Kima cha chini cha mshahara: Tsh 135,000/=

Mponji hao walimu hasa ndio wanawapigisha kura hasa wale wazee wasiojua kusoma au wasiiona, sasa kazi ipo kwao. Na wao wengi wao ndio wanaolipwa hicho kima cha chini na wanishia ktk mikopo na kuuza ubuyu na yule mwalimu mwenzao ambae sasa hivi ana ving'ora amewasahau kabisa
 
135,000 ni kidogo mno ndo maana watumishi wanakula rushwa kupita kiasi! Kilekile cha 315,000/= angalau kinaweza kutusukuma! hebu fikiria unga wa ugali ni tshs 800/= kwa kilo, sukari ni 1600, mchele ni 1600/= je ukipewa 135,000 itakufikisha siku 30?

You know what! wameamua kuswap digits wakabadilisha 315 kuwa 135. Lets hope next time watachukua digit inayofuata tena ili itengeneze kima cha chini cha 531,000/=
 
Mponji hao walimu hasa ndio wanawapigisha kura hasa wale wazee wasiojua kusoma au wasiiona, sasa kazi ipo kwao. Na wao wengi wao ndio wanaolipwa hicho kima cha chini na wanishia ktk mikopo na kuuza ubuyu na yule mwalimu mwenzao ambae sasa hivi ana ving'ora amewasahau kabisa

Hapo umegonga penyewe mkuu.
Pamoja tunasema JK hajui mamlaka yake aliyonayo lakini nafikiri wafanyakazi nao hawajui mamla na nguvu waliyonayo. Hao walimu na wafanyakazi wengine hapo chini hata wakiiamuwa kumwibia kura jk inawezekena. Kule kwetu kuna kituo cha polisi makao makuu ya tarafa tu na polisi wenyewe ni wawili tu ktk hicho kituo.

Na hata hivyo kwani hao polisi hawadai hiyo kima ya chini? ama wao si wanachama wa TUCTA.? Mtamlaumu bure JK lakini tatizo la msingi hatulioni.
 
ndugu wana jamii kama jk alivyosema inatakiwa wafanyakazi wawe kama mbayuwayu,maadam kima cha chini ndio hicho basi hiyo ni akili ya kuambiwa na serikali,kwa hiyo wafanyakazi wakichanganya na akili zao wenyewe(rushwa),basi mwisho wa mwezi utapata zaidi ya laki tatu,ambazo tucta wamependekeza.kumbuka mkapa aliposifia kauli kuwa mtaji wa maskini ni nguvu zake mwenyewe,utekaji nyara na wizi uliongezeka huku waathirika wakivuliwa nguo na kulazimishwa kuimba wimbo huo wa mtaji wa maskini ni nguvu zake mwenyewe.



nimeipenda hii sana tu, na wale waliokuwa wanampigia makofi jk watakiona cha mtema kuni maana bila ccd(chakula cha daktari) sijawatibu, rushwa ndio ufumbufu wa kuziba gap.ngoja sasa.
 
ndugu wana jamii kama jk alivyosema inatakiwa wafanyakazi wawe kama mbayuwayu,maadam kima cha chini ndio hicho basi hiyo ni akili ya kuambiwa na serikali,kwa hiyo wafanyakazi wakichanganya na akili zao wenyewe(rushwa),basi mwisho wa mwezi utapata zaidi ya laki tatu,ambazo tucta wamependekeza.kumbuka mkapa aliposifia kauli kuwa mtaji wa maskini ni nguvu zake mwenyewe,utekaji nyara na wizi uliongezeka huku waathirika wakivuliwa nguo na kulazimishwa kuimba wimbo huo wa mtaji wa maskini ni nguvu zake mwenyewe.


nimeipenda hii, rushwa ndio ufumbuzi wa kuziba gap la kutoka ths 135,000 mpaka 315,000.bila c.c.d hakuna huduma hospital.mambayuwayu rushwa oyeeeee.
 
Inasikitisha kuona kuwa serikali haiwezi kuongeza kima cha chini kufikia walau 200,000/-Kwa kiasi hiki(135,000/-) ni vipi maisha ya mfanyakazi ambaye ni mtanzania yanaweza kuwa bora? KUNA HAJA GANI YA KUSEMA MAISHA BORA KWA KILA MTANZANIA WAKATI UWEZO HATUNA. HUKO SIO KUJIPENDEKEZA TU?
 
315,000 and 135,000? Inaelekea wamecheza na namba tu!

