Kimbunga cha Ole Millya chazidi kuifagia CCM-gazet la mwananchi

Baba Jotham

Member
Mar 6, 2012
84
40
wimbi la kujiunga na Chadema mkoani Arusha limezidi kuongezeka baada ya wenyeviti watano wa vitongoji na wanachama 2,402 wilayani Ngorongoro kukihama chama hicho jana.
Mbali na viongozi hao, pia Mwenyekiti wa UVCCM Wilaya ya Monduli, Julius Kalanga na Diwani wa Kata ya Nyampulukano wilayani Sengerema, mkoani Mwanza Hamis Mwagoa, jana walitangaza kuhamia Chadema.
Hata hivyo, Mwenyekiti huyo wa UVCCM alisema atachukua rasmi kadi ya Chadema kesho akiwa na wenzake kadhaa ambao hakutaka kuwataja.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti jana, makada hao wapya wa Chademawalisema wameamua kuihama CCM kwa kile walichosema wamechoshwa na chama hicho na Serikali yake kushindwa kushughulikia matatizo ya wananchi ikiwamo kupanda kwa gharama za maisha.
Habari zilizopatikana kutoka Ngorongoro na baadaye kuthibitishwa na Katibu wa Chadema Mkoa wa Arusha, Amani Golugwa, zimeeleza kuwa viongozi na
wanachama hao walirudisha kadi za CCM na kupokelewa na uongozi wa chama hicho wilayani humo jana.
Golugwa aliwataja viongozi wa vitongoji waliorudisha kadi za CCM na kujiunga na Chadema kuwa ni
Saitabau Tereto aliyekuwa Mwenyekitiwa Kitongoji cha Enduleni katika Kijiji cha Esluway ambaye aliongoza wanachama wengine 478 wa CCM kuhamia Chadema.
Wengine ni Mwenyekiti wa Kitongoji cha Ngiani, Kone Tema aliyejiunga akiwa na wananchi wake 590, wakati Mwenyekiti wa Kitongoji cha Ngoyapase, Marko Mbeme alirejesha kadi ya CCM na kujiunga Chadema
akiongozana na wananchi wengine 590.
Golugwa aliyeeleza kuwa wimbi la wana CCM kuhamia Chadema linatarajiwa kuendelea leo, alimtaja Mwenyekiti wa Kitongoji cha Embaruale, Saluni Meng¡¯alana aliyeongozana na watu 224 huku mwenzake wa kitongoji cha madukani,Robert Edward akiongoza wananchi 520 kujiunga na Chadema.
Alisema katika maelezo yao mafupi waliyotoa kabla na baada ya kurejeshakadi za
 
Back
Top Bottom