Kimbunga cha M4C chaitikisa CCM Morogoro

Scolari Ndenga

JF-Expert Member
Aug 4, 2008
271
43
Operesheni Sangara ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA inayoendelea mkoani Morogoro imeendelea kuwa mwiba mchungu kwa CCM na serikali baada ya viongozi wa serikali za vijiji mbalimbali kuamua kujiuzulu nyadhifa zao na kujiunga na CHADEMA. Walioamua kujiuzulu nayadhifa zoa ni pamoja na aliyekua katibu mwenezi wa CCM kata ya Muhonda Mzee Ngoya, Mwenyekiti wa serikali ya kitongoji cha Kododo kata ya Luwale bwana Charles Kiwaga, Mwenyekiti wa serikali ya Mlali Lucas Membe na Alexander John wa kijiji cha Ng'ungulu. Katibu mwenezi wa kata ya Luwale na Mwenyekiti wa Kitongoji kupitia CCM walijiuzulu nyadhifa zao mbele ya Katibu Mkuu wa BAVICHA, Deogratias Munishi na kukabidhiwa kadi za CHADEMA kama inavyoonekana hapa H@ki Ngowi: Operesheni Sangara Ya Chadema ndani ya Mvomero-Morogoro Yazidi Kupasua Vijiji! Wakati CHADEMA ikiendelea kuchanja mbuga ya kuhamasisha wananchi kijiji kwa kijiji na ikitarajia kufunga operesheni yake kwa maandamano makubwa na ya kihistoria mjini Morogoro tarehe 27/08/2012, kwa upande wake Chama Cha Mapinduzi kinahaha kuhakikisha mikutano ya mjini Morogoro ukiwamo na ule wa kufunga haufanikiwi. Wiki iliyopita, katibu wa itikadi na uenezi wa chama hicho Nape Nnauye kwa kile kilichoitwa kuwafuturisha mabalozi wa CCM wa mjini Morogoro, aliagiza mabalozi hao kufanya juu chini ili CHADEMA wapate aibu ya mwaka ikiwamo kuandaa vijana wa CCM watakaovaa Kombati za CHADEMA wafanye vurugu katika mikutano hiyo. Katika kuweka msisitizo wa mbinu chafu hizo, tarehe 21/08/2012, mweka hazina wa CCM ambaye anadaiwa na CHADEMA kukodisha vijana wahuni kutoka manzese Dar es Salaam walifanya vurugu katika mikutano ya chama hicho mkoani Singida mwezi wa saba mwaka huu, Mwigulu Nchemba alikua mkoani Morogoro kusuka mipango hiyo ya kuihujumu CHADEMA jambo linaloonekana kushindwa mpaka sasa hivi.
 
Ukiona chama kinategemea Mwigulu na Nape kama strategist wake ujue chama hicho kinaelekea kaburini. Maskini CCM ndo inatutoka polepole sababu ya UDHAIFU wa uongozi
 
Ukijaribu kuzuia kimbuka kwa beseni mwisho wake ni aibu...! nyinyiem watekeleze ahadi zao ndipo wananchi watawaelewa mwisho wa ubaya nia aibu
 
Wanafunzi 652 mwalimu 1???????? Hayo ndio mafanikio ya rerikali ya CCM kwa miaka 51 ya Uhuru? Kweli nimeamini CDM ni kimbunga. CCM kaeni chonjo mtazolewa mpotezwe msijulikane mtakapotupwa. Asante kamanda Munishi kwa ukaguzi wako. Chapeni kazi daima.
 
Sasa nauona mwisho wa magamba! Kwa staili hii ya kijiji kwa kijiji ya CDM ni bora CCM wajiandae kuwa wapinzani na waanze kupaki. Inapendeza sana kuona moto wa BAVICHA ikiwawakia magamba kiasi hiki. Hongerea kamanda MUNISHI
 
