Kinachotokea Zanzibar ni kushindwa kwa uongozi wa CCM

[video=youtube_share;J_3Y2TNSTb0]http://youtu.be/J_3Y2TNSTb0[/video]
Yaliyotokea Zanzibar leo na yale yanayoendelea ni matokeo ya kushindwa kwa utawala wa CCM kutatua matatizo ya Muungano. Lakini pia ni ishara ya kushindwa kwa viongozi wetu wa kisiasa nchini kuutetea Muungano na kujenga hoja za kwanini yapaswa uendelee. Kwa muda mrefu kikundi cha watu wachache kimekuwe kikisukumiza hoja dhidi ya Muungano na baadhi yao kuzawadiwa nafasi za uongozi licha ya msimamo wao juu ya Muungano kujulikana. Hivyo siku baada ya Muungani (A Day After the Union) itakapofika siyo Wananchi wa kawaida watakaolalamikiwa bali viongozi wale ambao wameacha siku hiyo ifike. Ukimya wa Wazanzibari wenye kuamini katika Muungano kumewachochea kundi hilo dogo. Tusije kushangaa tunashuhudia kuzaliwa kwa kikundi cha "Boko Haram" cha Tanzania!!! Yote yatakuwa ni kwa sababu ya kushindwa kwa utawala wa CCM kutoa uongozi!

Hatujasikia viongozi wa CCM wakitetea Muungano kama wanavyotetea chama chao; hatujawasikia wakiwapinga anti-unionists kwa hoja zenye nguvu bali wamekuwa wakiwapa baraza huru; na hatujawaona hata viongozi wao wa serikali - walioapa kulinda Katiba ya Muungano - wakitetea Muungano huo.

Ni kana kwamba wameshakubali kisichoepukika - kufa kwa Muungano. Sasa, kama hili ndilo wanalolitaka hakuna haja ya kuumizana, kupigana mabomu, wala kushindana. Kama kuvunjika kwa Muungano ni inevitable - basi hekima inatutaka tuweke mfumo wa kuvunja Muungano huu vizuri na kwa makusudi ili mahusiano ya kidiplomasia baina ya nchi mbili yaanze. Jamani, Muungano uwepo au usikuwepo watu wa Zanzibar hawaendi popote na watu wa bara hawaendi popote. Hata watu waombee vipi Wazanzibar wataendelea kuwepo na watu wa bara wataendelea kuwepo. Sasa kama hii ni kweli basi ni kushindwa tu kwa viongozi wetu na hasa kushindwa kwa sera zao mbovu ndiko kunakofanya mgogoro huu uwe mkubwa kuliko inavyopaswa.

Tusizungushe maneno! Kuvunjika kwa Muungano kutakuja si kwa sababu ya Uamsho au vikundi vya kidini; kutakuja kwa sababu wanasiasa wetu wameshindwa!

Let me be very blunt: Ajenda ya kisiasa ya Zanzibar sasa hivi inaendeshwa na watu wa CUF; wana CCM Zanzibar wamefyata mkia. hawawezi kuwapinga CUF bila kuonekana "hawaitakii mema Zanzibar" na wale wanaoamini katika Muungano hawana ujasiri wa kuwapinga hawa wengine. CUF ndio wanaendesha siasa za Zanzibar sasa.Tumeona katika jaribio lao la kuwapiga marufuku watu wa bara kufanya kazi Zanzibar. CCM imedhoofika siyo bara tu bali hadi Zanzibar!

Hakuna ulichoongea zaidi ya chuki kwa Wazanzibari na chama cha CUF, nani kakwambia wanaokataa muungano ni wachache, si umeoona matembezi yalivokuwa na bado hayakuwa rasmi. Kwa taarifa tu licha ya wana CUF lakini zaidi ya 60% ya wana CCM Z'bar hawautaki muungano isipokuwa wanawaogopa Watanganyika kama alivosema mwakilishi Mansour Yusuf, Hamza Juma etc. Na ndio maana wamekaa kimya.

Na sasa rungu la kuitetea Z'bar limekabidhiwa UAMSHO ili kuorganised waislam wa Zenji kuitetea nchi yao.
Wacha kutupotosha Mkuu tupo macho kwelikweli kwa hili, na hamuwezi kutumia njia ya kuwagawa Wazanzibari kama ilivokuwa huko nyuma ili mpate kuwatawala.
Pia inajulikana kwamba hii serikali ya umoja wa kitaifa imekuwa ni mwiba mkali kwa Watanganyika na ndio maana mnajaribu kuzihusisha harakati za uhuru wa Z'bar na chama cha CUF ili muwagawe Wazanzibari lakini mmechelewa kwa sasa.
Inshaallah Zanzibar itakuwa huru hata kama itabidi kujitoa muhanga tuko tayari Mkuu.
Samahani kama nimekukosea kaka, lakini jaribu kuleta 7bu za msingi usilete hoja za kutugawa Wazenji.

Wazanzibari hatuzungumzii tena UCCM wala UCUF, tunachodeal nacho ni Uzanzibari kwanza ndio ukaona tumesimama kwenye Uislam zaidi (UAMSHO).
 
This Union was between Nyerere and Karume and they are all gone. Let it go.
 
Wazanzibar kuchoma makanisa kwa kisingizio cha kuupinga muungano ni kuwaonea wakristo au nikitendo cha kuiogopa serekali yao.kwani walio uleta muungano ni nyerere na karume ambao walikuwa ni viongozi wa serekali wakati huo makanisa haya kuhusika. kama wanaona kuna makosa yalifanyika basi waadhibiwe walio fanya makosa kuliko kumwadhibu mtu ambae hakuhusika.
 
Ni time tu inafika hali hii haikwepeki wala havuhusiani kushindwa kwa uongozi ktk hili. Watu wakishakuwa na misingi ya kwamba wanaonewa ama hawatendewi haki, hata ufanye nini hutawalizisha.

Sema busara tu inatakiwa kutumika kuwaruhusu watu wafanye maamuzi kama kweli wanataka ama la. Mfano, sifikiri kama uongozi wa UK umefeli kua-adress matatizo yao ya muungano mpaka Scotland watafanya hiyo referundamu mwaka 2014. Wakati ukishafika umefika tu,
 
WanaJF!
salamu kwenu, nimesoma aliyoandika MM pamoja na wachangiaji wengi ambayo kwa kiasi fulani yana ukweli japo the approach we take in discussing this issue at least from my point of view is completely unproductive,if we can talk of productivity!!

there is no way you can discuss the union agony at its actual state without analyzing the different phases it has undergone. I absolute agree with the concept that CCM has failed in the leadership camp but this was well known before the disappearance of the tyranosaurus rex!!!! The LACK OF LEADERSHIP is what ignited the expulsion of ABOUD JUMBE when he brought what are called ZANZIBAR's REVINDICATIONS on the table na hii ilitokea katika halmashauri kuu ya CCM - what happened to him?? HE WAS SUCKED and this was not yesterday!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
Mind you(for those who were young or for some reasons not interested in politics might not know this) JUMBE was a PRESIDENT of REVOLUTIONARY GOVERNMENT. That was a first wake up alarm and CCM kept on snoozing!!!

the second wake up call came when SEIF SHARIFF HAMADI was WAZIRI KIONGOZI katika serikali ya mapinduzi ya Zanzibar - yakatokea yale yale na finale ikawa ni ile ile!!! Seif akafukuzwa CCM na akaishia jela what followed should be left to the historians!!!

when the wake up call allarm rings what you have to do is to "wake up!!!!" and not to discard the ringing device as that wont stop or freeze the day or night whatsoever!!!
Tumekataa kuamka wakati alarm ilipolia sasa tunaanza kulaumiana - i'm afraid it's too late.
Niliwahi kuandika hapo nyuma(ref. JUSSA AMTUKANA SITTA) kuwa njia pekee ya kuulinda Muungano ni kujadili kwa uwazi kero zake na KUZITATUA kama zinatatulika na kama hazitatuliki, arrivederci e buongiorno, basi tuachane kwa amani kama mlivyosema vizuri tu katika post zenu hapo juu. Tanganyika(naanza kufanya mazoezi ya kuiita nchi"mpya) lazima tujifunze kuwa katika Muungano hakuna dogmas wala taboos na nimeona Kikwete in the expression of his highest political strabismus ametamka kuwa Muungano si wakujadili katika mabadiliko ya katiba - what a joke!!!!

my take :
"We can't solve problems by using the same kind of thinking we used when we created them." - Albert Einstein

** kimakosa nilimuita mzee JUMBE kwa jina la MOHAMED ukweli jina lake ni ABOUD samahani kwa kuwachanganya**
 
Hakuna ulichoongea zaidi ya chuki kwa Wazanzibari na chama cha CUF, nani kakwambia wanaokataa muungano ni wachache, si umeoona matembezi yalivokuwa na bado hayakuwa rasmi. Kwa taarifa tu licha ya wana CUF lakini zaidi ya 60% ya wana CCM Z'bar hawautaki muungano isipokuwa wanawaogopa Watanganyika kama alivosema mwakilishi Mansour Yusuf, Hamza Juma etc. Na ndio maana wamekaa kimya.

Inshaallah Zanzibar itakuwa huru hata kama itabidi kujitoa muhanga tuko tayari Mkuu.
Samahani kama nimekukosea kaka, lakini jaribu kuleta 7bu za msingi usilete hoja za kutugawa Wazenji.

Wazanzibari hatuzungumzii tena UCCM wala UCUF, tunachodeal nacho ni Uzanzibari kwanza ndio ukaona tumesimama kwenye Uislam zaidi (UAMSHO).

Bado sijaelewa hapo ni kitu gani hasa hakitakiwi: watanganyika au wakristo?
 
wakuu nina maswali
hivi madhara ya kuvunja huu mungano nini...?

kwanini una kero nyingi kuliko faida..?

mbona wanzanzibar wanaonekana wananyanyasika sana..?

kwanini tusipige kura ya maoni kuhusu huu muungano..?

misamamo wangu binafsi kwa sasa ningependa tuvunje muungano ..
 
Actually most of us hate the so called muungano, it doesnt benefit tanganyikans! I hate it! It only helps zanzibaris!

Kaimba G!
Heshima yako!
Inverting Tanganyika with Zanzibar leaving other variables of your affirmation unchanged, you get exactly what Zanzibaris say regarding the UNION - there is something wrong with the muungano!
 
Wazanzibari mnatakiwa kudai mamlaka yenu kwa njia ambayo ni lazima mchome makanisa? Kwani hayo makanisa ndo yaliyowaingiza katika muungano? Hili mnalolifanya ni ubaguzi wa kinyanyasaji na ni dhambi isiyofutika maana mnawavamia watu wasio na hatia. Kama alivyokwisha wahi kusema nyerere dhambi hii itawatafuna milele. Mkishamaliza kudai uhuru toka katika muungano mtaendesha chuki na vita dhidi ya wakristo watakaokuwa zanzibar na mkimaliza hapo mtaanza chuki ya upemba na waunguja. Sie yetu macho.... Wakati huo huku M4C itakuwa imefanikiwa, maisha yametengamaa tutawapa hifadhi kama wakimbizi.
 
Bado sijaelewa hapo ni kitu gani hasa hakitakiwi: watanganyika au wakristo?

Wacha kubadilisha maneno...Wakristo na watanganyika wamekuwa wakiishi Zanzibar hata kabla ya Muungano na miaka yote hiyo hapakuwa na chuki baina ya wakristo na waislamu. Wanzanzibari wamekuwa wakikataa Muungano kwa sababu za msingi, ikiwemo kero za Muungano zilizodumu kwa miaka 48 bila ya utatuzi.
 
Wazanzibar kuchoma makanisa kwa kisingizio cha kuupinga muungano ni kuwaonea wakristo au nikitendo cha kuiogopa serekali yao.kwani walio uleta muungano ni nyerere na karume ambao walikuwa ni viongozi wa serekali wakati huo makanisa haya kuhusika. kama wanaona kuna makosa yalifanyika basi waadhibiwe walio fanya makosa kuliko kumwadhibu mtu ambae hakuhusika.
This tells you wazanzibar sio swala la muungano linawapeleka kufanya yote haya... swala la udini limeota mizizi ndio sababu ya yote haya. Nasi tuanze kuwafukuza wapemba toka kwetu.. Kila mtu arudi kwao watuache sisi tubaki na umaskini wetu wanafikiri utajiri wa haraka wakidanganywa na waarabu ngoja wachinjane sisi huku kwetu shwaaaaariii ni mpambano wa ccm na upinzani ndio raha yetu. Nendeni bana kwani muungano wa nini! Namshukuru Mungu wangu nilizaliwa Tanganyika. Chinjaneni tu ndipo mtajuwa vita sio lelemama.
 
Muungano hauna tatizo kubwa sana kama tatizo lililojicha ambalo ni gumu sana kuliona kwa haraka haraka.
Wasomi wote na wazanzibar ambao ufahamu wao ni zaidi ya Zanzibar ikiwa ni pamoja na viongozi wa Zbar ndani ya serikali,bunge n.k wanakubali kuwa muungano ni jambo jema na kama yapo matatizo basi yaongelewe.
Ndiyo maana kila siku hutasikia wakisema muungano hapana, utawasikia wakisema Mkataba au Serikali tatu.

Kuna kundi la watu wasioamini kuwa mapinduzi ya mwaka 1964 kumuondoa sultani yalikuwa halali.
Kundi hili linaongozwa na akina maalim Seif na Jussa. Kinachowashinda kujitokeza ni kutokuwa na uhakika na matokeo ya fikra zao.

Endapo muungano utabaki na kuimarishwa basi watakuwa hawana mahali pa kukidhi haja za maisha, wakati huo huo wanaogopa kutetea hata mkataba kwasababu watakuwa wamesaliti kundi lenye nguvu, na muungano ukivunjika watakuwa hawana pa kushika.

Kundi hili limeamua kutumbukiza mbegu ya udini. Mbegu hiyo imetumbukizwa kwa wafuasi wasioelewa na wasio na ufahamu. Ukisikiliza mihadhara ya UAMSHO, utagundua wanaozungumza zaidi ya kusema hutataki muungano hawana hoja nyingine. Ndiyo maana wanashangilia hata wakiambiwa aliyevunja EAC 1977 ni Nyerere! masikini hawajui wanaitikia tu.

Kundi hili linaloitikia lina nguvu sana kwasababu limeaminishwa kuwa kinachosababisha umasikini wao ni dini yao na kwamba Zbar itakapojitenga basi neema kutoka kila pande ya dunia itateremka. Itikadi ndiyo inaliongoza kundi hili na hata kufikia kuchoma moto na vurugu. Itikadi isiyo na nguvu za hoja kidini au kijamii. Itikadi hiyo siyo tu inadhalilisha dini kwa kuchomeka hoja dhaifu zinazopingana na imani, bali pia inadhalilisha wazanzibar.

Ukitaka kujua kundi la wasio na ufahamu lina nguvu za kuburuzwa, soma tamko la Uamsho! Hawa UAMSHO ni wajanja na wanajua hatari ya udini na kugawa watu. Utashangaa leo wanasema si vema kuchoma makanisa wakati video zao zote zinahamasisha chuki dhidi ya makanisa. Uamsho kazi yao ni kutumbukiza sumu mengine yatafuata!

Wazanzibar badala ya kujikita katika vurugu walipaswa kufanya jambo moja, kupigania kura ya maoni. Ni kura ya maoni pekee ingeonyesha kwa kiasi gani na kiwango gani wazanzibar hawapendi muungano. Kuna uwezekano ni kundi dogo tu lenye masilahi binafsi linalopiga kelele.
 
Let me be very blunt: A jenda ya kisiasa ya Zanzibar sasa hivi inaendeshwa na watu wa CUF; wana CCM Zanzibar wamefyata mkia. hawawezi kuwapinga CUF bila kuonekana "hawaitakii mema Zanzibar" na wale wanaoamini katika Muungano hawana ujasiri wa kuwapinga hawa wengine. CUF ndio wanaendesha siasa za Zanzibar sasa.Tumeona katika jaribio lao la kuwapiga marufuku watu wa bara kufanya kazi Zanzibar. CCM imedhoofika siyo bara tu bali hadi Zanzibar!

SIKU ZOTE NILIKUWA NAJIULIZA MAALIM SEIF ALIKUBALIJE KUWA MPOLE AKAKUBALI KUINGIA/KUOLEWA NA CCM NAANZA KUPATA MWANGA ALITAKA TU AINGIE NDANI NDO AANZE KUONYESHA MAKUCHA,HABARI YA KUJITENGA KUTOKA BARA SIKU ZOTE NDO NDOTO ZA MAALIM SEIF HATA BILAL NAE ANA MLENGO HUO HATA WAKAMFICHA BARA NA UMAKAMU
 
Back
Top Bottom