Kilio cha msaada wa dhati, nateseka

Ahsante mdau kwa mawazo na mchango wako wa kina.
@mazikukulwa,

tayarisha cv yako vizuri na wasiliana na 'recruitment agencies' kama radar. Kuomba mungu peke yake haitoshi maana kumbuka ni mungu huyu huyu anaombwa asaidie watu wanakufa njaa somalia, kuokoa maisha ya kwenye nchi zenye vita n.k. Kwa hiyo hata kwa logic ya kawaida kwenye list ya maombi mungu ataanza na walio kwenye '11th hour'. So you have to be on your feet na psychologically inabidi 'uamue' narudia 'uamue' kwamba lazima upate kazi! Ukishaamua utajisikia kabisa kwamba unayo nguvu ya kupata kazi.

Website ya radar hii hapa; radar recruitment the leading recruitment agency in tanzania: Home

kingine: Hao wadogo zake wanaokutegemea pia nao waanze kutafuta kazi i.e supermakets. Haitoshi kukaa na kuhuzunika kila mmoja achacharike vinginevyo utajikuta siku zote una mzigo mzito.

Pole sana kaka, kwa Mungu hakuna lisilowezekana, omba kwa imani na kumaanisha na atajibu maombi yako soon. Ila si vema kama utatupa feedback kama fjm ameshakusaidia, pia jitahidi kusoma magazeti kuna nafasi mbalimbali za proffessional yako huwa zinatangazwa, ukiona omba bila kuchoka, a day will come utapa tu kazi

Pole sana mkuu, then try kutafuta hata shule ya private upige ufundishe angalau upate hela ya mboga.
Mimi nilisoma raman mapema japo 4m 6 nilipiga 1 nilianza kusomea ualimu nimekamata ajira then later naendelea na B.a human resource hapo hata huko mbele deal zikibuma narudi kukamata chaki maisha yanasonga.

Nakuombea kwa Mungu upate kazi.

Pole sana ndugu yangu, hayo ni mapito katika maisha. Amini na kuambia kila jaribu lina mlango wa kutokea... maana Bwana Mungu alie hai atakufanya njia (zaburi 34:7).
Napenda nikufariji kwa neno hili mtazame Mungu ndio suluhisho la mapito yako, Mwandishi wa Zaburi anasema,(Zab 121:1-2) Nitayainua macho nitazame milima, msaada wangu utatoka wapi......Hakika msaada wako utatoka kwa bwana Mungu wa majeshi aliye alpha na Omega..
Katika Mithali tunasoma, Mtumaini Bwana kwa moyo wako wote na wala usitegemee akili zako mwenyewe (Methali 3:4-6).
Hakika utamuona Bwana akikupa mpenyo katika maisha yako

Ninatamani tufanye maombi kwa ajili yako!

Pole sana Mpwa, mimi nakuomba pamoja na Kumuomba na kumtegemea sana MUNGU (jambo ambalo naliafiki na kuliamini 100%) jitahidi upate sehemu ya ku-volunteer, mimi binafsi nilisha volunteer sana sana lakini kotea huko kila waliponikubalia kufanya hivyo nilijikuta wananilipa kapesa kazuri tu na hatimae mwisho naondoka na cheti ambacho ni muhimu sana, sehemy ya mwisho ku-volunteer ilikuwa ni kwenye shirika fulani la kijamii (NGO) siku hio nilikua pale Open University nikipitia dissertation yangu ya Masters (kumbuka nimejisomesha masters mwenyewe bila mfadhili na bila kazi) nikiwa katika hali ya mwisho kabisa (pengine kama hali uliyonayo wewe leo) nikajipa moyo, nikafungua ka-laptop kangu, nikapitia anuani za mashirika kibao ya hapa Bongo, Care, Africare, Sight Savers, Save the Children n.k nikawatumia mail kwamba naomba japo kufanya Internship, huwezi amini japo ilikua siku ya jumamosi pale pale e-mail yangu ilijibiwa na moja ya shirika na baada ya kufuatilia kama wiki hivi, nilipata post hio kwa posho kubwa na nzuri

lengo la ushuhuda huu ni kukutia moyo kwamba in the last minute, unaposema nimechoka, siwezi tena, narudi nyuma sasa, inatosha; Hapo unatakiwa kuwaza vingenevyo kuwa Naweza, Ntaendelea mbele kidogo, mimi si wa kwanza, sikatishwi tamaa na ambo haya, namwamini MUNGU na hapo ndipo unapoona something different and unbelievable kinapotokea. Ni kweli kazi nyingi siku hizi zinatumia tumia principle ya TECHO-WHO na si TECHNO-HOW. LAKINI kama wakati wako umefika, no turning back, niamini No truning back. Kubwa tu, ondoa moyoni mwako visasi kwamba nikipata kazi na mshiko WATANIKOMA!!

Nimeandika kwa kirefu kwasababu I also went through it somedays, MUNGU akutangulie na akutie NGUVU ukauone wema wa MUNGU wako unaemtumikia, kumbuka wana Israel walipokaribia bahari, hakuna njia, hawana mtumbwi wala ngalawa, na nyuma jeshi la Farao linawafuata kwa ghadhabu kubwa, kilitokea nini? Be blessed. Mpwao Ellli

Pole sana mkuu. Kama wadau wengine walivyosema omba mungu kwa bidii, kwa uwezo wake atakuonyesha njia siku moja. Pia waweza jaribu kwa watu wa elimu, I mean waweza jaribu kwenda wizara ya elimu pale watakupa mwongozo wa namna ya kupata kazi ya ualimu kwa watu waliomaliza degree tofauti na ualimu, if you don't mind teaching. Kama upo mikoani waweza jaribu kuulizia kwa wakurugenzi au maafisa elimu kama sijakosea, watakupa muongozo wa nini cha kufanya japo ukapata pa kuanzia ili uweze kujipanga upya.

Mkuu pole sana na hongera sana kwa kujitahidi kujiajiri mwenyewe na ndio njia nzuri na sahihi na sababu haikufanikiwa mwanzo usife moyo...

Ushauri wangu in short term endelea kutafuta kazi na usisubiri tu kuona matangazo ya kazi bali waulize ndugu jamaa na marafiki sababu sio kazi zote huwa wanatoa matangazo bali nyingine huwa wanatoa tangazo internal pia....

Long Term
Sababu umeweza kupata hata hao wateja wawili inaonyesha unao ujuzi wa hii kazi (labda inatakiwa promotion zaidi na kujikita kwenye wateja tofauti tofauti, na sio individuals pekee, unaweza ukawa unafanya training kwenye kampuni tofauti....hata za serikali na ukila na maboss watakaokupa kazi basi utapata semina/kazi nyingi)

Kosa la kwanza ulilofanya ni kuanza kupata overheads kubwa (ofisi n.k.) kabla ya kuwa na uhakika wa wateja. Hii karne ya simu huitaji kurent ofisi yako peke yako ungeweza hata kushare kimeza tu au bango lako kwenye ofisi ya mtu na kazi zikija anakwambia na wewe unamlipa huyo pesa kidogo.

Kwahiyo mkuu ushauri wangu hata utakapopata hii kazi nyingine lakini unaweza kuendelea na hii business yako part time.., ongea tu na rafiki yako yoyote ili uweze kuweka Bango lako la biashara yako ili uonekane unayo ofisi lakini message utakuwa unapata kwa simu na kama mtu anataka kukuona unaweza ukawa unapanga appointment kukutana nao kwenye hii ofisi unayoshare na rafiki yako.

Please Keep Overheads to a Minimum... (hili ni kosa kubwa sana ambalo startup business nyingi wanafanya) kwenye hii biashara yako ungeweza ukaanza with a minimum na sio lazima kuwa na ofisi yako (omba kujishikiza sehemu au share rent na mtu ambae biashara zenu zina-compliment au ambazo hakuna ushindani)

jaribu lupelek CV ktk headquartes za mabeki yote hapa nchini TZ. One day unaweza kuitwa. Kwa kawaida mabenki huwa hawatangazi kazi. Jaribu kaka utafanikiwa.
Kila la kheri

Ahsante sana mdau wangu nimekupata sahihi kabisa...
Pole sana Mpwa, mimi nakuomba pamoja na Kumuomba na kumtegemea sana MUNGU (jambo ambalo naliafiki na kuliamini 100%) jitahidi upate sehemu ya ku-volunteer, mimi binafsi nilisha volunteer sana sana lakini kotea huko kila waliponikubalia kufanya hivyo nilijikuta wananilipa kapesa kazuri tu na hatimae mwisho naondoka na cheti ambacho ni muhimu sana, sehemy ya mwisho ku-volunteer ilikuwa ni kwenye shirika fulani la kijamii (NGO) siku hio nilikua pale Open University nikipitia dissertation yangu ya Masters (kumbuka nimejisomesha masters mwenyewe bila mfadhili na bila kazi) nikiwa katika hali ya mwisho kabisa (pengine kama hali uliyonayo wewe leo) nikajipa moyo, nikafungua ka-laptop kangu, nikapitia anuani za mashirika kibao ya hapa Bongo, Care, Africare, Sight Savers, Save the Children n.k nikawatumia mail kwamba naomba japo kufanya Internship, huwezi amini japo ilikua siku ya jumamosi pale pale e-mail yangu ilijibiwa na moja ya shirika na baada ya kufuatilia kama wiki hivi, nilipata post hio kwa posho kubwa na nzuri

lengo la ushuhuda huu ni kukutia moyo kwamba in the last minute, unaposema nimechoka, siwezi tena, narudi nyuma sasa, inatosha; Hapo unatakiwa kuwaza vingenevyo kuwa Naweza, Ntaendelea mbele kidogo, mimi si wa kwanza, sikatishwi tamaa na ambo haya, namwamini MUNGU na hapo ndipo unapoona something different and unbelievable kinapotokea. Ni kweli kazi nyingi siku hizi zinatumia tumia principle ya TECHO-WHO na si TECHNO-HOW. LAKINI kama wakati wako umefika, no turning back, niamini No truning back. Kubwa tu, ondoa moyoni mwako visasi kwamba nikipata kazi na mshiko WATANIKOMA!!

