Kilimo Kwanza: Sweet potatoes

Shukran kwa share mkuu... Nitaifanyia kazi.

Nafuta Kauli yangu waheshimiwa wanajamvi... Nimedownload na kuiangalia hii clip mara kadhaa, na kufikia maamuzi ya kuwa mkweli... SITOWEZA KUIFANYIA KAZI.. Hizi ni Next Level stuff..
Ndio maana wazungu wanaendelea aisee... Shamba la Ukweli...

NB: Tunaropoka kuhusu Kilimo kwanza na miradi yetu ya kisisiemu inayowafanya wachache waneemeke....Wakati Nchi haina kituo cha uhakika chochote kinachofanya soil analysis... !!! Tutalimaje???
 
Mimi nimeipenda hii clip kwani inaonyesha ujanja wanaotumia wenzetu kwenye kilimo, mbegu inatumiwa kutengeneza vimiche kibao vya kupandikiza kwenye "main" shamba. Machine zinarahisisha kazi ila kwa hapa kwetu hata nguvu kazi pia inaweza kutumika ili kutoa ajira. Cha msingi ni kusindika hilo zao na hapo ndio "value" inaongezeka.

Je shughuli hii inaweza kufanyika? na kama sio sweet potatoes, je, mihogo je inawezekana kwa ukubwa huu?

Hapa ni kiasi cha kuunganisha nguvu kutimiza mahitaji ya kifedha ya shughuli kama hii.
 
Mkuu Kontikarwak,
Shukrani mkuu, nimejifunza kitu!
Sikujua kama viazi vitamu vinahitaji kuvundikwa ili kubadili Starch kua Sweetsugar, That the sweet truth.
The sour truth is about Kilimo kwanza, not even with a single research lab for seeds and soil analysis.
 
Mimi nimeipenda hii clip kwani inaonyesha ujanja wanaotumia wenzetu kwenye kilimo, mbegu inatumiwa kutengeneza vimiche kibao vya kupandikiza kwenye "main" shamba. Machine zinarahisisha kazi ila kwa hapa kwetu hata nguvu kazi pia inaweza kutumika ili kutoa ajira. Cha msingi ni kusindika hilo zao na hapo ndio "value" inaongezeka.

Je shughuli hii inaweza kufanyika? na kama sio sweet potatoes, je, mihogo je inawezekana kwa ukubwa huu?

Hapa ni kiasi cha kuunganisha nguvu kutimiza mahitaji ya kifedha ya shughuli kama hii.

mkuu ni clip nzuri sana, hawa ndio wakulima wa kubwa kwa nchi za wenzetu na hiki ndio kilimo cha kisasa, kwa haraka haraka unaweza kusema kilimo cha namna hii hakiwezekani kwa mtz lkn mimi naamini kabisa kwa mtu mwenye malengo ya juu na kilimo anaweza kabisa kuinvest miradi ya namna hii ukizingatia zana za kilimo kama hizo planting, harvesting, storage & packaging machines bei zake si za kutisha na pia zinapunguza sana gharama za uendeshaji wa shamba, mfano hapo unaona wana watu chini ya 15.. sasa iwapo wangetumia traditional farming wangehitaji watu zaidi ya 50 kwa shamba hilo hilo.

ili kubalance mambo kwanza unatakiwa uwe na shamba kubwa na irrigation system ya uhakika, tz tuna vituo na wataalam wa kilimo wengi sana kutoka vyuo vya kilimo lakini hatuwatumii ipasavyo.. kuhusu swala la kuendesha mitambo si tatizo c'se kuna vijana wengi sana wa elimu ya juu na kati hawana ajira

NB: Ni muhimu kuanza na nja za asili..then... ongeza ukubwa wa shamba kidogo kidogo kabla hujafikia hatua ya kulima hekari zaidi ya 100 kwa mkupuo [lengo ni kupata uzoefu na changamoto za kilimo kikubwa] pia swala la umiliki wa machine/kilimo kwa kuunganisha nguvu ni jambo la msingi sana sana c'se machine zitakuwa idle muda mrefu
 
Narubongo,
Hapa cha kuangalia zaidi ni investment ya kufikia kiwango hiki cha ukulima. Mtu mmoja mmoja tutabaki kuwa subsistence farmers na ndio nauliza, je, haiwezekani investment kama hii kuwaunganisha interested parties kuwekeza ndio kutimiza mahitaji ya kifedha?
Niliangali clip nyingine kuhusu mining, machine zenyewe zikatajwa kuwa ni kati ya lati 7 na million 1 USD, na chimboni kuna sio chini ya machine 15 zinafanya kazi kila siku. Sasa hapa mtu mmoja mmoja kweli sio wengi wanawez lakini hapa hapa JF kila leo mtu anauliza afanye nini na mil5 zake? ndio labda kuna wengine wengi ambao wanaweza kuwekeza katika miradi na wao kupokea tu mafao yao mwisho wa mwezi/mwaka nk. cha msingi ni kuwa na huu utaratibu wa kuwa na fursa ya kujua ni miradi ipi ipo implemented/ ipo njiani na mtu kujipanga kuwekeza.

Ndio labda tunayo stock exchange, lakini upana wake ni mdogo na ni ya mashirika yaliyo simama tayari na sio hizi prospecting ideas.
Saccos kila kona ya mji, lakini sijasikia umoja unaowaunganisha watu kufanya kitu fulani, kuwaunganisha watu wenye nia ya kulima pamba, kulima matunda nk, SACCOS wanasubiri mtu huyo mmoja mmoja aje kuomba pesa za "kujikimu", na sio za kuendeleza mradi katika viwango hivi vya kimataifa.
 
kotinkarwak tatizo kubwa la watz ni kupenda shortcuts na faida za haraka haraka, na pia wengi wanafanya Ujasiriamali kama njia ya kujiongezea kipato cha ziada na si kuufanya Ujasiriamali kuwa mfumo wa kuendesha maisha. Kuna mijadala mingi sana ya kuunganisha nguvu changamoto zake na mmojawapo ni huu chini
Http://www.Jamiiforums.com/Ujasiriamali/251056-kuunganisha-nguvu-kwa-wenye-matching-aidea.html

kuhusu swala la vikundi vya saccos na vicoba hiyo ni baadhi ya mifano michache kama ulivyoeleza. Ukienda vijijini utakuta matractor 20 ambapo kila mwenye hekari 40 ana tractor lake binafsi, sasa hapa hawa watu wangeweza kabisa kuungana na kuwa na tractor 3, machine za kupandia, kuvuna, kuhifadhi kama hizo za kwenye hiyo clip na wote wangeweza kuzitumia. Maeneo ya migodini napo matatizo ni yale yale kila mtu na kitalu chake na sululu zake halafu wawekezaji wa nje wakija tunaanza kulalamika hovyo serikali inatuuza.

Investments kubwa za namna hii zinawezekana kabisa kwa wenye nia ya Ujasiriamali na malengo ya juu.. [tatizo ni wachache sana wenye moyo wa kujitoa muhanga], nipo mbioni kufanya uamuzi mgumu
 
Last edited by a moderator:

Similar Discussions

Back
Top Bottom