Kina Dada sometimez tunajitakia matatizo hii mnaionaje ?

Huna wivu???!!!!!!!!!! I dont think so. Kinachotokea nadhani uliumizwa sana kiasi una wasiwasi mkubwa sana unaokufanya ushindwe kuji-commit kwa mtu yeyote kwa 100%. Otherwise mummy kama umependa wivu ni kwa kwenda mbele.


Kumbe !
 
FL! darling huyo ni kipenzi cha moyo wangu mwenye kuuponya hayo majeraha uyaonayo. Ameniinua pale nilipoanguka, na kunibembeleza pale nilipolia, anayajua machungu yangu, na kuyapunguza makali..... loh

Hongera Mbu kwa kuuokoa huu moyo wa MJ1 uliokuwa umevunjwa na watu wasiojua thamani ya kupendwa na kupenda sasa nimeelewa :A S-rose:
 
shida hiyo ilimpata dada mmoja,aliamua kubeba mimba ya kijana ili apate uhakika wa kuwa ni wake pekee,cha kushangaza,kuolewa hajaolewa mpaka leo,na kijana anamega na wasichana wengine,tena anasema live kuwa hawezi kumwoa,cha kusikitisha ni kwamba,kijana na wazazi wake wanadai mtoto anaweza kuwa sio wake...mimi huo upuuzi sioutaki kabisa,kidogo nishawishike kipindi fulani nikaona ujinga...bora kubaki single kuliko kulazimisha ndoa!!!!!!
 
nampa pole sana huyu binti, anahitaji ushauri nasihi kuhusu maisha kwa jumla kwa sababu uzoefu unaonyesha mabinti wengi katika umri wa kati ya miaka 20 na 26 wanakuwa na shauku ya kuolewa na kwa bahati mbaya, naweza kusema hivyo, umri huo umemkuta akiwa katika maisha ya dhambi. nikimaanisha kutenda tendo ambalo kwa imani yoyote ya kidini na kimila linaruhusiwa kutendwa mtu akiwa ndani ya ndoa.

bila shaka ndiyo maana amejikuta akivuna majuto ambayo wakati mwingine -kwa mujibu wa maelezo ya huyu mshirika wake- yanamshawishi kujiua. ikumbukwe kuwa mshahara wa dhambi ni mauti. hili si la kudhihaki wala kufanyia mzaha, binti huyu anahitaji msaada wa dhati kiushauri kwa faida yake na mtoto wake zaidi na pengine kwa faida ya Taifa kwa sababu hakuna anayefahamu akivuka kizingiti hicho kinachomkabili anaweza kuibukia wapi na anaweza kufanya nini kwa ajili yake na taifa kwa jumla.

Ni kweli alilotenda ni kosa lakini hata na wewe kaka usidhani upo salama katika hilo. umeshiriki naye dhambi hivyo siamini kuwa adhabu ya dhambi hiyo ataibeba peke yake. kwa vyovyote nawe unayo sehemu ya adhabu ya dhambi hiyo hivyo- mwenzako akinyolewa...,

Ushauri wangu kwako, hulazimishwi kumuoa lakini tafakari aina ya familia unayotaka kuleta kwenye uso wa dunia. Unataka iwe na watoto wenye rangi ya blue,njano, nyekundu na nyeupe? kama ndivyo, endelea na safari kidume

Hujanishawishi kwamba hakukushirikisha hadi mimba ikiwa na miezi 7 kwa sababu kama mlikuwa wapenzi, mkishirikiana mpaka mkatiana ujauzito, sidhani kuwa ni rahisi kutobaini mabadiliko ya maziwa, tumbo kukuwa au hata hali ya kiafya ya mpenzi wako. kama ni kweli alikuficha hilo ni kosa lakini sidhani kama lina uwezo wa kuyeyusha penzi la mtu kwa mpenziwe kama kweli ulikuwa unampenda, huwezi kusema hilo limekuondoa katika nia hiyo na kama hukuwa na mpango huo, alipokuketisha kitako kukueleza mpango wake kwako hukutakiwa kumlaghai kwa lugha ya wakati ukiwadia tutayapanga ungemueleza tu kwamba huna mpango wa kuoa kwa wakati huo.

Ushauri wangu kwa binti huyo atafute wataalamu wa ustawi wa jamii-ikibidi aende chuo cha ustawi wa jamii pale Kinjitonyama, kama yupo Dar, akaombe kupatiwa huduma ya ushauri nasihi, wapo wakufunzi wa chuo wa kike kwa kiume ambao wanafaa sana katika masuala kama hayo.

naamini kwa kiwango alichonacho kielimu, akipatiwa ushauri mzuri kuhusu hali hiyo anayokabiliana nayo, atavuka salama, ikiwa kijana huyu hataki kumuoa wala hatamkumbuka maishani mwake zaidi ya kumwona kama binadamu mwingine ambaye hakuwahi kuwa na uhusiano naye. zaidi ya yote ataendelea ama na masomo yake au nashughuli yake kama ambavyo wanawake wengi wanaendeleza maisha wakiwa peke yao.

Hakuna haja ya kujutia matendo yaliyokwisha tendwa wakati uwezo wa kujirejesha katika nafasi ambayo itakufanya uonekane kama hukuwahi kuyatenda haupo. Kikubwa ni kutambua kuwa kweli alikosea kuamini mwanadamu, kujipanga upywa na kuendelea na maisha yake kwa sababu kuolewa ni majaaliwa ya Mungu ambaye ndiye aliyeumba mwanamke kwa ubavu wa mwanaume. Hivyo suala la kuolewa binti huyo anatakiwa kumwachia Mungu, na kwake hakuna kuwahi wala kuchelewa. Atulie, alee mtoto wake kama mume atakuja wakati ambao wala hakutarajia maana matendo ya Mungu ni makuu na yasiyotabirika.

Na wewe mvulana kama hutamuoa mwanamke huyo muache, jitenge naye kwa namna yoyote ile ili apate muda wa kubaki peke yake na kukubali hali hiyo. biashara ya mara unataka kumwona mtoto, mara unataka kupeleka matunzo ya mtoto, bila shaka inamfanya ahisi kuwa unaweza kuingia kwenye mstari kama anao uwezo wa kulea mtoto peke yake, mwache afanye hivyo maana kama kweli unampenda mtoto kiasi kwamba huwezi kuishi mbali naye ungempenda zaidi mama yake.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom