Ushauri wa kanuni bora za kilimo cha Migomba na Soko lake

AMARIDONG

JF-Expert Member
Jun 24, 2010
2,502
180
MIGOMBA - KANUNI ZA KILIMO BORA

Hapa Tanzania kilimo cha migomba kimekuwepo Kwa miaka mingi. Kilimo hiki ni maarufu sana kwa sababu zao la ndizi limekuwa likitumika kama chakula kikuu kwa baadhi ya mikoa kama vile Kagera, Kilimanjaro na Mbeya na hivyo kulifanya muhimu, kufuatia mazao ya mahindi, mpunga, mtama, muhogo,viazi na mazao ya jamii ya kunde kama vile maharage.

Zao la ndizi linaweza kuwa moja kati ya mazao ya biashara iwapo litazalishwa kwa kufuata kanuni bora za uzalishaji wa zao hilo, ikwa ni pamoja na kupanda aina bora ya migomba inayozaa ndizi zinazotambulika katika masoko ya kimataifa.

ASILI YA MIGOMBA
Asili ya migomba ni nchi za Malaysia na India ambazo ziko Kusini Mashariki mwa Asia. Migomba inayolimwa sasa imetokana na migomba ijulikanayo kama Musa balbisiana ambayo asili yake ni India, na Musa acuminata ambayo asili yake ni Malaysia. Kutoka Malaysia na India migomba ilifika Afrika Mashariki katika karne ya tano

MAENEO YANAYOLIMWA MIGOMBA NCHINI

Nchini Tanzania mikoa inayoshughulika na kilimo cha migomba na kuzalisha zao la ndizi kwa wingi ni pamoja na Kagera, Kilimanjaro, Mbeya, Arusha, Manyara, Mara, Tanga, Morogoro, Kigoma, na Pwani. Hata hivyo zao hili linaendelea kuenea katika mkoa mingine nchini ikiwa ni pamoja na Dar es salaam,, Mwanza, Ruvuma, Shinyanga na Lindi. Pia Dodoma na Singida.
Kilimo cha migomba kinaweza kufanyika katika kipindi chote cha mwaka kulingana na kiasi na mtawanyiko wa mvua hasa mabondeni au kwa umwagiliaji.



MATUMIZI
Kilimo cha migomba kina faida nyingi, baadhi ya faida za migomba na
zao la ndizi ni: -
- Zao la chakula
- Zao la Biashara
- Kutengenezea pombe
- Kulisha mifugo
- Kutengenezea mbolea (mboji)
- Matandazwa shambani (mulch)
- Kutoa kivuli
- Kutoa nyuzi
- Kutengenezea vitu vya sanaa
- Kamba
- Malighafi ya kutengeneza vyakula na vinywaji mbalimbali.
- Dawa
- Majani kama miamvuli, sahani, vikombe na kata
- Kuezekea.

Ndizi kwa ajili ya chakula hutumika kwa kutengeneza vitu mbalimbali-:
1 - Makangale (Banana figs)
2 - Poda (Powder)
3 - Chenge (chips)
4 - Jeya (flakes),
5 - Juisi,
6 - Lahamu (jam)
7 - Vinywaji baridi, kama soda
8 - Mvinyo (Wine)
9 - Pombe kali
10 - Hamira

UZALISHAJI
Zao la ndizi likizalishwa kwa utaalamu unaokubalika huweza kutoa mazao yenye ubora wa hali ya juu na kuongeza uzalishaji kwa eneo. Mambo yafuatayo yafaa kuzingatiwa katika uzalishaji wa zao hili.

(a) Hali ya hewa
Kiasi cha chini cha mvua kifaacho ni 100mm kwa mwezi au 1200mm kwa mwaka. Mwinuko ni kutoka usawa wa bahari hadi mita 1800 juu ya usawa wa bahari. Zaidi ya mwinuko huo migomba haikui vizuri. Kiasi cha joto kinachofaa ni nyuzi joto za sentigredi 25 hadi 30 chini ya nyuzi joto 16 migomba haikui vizuri. Migomba hustawi vizuri kwenye udongo wenye rutuba ya kutosha, kina kirefu, usiotuamisha maji na pia usiwe na chumvi. Chachu ya udongo inafaa iwe kati ya pH 5 hadi 8.

(b) Aina za ndizi
Kuna aina nyigi sana za ndizi. Nchini Tanzania ndizi zinazozalishwa, zipo za aina nyingi ambazo hutofautiana kwa majina kutokana na eneo au mkoa unaozalisha. Hata hivyo zinaweza kugawanywa katika makundi mawili. Aina ambayo huliwa kwa kuzichoma, kukaanga au kupikwa zikichanganywa na vyakula vingine kama vile nyama. Aina za ndizi hizo ni pamoja na Mzuzu, Mshale, Matoke, Bokoboko na Mkono wa Tembo.
Aina nyingine ni zile ambazo huliwa kama matunda, aina hizo ni kama vile Kisukari, Kimalindi, Mzungu na Mtwike.

Kuna aina nyingine za ndizi ambazo kwa sasa huzalishwa hapa nchini ambazo zina fahamika kwa ubora wake katika masoko ya ndizi ya kimataifa. Aina hizi ni pamoja na Williams, Grand Naine, Pazz, Jamaica, Gold Finger, Nyingine ni Uganda green, Embwailuma Giant na Chinese Cavendish.



(c) Utayarishaji wa shamba
1 - Safisha sehemu inayohusika kwa kutumia zana ulizonazo.
2 - Ng’oa visiki vyote na mizizi yake yote
3 - Lima sehemu hiyo kwa kutumia jembe la mkono, rato, au trekta ili kuwezesha mizizi laini ya migomba kupenya ardhini kwa urahisi.
4 - Baada ya visiki na magugu yote kuondolewa na hivyo ardhi kuwa wazi, uchimbaji wa mashimo ya kupandikiza machipukizi au miche ya migomba unaweza kufanyika.

(d) Nafasi ya kuchimba mashimo
Mashimo yatachimbwa kwa nafasi inayokusudiwa kutumika kati ya
mashina ya migomba na kati ya mistari kama ifuatavyo:-
1 - Migomba inaweza kupandwa kwa nafasi ya Umbali wa meta
2.75 kwa 2.75 kwa migomba mifupi kama Kimalindi na
Kisukari. (Mashina 1,331 kwa hekta )
2 - Umbali wa meta 3 kwa meta 3 kwa migomba ya urefu wa kati
kama Jamaica na Mshale (Mashina 1,110 kwa hekta)
3 - Umbali wa meta 3.6 kwa meta 3.6 kwa migomba mirefu zaidi kama
Uganda green Mashina 760 kwa hekta).

(e) Uchimbaji mashimo.
Uchimbaji mashimo inafaa ufanywe mapema kiasi cha juma moja hadi mwezi kabla ya muda wa kupanda. Shimo lichimbwe kwa kutenganisha udongo wa juu na wa chini.

Vipimo vya shimo ni vyema vikazingatiwa. Iwapo utachimba shimo la mviringo litafaa liwe na kipenyo cha sentimeta 60 hadi 90 na kina cha sentimeta 60 hadi 90. Iwapo utachimba shimo la mstatili au mraba litakuwa na urefu, upana na kina cha sentimeta 60 hadi 90, kutegemea kiasi cha mbolea kilichopo na kiasi cha kvua kinachonyesha sehemu hiyo. Uwekaji wa mbolea hufuatia mara baada ya mashimo kuwa tayari. Kiasi cha madebe 5 ya mbolea ya samadi iliyooza vizuri au mboji iwekwe kwenye lundo la udongo wa juu kando ya kila shimo na ichanganywe kisha mchanganyiko wa mbolea na udongo urudishiwe katika shimo kisha kijiti kichomekwe katikati ya shimo hilo, ilikuonyesha sehemu ambapo mche au chipukizi litapandwa.

(f) Kuchagua machipukizi bora
Machipukizi mazuri yanayofaa kwa mbegu ni yale yenye sifa hizi hapa chini: -
Sifa za chipukizi bora
1 - Liwe chipukizi sime, yaani lenye majani membamba na siyo
chipukizi maji yaani lisiwe lenye majani mapana.
2 - Litoke kwenye mgomba (shina) wenye afya nzuri, usiokuwa na
magonjwa, minyoo ya mizizi, wala vifukusi vya migomba.
3 - Litoke kwenye mgomba wenye sifa ya kuzaa mikungu
mikubwa.
4 - Liwe na afya nzuri na lisiwe na dalili za ugonjwa, wadudu, au
mayai ya vifukusi.
5 - Urefu uwe kati ya meta 1 na meta 2
6 - Kipenyo cha sehemu ya chini ya shina la chipukizi (tunguu) kiwe ni kati ya sentimeta 15 hadi 25.

(g) Upandaji wa machipukizi
Wakati unaofaa kupanda machipukizi ni mwanzoni mwa msimu wa mvua. Chomoa kile kijiti na chimba shimo la kiasi cha sentimeta 30x30 katikati ya shimo lililojazwa mchanganyiko wa udongo na samadi kisha panda chipukizi hilo.

Rudishia udongo na hakikisha tunguu lote limefunikwa vizuri. Shindilia udongo ili chipukizi lisimame wima imara. Machipukizi yanayo tarajiwa kupandwa yanatakiwa kuondolewa mizizi yote ili kudhibiti minyoofundo na fukuzi wa migomba. Pia maji ya moto au dawa kama vile furadani inaweza kutumika kuulia wadudu kwenye mizizi ya migomba.

UTUNZAJI WA SHAMBA NA MIMEA.
(a) Uwekaji wa matandazwa (mulching
)
Kazi hii ni vyema ikafanywa mara baada ya kupanda kama inawezekana. Matandazo yawe ni makavu na unene wa sentimeta 15 ili kuhifadhi unyevu, kuzuia magugu na yakioza yataongeza mbolea.

(b) Uongezaji wa mbolea
Baada kupanda ni vyema kuongeza mbolea madebe 2 kuzunguuka shina la migomba kila baada ya miaka miwili au mitatu. Mbolea hii inatakiwa kuchanganywa na udongo na kufunikwa kwa matandazwa.

(c) Umwagiliaji maji shambani
Migomba huhitaji maji mengi. Wakati wa kiangazi. Inafaa kumwagilia ili kuto kupunguza sana ukubwa na wingi wa ndizi zinazotarajiwa kuvunwa kwa mwaka. Kiasi cha maji kinachotakiwa kwa wiki ni milimita 25, yaani eneo linalo zunguka shina la migomba lilowe kabisa.

(d) Kupunguzia machipukizi
Inatakiwa kupunguza mimea ya migomba kwa kila shina na kubaki mimea mitatu tu, yaani Mgomba wenye ndizi (Mama), Mgomba mkubwa ambao bado haujazaa lakini unakaribia kuchanua (Mtoto), Mgomba mchanga uliochipua hivi karibuni ( Mjukuu)

(e) Uondoaji wa Majani Makavu
Mimea ya migomba inafaa iondolewe majani yote makavu ili kuondoa uwezekano wa kuwepo mazalia ya wadudu na magonjwa, kuruhusu mionzi ya jua na kufanya urahisi wa kuhudumia shamba .Pia hufanya shamba kuonekana safi.

(f) Uondoaji wa ncha mwishoni mwa matunda
Baada ya mkungu kutoa ndizi, ua hunyauka na kubakiza ncha mwishoni mwa matunda. Ncha hizo hupaswa kuondolewa .Huduma hii husaidia kupunguza uwezekano wa kujeruhi matunda wakati wa kusafirisha jambo ambalo kupunguza ubora wa tunda.

(g) Kuweka Miega
Miega ni nguzo au kamba ambazo hutumika kuzuia migomba iliyobeba mikungu mikubwa isianguke kutokana na uzito mkubwa. Miega ni ya lazima katika sehemu zenye upepo mkali. Kazi hii inatakiwa kufanywa kwa uangalifu ili isijeruhi ndizi na mgomba wenyewe.




(h) Uondoaji wa kichombezo cha ua la kiume (Shumba)
Uondoaji wa shumba huwezesha matunda kukua vizuri, kuongezeka uzito wa mkungu pia huzuia magonjwa kama vile ugonjwa wa mnyauko wa migomba (Banana Baterial Wilt), ugonjwa wa Majivu nchani mwa matunda (Cigar end rot). Ukataji hufanyika juu ya kovu la pili baada ya kichana cha mwisho, kwa kutumia kisu kikali.

UVUNAJI
Zao la ndizi huweza kuanza kuvunwa katika kipindi cha miezi 9 hadi miezi 15 tangu kupandwa kwa chipukizi. Muda wa kuvunwa hutegemea hali ya hewa. Katika sehemu za joto ndizi huvunwa mapema zaidi kuliko sehemu za baridi. Pia migomba iliyopandwa kwa kutumia machipukizi huzaa mapema kuliko iliyopandwa miche iliyozalishwa kwa chupa (tissue culture)

MATUMIZI YA RIBONI

Riboni za rangi moja (au alama ya kamba) hufungwa kwenye migomba ya umri mmoja mara tu inapoanza kuchanua, na riboni ya rangi nyingine hufungwa kwenye migomba itakayoanza kuchanua wiki mbili hivi zinazofuata na kuendelea hivyo ili kurahisisha kuitambulisha mikungu ambayo itavunwa kwa wakati mmoja. Pia matumizi ya riboni hurahisiha utunzaji wa kumbukumbu ili kujua ni lini na ni mikungu mingapi itavunwa.

WAKATI UNAOFAA KUVUNA
Mkungu wa ndizi huweza kuvunwa katika hatua tofauti kulingana na matumizi, aina na mahitaji ya soko. Mkungu huachwa kwenye mgomba mpaka vidole (matunda ) vimejaa. Uzito wa mkungu hongezeka haraka katika wiki mbili za mwisho, ambapo migongo ya ndizi hutoweka.
Ndizi zinaweza kuvunwa zikiwa zimekomaa na zimeiva kwa kiasi cha asilimia 75 kwa ajili ya kusafirishwa mbali, pia zinaweza kuvunwa zikiwa kukomaa na zimeanza kuiva kwa ajili ya soko la karibu, au zikiwa zimekomaa na kuiva kabisa kwa ajili ya soko na matumizi ya nyumbani Njia bora ya kukata mkungu, ni ile inayohakikisha kuwa mkungu wa ndizi hauanguki chini na kuvunja, kuchubuan au kuharibu ndizi, jambo ambalo litapunguza ubora. Ukichelewa kuvuna ndizi zinaweza kuharibiwa na ndege, wanyama, wadudu au kuibiwa.

MKUNGU WA NDIZI AMBAO UMEONDOLEWA SHUMBA


UBORA WA NDIZI
Ndizi zenye sifa nzuri sokoni ni zile ambazo zimekomaa kwa kiasi kinachotakiwa na zenye vidole vyenye urefu mzuri na visivyo na michubuko. Pia ziwe hazijashambuliwa na magonjwa wala wadudu waharibifu.

KIASI CHA MAVUNO
Mavuno ya ndizi hutegemea zaidi aina ya migomba, hali ya hewa, utunzaji wa mimea shambani. Mavuno huweza kufikia hadi tani 60 au zaidi kwa hekta kwa mwaka. Hata hivyo mavuno mazuri kwa mkulima wa kawaida yasipungue kati ya tani 20 hadi 30 kwa hekta kwa mwaka.

MAGONJWA
Ugonjwa wa hatari sana ulioingia hivi karibuni katika wilaya ya Muleba na maeneo mengine mkoani Kagera kutoka nchi jirani ya Uganda ni wa Mnyauko wa migomba unaosababishwa na bakteria (Banana Bacterial Wilt). Magonjwa mengine yanayosumbua zao hili ni Kuoza tunguu, Ugonjwa wa panama, Ugonjwa wa majivu nchani mwa tunda, Sigatoka, na Moko.

WADUDU WAHARIBIFU
Wadudu wanaosumbua zaidi hili ni Minyoo fundo (Banana nematodes), na Vifukuzi (Banana weevils).

UDHIBITI WA MAGONJWA NA WADUDU WAHARIBIFU
Magonjwa na wadudu hawa huweza kuepukwa kwa kufuata kanuni bora za uzalishaji wa zao hili. kama usafi wa shamba na kuchagua chipukizi bora. Au kupanda miche iliyozalishwa kwa chupa (Tissue culture banana seedlings) Hata hivyo mara mataizo haya yakitokea muone mtaalam wa kilimo aliye karibu ili aweze kukupa ushauri wa dalili za ugonjwa wa mnyauko wa migomba unaosababishwa na bakteria
 
Mimi napenda kuangalia ukulima wa mazao mbalimbali. Kuhusu ndizi nikapata habari zilizonipendeza nikasema nishirikiane nanyi.

Ukipanda ndizi leo itachukua kati ya miezi kumi hadi kumi na mbili kuzaa mkungu. Pia itategemea hali ya maji maana ndizi zinahitaji maji mengi sana. Ukishuvuna mkungu huo mmea unaukata na itachukua miezi mingine kama hiyo kwa machipukizi ya ndizi kuvunwa.Kuvuna huku kunaweza endelea kwa miaka 25 hapo ndio mtu unaweza kutoa mimea yote na kuanza upya.Twende kwenye uzaaji.

Kwa wakulima wa kawaida ekari ya ndizi huzaa tani 7 za ndizi ambazo ni sawa na kg 7000.

Kwenye vituo vya utafiti ilionekana ekari moja inaweza kuzalisha mpaka tani 24 yaani kg 24000.

Mkungu mmoja wa ndizi kwa wastani una uzito wa kg 12. kwa hiyo ukipata kilo 7000 utakuwa umepata mikungu 583 ya ndizi.

Kwa Dar es salaam mkungu mmoja wa ndizi ni kati ya tsh 12000-18000 ikitegemea na kipindi.Basi kwa mikungu 583 utapata tsh millioni 7 hadi milllioni 10!!.

Je, ukiwa na ekari 10, 20 au 30 utakuwa wapi?.

Mambo ya kuzingatia ni kuhakikisha migomba yako inapata maji ya kutosha na unaikinga na magonjwa na panya wala mizizi.

Pia ni vizuri ukalima eneo kubwa kidogo au mkakubaliana na majirani ili kuepuka kusafirisha mzigo kidogokidogo kitu kinachoweza kukupa hasara.

Wenye experiance na nyongeza naombeni muongezee. Malila, Chasha, Sabayi, Kubota etc

update 26/3/2015

Wakuu nimepata ekari tatu nimeanza kuzipanda kidogokidogo.Mpaka sasa nimepanda miche 200 niliyopanda mwezi wa February. Ila napanga mpaka mwezi wa saba niwe nimemaliza. Nimefanya utafiti na kwa kauzoefu nilikopata nimejifunza yafuatayo.

- Watafiti wa Uganda walifanya utafiti kuhusu spacing ya migomba. Kuna waliyoweka 3mx3m na kupanda migomba 400 kwa ekari. Mikungu iliyozaliwa ilikuwa na kilo 14. 2.5x2.5 walipanda migomba 640 kwa ekari na ilikuwa na mikungu ya kilo 12.5 hadi 13. Kuna mingine ilikuwa 2x2 na walipanda migomba 1000 kwa ekari na mikungu yake ilikuwa kilo 11.

Kutokana na hivyo mi napanda 2.5x2, ambayo itatoa migomba 800 kwa ekari. Huu ulikuwa utafiti wa ndizi Uganda ila mimi napanda mzuzu.

Shimo linakuwa kipenyo cha 60cm na urefu wa 60cm. au urefu wa hadi gotini kwa mtu mzima. Kila shimo wanachimbia sh 300 hadi 500 kulingana na ugumu. Maximum 400,000 kwa ekari.

Kila mche nanunua tsh 300 na kubeba hadi shambani ni tsh 200. Jumla itakuwa 400,000 kwa ekari.

Napandia debe moja la samadikila shimo. Nimeinunua 20,000 na kila debe wanabebea tsh 400. Jumla ni 340,000 kwa ekari. Kupanda ni 100 sawa na 80,000 kwa ekari.

Jumla ya kukamilisha eka itakuwa 1, 220,000. Gharama za palizi na zingine ntakuwa nawaupdate.
 
Mkuu uko sahihi kabisa,

Ktk kilimo napenda migomba ( kwa sasa natafuta shamba),nyuki,cocoa ( wizi wa matunda),miti ya mbao,samaki na ufugaji( kwa sasa swine bado). Hivi vitu unaweza kuvifanya bila shinikizo la damu kukupanda na mavuno yake yako bayana kwa maana ya soko.

Mkuu nilikwenda sokoni Tandale pale Mbingu Ifakara 2011 kutafuta shamba, mashamba yako juu sana.Kule Mby mashamba ni ghari sana, sijakata tamaa. Kuna mdizi mmoja niliuona mahali fulani kule Mwalusembe, ni balaa. Maeneo yale mzuzu unazaa vizuri sana.

Mzuzu na mshale unaweza kukaa muda mrefu sana bila kuharibika. Mazao ya ndizi kutoka ktk eka kumi yanaweza kuendesha miradi mingine. Kuna bonde fulani nalifanyia upekuzi, nikiona liko vizuri basi nitarudi jamvini ili wanaotaka kulima pamoja na mimi tujitose.

Asante kwa kurusha hii kitu jukwaani.
 
Mkuu Saluti nyingi sana kwa huu uzi.

Unachoongea ni kweli kabisa Ndizi zinalipa sana ila tusiangalie soko la Tandale tu ukiweza kufanya in large scale kuna soko kubwa sana Botswana na Pia ulaya ambapo waganda huwa wanacross boarder kuja kuzinunua Bukoba na kuzipeleka Ulaya unaweza fanya hii kitu mwenyewe.
 
Mkuu uko sahihi kabisa,

Ktk kilimo napenda migomba ( kwa sasa natafuta shamba),nyuki,cocoa ( wizi wa matunda),miti ya mbao,samaki na ufugaji( kwa sasa swine bado). Hivi vitu unaweza kuvifanya bila shinikizo la damu kukupanda na mavuno yake yako bayana kwa maana ya soko.

