keynessian
JF-Expert Member
- Feb 28, 2014
- 588
- 407
Nenda jukwaa la biashara na uchumi utapata details za kutosha
Kilimo cha Alzet kina hitaji mvua za wastan na kipindi cha kuvua kinahitaji jua.
Hk 1 hutoa gunia 7-12.
Gunia 1 lina uzito wa kg 65-70.
ndugu zangu sisi tumeanza kuungana baadhi ya members wa JF ili tulime kwa pamoja!!..
igembe nsambo nitakutafuta maana kuna mambo mazuri ya kujadili
bei ya gunia wanauzaje? asante sana mkuu.
Asalaaam wanaJF, nimetafuta jukwaa la Kilimo sijaliona, nadhani hata hapa sijakosea jukwaa, nataka kuanza kilimo cha alizeti, ningependa kupata elimu kidogo juu ya kilimo hiki, hali ya hewa inayohitajika, madawa, upandaji na mengine mengine juu ya zao hili. Natanguliza shukrani zangu za dhati kwenu nyote.
kwa alizeti navyojua haitaki mvua nyingi na inalimwa sana singida. mi nimepanda january katikati na natarajia kuvuna may. hawauzi kwa kilo ila gunia. gunia huwa linafika mpaka 65,000/-. kwa ekari moja unaeza toa gunia 12 mpaka 14 ukilima kitaalam.
Umelima eka ngapi? Mashamba yanapatikana huko? Nahitaji ya kukodi.
mi nilipata kwa mwanakijiji so sijalipia kukodi ila nimegharamia kulima na mbegu tu. now nafanya palizi na by next week natarajia kwenda Singida. nitakuulizia kwa wenyeji wangu kuhusu kukodi then tutawasiliana. ila kwa sasa msimu uko katikati..
Nataka nilime eka za kutosha mwakani, mwaka huu nimeshindwa kwasababu sikuwa nataarifa za kutosha.
ok fine.. nikifika Singida nitakujuza.. ila ni zao ambalo halisumbui sana maana hata palizi ni mara moja tu
Nimekuwa navutiwa sana na ukulima wa alizeti kama zao la biashara. Naomba mawazo ya mdau yeyote mwenye uzoefu na kilimo hiki na namna gani unaweza kupata faida; Masoko yanapatikanaje na pia je ni faida zaidi kulima alizeti na kuuza ama kulima na kukamua mafuta? Naleta hoja.
Jalibu kuggoogle utapa maelekezo yatayo kusaidia.Habari za week end wakuu,
Mwaka huu nimedhamiria kujikita kwenye kilimo cha biashara,hasa zao la alizeti.
Kabla ya kuingia kichwa kichwa ningependa kupata mawazo kutoka kwa wataalamu au wazoefu ambao pia wamejikita kwenye kilimo cha biashara cha zao hili.
Haijalishi ni eneo gani unafanyia kilimo chako,lakini ingekua vyema kama tungepeana mafanikio na changamoto zilizopo ktk kilimo hiki hasa tukiangazia kwenye mambo muhimu kama,
1.Aina ya shamba(udongo)
2.Hali ya hewa
3.Vitendea kazi
4.Uchaguzi wa aina ya mbegu sahihi.
5.Utaalamu katika upandaji wa mbegu.
6.Changamoto za Ndege,wadudu na magugu korofi.
7.Virutubisho /Mbolea
8.Umwagiliaji (kama unahitajika)
9.Ulinzi wa shamba.
10.Uvunaji
11.Uhifadhi
12.Masoko.
Naamini kunawengi hapa jf wanajishughulisha au wanauelewa juu ya kilimo hiki.
Mnakaribishwa kuchangia.