Kilimo cha Alizeti (Sunflower): Masoko, Mbinu na Ushauri toka kwa wadau

For anyone interested in Joint venture forces ......

mimi nina eneo lipo dar ambapo tayari kuna Factory building iliyo tayari .... inafaa kabisa kwa ajili ya kiwanda kidogo cha kukamulia mafuta ya alizeti au karanga ..... factory building ina floor area ya 98sqm ....

any experienced in this field or fresh to start can contact
 
  • Thanks
Reactions: SG8
Nimekuwa navutiwa sana na ukulima wa alizeti kama zao la biashara. Naomba mawazo ya mdau yeyote mwenye uzoefu na kilimo hiki na namna gani unaweza kupata faida; Masoko yanapatikanaje na pia je ni faida zaidi kulima alizeti na kuuza ama kulima na kukamua mafuta? Naleta hoja.

Mkuu mafuta ya alzeti yana Demand kubwa sana hata nje ya nchi, tatizo ni Quantity, kuna makampuni kibao ya nje huwa yanataka mafuta ya Alzeti ila wanataka tani za kufa mtu,

Alzeti ili upate faida ni lazima Ulime na kukamua mwenyewe, na ukiwa na kiwanda chako ni lazima ununue na za wengine, make hapo utauza MAFUTA NA MASHUDU
 
mwenye link ya mashine ya kukamua alizeti (oil mill) ya india naomba aniwekee tafadhali, probably ya kuagiza huko huko

======================

update

nimepata quotation ya hii machine from india ... !!!

8Ton Expeller-30hp-1.jpg Quotation

S.
No
ITEMS
UNIT PRICE
QTY
AMOUNT
1) a) 30 HP Double Chamber Expeller complete with long steam kettle with pulley set. Heavy duty inter Gear box, Shafts are Alloy Steel Made b) 30 HP Motor, c) 30HP Starters for above Motor. d) Main Switch e) Change over switch (Reverse and Forward) f) V' Belts Set
Note :Capacity of One Expeller is 7-8 Tons in 24 hours
15500.00
1 set
15500.00

hii bei iko juu sana wadau au ???????
 
LAT hiyo price ni USD sio? kwa capacity hiyo in 24hrs i think it's reasonable price. Vipi kuhusu export & import duty (range)?. Je hii machine ndio ile yenye pressing nzuri above 90%? je, siku hizi unaweza kununua kitu kutoka kwa muhindi na ukaamini kabisa ubora wake?
Ni vizuri kwenda mwenyewe kufanya utafiti huko babati kabla ya kuamua kununua, hata ukitumia laki 2 kwa utafiti si mbaya.
 
Narubongo ...Nakushukuru sana kwa mchango wako ....hili ni wazo ambalo hata mimi nilikuwa nalo kwamba nijitahidi kuwa na data ya aina tatu hivi za mashine tafauti especially kwenye maeneo makuu ya ukamuaji wa alizeti kama Babati na singda halafu nifanye comparison ya aina gani ni nzuri ...so far mashine za wahindi ndizo best kwa sasa hapa Tz ila sijajua ni brand gani ... wahindi wanaziuza mpaka 15M at 4tons capacity ... SIDO wanazo ila ndiyo nataka nifuatilie ... nimefuatilia za china ila sina records za matumizi yake hapa Tz, ila wanaonekana kuwa modern zaidi na kujaribu kuwa compatible zadi

Hawa wahindi nimewapigia simu wakajisifia sana na wameniambia wamesha supply over 50 pcs in Tz ... off course thats obvious wako kwenye biashara ... hiyo bei yes ni USD ....

kikubwa hapa najaribu kupata bottle filling,caping and labelling machine kutoka china ili niwe na superior quality of packaging ... pia nikiweza kupata refinery one equipemnt ili niwe na product nzuri

lets hope for the best

Labda KOMANDOO atanisadia aina ya mashine zinazopatikana babati ili niokoe usumbufu wa kwenda huko
 
For anyone interested in Joint venture forces ......

mimi nina eneo lipo dar ambapo tayari kuna Factory building iliyo tayari .... inafaa kabisa kwa ajili ya kiwanda kidogo cha kukamulia mafuta ya alizeti au karanga ..... factory building ina floor area ya 98sqm ....

any experienced in this field or fresh to start can contact

Mkuu eneo lako lipo mitaa gani
OTIS
 
Ktk hili la kutafuta mashine, naomba ikiwezekana kila aliye karibu na mashine hizi ajaribu kupata aina za mashine zilizopo hapo. Kutokea hapo tunaweza kupata aina za mashine zinazopendwa zaidi( hatimaye tutapata sifa/siri ya hizo mashine).

Nipendekeze kitu hapa, kama una-plan ya kuingia ktk usindikaji wa mazao kama alizeti/ufuta, ni vizuri kujua proper location za siku zijazo hasa kwa sisi tulio hapa Dar.

Naamini Chalinze/Mdaula/Moro surbubs/Lugoba/Mlandizi ni maeneo mwafaka ili kuwa karibu na wakulima.
 
