Kilimo cha Alizeti (Sunflower): Masoko, Mbinu na Ushauri toka kwa wadau

Habari za week end wakuu,
Mwaka huu nimedhamiria kujikita kwenye kilimo cha biashara,hasa zao la alizeti.

Kabla ya kuingia kichwa kichwa ningependa kupata mawazo kutoka kwa wataalamu au wazoefu ambao pia wamejikita kwenye kilimo cha biashara cha zao hili.

Haijalishi ni eneo gani unafanyia kilimo chako,lakini ingekua vyema kama tungepeana mafanikio na changamoto zilizopo ktk kilimo hiki hasa tukiangazia kwenye mambo muhimu kama,

1.Aina ya shamba(udongo)
2.Hali ya hewa
3.Vitendea kazi
4.Uchaguzi wa aina ya mbegu sahihi.
5.Utaalamu katika upandaji wa mbegu.
6.Changamoto za Ndege,wadudu na magugu korofi.
7.Virutubisho /Mbolea
8.Umwagiliaji (kama unahitajika)
9.Ulinzi wa shamba.
10.Uvunaji
11.Uhifadhi
12.Masoko.

Naamini kunawengi hapa jf wanajishughulisha au wanauelewa juu ya kilimo hiki.
Mnakaribishwa kuchangia.
 
ImageUploadedByJamiiForums1456545404.736348.jpg

Wakuu nilibahatika kutembelea sido kucheki mashine zao wanazotengeneza bei zao Kama hiyo mil 7.
Hiyo hapo haina Filter inabidi ukanunue filter .
Wao wanasema wanakupa warranty ya miezi 9.
Kazi kwenu wadau.
 
Alizeti hulimwa kwa wingi katika mikoa ya Shinyanga, Singida, Dodoma, Iringa, Tabora, Morogoro, Ruvuma, Mbeya, Arusha, Manyara, na RukwaZao hili hulimwa kwa ajili ya chakula na biashara.

Mambo muhimu ya kuzingatia wakati wa uzalishaji
  • Kuchagua aina bora ya mbegu
    Chagua aina bora ya mbegu inayovumilia magonjwa, wadudu, inayotoa mazao mengi na kiwango kikubwa cha mafuta.
  • Vilevile chagua aina ya mbegu ambayo hukomaa kwa wakati mmoja ili kurahisisha uvunaji.
Kuweka mbolea
Rutubisha udongo kwa kutumia mbolea za mboji na samadi ili kupata mazao mengi na bora.

Kudhibiti wadudu na magonjwa
Alizeti hushambuliwa na magonjwa ya majani, mizizi na masuke ambayo husababisha upungufu wa mavunoHivyo ni muhimu kuyadhibiti ili kupata mavuno mengi na boraPia ndege hupunguza mavuno kwa kiasi cha asilimia 50 au zaidiNjia ya kudhibiti ndege ni kwa kuwafukuza na kupanda mbegu zinazokomaa mapema.

Maandalizi kabla ya kuvuna;
Ukaguzi

Kagua shamba kuona kama alizeti imekomaaAlizeti hukomaa kati ya miezi minne hadi sita tangu kupandaWakati huo punje huwa na unyevu wa asilimia 25Ni muhimu kuvuna alizeti mapema ili kuepuka mashambulizi ya panya, mchwa na ndege waharibifu

Dalili za alizeti iliyokomaa
  • Suke hubadilika rangi kutoka manjano na kuelekea kuwa nyeusi.
  • Viuwa vya pembeni mwa suke hunyauka na hubadilika kutoka rangi ya manjano na kuwa ya kahawia
Uvunaji, ukaushaji na ubebaji