Mkuu nilikwenda sokoni Tandale pale Mbingu Ifakara 2011 kutafuta shamba, mashamba yako juu sana.Kule Mby mashamba ni ghari sana, sijakata tamaa. Kuna mdizi mmoja niliuona mahali fulani kule Mwalusembe, ni balaa. Maeneo yale mzuzu unazaa vizuri sana. Mzuzu na mshale unaweza kukaa muda mrefu sana bila kuharibika. Mazao ya ndizi kutoka ktk eka kumi yanaweza kuendesha miradi mingine. Kuna bonde fulani nalifanyia upekuzi, nikiona liko vizuri basi nitarudi jamvini ili wanaotaka kulima pamoja na mimi tujitose.

Asante kwa kurusha hii kitu jukwaani.

Mkuu Malila
Nimekuwa nikifanya utafiti juu hili zao kama linakubali ukanda wa kati na Pwani kama Dodoma na Pwani yote
Je zao hili linataka nini hasa ni hali ya hewa ya ubaridi au ni maji?
 
Sabayi kwa vile hili ni zao la kitropiki nafikiri halihitaji baridi maana kama wiki mbili zilizopita nilikuwa ifakara kuna joto na zimestawi sana, nahisi zinataka maji kwa wingi tu. labda na udongo wa pwani wa kichanga unaweza kuwa tatizo.

Pia kama ukitoka rungwe ukifika milima ya uporoto hili zao halistawi na niliambiwa ni sababu ya baridi kuwa kali sana.
 
Last edited by a moderator:
Mkuu Malila
Nimekuwa nikifanya utafiti juu hili zao kama linakubali ukanda wa kati na Pwani kama Dodoma na Pwani yote
Je zao hili linataka nini hasa ni hali ya hewa ya ubaridi au ni maji?

Mkuu Sabayi na wadau wengine wote

Nimeona article hii hapa kwenye internet kuhusu zao la ndizi.

Inaweza kuwa ni mwomngozo mzuri kwetu, na kwa wengineo pia.
Asanteni.
 

Attachments

  • How to grow banana plants and keep them happy.pdf
    118.9 KB · Views: 1,302
Sabayi kwa vile hili ni zao la kitropiki nafikiri halihitaji baridi maana kama wiki mbili zilizopita nilikuwa ifakara kuna joto na zimestawi sana, nahisi zinataka maji kwa wingi tu. labda na udongo wa pwani wa kichanga unaweza kuwa tatizo. pia kama ukitoka rungwe ukifika milima ya uporoto hili zao halistawi na niliambiwa ni sababu ya baridi kuwa kali sana.

Mkuu nakumbuka miaka ya Tisini mwanzoni tulikuwa na migomba nyumbani kwetu Dar na ilikuwa inakubali vizuri tu nahisi labda inahitaji sana Maji na ndo maana Tukuyu ambako mvua inanyesha sana hii migomba inakubali sana
 
Mkuu Sabayi na wadau wengine wote,
Nimeona article hii hapa kwenye internet kuhusu zao la ndizi.
Inaweza kuwa ni mwomngozo mzuri kwetu, na kwa wengineo pia.
Asanteni.

Ubarikiwe mheshimiwa nimeshaipakua ngoja niipitie
 
Mu-Israeli nimeipenda article yako, ntaisoma tena na tena. imeeleza kwamba ndizi zinataka joto la kati ya 26-30 [SUP]0[/SUP]C.

Yes !! Hapo ndio pazuri sana hapo !
Hii ina maana kuwa hata mkoa wa pwani ndizi zinakubali sana.
Pia wamesema kuwa ndizi zinahitaji 'dark fertile soil'.

Hii nimeipenda sana maana nina shamba maeneo ya Ruvu kuna udongo mzito mweusi wenye rutuba sana. changamoto ni maji tu, maana wamesema kuwa ndizi zinahitaji maji mengi.
 
Mkuu Saluti nyingi sana kwa huu uzi
Unachoongea ni kweli kabisa Ndizi zinalipa sana ila tusiangalie soko la Tandale tu ukiweza kufanya in large scale kuna soko kubwa sana Botswana na Pia ulaya ambapo waganda huwa wanacross boarder kuja kuzinunua Bukoba na kuzipeleka Ulaya unaweza fanya hii kitu mwenyewe.

Teheeee,

Hapa nilijua watu mtanasa,
Tandale ninayoisema iko Mbingu Ifakara. Tandale ya Mbingu ndipo wakulima wa ndizi wa kanda ile hufikisha mikungu yao toka shambani tayari kwa mnada kwa watu wasafirishao kuja Dar. Pale ndipo lilipo gulio la ndizi, kunakuwa na foleni ya fuso na canter wakati fulani.