Malila

maneno mazito sana haya na yaliyojaa tija ...natumaini ushauri huu utazingatiwa 100%

ahsante
 
Kaka cjajua kwanini kiwanda kiko Dar?Je ni kwa ajili ya uhakika wa umeme, soko la mafuta na mashudu ama nini? Vinginevyo nadhani ungepunguza pressure ya kusafirisha alizeti kwa kuestablish kiwanda wanapozalisha kisha ukasafirisha mashudu au mafuta...actually mashudu wanakuja wenyewe hapo hapo kiwandani. Wakati mnafikiria kuanzisha mafuta ya alizeti,ni vema kukumbuka suala la purification, mafuta haya yanapigwa madongo na wale waingizao mafuta toka nje kwa kuwa hadi sasa hakuna utaratibu mzuri wa kufanya purification.
For anyone interested in Joint venture forces ......

mimi nina eneo lipo dar ambapo tayari kuna Factory building iliyo tayari .... inafaa kabisa kwa ajili ya kiwanda kidogo cha kukamulia mafuta ya alizeti au karanga ..... factory building ina floor area ya 98sqm ....

any experienced in this field or fresh to start can contact
 
  • Thanks
Reactions: LAT
Kaka cjajua kwanini kiwanda kiko Dar?Je ni kwa ajili ya uhakika wa umeme, soko la mafuta na mashudu ama nini? Vinginevyo nadhani ungepunguza pressure ya kusafirisha alizeti kwa kuestablish kiwanda wanapozalisha kisha ukasafirisha mashudu au mafuta...actually mashudu wanakuja wenyewe hapo hapo kiwandani. Wakati mnafikiria kuanzisha mafuta ya alizeti,ni vema kukumbuka suala la purification, mafuta haya yanapigwa madongo na wale waingizao mafuta toka nje kwa kuwa hadi sasa hakuna utaratibu mzuri wa kufanya purification.

mkuu ... asante kwa changamoto .... study imeshafanyika na kuna haja sasa ya kufanya state of the art processing kwenye sehemu zenye soko direct .... hii inaitwa product placement .... pia cost benefit analysis imezingatiwa ... kusafirisha mafuta against kusafirisha raw material ya alizeti to dar ...angalia pia kusafirisha packaging material to the source point kama singida halafu uyarudishe tena kwenye soko Dar es salaam

pia zingatia au nisome kwenye post No. #45 ... nanukuu hapa chini

kikubwa hapa najaribu kupata bottle filling,caping and labelling machine kutoka china ili niwe na superior quality of packaging ... pia nikiweza kupata refinery one equipemnt ili niwe na product nzuri

lets hope for the best

Labda KOMANDOO atanisadia aina ya mashine zinazopatikana babati ili niokoe usumbufu wa kwenda huko
 
Mkuu nashukuru kwa mtazamo huu> Labda twende level ya pili. Why Dar? Je ni kwa kuwa unataka ku-export au ready market? Kama ni ready market ya Dar (achilia mbali kuexport) umejua consumption ya Dar ikoje? Labda nikupe changamoto nyingine. Wakati wakazi wa Dar wanakadiriwa kati ya 3.5-4milioni, nadhani ni nusu (au pungufu) tu ndo wanakula products(seedcake na mengine) za sunflower. Nilidhani unaweza kuwa na outward looking kwa kuangalia opportunities zilizoko kwa masoko ya Rwanda, Burundi, Uganda, Zambia na DRC ambazo ziko karibu na central Tz kuliko ilivyo Dar. Kwa nini nasema hivyo? Kwa sasa nipo Kibaigwa hapa Dodoma. Lakini unaweza kuangalia magari yanayopakia mahindi kuelekea Dar na Magari yanayopakia Unga kutoka Dar kurudi mikoa ya Kati!!!! Utashangaa...natamani mtu mmoja siku moja anifanyie uchambuzi wa kiuchumi nione hii. Hata mikoa ya Lindi na Mtwara hununua unga toka Dar, sasa najiuliza kwa nini serious investors wasiwekeze kwenye viwanda vya unga na good package hapa Dodoma badala ya kusafirisha kwenda Dar?
 
mkuu ... you have a good point .... why Dar ... yes mara nyingi tunaanza na sehemu zenye ready market or you can call it market potential ... both seed oil and seed cake then una expand kwa lengola kuwa umeshatengeneza a brand that is superior ... in either way ... by marketing tools and spread of product quality ... hivyo pia available resources zinaweza kuwa na factor inayoweza kufanya ukainvest at a particular location

mkuu nimeshangaa pia kuona bidhaa nyingi za kutengenezea poultry feeds zipo mikoa ya shinyanga,mwanza lakini vitu vyote vinasafirishwa dar halafu chakula cha mifugokinarudi tena mikoani ...very interesting

tupambane na yote ... changamoto zote zitafanya tufanikiwe ... hebu check bei ya alizeti kwasa mkuu utupatie data ....
 
ninajifunza kitu hapa. Kuongezea tu, Dar uhakika wa soko la vyote upo na kwa bei nzuri wakati ukitafuta soko la nje, pia usafiri toka huku ni mzuri tu. Kama final product unataka iwe juu fikiria kusafirisha mafuta toka Magugu, Babati, barabara mbaya unafika na madumu machafu. Na ndio hali hiyo sehemu nyingi zenye mazao. Pili watu mikoani na vijiji vinavyolima alizeti wana njia zao simple za kutumia kukamua mafuta hawatanunua mafuta yako. Na mwisho ni kuwa Dar karibu kila mkoa unaleta mazao hapa. Kwa hiyo tunapokea toka Manyara, Iringa hata Dodoma na Singida. Dar kuna uhakika wa umeme na good packaging kwani viwanda vingi vipo hapa. Mie naona kwa hali ilivyo sasa bora hapa Dar.
 
