Kinachoibeba Mzumbe university na kuonekana ni bora

mkuu samahani kutoka nje ya mada, nilitaka kufahamu ukimaliza kozi za agriculture engineering na irrigation and water resources engineering unapangiwa kazi na serikali au unatafuta mwenyewe?????

Nani akutafute?thubutuu,kuna course ya kutafutwa cku hz,huo udaktar mpaka uombe sio upo nyumban waje wakugongee..
 
Mbna mnahangaika kwa v2 vsvyo kuwa na maana,ukisha jua ni bora what for now,,Cku ynu ya kuzikwa 2tawazika na vyuo venu bora.from SOIL TO SOIL university
 
Nachofahamu ubora wa chuo ni pamoja na products zinazotoka. Wanafunzi wengi wa SUA, ni bora na wanajituma sana wakiwa makazini ukilinganisha na kutoka vyuo vingine.

Hii inatokana na ubora wa elimu inayotolewa katika chuo kile. Mwanafunzi GOIGOI akienda pale hata Semester moja hamalizi.
Kujituma ni suala binafsi kati ya mtu na mtu,mfano wafanyakazi wawili waliosoma UDSM mmoja akajituma na wa pili akawa hajitumi na ni kozi moja wamesoma.
 
NasDaz
Najua siwezi pata shida kuwashawishi watu kwamba UDSM ni bora kuliko Mzumbe; lakini naweza hata kutupiwa mawe kujaribu kuwaambia wadau kwamba SUA ni bora kuliko Mzumbe! Kwavile ni ngumu kuwashawishi watu (sio wana JF pekee; bali hata wale walio nje ya JF) kuamini kwamba SUA ni bora kuliko Mzumbe lakini ni rahisi kuwashawishi watu kwamba UDSM ni bora kuliko Mzumbe; basi ni bora nikaijadili Mzumbe na SUA!

Mkuu hapa pengine ungelinganisha vyuo vyenyewe kwa vyenyewe vinavyoshabiana kutokana na programmes zinazotolewa na vyuo kama starting point. Bahati mbaya SUA iko unique kuwa chuo pekee kinachotoa programmes zenye mwelekeo wa Kilimo na Mifugo ingawa imeanza kuingiza programmes unazoziita za kina "domo kaya. Kwa programmes ambazo ni "mpya" hapo SUA na zipo MZUMBE nadiriki kuungana na ndugu yako ni heri aende MZUMBE kwa vile wana uzoefu wa kufundisha programmes hizo kwa muda mrefu ukilinganisha na SUA. pamoja na kwamba MZUMBE huko nyuma ikianza ilikuwa inakodi baadhi ya walimu toka SUA kama SUA ilivyokuwa inakodi walimu to UDSM.

Nilijaribu kutafakari uwepo wa idadi kubwa maradufu ya wahadhiri wenye PhD ukilinganisha na wale wenye Masters! Kwa mtizamo wangu, nimeona mambo mawili yamechangia SUA kuwa na PhD holders wengi. Kwanza, kuna kila dalili kwamba wale waliokuwa wanasoma shahada zao za kwanza (ambazo nyingi zake enzi hizo ni za Kilimo) walikuwa hawataki kufanya kazi zinazoendana na fani yao! Kama si hivyo, basi inawezekana kabisa hata hizo ajira zenyewe kwao kupata ilikuwa shida kwavile hatukuwa na kilimo cha ku-accomodate graduates! Kwahiyo si ajabu, wengi wao walikuwa wana-opt kurudi tena darasani na kuchukua Masters na PhD! Sababu nyingine ni kwamba, I guess wafadhili wengi walipendelea zaidi kuisaidia TZ kwenye suala zima la maendeleo ya kilimo, hivyo hii iliwapatia graduates wa SUA kupata scholarship kirahisi kwenda nje ya nchi kusoma!

Mkuu sio kuhisi bali huo ndo ukweli wenyewe na nadiriki kusema kuwa miaka michache baada ya uhuru Kilimo na Mifugo ilikuwa na graduates hadi PhD wengi zaidi kuliko fani nyingine. Awamu ya kwanza ilikiinua Kilimo partly katika kuelimisha zaidi. Hata mishahara ilikuwa mikubwa - Graduate alikuwa anapata mshahara sawa na Diploma holder kutoka Bukalasa Uganda na Egerton College kenya ambayo sasa ni University. SUA ilikuwa ukiwa Tutorial Assistant ni lazima usome (scholarships zilikuwa kebekebe). scholaships kibao wizara ya Kilimo ilikuwa inapata toka kwa wafadhili mbalimbali.

Likewise, SUA wana some monopoly power kutokana na kuwa the sole agricultural university in TZ! Hivyo basi, msomi yeyote wa kilimo na forestry anaye-opt kuwa lecturer atakuwa hana option(otherwise, ata-enjoy limited option) zaidi ya kwenda SUA! Hii nayo ina-play kama comparative advantage kwa SUA kuweza kuhodhi idadi kubwa ya wasomi wa aina yake tofauti na wasomi wa fani zingine!

Kweli kabisa

Kwanini Mzumbe ni maarufu mno kuliko SUA?! Jibu lake ni jepesi mno! Program za asili pale Mzumbe ni za wapiga domo(Wanasiasa)! Wengi wao ni wale waliosomea masomo ya arts ambao kwa asili ni wapiga domo! Na ndio maana hadi leo hii endapo watu tutaulizwa ni wasomi gani wanatoka UDSM, basi wengi wetu tutawataja wale wanaotoka departments za History, Political Science na Law kwavile ndio pekee wanaopenda kuuza sura kwenye TV na vyombo vingine vya habari! Ni nani anaweza kututajia wasomi toka Faculty of Engineering ya UDSM? Kuna ma-PhD holders kibao lakini hawafahamiki! Ni nani anaweza kututajia wasomi wa Muhimbili University? Ni nani anaweza kututajia wasomi wa Ardhi University? Ni wa-TZ wangapi wanafahamu juu ya kuwepo kwa Muhimbili na Ardhi ya University? Nature ya taaluma zao si za kupiga domo! Leo hii Ikulu ikilipuliwa, Profesa Baregu au Profesa Xavery watakaa chonjo kusubiria mwaliko wa vyombo vya habari ili wahojiwe na wao kutoa maoni yao jambo ambalo halitatokea kwa ma-profesa wa ama SUA, Ardhi au Muhimbili!

Sikubaliani na hili. Hawa unaowaita "domo kaya" wanajitokeza kusaidia kutukwamua kwenye sticky points katika kulifanya Taifa liende.
Nachelea kusema kuna wataalamu/wasomi wengi SUA lakini wana-SHY OUT kujitokeza hadharani kulisaidia Taifa katika kufuta njia za kulikwamua taifa hili katika masuala mbalimbali ya kijamii, uchumi na kilimo(mazao na mifugo) ambayo taifa linakabiliwa nalo - badala yake wanaachia wanasiasa wanatoa majibu yenye utata - sio kosa lao bali hawa wataalamu wetu wana soni au HAWAJIAMINI kutoa utatuzi wao kwa masuala ya kitaifa.

Farady alipogundua nishati ya umeme alimwalika waziri mkuu wa enzi hizo uingereza kwenye maonesho. waziri mkuu akamwambia na hii ni nini na ina faida gani kama sio kupoteezana wakati. Farady kwa unyenyekevu akamwambia waziri mku kuwa faida yake utakuja iona UTAKAVYOKUJA KUSANYA KODI NA NCHI KUJIPATIA MAPATO kwa uchache. Wataalam wetu wafanye hivyo wasiogope watakuwa labeled kuwa ni DOMO KAYA.
 
Halafu mnavokuwa mnalinganisha hivyo vyuo vyenu hebu kiweke UDSM pembeni kwa Tanzania na Afrika mashariki nzima hakuna kinachokifikia kwa ubora... kwa maana kwa utafiti wa mwaka 2013 kilikuwa chuo cha 4 Afrika kikizidiwa na vyuo vitatu vya south Africa tu..... Endeleeni na mjadala wako wa Mzumbe na Sua ukipenda ongeza Udom.....tena afadhali ungesema Kairuki ambacho afadhali kipo kwenye top twenty za Africa...
 
Back
Top Bottom