Bei ya vitunguu yazidi kupanda na hivyo kuzidi kuwanufaisha wakulima. Mwezi August na September 2011 bei ya vitunguu ilikuwa ni kati ya TZS 55,000 - TZS 60,000 kwa gunia. Mwezi huu wa November bei imepanda na kufikia TZS 85,000 - TZS 90,000 kwa gunia. Nchi zinazonunua bidhaa hiyo kwa wingi zimetajwa kuwa ni kenya, msumbiji, madagascar na Comoro.

Hongereni wakulima wa vitunguu!

Source: ITV taarifa ya habari za biashara

At least leo nimesoma habari tofauti na zile nilizozoea kuzisoma. Hii ikipigiwa debe kubwa inaweza kuwasaidia wale ndugu zangu wanaolima vitunguu vijijini kuamka na kuchangamkia biashara. Tuwaache wanasiasa waendelee kuvuana magamba kadri wanavyoweza.
 
Nang'ola iko wapi?
Ekari moja wanakodisha sh. ngapi kwa msimu/ kwa mwaka?
Unaweza kupata maximum ekari ngapi?
Gharama ya kulima na kutunza ekari moja ni sh. ngapi>
Ekari moja inatoa gunia ngapi? Minimum na maximum?
Huko Mang'ola gunia moja mnauza bei gani?
Mtu anaweza kununua gunia 250 kwa siku ngapi?

Iko Arusha - Karatu
Ekari inategemea eneo na msimu na ni kati ya 180,000 -250,000 hivi
Mavuno yanategemea matunzo, mbegu na kama mvua haitakuua, pia wadudu. Siwezi kutoa estimate hapa ila gunia 100 ni possible hata zaidi
Ekari moja ni "jaruba" 250 hivi, utahitaji angalua 2 mil. za matunzo.
Bei inategemea nyie wa mjini, demand and supply. Huwezi kuhifadhi kwa zaidi ya miezi 4 hivi.
Kupata gunia hata 1000 inategemea na hali ya msimu na hali ya soko, kwa gunia 250 utahitaji hadi siku tatu hivi.
 
Duu, mkuu kama ni msaada hii sasa imezidi! Yaani unataka kutengeneza mchanganuo moja kwa moja tena bureeee bila hata kulipia consultancy fee. hata kama msaada hii sasa imezidi. Nna wasiwasi kama wewe ni mkulima/mfanyabiashara maana ni kama huna ujualo completely!

Sharing is caring, karibu JF
 
Nang'ola iko wapi?
Ekari moja wanakodisha sh. ngapi kwa msimu/ kwa mwaka?
Unaweza kupata maximum ekari ngapi?
Gharama ya kulima na kutunza ekari moja ni sh. ngapi>
Ekari moja inatoa gunia ngapi? Minimum na maximum?
Huko Mang'ola gunia moja mnauza bei gani?
Mtu anaweza kununua gunia 250 kwa siku ngapi?[/QU

Duu, mkuu kama ni msaada hii sasa imezidi! Yaani unataka kutengeneza mchanganuo moja kwa moja tena bureeee bila hata kulipia consultancy fee. hata kama msaada hii sasa imezidi. Nna wasiwasi kama wewe ni mkulima/mfanyabiashara maana ni kama huna ujualo completely!

Huyo ndiyo mfanyabiashara/ mwekezaji wa karne ya 21. Majibu ya hayo maswali hapo juu yanaweza kutolewa na mtu 1. Yule anayefanya kilimo kama Biashara na sio yule anayefanya kilimo ili azalishe chakula cha kujikimu halafu ziada auze akanunue mahtaji madogo madogo. Kilimo hcho kimeptwa na wakati, Mapinduzi ya kijani yatakuja kama tutawekeza ktk kilimo, kama tutafanya kilimo cha biashara, kama tutajiuliza maswali kama ya Che na mengneyo kabla ya kuwekeza (ktk kilimo chetu)
 
Apa kuna akili sana, vitunguu mara nyungi vinakubali sehemu mbalimbali jaribu mahala popote ata matuta mawili ivi, nunua miche iliyokwisha oteshwa weka mboji nyingi. alafu shida yake ni utunzaji baada ya kuvuna.
 
