kasopa
JF-Expert Member
- Aug 29, 2010
- 302
- 56
nilipata fursa ya kwenda Kiteto hivi karibuni.. nimejifunza yafuatayo:
- Ardhi ya kule ni karibu sawa na bure na bado ipo virgin --ekari inauzwa Tsh 10,000 kwa ekari.. cha kushangaza zaidi kukodisha shamba inakuwa 10,000 kwa ekari vilevile
- watu wanajitahidi kulima mahindi, maharage, choroko na sunflowers (alizeti) na soko la mazao hayo lipo sana
- tatizo kubwa la kiteto ni upatikanaji wa maji. Msimu wa mvua mara nyingi ni mmoja. kwa hiyo ukipatia mvua ikanyesha kwa wingi unakula bingo. ikigoma inakula kwako
- kama mtu upo tayari kucheza na risk unaweza kujaribisha kulima huko (kilichonitia moyo wapo watu wengi wanalima na wamefanikiwa-- MIMI NITAWEKEZA KIDOGO kwanza ili kuona nitapata nini!!!
Mkuu kanyagio ubarikiwe naimani upo ok Kiteto ipo mkoa gani huwa nasikia tu na niumbaligani toka Dar