Vifaa vya kuvunia na kubebea kutoka shambani
  • Kisu
  • Vikapu
  • Magunia
  • Matenga Vifaa vya kukaushia
  • Maturubai
  • Mikeka
  • Kichanja bora Vyombo vya usafiri kutoka shambani
  • Matoroli
  • Matela ya matrekta
  • Mikokoteni ya kukokotwa na wanyama
  • Magari KUVUNA Alizeti huvunwa kwa kutumia mikono ambapo suke hukatwa kwa kutumia kisuPia mashine (combine harvester) hutumika kuvunia alizeti katika nchi zinazolima alizeti kwa wingiMasuke ya alizeti huwekwa kwenye vikapu ambavyo hutumika kusomba alizeti ndani ya shambaKisha alizeti hufungashwa kwenye magunia na kusafirishwa hadi nyumbani tayari kwa kukausha
Kukausha
Kuna hatua mbili za kukausha alizeti; kukausha masuke na kukausha mbegu za alizeti
  • Kukausha masuke - Masuke hutandazwa kwenye kichanja bora katika kina kisichozidi sentimita 30 ili yaweze kukauka vizuri.
    Vilevile huweza kutandazwa kwenye maturubai, mikeka au sakafu safi. Lengo la hatua hii ni kukausha masuke ya alizeti ili kurahisisha upuraji
    KUPURA
    Upuraji hufanyika baada ya kuhakikisha kuwa masuke ya alizeti yamekauka vizuri. Masuke ya alizeti hupurwa kwa kutumia mikono ambapo mbegu hutenganishwa kwa kupiga masuke taratibu kutumia mtiNi muhimu kupiga masuke taratibu ili kuepuka kupasua mbegu
    Pura kwenye kichanja bora, maturubai au mikeka
  • Kukausha mbegu
    Mbegu za alizeti hukaushwa juani kwa kutandazwa kwenye vichanja bora, maturubai, mikeka au sakafu safi
    Tandaza mbegu katika kina kisichozidi sentimita 4 ili ziweze kukauka vizuri.
    Lengo la hatua hii ni kukausha mbegu baada ya kupura ili kufikia kiwango cha unyevu kinachotakiwa kwa hifadhi salama ambacho ni asilimia 8
Jinsi ya kutambua mbegu zilizokauka vizuri
  • Kufikicha mbegu
  • Mbegu zilizokauka maganda yake hutoka kwa urahisi zinapofikichwaKumimina kwenye chombo kama debe
  • Mbegu zilizokauka hutoa mlio mkali zinapomiminwa kwenye vyombo hivyo
  • Mbegu zilizokauka hung'ara Kutumia kipima unyevu.
  • Mbegu zilizokauka vizuri kipimo huonyesha asilimia 8
Kupepeta na kupembua
Kupepeta na kupembua hufanyika ili kuondoa takataka kama vile mawe, wadudu, mapepe, mbegu zilizooza au kupasukaMbegu za alizeti hupepetwa kwa kutumia ungo au mashine zinazoendeshwa kwa mkono, injini au umemeMashine hizi zina uwezo wa kupepeta na kupembua kilo 60 hadi 350 kwa saa kutegemea aina ya mashine na ukubwa wa mashine yenyewe

Kuhifadhi
Alizeti iliyopurwa huhifadhiwa katika hali ya kichele kwenye maghala bora, yaani vihenge, sailo au biniAlizeti ya kuhifadhi kwenye maghala ya nyumba ifungashwe kwenye magunia na ipangwe kwenye chaga kwa kupishanishaIli kurahisisha kazi ya kukagua ghala, acha nafasi ya mita moja kutoka kwenye ukutaZiba sehemu zote za ghala ili kuzuia panya kuingiaPanya hupenda sana kula punje za alizeti, na husababisha upungufu mkubwa wa punje ambao husababisha upotevu wa asilimia 30 kwa kipindi cha miezi mitatu ya hifadhiAsilimia ya upotevu inaweza kuwa kubwa zaidi kutegemea idadi ya panya na upatikanaji wa vyakula vingine kwa wakati huoMatumizi ya Mbegu za Alizeti Mbegu za alizeti hasa zenye mistari zinaweza kuliwa baada ya kukaangwa au kukaushwaPia zinatumika katika utengenezaji wa mikateMbegu za alizeti husindikwa kupata bidhaa ya mafuta