On a serius note, kwa ninavyojua mimi kilichabadilishwa sio kima cha chini cha mishahara bali ni kiwango cha mapato kisichozozwa kodi (kwenye PAYE) kimeongezwa kutoka 100,000 kwenda 135,000.
 
Nilishawaabia JK ANADHARAU. Alituambia, HABEMBELEZI KURA ZA WATANZANIA, chagueni kusuka au kunyoa.
 
Hebu tuangalie kima chini hicho kama kinatosha kwa mfanyakazi mwenye familia ya mtoto mmoja kwa matumizi ya kujibana huyu mtoto awe anasoma

1. Unga wa mahindi 1.5kg@ 800/= kwa mlo wa mchana na usiku kwa 30 days 36000/=
2. Mkaa kipimo 2@600/= kwa siku 30 36000/=
3.Maharage nusu kilo 400/= kwa siku 30 12000/=
4. nyanya fungu 1 @ 200/= siku 30 6000/=
5. nauli kwenda kazini na kurudi 1000/= siku 30 hapa mchana huli 30000/=
6. vitunguu 100/= kwa siku 30 days 3000/=
7.mtoto nauli ya shule na kula mchana 500/=siku 30 15000/=
8.Kodi ya chumba kwa mwezi 20000/=
9.umeme kwa mwezi minimum 5000/=
10.Maji assume yawe yanatoka bombani na si kununua 2000/=
11.sabuni kipande mbuni 100@ siku 30 3000/=
12. mavazi kwa mwezi kwa kujibana 10000/=
13.Dharura 30000/=

Jumla 208000/=

Yaani hapa huyu mtu kajibana wala hawezi kula nyama atatumia 208000 kwa mwezi wakati kima cha chini ni 135000/= kuna tofauti ya 73000/= hivi hili hatulioni kweli maana nashangaa watu wanavyoandamana kwenye chama twawala kuwasindikiza wabunge kuchukua fomu kwakweli tunahitaji mabadiliko ya kifikira. Na kwakuwa hahitaji kura zetu hivi huyu atatusikiliza kweli tukimua mbia hata tukijibana bado tunahitaji kuongezewa walau 73000/=?

Ewe mfanyakazi tumia kura yako kuchagua kiongozi atakaye tusikiliza na sio mbayuwayu

Jamani kwanini tusibadili upepo kwa kuwaelimisha ndugu zetu kule vijijini na mijini kuwa hatuwezi kuwatumie hela za kuwasidia kwasababu ya serikali iliyopo madarakani hivyo tuwaelimishe waweze kuchagua chama kingine?

kama kila mfanya kazi ana ndugu 10 hii itawezesha kubadili system na kumfanya ajutie kauli yake


 
Hulipwi ili utimize mahitaji yako,unalipwa kulingana na makubaliano yako na mwajiri na kulingana na uwezo wako kuanzia kielimu mpaka kiutendaji. Kama mtu anaona mshahara wa kima cha chini cha 135,000 kidogo basi aangalie utaratibu mwingine.

Mahitaji ya mtu hayaishi,muhimu serikali iangalie kiwango cha mishahara inayolipwa na nchi nyingine zinalolingana na zetu kwa elimu kama za waajiriwa wake. Kwani kama matumizi ya mtu kwa mwezi ni Tshs 10,000, mtu alipwe kiasi hicho hicho ili kutimiza mahitaji yake? Mtu alipwe kutokana na utendaji na elimu yake.

Hawa ndiyo waleta matatizo katika nchi hii. Hivi unaweza kuniambia nikiwa mlinzi pale wizarani na nikafanya kazi zangu kwa bidii hakuna wizi unatokea mtaniandisha hadi nipate mshahara wa juu zaidi ya 135,000 x ....... = ..............? Nitafanyaje kazi vizuri ukapata tija unayohitaji wakati sijui leo na kesho sijui nitakula nini zaidi ya kufanya mpango wa kuhamisha tyre la shangingi niliuze 5000 nigange njaa. Acheni hizo wakumbukeni na wenzeni.

Hivi basic needs za binadamu mmezisahau, Chakula na pakulala tu inazidi hiyo kima cha chini wewe unatuambia elimu. Atamsomeshaje mtoto wake huyu kwa ada zenu za hovyo, atamudu kuchangia chuo kikuu huyu au na mtoto wake tunataka awe hivyo hivyo kima cha chini. Serikali imerogwa hii
 
Back
Top Bottom