Kilimo cha Alizeti (Sunflower): Masoko, Mbinu na Ushauri toka kwa wadau

JamiiForums

JF Official Account
Nov 9, 2006
6,202
5,012
alizeti.png

Alizeti hulimwa kwa wingi katika mikoa ya Shinyanga, Singida, Dodoma, Iringa, Tabora, Morogoro, Ruvuma, Mbeya, Arusha, Manyara, na Rukwa. Zao hili hulimwa kwa ajili ya chakula na biashara.

MAMBO MUHIMU YA KUZINGATIA WAKATI WA UZALISHAJI

Kuchagua aina bora ya mbegu

- Chagua aina bora ya mbegu inayovumilia magonjwa, wadudu, inayotoa mazao mengi na kiwango kikubwa cha mafuta.
- Vilevile chagua aina ya mbegu ambayo hukomaa kwa wakati mmoja ili kurahisisha uvunaji.

KUWEKA MBOLEA
- Rutubisha udongo kwa kutumia mbolea za mboji na samadi ili kupata mazao mengi na bora.

KUDHIBITI WADUDU NA MAGONJWA
Alizeti hushambuliwa na magonjwa ya majani, mizizi na masuke ambayo husababisha upungufu wa mavuno. Hivyo ni muhimu kuyadhibiti ili kupata mavuno mengi na bora. Pia ndege hupunguza mavuno kwa kiasi cha asilimia 50 au zaidi. Njia ya kudhibiti ndege ni kwa kuwafukuza na kupanda mbegu zinazokomaa mapema.

MAANDALIZI KABLA YA KUVUNA;

UKAGUZI
Kagua shamba kuona kama alizeti imekomaa. Alizeti hukomaa kati ya miezi minne hadi sita tangu kupanda. Wakati huo punje huwa na unyevu wa asilimia 25. Ni muhimu kuvuna alizeti mapema ili kuepuka mashambulizi ya panya, mchwa na ndege waharibifu.

DALILI ZA ALIZETI ILIYOKOMAA
- Suke hubadilika rangi kutoka manjano na kuelekea kuwa nyeusi.
- Viuwa vya pembeni mwa suke hunyauka na hubadilika kutoka rangi ya manjano na kuwa ya kahawia.

UVUNAJI, UKAUSHAJI NA UBEBAJI
Vifaa vya kuvunia na kubebea kutoka shambani
- Kisu
- Vikapu
- Magunia
- Matenga Vifaa vya kukaushia
- Maturubai
- Mikeka
- Kichanja bora Vyombo vya usafiri kutoka shambani
- Matoroli
- Matela ya matrekta
- Mikokoteni ya kukokotwa na wanyama
- Magari KUVUNA Alizeti huvunwa kwa kutumia mikono ambapo suke hukatwa kwa kutumia kisu. Pia mashine (combine harvester) hutumika kuvunia alizeti katika nchi zinazolima alizeti kwa wingi. Masuke ya alizeti huwekwa kwenye vikapu ambavyo hutumika kusomba alizeti ndani ya shamba. Kisha alizeti hufungashwa kwenye magunia na kusafirishwa hadi nyumbani tayari kwa kukausha.

KUKAUSHA
Kuna hatua mbili za kukausha alizeti; kukausha masuke na kukausha mbegu za alizeti. Kukausha masuke
- Masuke hutandazwa kwenye kichanja bora katika kina kisichozidi sentimita 30 ili yaweze kukauka vizuri.
- Vilevile huweza kutandazwa kwenye maturubai, mikeka au sakafu safi.
- Lengo la hatua hii ni kukausha masuke ya alizeti ili kurahisisha upuraji. KUPURA Upuraji hufanyika baada ya kuhakikisha kuwa masuke ya alizeti yamekauka vizuri. Masuke ya alizeti hupurwa kwa kutumia mikono ambapo mbegu hutenganishwa kwa kupiga masuke taratibu kutumia mti. Ni muhimu kupiga masuke taratibu ili kuepuka kupasua mbegu
- Pura kwenye kichanja bora, maturubai au mikeka.

KUKAUSHA MBEGU
> Mbegu za alizeti hukaushwa juani kwa kutandazwa kwenye vichanja bora, maturubai, mikeka au sakafu safi.
> Tandaza mbegu katika kina kisichozidi sentimita 4 ili ziweze kukauka vizuri.
> Lengo la hatua hii ni kukausha mbegu baada ya kupura ili kufikia kiwango cha unyevu kinachotakiwa kwa hifadhi salama ambacho ni asilimia 8.

JINSI YA KUTAMBUA MBEGU ZILIZOKAUKA VIZURI
Kufikicha mbegu
> Mbegu zilizokauka maganda yake hutoka kwa urahisi zinapofikichwa. Kumimina kwenye chombo kama debe
> Mbegu zilizokauka hutoa mlio mkali zinapomiminwa kwenye vyombo hivyo.
> Mbegu zilizokauka hung'ara Kutumia kipima unyevu.
> Mbegu zilizokauka vizuri kipimo huonyesha asilimia 8

KUPEPETA NA KUPEMBUA
Kupepeta na kupembua hufanyika ili kuondoa takataka kama vile mawe, wadudu, mapepe, mbegu zilizooza au kupasuka. Mbegu za alizeti hupepetwa kwa kutumia ungo au mashine zinazoendeshwa kwa mkono, injini au umeme. Mashine hizi zina uwezo wa kupepeta na kupembua kilo 60 hadi 350 kwa saa kutegemea aina ya mashine na ukubwa wa mashine yenyewe

KUHIFADHI
Alizeti iliyopurwa huhifadhiwa katika hali ya kichele kwenye maghala bora, yaani vihenge, sailo au bini. Alizeti ya kuhifadhi kwenye maghala ya nyumba ifungashwe kwenye magunia na ipangwe kwenye chaga kwa kupishanisha. Ili kurahisisha kazi ya kukagua ghala, acha nafasi ya mita moja kutoka kwenye ukuta. Ziba sehemu zote za ghala ili kuzuia panya kuingia.

Panya hupenda sana kula punje za alizeti, na husababisha upungufu mkubwa wa punje ambao husababisha upotevu wa asilimia 30 kwa kipindi cha miezi mitatu ya hifadhi. Asilimia ya upotevu inaweza kuwa kubwa zaidi kutegemea idadi ya panya na upatikanaji wa vyakula vingine kwa wakati huo.

Matumizi ya Mbegu za Alizeti
Mbegu za alizeti hasa zenye mistari zinaweza kuliwa baada ya kukaangwa au kukaushwa. Pia zinatumika katika utengenezaji wa mikate. Mbegu za alizeti husindikwa kupata bidhaa ya mafuta.

KUSINDIKA MBEGU ZA ALIZETI KUPATA MAFUTA
Vifaa
> Mashine ya kukamua mafuta
> Chujio safi
> Ndoo
> Vifungashio
> Sufuria
> Mizani Malighafi
> Mbegu za alizeti
> Maji
> Chumvi

NJIA YA KUKAMUA MAFUTA
- Chagua mbegu bora za alizeti
- Zianike kwenye jua kwa muda wa saa 1 hadi 2
- Weka kwenye mashine ya kukamulia ya daraja au Ram
- Kamua mafuta
- Chuja mafuta kwa kitambaa au chujio safi
- Pima mafuta yaliyokamuliwa.
- Ongeza maji na chumvi. Katika lita 10 za mafuta weka lita moja ya maji na gramu 200 za chumvi.
- Weka mafuta kwenye chombo cha kuchemshia (sufuria)
- Chemsha hadi maji yote yaishe
- Sauti ya kuchemka ikiisha ni dalili kuwa maji yamekwisha.
- Ipua, acha yapoe, kisha chuja kwa kitambaa safi au chujio
- Fungasha kwenye vyombo safi na vikavu na vyenye mifuniko
- Weka lakiri na lebo
- Hifadhi kwenye sehemu safi, kavu na yenye mwanga hafifu.

