Kilimo cha Alizeti (Sunflower): Masoko, Mbinu na Ushauri toka kwa wadau

Unataka kuwekeza mkoa gani? Kwa ufahamu wangu mimi alizeti ni zao bora sana ukiachana na swala la soko hata wewe mwenyewe unaweza ukazalisha mafuta kama kwa Dsm bei ya sasa dumu la lita tano ni elfu kumi na saba wewe wekeza kwa speed zote zao la alizeti ni zuri sana

asante sana mkuu kwa mawazo ya kunipa moyo sasa naona nguvu ya kuingia kwa miguu yote
 
Ahsante mkuu wangu, je zao hilo lahitaji pembejeo pia kama vile mbolea, madawa kupulizia ama nawezaje kulimudu?

ukitumia ile mbegu ya miezi mitatu, waweza kuweka mbolea aina ya DAP (nilitumia mimi kule isanza-mbozi-mbeya) na dawa za kupulizia wadudu ni muhimu sana.
 
ukitumia ile mbegu ya miezi mitatu, waweza kuweka mbolea aina ya DAP (nilitumia mimi kule isanza-mbozi-mbeya) na dawa za kupulizia wadudu ni muhimu sana.

Unaweza kutufafanulia hii mbegu? Nataka kulima Handeni vipi itamea?
 
Unaweza kutufafanulia hii mbegu? Nataka kulima Handeni vipi itamea?

Samahani nimeisahau kwa jina la hiyo mbegu, ila ukienda kwenye duka la pembejeo hasa haya ya serikali (maduka mengi ya kule mbeya yale ya watubinafsi, wanachakachua mbegu!) ulizia mbegu ya miezi mitatu ya tanzania na hasa ya makambako na ni nyeusi na ikiota na kukua huwa inatengeneza ua moja tu ingawa kuna hata ile ya kenya lakini mie nilishauriwa na wenyeji wangu kuwa nichukue ile ya tanzania-makambako ambayo ni ya miezi 3 au nitumie ya kienyeji ya miezi5-6 japo haina mafuta mengi

hii mbegu ya miezi mitatu ikikuwa haiendi juu, ni fupi ukilinganisha naile ya kienyeji, kwa usambara sifahamu vile cjafika huko lakini nachojua alizeti inastawi sehemu za joto na baridi (iringa, njombe, mbeya-mbozi na morogoro, mkuu jaribu kutathmini kwa wenyeji wa huko usambara watakupa mengi juu ya alizeti.

Pia hapa jukwaani kuna wakulima wazoefu sana na maarufu mimi bado ni 'junior' kwa kilimo na kwa zao hili, tunawaomba mje mtupe ABCs ya hili zao na mengineyo, asante.
 
Mkuu Matanzia na wengine;

Kitu muhimu sana kabla ya kujihusisha na kilimo cha zao lolote , zingatia yafuatayo

1) Kihistoria wenyeji wa eneo hilo huwa wanalima nini, wanatumia mbinu gani: Daima historia itakusaidia kukupa mwanga fulani.

2) Jua aina ya udongo uliopo eneo hilo na kama kuna mtaalamu wa soil karibu au afisa kilimo: hasa wilayani omba ushauri wa aina gani ya zao ni best in that location

3) Kwa nchi yetu -- Alizeti ni zao linalokubali maeneo mengi haswa yenye jua kali (Mid arid --) kama singida, dodoma, Lindi, Pwani ( Japo hii haimaanishi pwani yote au singida yote - tunarudi pale namba 2 kwenye ushauri wa afisa kilimo juu ya aina ya udongo )

4) Ukiamua kulima alizeti : Pata tena ushauri kuwa ni mbegu gani yafaa kwa eneo hilo; Angalizo : Usije ona rafiki yako katumia hybrid arpicot daisy sunflower seeds kule tanga na ikakubali basi wewe wa morogoro ukachukua hiyo ukapanda- la hasha. kila seed type inaendana na eneo, udongo, hali ya hewa na wingi wa mvua wa sehemu hiyo.

5) Aina ya mbolea: Wengine hutumia CAN, SA depending on soil type.

6) Dawa; Kutegemea na wadudu wa eneo hilo wanaoshambulia alizeti: Mtaalam wa kilimo atakushauri aina ya dawa na kipimo. Maeneo mengine hayana kabisa viwavi wala magugu tegemezi (parasitic plants yanayonyonya virutubishi) . Pia kuwa makini na ndege wanaharidu mbegu pindi inapochanua.