Kusindika mbegu za alizeti kupata mafuta
Vifaa
  • Mashine ya kukamua mafuta
  • Chujio safi
  • Ndoo
  • Vifungashio
  • Sufuria
  • Mizani Malighafi
  • Mbegu za alizeti
  • Maji
  • Chumvi
Njia ya kukamua mafuta
  • Chagua mbegu bora za alizeti
  • Zianike kwenye jua kwa muda wa saa 1 hadi 2
  • Weka kwenye mashine ya kukamulia ya daraja au Ram
  • Kamua mafuta
  • Chuja mafuta kwa kitambaa au chujio safi
  • Pima mafuta yaliyokamuliwa
  • Ongeza maji na chumviKatika lita 10 za mafuta weka lita moja ya maji na gramu 200 za chumvi Weka mafuta kwenye chombo cha kuchemshia (sufuria)
  • Chemsha hadi maji yote yaishe
  • Sauti ya kuchemka ikiisha ni dalili kuwa maji yamekwisha.
  • Ipua, acha yapoe, kisha chuja kwa kitambaa safi au chujio
  • Fungasha kwenye vyombo safi na vikavu na vyenye mifuniko
  • Weka lakiri na lebo Hifadhi kwenye sehemu safi, kavu na yenye mwanga hafifu
Matumizi
Mafuta hutumika katika mapishi mbalimbali na yana virutubishi vifuatavyo: - Mafuta gramu 100 Nguvu kilokalori 900

Kwa maelezo zaidi na mazao mengine tembelea
 
  • Thanks
Reactions: SMU
ok fine.. nikifika Singida nitakujuza.. ila ni zao ambalo halisumbui sana maana hata palizi ni mara moja tu
mkuu bado tunasubili mrejesho baada ya kufika huko singida kwani taarifa yako ni muhimu hata kwetu wengine pia, nitashukuru sana ukirudi na kutupatia taarifa zote muhimu, ahsante sana
 
Ntashukuru
Bulldog vipi mkuu matenge alikujibu hoja yako hapo juu? kama ndio naomba utuwekee hapa iweze kutusaidia na wengine, tuweze kujipanga maana mtu atajikomboa kwa juhudi zake mwenyewe kwa kutumia fursa zilizopo. natumaini utanisaidia katika hili, natanguliza shukrani.
 
KUWEKA MBOLEA
• Rutubisha udongo kwa kutumia mbolea za mboji na samadi ili kupata mazao mengi na bora.
Hivi nilisikia Alizeti haihitaji kuwekwa mbolea kwani ikiwa na mbolea sana inakuwa nene sana na mbegu zake pia zinakuwa nene ila kiini kinachohifadhi mafuta kinakuwa kidogo sana au kuwa mapepe kabisa.Sijui hii dhana ni sahihi.
 
Naomba mnipe ushauri ni mashine gani bora zaidi kwa kukamulia mafuta ya mbogamboga.
Na bei zake
 
wakuu PainKiller , Rider mbona mie nimezuiliwa kuweka thread mpya karibu nusu nziama ya JF , sikidhi vigezo ama akuna namna? yaani anishia kwenye siasa tuuuuuu nsio jukwaa langu pendwa la wapambanaji
 
Kilimo ni biashara kama zingine hoja na ushauri mbalimbali nimeelewa ila ninachokiomba ni mashine nzuri ya gharama isiyozidi milioni tatu mpaka nne ili mtu ajipange na hapo atakuwa anajifunza uendeshaji wa kiwanda baadae ndio inunuliwe hiyo ya milioni saba hadi nane maana mwanzo ni mgumu
 
Mmmh sina hakika sana na kupata mashine NZURI kwa bei uitajayo hapo juu, sema unalenga kitu cha kukusukuma ukijipanga upate kitu bora zaidi; hata hivyo hujatuambia ni kiasi gani cha mafuta umepanga kuwa utayakamua kila siku
 
Alizeti ni zao zuri sana la biashara linalimwa sehemu nyingi nchini kwetu ila mimi najua Iringa inaongoza,pia Dodoma na Singida nako wanalima sana tu.

Ukipata shamba zuri ekari moja ya alizeti huweza kukupatia kati ya magunia5-10 kutegemeana na aina ya mbegu uliyotumia na pia namna shamba lako ulivyolihudumia.

Gunia moja la alizeti yaani madebe sita huweza kutoa lita 20 za mafuta baada ya kusafishwa,mafuta haya unaweza kuuza kati ya shilingi 28,000-36000 kwa ndoo ya lita 20,pia utaweza kuuza mashudu yako ya alizeti kwa wafugaji.

Ukiwa wewe ni mfanyabiashara mzuri na una mtaji mkubwa fuata ushauri wa ama kwa kununua mashine ya kukamua alizeti kwani ukiwa na mashine hii itakulipa zaidi kwani utauza product yako mwenyewe yenye label ya kiwanda chako,this is very common in Singida,Iringa and in Mpwapwa-Dodoma.

Kama mnataka mali mtayapata shambani,braza umesahau shairi hili la darasa la nne enzi zile?
Gunia moja la alizeti ni sawa na kilo ngapi samahani?
 
duuh mkuu dumu la lita 20 ya alizet bei imekua mbaya sana uwa aishuki chini ya elf 50..hata kama kipind ziwenying zinavunwa..kwa mbeya lakn sijuh hyo bei yako ni mkoa gan..na mbeya alizet zinalimwa sana
 
Kamani ni kitu gani wanawekaga kutoa ile harufu ya mafuta ya alzeti maana nikiwaga safarin to Mwanza nikipita pale singida wanga na nunua yanakuwa na harufu bat nikiwa uku dar nikinunua singida oil haina harufu
 
Zao la alzeti Zuri kama umelima ekari nyingi mkuu kuanzia 15.....hila kwa ekari za hapa kazi tu 1-6 itakula upande wako.....otherwise huwe unalima, na kukamua na kuuza mafuta hapo sawa na mashudu unauza wewe pia.
 
Nakushauri usilime alizeti kwasababu bei yake iko chini sana,labda ukamue mwenyewe itakulipa.nilishawahi kulima alizeti mwaka juzi ilibidi ninunue mashine SIDO ili kukwepa kulaliwa na wafanya biashara waliokuwa wananunua kwa bei ya chini sana.
Habari yako mdau
Mimi nahitaji msaada wa mafunzo ili nipate uzoefu wa ukamuzi wa mafuta,utanisaidiaje kwa hilo?
 
Habari zenu wapendwa mimi ni member wa humu jamvini napenda sana kilimo ila sijui naazaje ila kwa kuanzia nilitaka nilime alzeti maeneo ya Singida mimi naishi Dar.

Naombeni msaada wenu wa kimawazo na wa kitaalamu na changamoto zilizopo.

Natanguliza shukrani zangu dhati kwenu.
 
Alizeti ni zao zuri sana la biashara linalimwa sehemu nyingi nchini kwetu ila mimi najua Iringa inaongoza,pia Dodoma na Singida nako wanalima sana tu.

Ukipata shamba zuri ekari moja ya alizeti huweza kukupatia kati ya magunia5-10 kutegemeana na aina ya mbegu uliyotumia na pia namna shamba lako ulivyolihudumia.

Gunia moja la alizeti yaani madebe sita huweza kutoa lita 20 za mafuta baada ya kusafishwa,mafuta haya unaweza kuuza kati ya shilingi 28,000-36000 kwa ndoo ya lita 20,pia utaweza kuuza mashudu yako ya alizeti kwa wafugaji.

Ukiwa wewe ni mfanyabiashara mzuri na una mtaji mkubwa fuata ushauri wa ama kwa kununua mashine ya kukamua alizeti kwani ukiwa na mashine hii itakulipa zaidi kwani utauza product yako mwenyewe yenye label ya kiwanda chako,this is very common in Singida,Iringa and in Mpwapwa-Dodoma.

Kama mnataka mali mtayapata shambani,braza umesahau shairi hili la darasa la nne enzi zile?
babati pia wanalima sana hili zao!!!!
 
Niliwahi kulima zao hili, ingawa sikuvuna kama nilivyotegemea. Nililima babati eneo maarufu sana kwa uzalishaji wa zao hili. Niliwekeza sh 2ml na baada ya kuvuna nikaambulia 450000. Huo ulikuwa ni mwisho wa kulima. Nashauri nunua mazao badala ya kulima.
 
Back
Top Bottom