Kimenuka border ya Kasumbaresa.

Kiby

JF-Expert Member
Nov 16, 2009
6,897
4,620
Kukosekana kwa utawala wa sheria kunaligharimu sana bara la Africa. Border ya Kasumbaresa kwa sasa imefungwa kwa sababu ya raia wa Kongo kumchoma moto pamoja na track lake dereva mmoja wa Zambia. Dereva huyo akiendesha gari upande wa kungo alikutana na umati uliokuwa ukitoka kuzika na kuuparamia na kusababisha kifo cha watu watatu. Jambo lililopelekea wanakijiji hicho kulichoma moto gari na dereva akiwa amejifungia ndani. Sasa hivi kinachoendelea ni wakongo wamesimama upande wa kwao wakiwa wameshikilia mawe baada ya kupigwa marufuku kuingia upande wa zambia ambako kimsingi ndiko kuliko na biashara yao inayowapatia mlo wa kila siku. Msururu wa matraki pande zote unakaribia kilometa tano kwa urefu.
My take: Huku kukosekana kwa utawala wa kisheria katika nchi zetu za Africa hatuoni kunatugharimu sana kwa kuzuia maendeleo yetu kama siyo kuyarudisha nyuma?
.
 
Poleni, wanadiplomasia waingilie kati, ni suala linalozungumzika!
 
kwa mujibu wa gazeti moja nchini zambia inasemekana kuwa hilo track la zambia kilikua limebeba cement likipeleka cement congo umbali kilometer 20 hivi kukatokea gari aina center na kumuamrisha driver ageuze gari kwa madai ya kupisha msafara wa mazishi bila kubisha driver akageuza gari hapo hapo topic ikabadrika na kumuamuru drive atelemke na kumshambulia na kisha kumchoma moto.....
 
Ahsnate kwa taarifa, poleni kwa usumbufu mnaopata mliopo katika maeneo hayo!
 
Bila shaka yalikuwa mazishi ya mwana uamusho. Maana hao wenzetu kila kukicha wanatekenywa kumwaga damu tu.
 
Bila shaka yalikuwa mazishi ya mwana uamusho. Maana hao wenzetu kila kukicha wanatekenywa kumwaga damu tu.

.
Sio wana uamsho mzee, wakongo wote ni watata. Halafu adhabu yao wanakula kwa macho leo maana soko lao lililo upande wa Zambian wanaliona kwa macho ila hawaruhusiwi kutia mguu.
.
 
Back
Top Bottom