Katika yote- Spend more time planning and implementation itakuwa rahisi. Ukilima kisasa na kuzingatia ushauri wa wataalamu utavuna gunia 15-20 kwa hekari moja. All the best
 
Za asubuhi wapendwa:

Maisha yamekuwa magumu nikaona njia ya kujikwamua ni kilimo tu.
Miezi kadhaa iliyopita nilinunua ekari5 huko mpanda mwenyeji wangu akaniambia kilimo cha maharage na lizeti kinalipa sana kule.
Mwezi huku nimeshalima tayari kwa kupanda,kabla cjaanza labda ningependa kupata ujuzi toka kwenu?

Je?Ekari moja hutoa kiasi gani cha maharage?na kilo ni shs ngap?

Je? wadudu gani hushambulia mazao hayo na dawa yake ni ipi?

nikihitaji elimu ama kipeperushi kuhusu kilimo hichi niende wap?

Ni hayo tu..
 
ngoja wajuzi waje, mwenyewe nnampango wa kulima alizeti mwakani.
 
alizeti mi nimeona singida inatoa gunia saba hadi kumi na mbili mvua ikiwa vizuri na ardhi yenye rutuba sijajua huko mpanda hali ikoje jaribu kufanya utafiti kwa wenyeji wa huko mpanda ili ujue
 
Kwa maharage ekari moja hutoa magunia 5 hadi 6 kwa wastani wa gunia la kilo 100 na kilo moja ni Tsh.1100 -1400/= na wadudu wapo lakini si wakutisha umwone Afisa Ugani wa eneo hilo.
 
Mimi nataka kuwa nanunua crude oil singida then naileta dar kwa refinery je machine za kurefinery mafuta ya alizeti zinapatikana wapi?
 
Mashine zinapatikana sido na kwa wahindi. Nimemnunulia mjombangu mashine moja kwa milioni nane pamoja na filter ina mabomba kumi na mbili. Igembe Nsabo nisaidie, Unauza lita ishirini za mafuta kwa bei gani. Nadhani bei ya shilingi 2,500 kwa lita itakupa shilingi elfu hamsini kwa lita 20. Naogopa kidogo, Kuhusu kulima wengi wanalima kwa njia za asili. Ukilima kitaalam, utapata tani nne za alizeti kwa ekari moja. Huende ukishirikisha wataalaam utalima kwa faida. Mimi nimefanya utafiti wa kilimo cha mpungu cha umwagiliaji. Ekari moja gharama yote ni shs 300,000. Mavuno ni magunia 40 minimum. Una uhakika wa kuuza shs 2,500,000 kwa ekari moja. Kilimo ni ukombozi ni vizuri tunaopenda kilimo tulime sehemu moja ili kupunguza gharama. Tuchangie gharama za mtaalam, gharama za kusafirisha pembejeo na hata usafiri wetu wa kwenda na kurudi shamba.
Samahani,

Umesema kilimo cha mpungu ama mpunga?

Pia umesema kwa heka ni laki ama?..hii ni pamoja na kukodi shamba?..Kama sio pamoja na shamba Ukijumlisha na cost za kukodi itafika shiling ngap??
Pia haya maeneo yanapatikana wp??
 
Samahani,

Umesema kilimo cha mpungu ama mpunga?

Pia umesema kwa heka ni laki ama?..hii ni pamoja na kukodi shamba?..Kama sio pamoja na shamba Ukijumlisha na cost za kukodi itafika shiling ngap??
Pia haya maeneo yanapatikana wp??

Ni Mpunga. Gharama zote ni takribani shs laki 8 kama itahusu irrigation. Hii itajumuisha kukodi shamba, kulima, mbegu, kupanda, kupiga hallow, palizi, maji, mbolea, gharama za meneja atakayelisimamia shamba, kuvuna. Matarajio ya mavuni ni magunia 40 ya mpunga.
 
Asalaaam wanaJF, nimetafuta jukwaa la Kilimo sijaliona, nadhani hata hapa sijakosea jukwaa, nataka kuanza kilimo cha alizeti, ningependa kupata elimu kidogo juu ya kilimo hiki, hali ya hewa inayohitajika, madawa, upandaji na mengine mengine juu ya zao hili. Natanguliza shukrani zangu za dhati kwenu nyote.
 
Kilimo cha Alzet kina hitaji mvua za wastan na kipindi cha kuvua kinahitaji jua.

Hk 1 hutoa gunia 7-12.

Gunia 1 lina uzito wa kg 65-70.
 
Back
Top Bottom