Kinachoweza kutokea huko uarabuni ni hatari kwetu kuliko mgomo wa madaktari

Sangarara

JF-Expert Member
Sep 29, 2011
13,100
5,649
Wandugu
Mkakati wa kuidhibi Irani wa Marekani na washirika wake hauna tofauti na kumfungia Paka ndani
kisha uanze kumuangushia kichapo. nadhani maamuzi atakayochukua yanajurikana.

Hiki ndio hasa kinachokaribia kutokea huko Irani, Baada ya Israel kutishia kuishambulia Irani Muda
wowote na wao wamedai muda wowote wataufunga mfereji wa hormuz na kwamba wataishambulia
vilivyo nchi yoyote iliyokaribu nayo itakayokubali kutumika kuratibu harakati za kijeshi dhidi yake.

Lolote kati haya likitokea litasababisha vitu viwili
1. Ukosefu wa Mafauta kwa muda mrefu tu
2. Vita ambavyo kutokana na instability iliyotapakaa kote arabuni inaweza ikasambaa mpaka pande
zetu ama moja kwa moja ama kwa hathari za kuunga unga.

Yoyote kati ya haya yatatuletea matatizo makubwa sana, Na hapa naomba kutoa wasi wasi wangu,
Iran is weill prepared for any thing.
Naomba kwa yeyote atayepata rehema akumbuke kumsihi Mwenyezi Mungu ikiwezekana alicheleweshe
hili dhahama japo kidogo.

Sioni wakati mwingine wa vita ya dunia kutokea zaidi ya huu. sababu Binaadamu wote, kote duniani
tuko very dissatified na kila kinachoendelea. Kote duniani.
 
Sidhani kama hiyo vita ya Iran Vs Israel/USA itaongeza ama kupunguza kipigo cha mbwa mwizi ambacho tayari tunakipokea kutokana na ugumu wa maisha unaoongezeka kila siku ukichochewa na mfumko wa bei. Vita hiyo iwepo isiwepo kipigo chetu kiko palepale mpaka hapo tutakapojua kutumia vichwa vyetu (badala ya matumbo) kuchagua viongozi wa kisiasa -i.e. wenyeviti wa mitaa, madiwani, wabunge, na rais.
 
Hii kitu naifatilia kwa muda mrefu now, namuomba mungu isitokee hii vita. Binafsi nayachukia mataifa makubwa maonevu like USA, UK, France, Germany, na vibaraka wao. Mpango uliopo kwa mataifa hayo niliyoyaorodhesha ni kuidhofisha Dola ya IRAN kwa namna yoyote na hata ikiwezekana kuivamia IRAN kijeshi, nafikiri ndicho kinachotaka kutokea sasa.
 
Kinachonitisha ni kwamba
si Bunge letu wala Serikali inayofanya maandalizi yoyote ya kukabiliana na hathari
za matukuo ya uko. Itaniuma sana siku Jakaya akijitokeza kwenye TV sebureni kwangu
kuniambia kwamba mfumuko wa bei ama baa la njaa kwenye baadhi ya maeneo nchini
umechangikiwa kwa kiasi kikubwa na ama kufungwa kwa mlango wa hormuz ama
vita.

Ninategemea kumsikia akitoa maelekezo sasa, hivi sisi tutakuwa watu wa kuwa wahanga
wa maamuzi ya mataifa mengine na wafanyabiashara mpaka lini?

Historia inatuambia kwamba Mababu zetu walishiriki vita ya Pili ya dunia bila ridhaa yao,
hawakujua sababu wala hawakuwa na interest yoyote katika vita ile, lakini wao na
kizazi chao ndio waliokuwa wahanga wakubwa wa vita hiyo, mara tu baada ya vita
marekani ilitoa misaada mikubwa sana ya kiuchumi karibia kwa mataifa yote ya ulaya
na kuzinua kiuchumi nchi hizo, sisi mpaka leo bado tunamakovu ya vita hiyo.

Na hata sasa, bado tumekuwa kama nyasi kwenye vita vya tembo. Hata chokochoko
za maneno tu baina wa waarabu na USA & CO zinasababisha maelfu ya Waafrica Kufa
kwa njaa ama kwa kukosa huduma za kiafya. Kama sio Tanzania basi Africa needs to wake up.
 
Vita yoyote ktk eneo la mashariki ya kati lazima itakuwa na athari zake kwa uchumi wa nchi ndogo na kubwa. Lakini hiyo si sababu ya kudanganyana kuwa iran ikishambuliwa eti ndo itakuwa vita kuu ya dunia!!! Tuko kwenye 'wakati wa vita na matetesi ya vita' Warusi au Wachina kwa sasa hawako ktk nafasi ya kuingia ktk vita ya jumla ili kuifanya iwe vita kuu. Mikwara na kelele za watu wa mashariki ya kati kuwa 'patachimbika' siku zote inajulikana. Muda wa iran kupigwa atapigwa kama kawaida, na silaha zitakazotumika kuiteketeza zitaamuliwa na iran yenyewe! Akitumia silaha kali wababe wao watatumia kali zaidi ya mara kumi...
 
Back
Top Bottom