Kilimo cha zao la Ufuta: Masoko, Mbinu na Ushauri Toka kwa Wadau

Mkuu GEBA2013 Sema uletewe vijana wa kung'oa visiki kwenye hilo shamba lenu. Msimu wa kulimo bado mbali sana mpaka Feb hecta 25 watakuwa wamebomoa. Cha muhimu zaidi nunueni chainsaw wakati madogo wanang'oa miti nyie huku nyuma mnalingua magogo na kufunga biwi au mnaimport Wamalila kutoka mbeya special kwa kuchoma mkaa. Ndani ya miezi sita shamba litakuwa jeupe pee tayari kwa kulima na tractor.

Njia rahisi greda.
 
Last edited by a moderator:
Mbegu yako ni ya kampuni gani? Nimepata shamba km eka mia moro ila inahitaji kusafishwa sbb ni shamba jipya.vp unaweza ukanisaidia uwezekano wakupata shamba lingne yakukodi lililosafishwa?yenye uwezekano wakulima na trecta?msaada pls kwako na kwa wengneo wahumu na nje ya jf{wasomaji} 0752317974,wanicheki kwenye hi namba

Unasumbuka nn kodi greda.ndani ya mda mfupi tayari kazi yako tayari
 
iko sehemu gani hyo shamba.taget ni shamba lilosafisha yakuingiza tractor.mashamba yasiyosafisha tunazo moro na tanga ila mda nikm hautaturuhusu kusafisha kwa mda nakuwah kilimo.taget yetu ni eka mia iliyosafishwa.km unaweza kutupatia tutashukuru.

Kwa Morogoro msimu unaanza lini?
 
Nimeanza kuvuna ufuta shambani kwangu, kwa sasa nafanya comparison ya bei na wanunuzi. JF ni jungu kuu naombeni member wenye kujua wanunuzi mbali mbali wanipe contacts zao ile nilinganishe bei nifanye right choice ktk kuuza mzigo.
Thanks wadau wote.

Mrejesho:

  • kati ya eka 30 nilizopanda ufuta ulistawi vzuri na kuvunwa eka 17..hii ilisababishwa na uangalizi mbovu wa aliyekuwa ananisimamia shamba.
  • kila eka nilivuna wastani wa kilo 350, kipindi hiki ( july 2011-2012) wanunuzi binafsi hawakuruhusiwa lindi kununua ufuta, so niliuza kwa utaratibu wa stakabadhi ghalani @ 1200/= kwa kilo jumla nilipata kama milion 7 kwa msimu mmoja (gharama za kusafisha msitu wa eka 30, mbegu na malipo ya wafanyakazi zilikuwa ni 3.5 milion), sikuingia gharama ya kusafirisha kwa kuwa walinifata shambani.
  • Mwaka 2013 sikulima nilipumzisha shamba kwa kulisafisha eka zangu zote 50 na kutanua kidogo (hili shamba lilikuwa ni msitu wakati nalichukua)
  • mwaka huo wa 2013 ulikuwa ni mzuri sana kwa upande wa bei, chomachoma (wanunuzi binafsi) waliruhusiwa na ufuta ulipanda bei hadi kufikia 2500 kwa kilo na unalipwa cash hapo hapo. waliolima walipata pesa nzuri tu.
  • mwaka huu vijana wanamalizia kupanda shamba nimelima ekari 35, nilibadili team ya wafanyakazi wa shamba kwa kuwa wengi walinikwamisha kwa kuendekeza starehe badala ya kazi. natumaini wanunuzi binafsi wataruhusiwa.
  • watu wengi kutoka mikoa mbali mbali (wachaga kibao) wameanza kuvamia misitu na kuiuza au kulima so kwa sasa kumechangamka sana tofauti na 2011 wakati naanza.
  • expectations zangu mwaka huu ni ........35(eka) x 400(kg) x 2500(bei/kg)=35,000,000.
  • NB: 400kg kwa eka ni kiwango cha chini cha mavuno, wataalamu wa chuo cha naliendele waliniambia kwa mbegu zao za lindi 2002 na malada natakiwa nipate 1200kg kwa eka. Vijana wapo shamba wanachakarika na mi nipo mjini namtumikia mkoloni (ajira).

Thanks kwa wote:

UKITAKA KUUJUA UTAMU WA NGOMA .......UINGIE UCHEZE.

Habari mkuu. Vipi bado unaendelea na ulimajia wa zao la ufuta? Tupo mrejesho. Nina shauku ya kufanya aina hii ya kilimo.
 
Ndugu zangu kwanza habari zenu, mimi kijana kati ya wale waliopigwa na maisha, ila pamoja na ugumu uwo maisha bado sijakata tamaa, nina dhamira ya kujikwamua kimaisha, dhamira yangu kuu ni kujishughulisha na shughuli za kilimo, shida yangu kama mwenye utaalamu wa kilimo cha ufuta na hata soko lake.

Asanteni
 
ndugu zangu kwanza habari zenu, mimi kijana kati ya wale waliopigwa na maisha, ila pamoja na ugumu uwo maisha bado sijakata tamaa, nina dhamira ya kujikwamua kimaisha, dhamira yangu kuu ni kujishughulisha na shughuli za kilimo, shida yangu kama mwenye utaalamu wa kilimo cha ufuta na hata soko lake. asanteni

Mnnnnh ufuta tena mimi najua mashamba ya mpungu tu nenda mpanda utakimbia mwenyewe.

Jembe halimtupi mja wake.
 
Ufuta ni mzuri kulima tatizo ni kama madini ukipata sana usiingie tamaa. Mimi nimeshawai lima nikapata sana niliporudi kuwekeza mara ya pili kwa pesa nyingi mtaji wangu wote na pesa yangu yote ni kama niliizika kwa maana mvua zilisomba ufuta wote sikurdisha ata ghrama ya kutunza shamba hapa nilipo ni kama nanza upya maisha coz nilitegemea sana shamba nimeishia kuangaika kwa sasa.
 
Bei hiyo ni ya vipimo vya kijijini ambavyo huwa na kg 2 sawa TZS 5400 kwa huku lakini bei ya 1kg ni 2600 kwa sasa imeshuka watu wengi wameleta ufuta na mwakani itashuka sana maana watu wengi watalima.
 
Bei hiyo ni ya vipimo vya kijijini ambavyo huwa na kg 2 sawa TZS 5400 kwa huku lakini bei ya 1kg ni 2600 kwa sasa imeshuka watu wengi wameleta ufuta na mwakani itashuka sana maana watu wengi watalima.

Aisee, kumbe! Mbona wanivunja moyo mkuu, nilitaka kulima mwaka huu mwezi wa 11
 
Usivunjike moyo ufuta hautabiliki we lima kwa wingi utakuwa tajiri cha msingi ni kujua soko na bei nzuri tuwasiriane lkn ningependa jua unataka kulima wapi ili nikupe ushauri zaidi.

Asante mkuu. Natarajia kulimia maeneo ya huku ukanda wa Rufiji
 
Back
Top Bottom