Kinamama/dada msikanyage hapa!

Bishanga

JF-Expert Member
Jun 29, 2008
15,323
10,050
Napenda nichukue fursa hii kuwaomba kina baba ambao tumekula chumvi ya kutosha (Kyabushaija et al) mara kwa mara tuwe tunawapa hint vijana wa kiume wadau wa MMU ili mbele ya safari yasijewakuta yaliyotukuta sisi.
Kwa leo naanza mimi:
Ndugu vijana,ukijaliwa kuwa kwenye mahusiano yawe ya ndoa / urafiki wa karibu/uhawara,basi kipindi upo katika lindi la mapenzi jihadhari sana kutoa siri zako za ndani sana kwa mwenza wako.Mathalani ukiwa mfanyabiashara jihadhari kumweleza mwenza wako jinsi unavyopambana na competititors,TRA na regulators wengine. Kama umeajiriwa jihadhari kuwasema vibaya maboss wako mbele ya mama chanja wako na kama kuna mishemishe unafanya kazini ili kujiongezea kipato ndo kabisaaaaaa usithubutu kumjuza mwenza,ye mwache aone zinaingia tu. Naongelea hili kutokana na uzoefu na si wa kwangu tu lakini wa wanaume wengi. Ilivyo ni kwamba mkiwa kwenye malavidavi mke/girlfriend/hawara atakutunzia siri mpaka ya ndani sana lakini ole wako siku ukimkosea/mkidiffer chances are atamwaga razi kwa wahusika na usipoangalia utashtukia Hosea/Kova/maodita wanakupigia hodi.Ni ushauri tu na wakati unautafakari mkumbuke Shakespeare aliyesema na ninakuu 'hell knows no fury like a woman scorned'!
Weekend njema.
 
i think siri zinaweza vuja in both ways hata kwa wanaume wakiwa na hasira si unamuona jaffarai alivyobwabwaja?ooops kumbe ni kwa wanaume tu?:A S 13:
 
:A S 13::A S 13: wow....great piece of advice....opppsssssssssss,nimekosea njia.....byeeeeeeeeee!!!!!!!!!!!!!!!
 
Mmmmmh, mi naona sio wanawake tu, hata dume mwenzako, tena sometimes hata ndugu wa damu kabisa ukikorofishana nae pia anaweza kumwaga siri vilevile kama uliwahi kumwambia. Cha muhimu kama umeamua kutosema kitu basi usiseme kwa yeyote.
 
Nimevaa suruali kwahiyo nachangia!Sio kila mtu ana tabia hiyo...alafu siri ni mzigo tafuta unaemuamini ushee nae!
 
Mmmmmh, mi naona sio wanawake tu, hata dume mwenzako, tena sometimes hata ndugu wa damu kabisa ukikorofishana nae pia anaweza kumwaga siri vilevile kama uliwahi kumwambia. Cha muhimu kama umeamua kutosema kitu basi usiseme kwa yeyote.
CPU usicheze na wanawake, soft kwa nje lakini wana roho ngumu ni hatari!
 
ni kweli kabisa haitakiwi binadamu yeyote kumweleza yako ya msingi, ikiwa mfano wamwadithia rafiki yako kuhusu mipango yako anaweza akajifanya kuchangia mawazo tena mazuri lakini kumbe mwenzako moyoni hujui anataka kufanya nini, vilevile tunahitajika tuwe makini na kila jambo tunalotaka kusema, nakumbuka katika vikao vya jioni nilikutana na wazee waliwahi kunihabarisha kuwa kuna vitu vitatu twatakiwa kuvijua na kuvitenda yaani tumia muda mwingi kusikiliaza, maswali kidogo na usitumie muda mwingi kuchangia michango ya mawazo, nadhani walikuwa wanajua nini kinaweza kutokea kwa ushiriki wako wa mada mbali.

KIFUPI MSIRI WAKO NI MOYO WAKO PEKEEE
 
Asante mzee bishanga.
Nimekusikia mzee wangu.
Hapa atakula out za kutosha, kagari kake nataka nimbadilishie pia.ila asitake kuja sana zinakotoka.
 
Nashukuru kwa ushauri,uliyoyasema yamewahi nikuta na najuta kumwamini kiasi kile mchumba wangu
 
Urafiki upo kwa ajili ya kuaminiana
Siri ipo kwa ajili ya ku"share"
Vyenginevyo hakuna sheria, urafiki wala siri.
Ikiwa huamini mtu yeyote iko siku utakimbia hata kivuli chako.
 
ha hahaaaaaaaaa uwiiiiiiiii mbavu zangu mie leo Michelle, Lizzy na rose!!!!
 
Wanawake ni watu hatari wanapokorofishwa, Ni kweli mipaka katika Siri unatakiwa sana.
 
wanaume wa siku hizi mlonyimwa makoromelo,kwenye kupepeta hakuna tofauti kati ya mwanamke na mwanaume mpaka siri zenu mwabwabwaja:wink2:
 
Nimevaa suruali kwahiyo nachangia!Sio kila mtu ana tabia hiyo...alafu siri ni mzigo tafuta unaemuamini ushee nae!

siri ni ya m1 tu, akiijuwa mwenzako juwa upo mashakani labda tu iwe na yeye anahusika katika hilo dili/ishu mnayoifanya kuwa ni siri
 
....ikiwa mfano wamwadithia rafiki yako kuhusu mipango yako anaweza akajifanya kuchangia mawazo tena mazuri lakini kumbe mwenzako moyoni hujui anataka kufanya nini,.....

KIFUPI MSIRI WAKO NI MOYO WAKO PEKEEE

ooohh kuna watu na viatu duniani
ooohh kuna vyauma ndani kwa ndani
 
Back
Top Bottom