Tatizo ni kipande cha barabara toka Ifakara mpaka Mbingu, mvua ikinyesha ya kutosha unaweza ukashindwa kurudi mjini. Tazara iko hoi.

Zaidi sana hongereni kwa waliochangia wote.
 
Eka moja ya ndizi inaweza kuwa na miche mingapi? Je, miche ya migomba in large scale (kutosha ekari 20) inapatikana wapi?
 
Umeongelea mapato, vipi kuhusu gharama?

Gharama ktk kilimo hiki ziko ktk kupata shamba lenye sifa za kilimo cha migomba, pili kupata mbegu bora za migomba yenyewe ( Mshale na Mzuzu au Malindi) haya mengine kama Kiguruwe,jamaica/Mtwike sio mazuri kwa soko la mbali,maana kukusanya miche ya kutosha eka 20 kama mdau anavyouliza hapo juu si kazi nyepesi.

Palizi yake si ngumu. Sijajua gharama za magonjwa kama yalivyoshambulia kule Kagera zikoje. Kwa mazingira ya kawaida kilimo hiki ni rahisi zaidi kama utapata shamba mwafaka. Ugumu mwingine ni pale shamba linapokuwa off-road kidogo.
 
-Kwa kuongeza.. Malila nikweli nilishfanya kazi Kilombero.Mbingu kuna bonde la mto Kilobero na kuna mito mingi.

Barabara ndio changamoto,hata mpunga unalimwa sana kule na kuna mchina ana kama hekta 3000 anataka apige mpunga na aupeleke moja kwa moja uchina.

-Kwa wadau: Nilibahatika pia kufanya kazi Mahenge.Ndizi zinakuli balaa sababu bado ni bonde la mto Kilombero na udongo ni wa mbuga.

Maeneo ya Lukande na Malinyi yanafaa ka zao hili.

Mfano hai: Mwanajeshi Mstaafu amelima heka zake 5 pale Lukande.Kila mche akaweka dumu la lita 20 na amelitoboa matundu kiasi kwamba maji yanatoka kwa muda maalum. Akawe vibarua kuyajaza madu kila wiki maji yakiisha.

Akitoa mzigo si chini ya fuso 5 kwa siku zinatoka pale...!!

Msisahau pia kuna ujenzi wa barabara 2.

1. Ya Mmarekani anapitisha Lukande kwenda Namtumbo-Songea(kwenye mradi wa Uranium).

2. Ni serikali inapita Lupiro kupitia Kilosa kwa mpepo na kusonga hadi Ruvuma kurahisisha usafiri (Feasibility Study ya daraja la mto Kilombero umeshakamilika).Hivyo tupieni jicho ukanda huo.

Nilibahatika kupita Mvomero kuanzia Mji wa Mvomero kupitia Turiani hadi Mziha.Ni ukanda unaokubali mazao mengi ikiwemo ndizi na ardhi bado ni bei rahisi.

Mchina anajenga barbara kuazia Mikumi,Kilosa,Dumila,Turiani mpaka Handeni (hongera M.Mkulo) kurahisisha usafiri toka Kusini na Nyanda za Juu kuja Kanda ya Kaskazini.Changamkieni na huko.

Ahsanteni.
 
Last edited by a moderator:
-kwa kuongeza.. Malila nikweli nilishfanya kazi Kilombero... Mbingu kuna bonde la mto kilobero na kuna mito mingi.. barabara ndio changamoto... hata mpunga unalimwa sana kule na kuna mchina ana kama hekta 3000 anataka apige mpunga na aupeleke mojakwamoja uchina..
-Kwa wadau: Nilibahatika pia kufanya kazi mahenge.. Ndizi zinakubala sababu bado ni bonde la mto kilombero na udong ni wa mbuga... Maeneo ya Lukande na malinyu yanafaa ka zao hili..
Mfano hai: mwanajeshi Mstaafu amelima heka zake 5 pale Lukande.. kila mche akaweka dumu la lita 20 na amelitoboa matundu kiasi kwamba..maji yanatoka kwa muda maalumu.. akawe vibarua kuyajaza madu kila wiki maji ayakiisha... akitoa mzigo si ya fuso 5 kwa siku zinatoka pale...!! msisahau pia kuna ujenzi wa barabara 2.. 1 ya mmarekani anapitisha Lukande kwenda Namtumbo-Songea(kwenye mradi wa Uranium)..2 ni serikali inapi Lupiro kupitia Kilosa kwa mpepo na kusonga hadi Ruvuma kurahisisha usafiri(Feasibility Study ya daraja la mto Kilombero umeshakamilika).. hivyo tupieni jicho ukanda huo..
Nilibahatika kupita mvomero ..kuanzia Mji wa mvomero kupitia Turiani hadi Mziha.. ni ukanda unaokubali mazo mengi ikiwemo ndizi na ardhi bado ni bei rahisi... Mchina anajenga barbara kuazia mikumi..Kilosa...Dumila.. Turiani mpaka Handeni(hongera M.Mkulo) kurahisisha usafiri toka Kusini na Nyanda za Juu kuja Kanda y kaskazini... changamkieni na huko..
Ahsanteni..
Nilibahatika pia kuwepo m