Operesheni Sangara ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA inayoendelea mkoani Morogoro imeendelea kuwa mwiba mchungu kwa CCM na serikali baada ya viongozi wa serikali za vijiji mbalimbali kuamua kujiuzulu nyadhifa zao na kujiunga na CHADEMA. Walioamua kujiuzulu nayadhifa zoa ni pamoja na aliyekua katibu mwenezi wa CCM kata ya Muhonda Mzee Ngoya, Mwenyekiti wa serikali ya kitongoji cha Kododo kata ya Luwale bwana Charles Kiwaga, Mwenyekiti wa serikali ya Mlali Lucas Membe na Alexander John wa kijiji cha Ng'ungulu. Katibu mwenezi wa kata ya Luwale na Mwenyekiti wa Kitongoji kupitia CCM walijiuzulu nyadhifa zao mbele ya Katibu Mkuu wa BAVICHA, Deogratias Munishi na kukabidhiwa kadi za CHADEMA kama inavyoonekana hapa H@ki Ngowi: Operesheni Sangara Ya Chadema ndani ya Mvomero-Morogoro Yazidi Kupasua Vijiji! Wakati CHADEMA ikiendelea kuchanja mbuga ya kuhamasisha wananchi kijiji kwa kijiji na ikitarajia kufunga operesheni yake kwa maandamano makubwa na ya kihistoria mjini Morogoro tarehe 27/08/2012, kwa upande wake Chama Cha Mapinduzi kinahaha kuhakikisha mikutano ya mjini Morogoro ukiwamo na ule wa kufunga haufanikiwi. Wiki iliyopita, katibu wa itikadi na uenezi wa chama hicho Nape Nnauye kwa kile kilichoitwa kuwafuturisha mabalozi wa CCM wa mjini Morogoro, aliagiza mabalozi hao kufanya juu chini ili CHADEMA wapate aibu ya mwaka ikiwamo kuandaa vijana wa CCM watakaovaa Kombati za CHADEMA wafanye vurugu katika mikutano hiyo. Katika kuweka msisitizo wa mbinu chafu hizo, tarehe 21/08/2012, mweka hazina wa CCM ambaye anadaiwa na CHADEMA kukodisha vijana wahuni kutoka manzese Dar es Salaam walifanya vurugu katika mikutano ya chama hicho mkoani Singida mwezi wa saba mwaka huu, Mwigulu Nchemba alikua mkoani Morogoro kusuka mipango hiyo ya kuihujumu CHADEMA jambo linaloonekana kushindwa mpaka sasa hivi.

Mfa maji kweli haachi kutapatapa, hizi thread za kila siku Kimbunga, kimbunga, kimbuga mbona ni kama za kutapatapa 2. Tulishasikia basi, tusubirini matendo 2015 ndiyo tujue ukweli.
 
Hao danganya toto nani asiyewajua CDM kwa uongo ss hv hata mtoto hamumdanganyi
 
Nape c alikua anapita akifuta nyayo za CDM pamoja na wale mawaziri sasa wamekuja kwa mbele maana nyayo zimegoma kufutika huko mbele atajikuta akiwa amepigwa gwanda
 
Mbona ticha 1/wanafunzi 652 ni sawa tu akifanya power deligation!? Hapo awape wanafunzi mamlaka, ndio mpango mzima mpaka kuwafundisha wengine. CCM imedondokea kwenye shimo refu sana, haitatolewa hata kwa winchi. Na sijui itatolewaje maana mkia ndio umebaki juu ,tukiushika unaweza katika. Kama mnavyojua mnyama akidondokea shimoni mkia ukibaki juu anavyouangaisha. Utauona huku na kule ukitafuta maisha japo kodooogo! Mkia wa ccm ni kina nape, mwigulu na kina kilango. wanahangaika lakini hamna ujanja maana mnyama akifa lazima mkia wake nao ufe pamoja na kuweweseka kote.
 
Ile mikutano ya CCM vipi imeishia wapi?
Inaendelea kupitia operation za kuwavalisha bendera mbwa, kubwabwaja kutokea Lumumba, kuzindua matawi ughaibuni, kuendeleza propaganda kupitia media na mafunzo ya kimafia kwa makada.
Tatizo pekee ni matokeo hafifu ya operation hizi.
 
Mwigulu ni muuaji kuweni makini naye CDM!!

Asante Mungu kwa kuiwezesha M4C kusonga mbele, "JINA LAKO LIHIMIDIWE!!"

Hapo kwenye red nimefarijika sana, siku zote wana-CHADEMA tumtangulize Jehova, allah mbele tutafanikiwa. Mungu ni chanzo cha haki, hawezi acha watu wake tulioitwa kwa jina lake tuendelee kuteseka.
 
Mfa maji kweli haachi kutapatapa, hizi thread za kila siku Kimbunga, kimbunga, kimbuga mbona ni kama za kutapatapa 2. Tulishasikia basi, tusubirini matendo 2015 ndiyo tujue ukweli.

Mkuu thatha, uwaeleze wakuu wako kuwa CHADEMA Ikichukua nchi woote mtafilisiwa na kubakiziwa mtaji wa kupika na kuuza komoni ndipo wajue ugumu wa maisha tunaoulalamikia watanzania.
 
Mwigulu ni Failure....Muulize matokeo ya chaguzi za Igunga na Arumeru Mashariki
 
Back
Top Bottom