Mama Joe ... ahsante kwa ufafanuzi mzuri ... kwa hali halisi ya nchi yetu ... miundo mbinu na facilities nyingine kweli Dar es salaam inabaki kuwa ndiyo location inayofaa kwa uzalishaji ... kubwa kabisa ni nyenzo za distribution channel amabayo ni vyema iwe karibu na uzalishaji

jinsi biashara ilivyo na ukitaka ufanikiwe ni kujitahidi kwamba kama upo kwenye uzalishaji basi mpatie mdau mwingine kitengo cha distribution (wholesale) yaani utaondoa usumbufu mkubwa sana .... tatizo ni kwamba wazalishaji wengine wanataka wafanye kila kitu wenyewe ... azalishe , afanye distribution na hata retail sales afanye mwenyewe.... hii ni ngumu, unaweza ukamwachia mtu margin kidogo ili akufanyie sales wewe ukajikita na uzalishaji wenye viwango

kikubwa ninachokisoma hapa na hasa BUBE amechangia ni changamoto ya quality ya mafuta ya alizeti ....kusema ukweli mafuta yanayozalishwa sehemu nyingi kama manyara, singida n.k hayana ubora kwani mafuta haya ya alizeti baada ya kukamuliwa yanakuwa katika form ya crude oil au mafuta ghafi .... kwanza yanatakiwa yafanyiwe refinery (including purification) ili kuweza kupata bidhaa kamili ya mafuta ya kupikia .... utakapofanya refinery unaongeza uzalishaji pia ... atakayezalisha crude oil na kuiuza hivyo hivyo analoose almost 0.3 in 1.0 ukilinganisha na yule atakayefanya refinery process

pia mafuta ya alizeti yanakosa branding na packaging nzuri zenye kuvutia
 
asante LAT kwakweli mimi huwa ninashangaa watu wanawezaje kula haya mafuta mengi yana harufu sana. Naona tubadilike sasa tunapaswa kutengeneza vitu vyenye viwango vya juu na hii EAC la tutapoteza soko kwakuwa bidhaa za wenzetu zitakuwa juu.
 
Mma Joe .... nashukuru kwa kulizungumza hili ambalo ndilo muhimu kuliko yote katika processing ya Sunflower oil .... "Refinery" ... kuna refinery 1 & 2 .... hapo ndipo unapata mafuta halisi ... haya unayosema tunakula yanaharufu ni crude oil ... mafuta ghafi ..... with all this pottential in sunflower seed .... kuna opportunity kubwa sana ya kufanya vizuri katika soko la Afrika Mashariki kama tutajikita kwenye uzalishaji wa end products ... i mean quality product ingridients and best packaging and branding

lets hope for the best
 
Mkuu mafuta ya alzeti yana Demand kubwa sana hata nje ya nchi, tatizo ni Quantity, kuna makampuni kibao ya nje huwa yanataka mafuta ya Alzeti ila wanataka tani za kufa mtu,

Alzeti ili upate faida ni lazima Ulime na kukamua mwenyewe, na ukiwa na kiwanda chako ni lazima ununue na za wengine, make hapo utauza MAFUTA NA MASHUDU

Mkuu hapo kwenye red unaweza kunipa ufafanuzi kidogo....kama mimi nikiwa na kiwanda kuprocess hapa DSM na kununua alizeti toka kwa wakulima mikoani itanilipa?
 
Thanks LAT tukiweza kuvuka hii part ya refinery we are going to have a big market in this, pia wakamuaji wengi ni small industries na nadhani hawajali registration nor product names kila unayekutana naye anakwambia mafuta ya alizeti... mtu unaogopa from experience ya crude oil ulizokwishaletewa kwa jina hilihili.... nadhani inabidi tufuate mfano wa mafuta ya pamba Supa Ghee na Okay hadi leo ni products zenye ubora wa juu na wanastahili kuuza kwa bei zao juu na ktk supermarkets na sehemu nyingi Tanzania nzima, Utaje tu hilo jina mtu anajua unamaanisha mafuta gani.

Hivyo wazalishaji wa sunflower oil inabidi waanze kuwaaminisha wateja kuwa kwasasa wanatengeneza mafuta yenye ubora na wafanye hivyo hadi kuweza kulishika soko...sio tu kuwatishia watu mafuta mengine yana kemikali na cholestoral no.
 
Last edited by a moderator:
  • Thanks
Reactions: LAT
Back
Top Bottom