MATUMIZI
Mafuta hutumika katika mapishi mbalimbali na yana virutubishi vifuatavyo:
- Mafuta gramu 100 Nguvu kilokalori 900
 
Nimekuwa navutiwa sana na ukulima wa alizeti kama zao la biashara.

Naomba mawazo ya mdau yeyote mwenye uzoefu na kilimo hiki na namna gani unaweza kupata faida; Masoko yanapatikanaje na pia je ni faida zaidi kulima alizeti na kuuza ama kulima na kukamua mafuta?

Naleta hoja.

=======
Majibu ya wadau:

(Soma makala hii pia > Kifahamu Kilimo cha Alizeti na Faida yake Kiuchumi kwa Mkulima na Taifa | Fikra Pevu )

Ni kweli mheshimiwa Kapuku: tarehe ya kupanda lazima ujue alizeti yako huchukua siku ngapi hadi kuvuna ili upande iweze kukomaa wakati kipindi cha mvua kimeshaisha. Alizeti ikikomaa huku mvua bado inanyesha vichwa vyake huoza.

Kuna imani kwamba alizeti iliyochelewa kupandwa huwa na mafuta mengi! Yawezekana ikawa na mafuta mengi kwa gunia moja lakini mavuno kwa shamba zima yakawa kidogo kiasi kwamba wingi wa mafuta kwenye hayo mavuno kidogo hauwezi kuzidi alizeti yenye mafuta kiasi lakini yenye mavuno makubwa.

Pamoja na kwamba alizeti inastahimili ukame lakini inahitaji mvua za kutosha pale zinapoweza kupatikana! Cha kuepuka ni isije ikakomaa huku mvua bado zinaendelea! Morogoro Mvua za kupandia alizeti ni za mwezi February mwishoni na mwezi wa March mwanzoni! Ukitaka alizeti yenye mafuta mengi panda mwezi wa April lakini utapata mavuno kidogo! Alizeti iliyositawi wastani wa mavuno ni magunia 15 ingawa wakulima wengi wanaishia gunia 8 hadi 10 tu kwa ekari moja.

Mikoa ya Arusha na Kilimanjaro walishaachana na mbegu ya aina ya Record siku nyingi, kuna alizeti fupi toka Kenya zinazaa sana na zina mafuta mengi. Pia kuna alizeti Hybrid nazo ni fupi na mambo yake ni makubwa! Kama umepania kujichimbia kwenye kilimo cha alizeti anzia na Record lakini ukipata fursa ya kuwasiliana na mikoa ya Kaskazini ulizia mbegu za kutoka Kenya utaona vitu vyake! Tanzania utafiti wetu unasua sua sana kiasi kwamba toka iwepo mbegu ya Record hawajatoa mbegu nyingine, Record imepitwa na muda, haina mavuno makubwa wala haina mafuta mengi kama mbegu maarufu ambazo zinapatikana mikoa ya Kaskazini!

Pia lazima ikumbukwe kuwa alizeti hukubali sana inapowekewa mbolea za kukuzia (Nitrogen) kama Urea, CAN, SA nk kulingana na aina yako ya udongo. Kwa hiyo kama ikitokea unaona zao lako halieleweki ujue rutuba haitoshi! Hebu fanya jaribio kidogo sehemu ndogo weka mbolea uone matokeo yake! Nchi zilizoendelea hawalimi mazao haya bila mbolea ili wapate kipato kikubwa! Pamoja na imani kwamba Morogoro ni nchi yenye rutuba zipo sehemu zingine ni choka mbaya tu unakuta mtu anavuna vichwa vya alizeti kama kichwa cha tochi ya Tiger mwee!! Wekeni mbolea!!

Nashukuru sana kwa hiyo topic naomba hata mie nichangie, Kilimo cha Alizeti sina uzoefu nacho ila ninachoweza kukusaidia tu ni uzoefu nilionao wa mwaka mmoja nikiendesha kiwanda cha kukamua mafuta ya alizeti hapa Dar es salaam.

Uzalishaji wa mbegu za alizeti kwa maeneo ya Iringa, Singida, Dodoma, n.k bado upo chini ukilinganisha ni demand ya mafuta yatokanayo na mimea ambayo yanakiwango kidogo cha LEHEMU (low level of cholestrol), ukiangalia mfano importation ya edible oil from indonesia, and other Asian country is almost 80% ya demand ya edible oil kwa nchi nzima, wakati mafuta haya yanakiwango kikubwa cha LEHEMU, na ukisoma machapisho (articles za PWC,World Bank na RLDC - ambazo zinaelezea Alizeti, utaona hiyo shortfall na kuwa inchi yetu inatumia fedha nyingi sana za kigeni kwenye ununuzi wa mafuta ghafi kutoka Asian country).

Ukitoa mafuta ya disel, petrol na mafuta ya taa, mafuta ghafi ya kula yanachukua nafasi ya pili kwa kutumia fedha za kigeni kwenye uagizaji wake nje ya nchi.

Hivyo basi demand ya mbegu kwa viwanda vidogo vidogo na vikubwa vya kukamua mafuta hayo ni kubwa na inasababisha kuwepo na shortage ya hizo mbengu. Mfano mwaka huu ngunia moja la kg 65-70 kwa sasa linauzwa kati ya Tsh36,000/= hadi 45,000/=(the current price is 45,000 - 60,000 per kg January 2011)) kutegemea na eneo wakati huo huo kwa mwaka jana ngunia hilo hilo liliweza kuuzwa kwa Tsh 22,000/= hadi 35,000/= kwa kipindi hicho hicho.

Point nayotaka ku-raise hapa ni kuwa ongezeko kubwa la viwanda vidogo vidogo limeongeza demand ya mbegu, na awareness ya watu kuhusu mafuta yenye kiwango kidogo cha LEHEMU imesababisha kuwepo na demand ya mafuta hayo.
Kwa mantiki hiyo basi kama unataka kulima kilimo cha KIBEPARI na cha KISASA kwa kuangalia ile opened window kwa ajili ya KILIMO KWANZA, that is a great opportunity, go for it!!!

My take: Ila kama tu unataka kwa ajili ya ku access ile mikopo ya TIB then upeleke pesa kwingine then i don't have any comment.

Mimi ni mdau naomba tushirikiane.
 
Nimekuwa navutiwa sana na ukulima wa alizeti kama zao la biashara. Naomba mawazo ya mdau yeyote mwenye uzoefu na kilimo hiki na namna gani unaweza kupata faida; Masoko yanapatikanaje na pia je ni faida zaidi kulima alizeti na kuuza ama kulima na kukamua mafuta? Naleta hoja.

1. Tafuta shamba
2. Lima
3. Mavuno hifadhi ghalani i.e usieze kwa walanguzi
4. Nunua mashine ya kukamua alizeti
5. Kamua alizeti zako
5. Uza mafuta nje ya nchi.
6. Pata faida
 
Alizeti ni zao zuri sana la biashara linalimwa sehemu nyingi nchini kwetu ila mimi najua Iringa inaongoza,pia Dodoma na Singida nako wanalima sana tu.

Ukipata shamba zuri ekari moja ya alizeti huweza kukupatia kati ya magunia5-10 kutegemeana na aina ya mbegu uliyotumia na pia namna shamba lako ulivyolihudumia.

Gunia moja la alizeti yaani madebe sita huweza kutoa lita 20 za mafuta baada ya kusafishwa,mafuta haya unaweza kuuza kati ya shilingi 28,000-36000 kwa ndoo ya lita 20,pia utaweza kuuza mashudu yako ya alizeti kwa wafugaji.

Ukiwa wewe ni mfanyabiashara mzuri na una mtaji mkubwa fuata ushauri wa ama kwa kununua mashine ya kukamua alizeti kwani ukiwa na mashine hii itakulipa zaidi kwani utauza product yako mwenyewe yenye label ya kiwanda chako,this is very common in Singida,Iringa and in Mpwapwa-Dodoma.