Ubarikiwe mkuu hii ndo comments tunazozitaka huku kwenye ujasiriamali
 
Gharama ktk kilimo hiki ziko ktk kupata shamba lenye sifa za kilimo cha migomba, pili kupata mbegu bora za migomba yenyewe ( Mshale na Mzuzu au Malindi) haya mengine kama Kiguruwe,jamaica/Mtwike sio mazuri kwa soko la mbali,maana kukusanya miche ya kutosha eka 20 kama mdau anavyouliza hapo juu si kazi nyepesi. Palizi yake si ngumu. Sijajua gharama za magonjwa kama yalivyoshambulia kule Kagera zikoje. Kwa mazingira ya kawaida kilimo hiki ni rahisi zaidi kama utapata shamba mwafaka. Ugumu mwingine ni pale shamba linapokuwa off-road kidogo.

Malila hujanijibu bado.
 
Last edited by a moderator:
-kwa kuongeza.. Malila nikweli nilishfanya kazi Kilombero... Mbingu kuna bonde la mto kilobero na kuna mito mingi.. barabara ndio changamoto... hata mpunga unalimwa sana kule na kuna mchina ana kama hekta 3000 anataka apige mpunga na aupeleke mojakwamoja uchina..
-Kwa wadau: Nilibahatika pia kufanya kazi mahenge.. Ndizi zinakubala sababu bado ni bonde la mto kilombero na udong ni wa mbuga... Maeneo ya Lukande na malinyu yanafaa ka zao hili..
Mfano hai: mwanajeshi Mstaafu amelima heka zake 5 pale Lukande.. kila mche akaweka dumu la lita 20 na amelitoboa matundu kiasi kwamba..maji yanatoka kwa muda maalumu.. akawe vibarua kuyajaza madu kila wiki maji ayakiisha... akitoa mzigo si ya fuso 5 kwa siku zinatoka pale...!! msisahau pia kuna ujenzi wa barabara 2.. 1 ya mmarekani anapitisha Lukande kwenda Namtumbo-Songea(kwenye mradi wa Uranium)..2 ni serikali inapi Lupiro kupitia Kilosa kwa mpepo na kusonga hadi Ruvuma kurahisisha usafiri(Feasibility Study ya daraja la mto Kilombero umeshakamilika).. hivyo tupieni jicho ukanda huo..
Nilibahatika kupita mvomero ..kuanzia Mji wa mvomero kupitia Turiani hadi Mziha.. ni ukanda unaokubali mazo mengi ikiwemo ndizi na ardhi bado ni bei rahisi... Mchina anajenga barbara kuazia mikumi..Kilosa...Dumila.. Turiani mpaka Handeni(hongera M.Mkulo) kurahisisha usafiri toka Kusini na Nyanda za Juu kuja Kanda y kaskazini... changamkieni na huko..
Ahsanteni..
Nilibahatika pia kuwepo m

Hapo kwenye nyekundu si kweli maana China kilimo cha mpunga kipo juu sana sema tu analima kwa biashara ya hapa kwetu maana ni dili zaidi ya kusafirisha
 
Malila hujanijibu bado.

Sijajibu sababu ya kukosa reference za uhakika. Kule kwetu wanalima sana migomba, lakini suala la gharama lina utata sana, sababu hatuna mfumo rasmi wa kilimo hiki. Pili hakuna mashamba ya mfano ya kilimo hiki ambayo tungetumia kama data base yetu.

Gharama zinazojulikana ni palizi ambayo sio uniform,kwa upande wa madawa ( labda tuwaulize Kagera ambao migomba yao imepigwa na mnyauko), miche nayo bei haiko wazi, maana unaweza pewa bure na jirani yako.

Na mimi kutoa data chini ya kiwango naogopa kuharibu jukwaa. Sio kwamba nimetulia, hapana natafuta kutoka kila kona ili nikipata niwajulishe na wenzangu, hasa kutoka SUA.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom