Kina mama wengine ni big soo

Bujibuji Simba Nyamaume

JF-Expert Member
Feb 4, 2009
74,739
155,436
Yanki katoka kwao kijijini kaja Dar katika hangaika yake akapata nafasi Bongo Movie, akapewa kipande ambacho aliekt kagongwa na gari akafa. Filamu ikasambazwa ikafika kijijini kwao mama yake kuona alilia sana akijua mwanae kisha kufa. Baada ya miezi miwili jamaa alipata nafasi ya kurudi kumsalimia mama yake, kwanza watu wote kijijini walimkimbia hata mama yake aliulaza, baada ya kuwabembeleza na kujieleza wakatulia, akampa mama yake laki mbili na nusu alizomwambia alipata kutokana na kugongwa na gari. Siku anaondoka mama yake akaona ampe baraka mwanae, 'Mwanangu ulipogongwa na kagari kadogo ulipata laki mbili na nusu, Mungu akusaidie ugongwe na basi safari ijayo urudi na milioni 2'
 
Back
Top Bottom