Kilio cha Mh. Alsheima Kwegir inabidi kiungwe mkono

Njaare

JF-Expert Member
Sep 26, 2010
1,081
275
Wana JF,

Jana Bungeni Mbunge wa viti maalum CCM mh. Kwegir (Samahani kama nimekosea kuandika jina lake) alitoa machozi kulalamikia jinsi maalibino wanavyodharauliwa. Alililalamika kuwa mauaji ya maalibino yanaengelea kutokea bila hatua za dhati kuchukuliwa kwa kuwakamata wahusika wakuu. Alilia kuona kuwa faru aliyeuawa Serengeti hatua kali zilichukuliwa mara moja. Je hao faru wana thamani kuliko maisha ya maalibino?

Mimi binafsi najiuliza, je serikali yetu inawajali wananchi wake na sii kwa maalibino tu? Ninauliza hivyo maana wale waliowapora wazungu huko Serengeti wamekamatwa mara moja. La kushangaza mpaka sasa shambulizi la mbunge wa ilemela na wa ukerewe bado ni tata, mauaji ya maalibino wengi waliohusika hawajakamatwa, tumesikia kukatwa mapanga kwa akina mama huko kanda ya ziwa na sasa utekaji na kuumizwa vibaya kwa Dr. Ulimboka.

Je, Serikali ya CCM inawathamini zaidi usalama wa wanyama na wageni na kuwapuuza raia wake?
 
Amelia machozi.........!!!!!!!!!!! Aende LHRC wamfundishe harakati aanzishe organization ili tumuunge mkono kwa hali na mali sio kukamata posho then kimyaaaa ndani ya black pimped v8 ..............kulia itasaidia nini......alilia mtu mzima zaid yake na hakuna impact kihivyooooo

Appealing to pitty.....she can do better than that
 
ndo manake

Mkuu Mtoto wa mjini umenena kweli,

Kumbe serikali ina pesa ila inataka liwalo na liwea. Watanzania wafe wasife, shauri yao.

Sitaki kuamini habari zilizopo katika magazeti ya Tanzania Daima na Habari leo (kwa mujibu wa uchambuzi wa magazeti radio one). Wakati Tanzania Daima ikidai kuwa baraza la mawaziri limekubali zitengwe bilioni mia mbili ili kuagiza madaktari kutoka nje, Habari leo linadai serikali imeingia mkataba na hospitali binafsi ili kuwatibu wagonjwa.

Hili ni jambo la ajabu sana kwani inaonekana kuwa serikali inazo hela ila inataka tu kwa maksudi kuzitelekeza hospitali za umma. Kama kweli serikali imetenga bilioni 200 kwa ajili ya kuwalipa madaktari toka nje ambao wakifika hawatafanya kazi kutokana na ukosefu wa vifaa, mimi nalifananisha hili na dili la ATCL kukodi ndege na kuanza kuilipia wakati haifanyi kazi. Kwa nini Serikali isitumie hizo fedha kukarabati hospitali na kununua hivyo vifaa?

Kuna mtu yeyote anaamini kuwa atakuja daktari toka nje alipwe anavyotaka halafu hakuna dawa wala vifaa hospitalini ajali maisha ya watanzania kama wanavyodai madaktari wazalendo?

Kama serikali inaingia mikataba na hospitali binafsi kuwatibu wagonjwa, hili nalo linafanana na kitendo cha ATCL kukataa kununua ndege moja kwa moja toka kwa mtengenezaji na kungangania kutaka atumike mtu wa kati. Hili linaonekana kuwa mawaziri wana maslahi binafsi na suala la huduma mbovu kwenye hospitali za umma. Hiki ni kiama kwa wananchi wa Tanzania kwani watakaotibiwa ni wachache na serikali italipa hela nyingi kuliko wanavyotenga bajeti katika sekta ya afya.

Chonde chonde serikali, Busara inahitajika katika kusuluhisha hili jambo. Mtakataa kuwalipa madaktari wakiwa katika hospitali zetu za umma ila mtawalipa kiasi wanachotaka wakiwa private na mtalipa na cha juu.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom