Kina Dada ni ya kweli haya....?

Mtoboasiri

JF-Expert Member
Aug 6, 2009
5,101
1,946
Kuna maada ilipatwa kuzungumzwa na kituo cha radio mahali. Wanawake walio kwenye ndoa walikuwa wanajieleza jinsi wanavyopanga kuwaacha waume zao - mara jambo fulani wanalolitegemea likikamilika. Mmoja alikuwa anasubiri mtoto wao wa mwisho aingie sekondari, mwingine alikuwa anasubiri amalize masomo aliyokuwa analipiwa na mumewe, n.k, n.k.

Kina dada, yaani unaweza kuingia kwenye ndoa ukiwa umepanga kabla na mapema kuwa baada ya hatua fulani kimaisha ikifikia unamuacha jamaa solemba??
 
Inawezekana...sawa na wanaoolewa kwa pesa tu!Kama kuna uwezakano wa kugawana mali mtu wa aina hiyo anakumwaga tu.Jua kwamba sio kila mtu anaingia kwenye ndoa kwasababu anaitaka hiyo ndoa!
 
Kuna maada ilipatwa kuzungumzwa na kituo cha radio mahali. Wanawake walio kwenye ndoa walikuwa wanajieleza jinsi wanavyopanga kuwaacha waume zao - mara jambo fulani wanalolitegemea likikamilika. Mmoja alikuwa anasubiri mtoto wao wa mwisho aingie sekondari, mwingine alikuwa anasubiri amalize masomo aliyokuwa analipiwa na mumewe, n.k, n.k.

Kina dada, yaani unaweza kuingia kwenye ndoa ukiwa umepanga kabla na mapema kuwa baada ya hatua fulani kimaisha ikifikia unamuacha jamaa solemba??

Hii ni kweli wengine wanajiwekea mikakati mapema akijienga nyumba kijijini kwao, akijenga nyumba mjini, akiwa na account yenye zaidi 10m anaanza vitimbi ili aachike aanze maisha mapya hii ipo sana na nimeshuhudia
 
Mtu mpaka anaamua hapo bold anakuwa amechoshwa na vituko vya mume ambavyo havibadilishiki, mfano umalaya uliopitiliza, nyumbani haonekani, matumizi anatoa kwa shida n.k so mmama anaona nikiwaacha wanangu wadogo watateseka ila huyu mdogo akimaliza tu sekondali najiepusha nikapumzishe akili.

Lazima kuna sababu mtu na akili zako huwezi amua uolewe kwa malengo then baada ya muda utoke, hata kama wapo ni wachache sana. Wengi huwa wanakimbia matatizo yaliyoshindikana.
 
Hii ni kweli wengine wanajiwekea mikakati mapema akijienga nyumba kijijini kwao, akijenga nyumba mjini, akiwa na account yenye zaidi 10m anaanza vitimbi ili aachike aanze maisha mapya hii ipo sana na nimeshuhudia

Hao walikuwa wanaume wa zamani, mwanaume gani wa sasa atakuachia hela yake mpaka ufanikishe kujenga nyumba kijijini kwenu au kuwa na account yenye hata 5m. Labda uwe umemuwekea (nchekea mbingu)
 
Yalikuwa yakitokea sana kwa ndugu zetu fulani wa kanda ya kaskazini,hata kuua.Kwa hivi sasa sina uhakika.
 
Hii ni kweli wengine wanajiwekea mikakati mapema akijienga nyumba kijijini kwao, akijenga nyumba mjini, akiwa na account yenye zaidi 10m anaanza vitimbi ili aachike aanze maisha mapya hii ipo sana na nimeshuhudia
Fidel wale wadada wa mjini wanajulikana sana kwanza nilisikia eti wanataka kuanzisha kikundi sijui kitu gani crap crap tupu kwenda mbele
 
Bora umesema maana usipotafuta ya kwako kwa bidii utalia maumivu kila siku

Hao walikuwa wanaume wa zamani, mwanaume gani wa sasa atakuachia hela yake mpaka ufanikishe kujenga nyumba kijijini kwenu au kuwa na account yenye hata 5. Labda uwe umemuwekea (nchekea mbingu)
 
Hao walikuwa wanaume wa zamani, mwanaume gani wa sasa atakuachia hela yake mpaka ufanikishe kujenga nyumba kijijini kwenu au kuwa na account yenye hata 5m. Labda uwe umemuwekea (nchekea mbingu)

Hela za mboga mnaweka kwenye kibubu
 
ndoa ni zaidi ya tuijuavyo,wanaozijua hawapendi kuzungumzia sana,ila ndoa za sasa ni utata,hata mimi dada angu kaachika,ila hua anafurai na husema amesha SAFISHA NYOTA.
 
Hii ni kweli mwanamke akishakuwa na kauwezo kidogo tu! Mara nyingi hizi huwa ndo fikra zao. Wanawake ambao bado hawajaingia kwnye ndoa hulipinga hili lakini. Kwa research niliyofanya hili swala lipo.....kitu kinacho tusaidia sisi wanaume tusiachike kama wanavyopanga ni watoto.
 
Hao wanawake ni lazima wanateseka katika ndoa zao na inabidi tu kuwa watimize malengo maisha yao yaendelee kuliko kufa na high bp etc

Hakuna anayeolewa na kupanga kumuacha mwanaume unless wamelazimishwa ndoa au walifata pesa na mengine ya kipuuzi ila wengi wakiingia ndoani ni kukuta mapenzi yanakufa ile raha ya lavi davi inaondokaga na ndio hapo sasa

Yote ni Mungu
 
Yote ni kuomba Mungu
 
Back
Top Bottom