Kama mnataka mali mtayapata shambani, braza umesahau shairi hili la darasa la nne enzi zile?
 
Amoeba

Mwaka jana nilikwenda Singida mjini,kuna mtaa wa sido,kuna viwanda vidogo vidogo vingi sana vya kukamua alizeti.

Nilichojifunza ni kwamba si bei kubwa kumiliki mtambo wa kukamulia alizeti na pili ni kweli kulima alizeti ni mchezo hatari kama unalima kwa ajili ya kuuza. Ila ili upate faida,nunua wakati wa mavuno kisha hifadhi na baadae uza. Ndicho wanachofanya wengi. Jitahidi uwe na lebel ya kazi zako.

Sikuishia mjini,nilikwenda mpaka Mtinko vijijini huko,nikagundua wakulima wanaibiwa kinoma. Ila kama unakamua na kuuza inalipa sana. Mwaka jana soko la alizeti mitaa ya Chalinze kwenda mto wami lilikuwa baya sana kwa wakulima ila kwa wafanyabiashara lilikuwa poa ile mbaya.
 
Last edited by a moderator:
Mwaka jana nilikwenda singida mjini,kuna mtaa wa sido,kuna viwanda vidogo vidogo vingi sana vya kukamua alizeti. Nilichojifunza ni kwamba si bei kubwa kumiliki mtambo wa kukamulia alizeti na pili ni kweli kulima alizeti ni mchezo hatari kama unalima kwa ajili ya kuuza. Ila ili upate faida,nunua wakati wa mavuno kisha hifadhi na baadae uza. Ndicho wanachofanya wengi. Jitahidi uwe na lebel ya kazi zako.

Sikuishia mjini,nilikwenda mpaka Mtinko vijijini huko,nikagundua wakulima wanaibiwa kinoma. Ila kama unakamua na kuuza inalipa sana. Mwaka jana soko la alizeti mitaa ya Chalinze kwenda mto wami lilikuwa baya sana kwa wakulima ila kwa wafanyabiashara lilikuwa poa ile mbaya.

Asante Malila,

Je mashine za kukamulia mafuta ya alizeti zinapatikana wapi hapa nchini? Au ni mpaka kuagiza nje ya nchi? Na zinahitajika shilingi ngapi ili kununu mashine moja?

Mimi nina shamba pia ambalo nina mpango wa kuanza kulima alizeti hizi karibuni. Najua soko la mafuta ya alizeti lipo kote kwenye ukanda huu wa Afrika ya Mashariki na kati!
 
Nakushauri usilime alizeti kwasababu bei yake iko chini sana,labda ukamue mwenyewe itakulipa.nilishawahi kulima alizeti mwaka juzi ilibidi ninunue mashine SIDO ili kukwepa kulaliwa na wafanya biashara waliokuwa wananunua kwa bei ya chini sana.
 
Kwa maneno mengine ni bora hizo pesa za kulimia alizeti zitumike kununulia mashine ya kukamua mafuta hayo, kisha kukusanay mazao toka kwa wakulima wa alizeti na kuyakamua?
 
Kwa maneno mengine ni bora hizo pesa za kulimia alizeti zitumike kununulia mashine ya kukamua mafuta hayo, kisha kukusanay mazao toka kwa wakulima wa alizeti na kuyakamua?

Ni kweli kabisa masaki, kulima kwa kutegemea kudra za Mungu mvua inyeshe, wadudu wasishambulie, wezi wasiingie kuanza kuvuna kabla wewe huvuna n.k n.k.

Kwa kweli ukulima kwa ujuma ni adha, na si adha tu lakini ni risk kubwa sana kwa mtaji wako. kwa uzoefu mdogo nilionao kupitia watu wa karibu wanaofanya biahsara hizi wanasema ni bora wakusanye pesa za kutosha, kununua alizeti msimu wa mavuno kwa wingi na bei huwa rahisi, then ukamue mwenyewe mafuta na pia unaweza ukauza akiba uliyokusanya msimu ambao zinahitajika kwa bei nzuri inalipa kuliko kulima mwenyewe.

The same applies to mpunga/mchele hasa maeneo ya ifakara ambako wachuuzi hupata faida kubwa kuliko wakulima.
 
ni kweli kabisa masaki, kulima kwa kutegemea kudra za mungu mvua inyeshe, wadudu wasishambulie, wezi wasiingie kuanza kuvuna kabla wewe huvuna n.k n.k. kwa kweli ukulima kwa ujuma ni adha, na si adha tu lakini ni risk kubwa sana kwa mtaji wako. kwa uzoefu mdogo nilionao kupitia watu wa karibu wanaofanya biahsara hizi wanasema ni bora wakusanye pesa za kutosha, kununua alizeti msimu wa mavuno kwa wingi na bei huwa rahisi, then ukamue mwenyewe mafuta na pia unaweza ukauza akiba uliyokusanya msimu ambao zinahitajika kwa bei nzuri inalipa kuliko kulima mwenyewe. The same applies to mpunga/mchele hasa maeneo ya ifakara ambako wachuuzi hupata faida kubwa kuliko wakulima.

Asante muhanga kwa ushauri wako mzuri. Akili yangu mwaka huu ipo kwenye kilimo, tena chenye tija! Ngoja nifanye utafiti binafsi katika hili ili nijue nini cha kufanya kwenye shamba langu. Nina kipande kikubwa cha ardhi na ninataka kukiendesha kibepari zaidi.

Juzi nimeona mjasiriamali mmoja kaanzisha ''yard'' ya kuuza matrekta yaliyotumika pale karibu ba Morocco. Amenivutia sana, maana mwaka huu 2010 KILIMO KWANZA!! :)
 
Nimewasikia na nimewakubali; sasa tuleteeni bei ya mashine ya kukamulia alizeti; na ukitaka ifanye kazi vizuri iwe na capacity gani na iweze kukamua magunia mangapi kwa siku?
 
Asante muhanga kwa ushauri wako mzuri. Akili yangu mwaka huu ipo kwenye kilimo, tena chenye tija! Ngoja nifanye utafiti binafsi katika hili ili nijue nini cha kufanya kwenye shamba langu. Nina kipande kikubwa cha ardhi na ninataka kukiendesha kibepari zaidi.

Juzi nimeona mjasiriamali mmoja kaanzisha ''yard'' ya kuuza matrekta yaliyotumika pale karibu ba Morocco. Amenivutia sana, maana mwaka huu 2010 KILIMO KWANZA!! :)

Hapo pekundu naomba unifafanulie, kuendesha kilimo kibebari ni kupi huko?
 
Asalaam aleikum, nimevutiwa na mjadala mzuri unaoonyesha ni jinsi gani wapo wajasiriamali wa kibongo wanavyojitahidi kuukimbia umasikini japokuwa kwa upande wa sehemu kubwa ya sera ya kilimo kwa bongo yetu imebaki siasa tu, wakati dunia zilizotangulia uchumi unaisukuma siasa, kwetu sie siasa ndo inasukuma uchumi, ee mola tujalie tufike salama.

Narudi kenye hoja yetu ya msingi mie mkulima mdogo, ni wapi zilipo mashine za kukamulia alizeti, japo tukafanye window shopping tukisubiri kuvuna?
 
Aleykumusalaam, Mkulima Mdogo. Nafikiri unaweza kutengeneza mafuta ya alizeti kwa mkono nyumbani. Gonga hapa ili wakuonyeshe Oil Press . au tembelea hapa Oilseed Processing for Small-Scale Producers http://www.youtube.com/watch?v=fTVe2LU4J0o . Ukikwama, tafadhali rudi hapa jamvini. Kilimo ndio uti wa mgongo. Halafu kwa wajasirimali, Gentlemen, kilimo ni biashara imara. Lamuhimu katika biashara yoyete ni kuplani, plani, plani. Wanasema usipoplani, plani yako ni kuporomoka.
 
