KILIMO: mazao yanayokubali wakati wa Masika

nat867

Member
Feb 14, 2008
97
5
Ndugu zangu nashukuru sana mada mbalimbali zinazojadilikwa kuhusu kilimo. na mimi ndo naanza kujikita katika kilimo.

Nina shamba langu katika wilaya ya bagamoyo (maeneo ya barabara ya Bagamoyo-Msata) sasa mimi ninataka kutumia mvua za masika kwa ajili ya kulima..nimenza kutayarisha shamba lenye ekari 7. Sasa ndugu zangu naomba kuuliza ni mazao gani ya muda mfupi ninayoweza kulima wakati wa msimu wa mvua za masika (machi-May)?.

Lengo ni kulima halafu nauza hayo mazao Dar es salaam.

Nimesoma threads za kilimo lakini nimeshindwa kupata taarifa ninayohitaji. Ndugu zangu kila atakayesoma ujumbe huu na anafahamu masuala ya kilimo naomba anisaidie.nitashukuru nikifahamishwa pia masuala ambayo natakiwa kuzingatia wakati wa kulima kwenye masika!

Natanguliza shukrani
 
mazao ya muda mfupi yenye tija kwa kipindi utakacho ni matango, kama viazi vitamu vinakubali lima pia,hicho kipindi ni hatari ukilima tikiti maji kwa sababu wakulima wengi wanakuwa wamelima, ama sivyo lima ufuta.

Nanasi/mhogo si la muda mfupi kivile ila ni zao la uhakika kwa sababu hata mvua zikipungua wewe utavuna kitu.
 
Malila ahsante sana kwa ushauri wako.. najua nanasi itachukua miezi 18.. nimependa wazo la ufuta!!.

sehemu yenyewe ni kuwa hakuna mto karibu kwa hiyo huwezi kumwagilia..

pamoja na maelezo ya kulima muhogo/nanasi yaliyotolewa... Je unaweza kulima CHOROKO, MAHINDI au MAHARAGE? Je mazao haya yatakubali wakati wa mvua nyingi au yataathiriwa na mvua? na kama inawezekana kuyalima je nikiyalima katikati ya msimu wa mvua kusudi ikikaribia wakati wa kutoa maua, mvua imepungua.. naombeni ushauri wenu kuhusu mazao hayo--- CHOROKO, MAHINDI, MAHARAGE!!
 
Back
Top Bottom