Nimeandika kwa kirefu kwasababu I also went through it somedays, MUNGU akutangulie na akutie NGUVU ukauone wema wa MUNGU wako unaemtumikia, kumbuka wana Israel walipokaribia bahari, hakuna njia, hawana mtumbwi wala ngalawa, na nyuma jeshi la Farao linawafuata kwa ghadhabu kubwa, kilitokea nini? Be blessed. Mpwao Ellli

WADAU SALAAMU!!

NAANDIKA UJUMBE HUU SAA NANE NA NUSU USIKU IKIWA NI KILIO KIKUBWA CHA MSAADA.

MIMI NI KIJANA WA KITANZANIA MWENYE MIAKA 29,MHITIMU WA CHUO KIKUU (BACHELOR OF PUBLIC ADMINISTRATION) MWAKA 2008 NIKFAULU KATIKA KIWANGO CHA UPPER-SECOND.

NIMEFANYA KILA NJIA NIWEZE KUPATA AJIRA BILA MAFANIKIO,NIMEJARIBU KUJIAJILI KWA KUFUNGUA KAMPUNI BINAFSI (HUMAN RESOURCES CONSULTANY FIRM) NA IMEFANYA KWA MUDA WA KARIBU MIAKA MIWILI NA NIMEPATA MTEJA WAWILI TU.MWISHO WAKE NIMESHINDWA KULIPIA OFISI NA GHRAMA ZINGINE KAMPUNI IMEKUFA NA SASA NIMEBAKI SINA KITU NA KATIKA HALI NGUMU SANA.

NA FAMILIA INAYONITEGEMEA NA HASA WADOGO ZANGU WATATU AMABAO NILIANZA KUWASOMESHA SEKONDARI TANGU NIKIWA CHUO KIKUU KWA KUSAVE KIASI KATIKA HELA YANGU MATUMIZI NILIOKUA NAPEWA NA LOANS BOARD.

SASA WADAU WOTE WAMESIMAMISHWA SHULE NA SIONI MWANGA WA MSAADA WOWOTE.

NIMAJARIBU KUTUMA MAOMBI KILA TANGAZO NALO BAHATIKA KULIONA BILA MAFANIKIO HATA YA KUITWA KWENYE USAILI.

NAOMBA SANA WADAU MSAADA WENU,NIKO TAYARI KUFANYA KAZI YOYOTE(YA HALALI) NA POPOTE PALE,ILI JAPO WADOGO ZANGU WAENDELEE NA MALENGO YAO YA ELIMU,KWANI WANAHUZUNI KUBWA.NISAIDIE JAMANI,NINGEKATA TAMAA LAKINI NAJUA LIPO TUMAINI NALO NI JAMII FORUMS.

AHSANTENI WOTE KWA MSAADA.

WASALAAM,

MAZIKU.

kulwamaziku@gmail.com
pole sana mkuu, kumbe kuna watu wanasota hivi? Nina wiki tatu toka nimalize na nimepata internship inayoanza 1st sept, kwa haya yaliyokukuta itabid niende tu, japo posho ni ndogo

Pole sana kaka yangu mengi wamesema wenzangu amini umeshapata kazi kwa jina la yesu zidi kumwomba mungu ,riziki yako ipo imeandaliwa na utaifulahia mungu akupe uvumilivu kwani ni mapito tu na yatashindwa kwa jina la yesu,(ubarikiwe)

pole sana kulwa. one trick that really works ni ya kuomba internship. ukiomba kujitolea kwanza unapata free internet na magazeti ambayo utaweza soma matangazo ya kazi.pili utajenga network, utakutana na watu na ideas mbalimbali. tatu ni kuwa utajua inside info kama kuna vacancy. usijali kuhusu kutokuwa na kitu mwanzoni, trust me ni sehemu ya kutokea. be agressive na kuwa mnyenyekevu kwa wakubwa na wadogo kwenye hiyo ofisi. impress, fanya hata kazi zisizokuhusu and god will do the rest!

Pole sana kaka naamini Mungu yupo atakupigania ila mwombe sana Mungu mimi pia nipo kwny mchakato wa kutafuta kazi ila nimeguswa sana na habari yako ila nakuomba usali na usikate tamaa kabisa amini tu utapata! Pia namshukuru huyo m2 hapo juu aliyekuambia utume Cv yako naamini atakusaidia amini utapata kazi Mungu akubariki sana usichoke kumwomba Mungu!

Dah!Ebana pole mkubwa,maisha ni magumu sana!Jipe moyo!Ongeza juhudi!

Dah! Pole kaka. Kila mdau anasema umuombe mungu. Mungu atakuwa busy sana jamani.
Fata ushauri wa king'asti hapo chini.

Back
Top Bottom