Nashukuru sana kwa hiyo topic naomba hata mie nichangie, Kilimo cha Alizeti sina uzoefu nacho ila ninachoweza kukusaidia tu ni uzoefu nilionao wa mwaka mmoja nikiendesha kiwanda cha kukamua mafuta ya alizeti hapa Dar es salaam.

Uzalishaji wa mbegu za alizeti kwa maeneo ya Iringa, Singida, Dodoma, n.k bado upo chini ukilinganisha ni demand ya mafuta yatokanayo na mimea ambayo yanakiwango kidogo cha LEHEMU (low level of cholestrol), ukiangalia mfano importation ya edible oil from indonesia, and other Asian country is almost 80% ya demand ya edible oil kwa nchi nzima, wakati mafuta haya yanakiwango kikubwa cha LEHEMU, na ukisoma machapisho (articles za PWC,World Bank na RLDC - ambazo zinaelezea Alizeti, utaona hiyo shortfall na kuwa inchi yetu inatumia fedha nyingi sana za kigeni kwenye ununuzi wa mafuta ghafi kutoka Asian country).

Ukitoa mafuta ya disel, petrol na mafuta ya taa, mafuta ghafi ya kula yanachukua nafasi ya pili kwa kutumia fedha za kigeni kwenye uagizaji wake nje ya nchi.

Hivyo basi demand ya mbegu kwa viwanda vidogo vidogo na vikubwa vya kukamua mafuta hayo ni kubwa na inasababisha kuwepo na shortage ya hizo mbengu. Mfano mwaka huu ngunia moja la kg 65-70 kwa sasa linauzwa kati ya Tsh36,000/= hadi 45,000/=(the current price is 45,000 - 60,000 per kg January 2011)) kutegemea na eneo wakati huo huo kwa mwaka jana ngunia hilo hilo liliweza kuuzwa kwa Tsh 22,000/= hadi 35,000/= kwa kipindi hicho hicho.

Point nayotaka ku-raise hapa ni kuwa ongezeko kubwa la viwanda vidogo vidogo limeongeza demand ya mbegu, na awareness ya watu kuhusu mafuta yenye kiwango kidogo cha LEHEMU imesababisha kuwepo na demand ya mafuta hayo.
Kwa mantiki hiyo basi kama unataka kulima kilimo cha KIBEPARI na cha KISASA kwa kuangalia ile opened window kwa ajili ya KILIMO KWANZA, that is a great opportunity, go for it!!!

My take: Ila kama tu unataka kwa ajili ya ku access ile mikopo ya TIB then upeleke pesa kwingine then i don't have any comment.

Mimi ni mdau naomba tushirikiane.
 
Aleykumusalaam, Mkulima Mdogo. Nafikiri unaweza kutengeneza mafuta ya alizeti kwa mkono nyumbani. Gonga hapa ili wakuonyeshe Oil Press . au tembelea hapa Oilseed Processing for Small-Scale Producers http://www.youtube.com/watch?v=fTVe2LU4J0o . Ukikwama, tafadhali rudi hapa jamvini. Kilimo ndio uti wa mgongo. Halafu kwa wajasirimali, Gentlemen, kilimo ni biashara imara. Lamuhimu katika biashara yoyete ni kuplani, plani, plani. Wanasema usipoplani, plani yako ni kuporomoka.
Thanks. Lakini hiyo mashine inayoonekana youtube ni kitchen type, very small scale kwa matumizi ya nyumbani.
 
Mashine zinapatikana SIDO, Kwa order maalumu. kuna oil expeller 3ml hadi 4ml. kuna chekeche 1,500,000. kuna filter 3ml. Unaweza kununua pamoja na refinery 3ml.
Je hizi ni bora kuliko wnazouza wahindi made in china-naona wanaziita kwa number tu e.g number 95, complete na motor ya 20HP,chekeche na filter kwa 4.5M complete set? hii ni refinery ni nini?
 
Back
Top Bottom