Mwezi wa 9 mwaka huu nilikuwa pale Tarakea border ya Tz na kenya ambayo ndiyo border post kubwa kuliko zote Afrika mashariki kwa upande wa kenya, niliona takriban fuso nane zinapita kwenda kenya from Tz zikiwa zimepakia vitunguu aina ya 'red bombay' wamepack 15kg kwenye mesh bags

Niliuliza bei nikaambiwa na dereva kuwa hata wao hawamjui mteja

Hivi vitunguu vinastawi sana moshi maeneo ya chekereni na uwanda wa lower moshi, mandaka n.k, one acre yield 60 - 90 bags (appr. 100kg bag) almost up to two or three seasons

Vijana wengi sasa hivi wapo safi kwa kilimo hiki
 
Apa kuna akili sana, vitunguu mara nyungi vinakubali sehemu mbalimbali jaribu mahala popote ata matuta mawili ivi, nunua miche iliyokwisha oteshwa weka mboji nyingi. alafu shida yake ni utunzaji baada ya kuvuna.

Hata Dodoma vinakubali. Nimejribu kwa ajili ya kula sasa najipanga zaidi, changamoto ya Dodoma ni maji ya kutosha!
 
hongera sana mkuu, niliwahi tembelea dodoma maeneo ya mpwapwa kijiji kimoja kinaitwa kitati. Wanalima sana vitunguu na karanga.......tatizo lipo kwenye usafiri, kwani barabara ni mbovu sana. Pia kuna eneo lipo mpakani mwa dodoma na morogoro kilosa ...linaitwa lumuma, kitunguu kinastawi sana. Napanga kwenda huko mwezi december Mungu akinijaalia uzima.
Hata Dodoma vinakubali........................nimejribu kwa ajili ya kula sasa najipanga zaidi, changamoto ya Dodoma ni maji ya kutosha!
 
Wadau naombeni ushauri wa kulima kitunguu kwa yoyote mwenye uzoefu na hiki kilimo. Napenda nijue mahitaji na gharama kwa heka 1
 

Attachments

  • kilimo cha vitunguu.pdf
    375.9 KB · Views: 1,781
Wadau naombeni ushauri wa kulima kitunguu kwa yoyote mwenye uzoefu na hiki kilimo.napenda nijue mahitaji na gharama kwa heka 1

Pamoja na kupitia link hizo hapo juu, kuna mtu mmoja kama sijakosea anaitwa Njowepo, yuko humu jamvini, kuna wakati alikuwa analima pale mahenge wilayani Kilolo Iringa, Mpe-PM anaweza kukupa majibu.
 
Kinalipa. Heka Moja ni wastani wa 1 million mpaka unavuna. Kinahitaji maji na uangalizi wa karibu. Msimu nao ni wa kuzingatia ili uvune wa kati demand ni kubwa kama mwaka huu Jan/Feb.

binafsi nimepoteza million 6 katika kilimo cha kitunguu. huko Maeneo ya Marwa Same. Mto Ruvu unapoanzia. Wadudu wa ajabu walishambulia mara baada ya kuhamisha baada ya mbegu kukua. Nilisia hapo hapo shambani. mbegu ikaota vizuri sana. nilipopanda baada ya wiki 2 ikaharibika.
 
Natarajia desember tuwe na trip mbili za Iringa, ya mwisho itakuwa baada ya x-mass hivi,naamini hii utashiriki mkuu. Nitakuwa na vijana wa jf baadhi.

Mkuu hizi Trip au ushirikiano huu wa wana jf unakuaje ,nijuze mkuu maana ugeni wa jukwaa hili nadhani unachangia,nitashukuru pia (ngataabel@yahoo.com )
 
Mkuu hizi Trip au ushirikiano huu wa wana jf unakuaje ,nijuze mkuu maana ugeni wa jukwaa hili nadhani unachangia,nitashukuru pia (ngataabel@yahoo.com )

baadhi ya jf members tunafanya projects zetu pamoja lakini kila mtu anamiliki kivyake. Unakuta kwa mfano huko kwenu Iringa tunawekeza pamoja kila mtu kwa kadri ya uwezo alio nao. Lakini kuna mambo tunashirikiana ili kupunguza gharama fulani fulani.

Na sio kwenu tu, hata huku Pwani pia tunashirikiana ktk miradi mingine. Nakuletea mail.
 
wakuu nilikuwa na-review hii thread, nikaona jinsi wazee mlivyomwaga nondo. sasa kwa wanaofahamu vizuri kilimo cha vitunguu. Je vitunguu vinakubali ardhi ya mkuranga na Bagamoyo? hasa ukichukulia case ambapo kuna mto usiokauka... au vinalimwa sehemu zenye ubaridi kama Iringa?- au kikubwa ni maji ya kumwagilia. nitashukuru kwa taarifa!!


Kanyagio brother. Nitwangie kwa namba yangu tafadhali.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom