haki ya kujua uovu wa serikali ya CCM ili wafanye uchagizi uliokwenda shule. Ukweli utabakia kuwa ukweli, Kinana anatakiwa kulifahamu hilo!

Kinana anachosema siasa ziendelee kama kawaida ili mafisadi waendelee bila bughudha.

Nielewavyo mimi fedha za maendeleo ya nchi zina chanzo kimoja tu nacho ni serikali. Sasa mfano bajeti ya 2010/11 ilishapita. Ahadi hizi je zimo kwenye bajeti yetu? Zina nafasi gani kwenye ilani ya chama cha mapinduzi au vyama vingine. Hapa ndipo swala la Kinana linatoa picha yake ya uelewa potofu. Maeneo ya kuelekezwa maendeleo YANATATIZWA na ufisadi unaopunguza au kuingilia matumizi ya maendeleo. Kwa wenye taaluma ya uendeshaji wa serikali ni wazi changamoto za ufisadi LAZIMA zikabiliwe kulinda vyanzo vya mapato ya serikali na matumizi yake. Kinana anataka nchi iendeshwe ki"business as ussual"
 
Lazima tuambiwe tulifikaje hapa(umaskini mkuu) na tutatokaje hapa kwenda kule (mafanikio) Wakutuambia ni CHADEMA
 
Kinana weeeeee,

Kama tutawambia wananchi nini tutafanya kwa njia ya sera na ilani sijui, si watatuuliza kuwa mbona hayo wameahidiwa na ccm miaka nenda rudi and nothing has done? Watasema kuwa kama ni sera na ahadi ccm inatuletea kila baada ya miaka mitano zikiwa na sura ya kutamanika lakini hakuna lolote, ni sawa na kuchukua panzi na kumuweka ndani ya chupa na kumuweka mbele ya kuku, unadhani kuku atajua panzi yuko katika chupa? yeye atajaribu kuendelea kudonoa chupa bila mafanikio. Sasa sisi tutawaamini vipi kuwapa nyinyi usukani?

Ni lazima kwanza watu waambiwe uovu wa ccm na kwa nini wako hivo walivyo tokana na sera za ccm na ndipo waambiwe Chadema itafanya nini.

Usitulaghai tuseme nini na tuache nini. 2010 Hatudanganyiki tena. Leo nilikuwa vijijini huko na sikuamini kugundua kwamba hata vijijini wameamka na wanamzungumzia sana Dr Slaa. Ajabu wengine ni viongozi wa ccm yenyewe. Nikagumdua kumbe hata wao wameshamchoka mbabaishaji huyu. Mmoja wa wale niliyezungumza naye akaniambia anawashangaa hawa viongozi wao wanawajali na kuwapapatikia wapinzani wanaorudi ccm na kuwapa vyeo huku wakiwatosa wao waliokihangaikia chama miaka nenda rudi. Akasema lazima nao wakitose sasa.

Unasikia wewe kinana?
 
Lakini nimejiuliza nilipomsikiliza mbona lugha ilikuwa imepowa na sauti ilikuwa ya kiuungwana ,sio ile tena ya kuonyesha kwamba tayari wamekata nchi iwe isiwe,nimejiuliza mengi nikasema nini wanachokiona mbele yao,msomali wa watu amekazana pia kuonyesha kwamba wao sio wanaotumia lugha za matusi,ukweli wananchi wanaujua nani mwenye matusi na ngebe

Kinana is a smart fellow, trust me! Ndio maana anapewa kazi kama hiyo ya kuongoza jahazi wakati wa kampeni maana akiwa mtu wa jazba ataharibu mambo.
 
Duh, kumbe CCM wanaogopa kuumbuliwa mapungufu yao mbele ya wananchi na ndio maana hawataki mdahalo baina ya wagombea ! Nafsi zao zinawasuta na wanataka kukimbia vivuli vyao jambo gumu na lisilowezekana kirahisi. Ningekuwa Kinana ningemshauri Kikwete awaombe wananchi radhi kwa kujipatia uongozi mwaka 2005 kwa njia za udanganyifu na rushwa - labda wapo Watanzania watakaomsamehe.
 
Japo siungani na msomali moja kwa moja, lakini hoja ya msingi ina mantiki tuu tusibakie kulaumu, kulalamika na kulalama tuu, bali kampeni ziseme tutafanya nini.
Yaani zisibakie kampeni za fault finding mission, bali trend setting mission, hayo mabaya ya nyjuma/CCM yatumike kama sababu, cause ya kutufikisha hapa tulipo, na isiwe ndio the only finger pointing CCM, CCM, tunawapa free publicity hawa CCM kwenye kampeni zetu.
Wameshindwa kuelewa kuwa wao wanatakiwa kutangaza sera zao.HATA mbatia alimsihi mgombea wake kuzungumzia sera za chama chake.
 
Wameshindwa kuelewa kuwa wao wanatakiwa kutangaza sera zao.HATA mbatia alimsihi mgombea wake kuzungumzia sera za chama chake.

kwani tatizo CCM ni sera au utekelezaji wa sera utakanao na ufisadi.idiota!!!!
 
Yaaani nikisikia makamba au huyu kinana anaongea kwenye tv nakimbia kusikiliza ili nicheke
 
Wameshindwa kuelewa kuwa wao wanatakiwa kutangaza sera zao.HATA mbatia alimsihi mgombea wake kuzungumzia sera za chama chake.

Mkuu Padri nenda kwenye mikutano ya Dr. Slaa ndo utaelewa vizuri. Jamaa katika saa moja ya mkutano karibu dk 57 anamwaga sera za kufa mtu na dakika 3 tu anazitumia kutoa kibwagizo kimoja ambacho kinadakwa kwa haraka sana na vyombo vya habari cos pamoja na mambo mengine nao wanataka kumake headlines.

Kama kuna mgombea anashuka nondo kwenye uchaguzi huu basi Dr. Slaa is second to none, trust me.
 
Hata Kikwete leo amewaambia wagombea wa CCM na viongozi waiweke pembeni Ilani ya uchaguzi ya CCM ya 2010 na badala yake wawazungumzie wananchi hali halisi iliyopo alitumia neno "Politics is local", kama eneo hakuna daraja kumwambia mawananchi ilani inasemaje hakutasaidia badala yake aambiwe namna daraja litakavyopatikana.

Hivyo wapinzani wanatakiwa kuwakumbusha wananchi ahadi ya Maisha Bora kwa Kila Mtanzania" iliyotolewa na CCM na Jakaya Kikwete 2005; kama wananchi walipata au kutopata maisha bora, na kuwafafanulia wananchi kwa ufasaha sababu ziizopelekea watanzania walio wengi kutopata maisha bora ukiachia mbali kikundi kidogo cha watawala.

Na pia kuwapatia mikakati ya kuchukua ili katika kipindi hiki cha 2010-2015 fedha na rasli mali za taifa viweze kusimamiwa vyema. Mkakati mmojawapo mkubwa ukiwa ni wananchi kuchukua hatua za makusudi kuongeza maradufu idiadi kabisa wabunge kutoka Kambi ya Upinzani kwa nia kulipatia Bunge uwezo zaidi wa kuisimamia Serikali,kuthibiti Ufisadi,wizi wa mali na fedha za umma, utoroshaji wa utajiri wa Tanzania n.k ambavyo kwa pamoja ndivyo vinaendelea kuchochea umaskini wa watanzania walio wengi licha ya Tanzania kuwa na utajiri mkubwa.
 
Tuna tatizo la kutokujua kazi za chama cha upinzani miongoni mwa makada wa CCM. Wakati wa kampeni, chama cha upinzani lazima kifanye mambo mawili ya msingi:

i) Lazima kionyeshe tatizo lilolopo kabla ya kutoa mbadala wa utatuzi wake. Katika kufanya hivi lazima kieleze udhaifu wa serikali iliyopo, ikiwemo kuiumbua na kuizodoa.
ii) Kikishaonyesha hali halisi iliyopo, lazima kieleze hali itakuwaje kama chenyewe kitapewa dhamana ya kuongoza nchi, kwa maana ya falsafa, sera na mikakati mbadala.

Kwa upande wake, chama kilichopo madarakani lazima kieleze mafanikio yake na jinsi ambavyo kitayaendeleza hayo mafanikio kwa ufanisi zaidi.

Kwa hiyo ni umbumbumbu wa kisiasa kudhani kuwa chama hakipaswi kuiokosoa, kuizodoa au kuimbua serikali. Wasipofanya hivi, hawana sababu ya kugombea maana watakuwa wameridhika na hali iliyopo. Wenzetu wa CCM hawajui kazi ya chama cha upinzani wakati na baada ya uchaguzi. Ndio maana ni muhimu sana wawekwe pembeni ili wakajifunze maana ya kuwa chama cha upinzani.
 
Japo siungani na msomali moja kwa moja, lakini hoja ya msingi ina mantiki tuu tusibakie kulaumu, kulalamika na kulalama tuu, bali kampeni ziseme tutafanya nini.
Yaani zisibakie kampeni za fault finding mission, bali trend setting mission, hayo mabaya ya nyjuma/CCM yatumike kama sababu, cause ya kutufikisha hapa tulipo, na isiwe ndio the only finger pointing CCM, CCM, tunawapa free publicity hawa CCM kwenye kampeni zetu.

Mkuu,

Bado sijaiona hiyo 'fault finding mission' hapa, wala 'finger pointing': Na hiyo 'trend' waliyoiweka si wengine bali chama tawala - inaitwa 'danganya wajinga kadiri uwezavyo'. Ghafla, wajinga wamepata kajielimu kadogo wakagutuka! Ndipo waongo wanahamaki na kutangaza takwimu, ahadi (namkumbuka anasemekana kuahidi daraja - akajibiwa halihitajiki kwani hakuna mto; akawahi upesi kusema 'basi nitaleta mto' ili daraja lihitajike)!, majigambo, fitina kuhusa maisha binafsi ya wagombea wasio kambi yao hata kama wapo chama chao, nk nk...

Sisi wajinga tumeona t-shirt haziliwi wala hazisomeshi, mabango hayatibu wala hayapalilii mashamba, fedha hazinunui mahitaji kwa kutosheleza japo juma moja. Kumbe kura zetu zina umuhimu mkubwa kuwawezesha 'wajanja' waendelee kutunyonya huku tukivumilia ati kwa kuwa anayekula ni 'zimwi likujualo' na hatatumaliza..... Atamaliza nini wakati kilichobaki ni mashimo, magofu na mifupa ambayo hata mbwa kaacha!?

Sasa chama tawala hawataki 'negative publicity', vema tu. Hizo 'sera' na 'ahadi' tutawanukuu nazo huko mbele wakika katika kambi inayowastahili! Muda si mrefu chama tawala kitakuwa chama cha upinzani! Huu si utabiri bali ni ukweli baada ya kufungua macho!
 
Kama wiki mbili tu za kampani wanaaza kuomba suluhu,kweli wakati wa sisiem kuanguka umefika!!!
 
Politics ni pamoja na kusema uozo wa serikali na kusema kila kitu maana policies zao ndio matunda na matokeo yake. Hivyo Kinana hana jipya zaidi majungu
 
Back
Top Bottom