Unakumbuka vizuri ziara ya JK mkoani Mbeya wakati wa uchaguzi?...unakumbuka kuwa aliwasisitiza wananchi kumchagua Mwandosya na kuwa anamhitaji sana mtu huyu.
Hakusema Mwandosya bali alisema prof.alikuwa ana maana huyo mwana mtandao waziri wa afya sijuhi anaitwa nani?
Msauzi,
Nafikiri una maana Prof. Mwakyusa. Huyu ndiye miaka yote ana matatizo makubwa kule kwake, mwaka 2000 ilibidi prof. Mwandosya ahamie kwenye jimbo lake kumsaidia. Hata mwaka 2005 bado alikuwa na matatizo mengi.
Prof. Mwandosya alipita bila kupingwa chaguzi zote mbili yaani 2000 na 2005.
Prof. Mwakyusa ni mwanamtandao na watu walikuja kujua ikiwa too late vinginevyo kwenye mchujo wa CCM huenda asingelipita. Pia inaelekea atakuwa na kibarua kigumu sana mwaka 2010 kule jimboni kwake.