Fahamu kuhusu kilimo bora cha Hiliki

Yayo

Member
Aug 7, 2012
15
1
1601824352159.png
Iliki ni moja kati ya mazao ambayo yanatumika sana karibia kila siku kwenye matumizi ya nyumbani,utumika kama viungo kwenye chakula na pia utumika kama tiba ya magonjwa mbalimbali.na pia ni mmea mfupi ambao unatoa matunda kwa miaka mingi.

kunanjia mbili za kuotesha iliki unaweza kupanda mbegu au ukapanda miche midogo(spilits)sia mbegu kwenye kitalu pandikiza mche shambani zikiwa na umri wa miezi 3-4 au zaidi zenye ukubwa wa sm 15 au zaidi au tenganisha vimiche vinavyo zaliwa kwenye tunguu moja chini ya ardhi na pandikiza shambani na utengeneze mashimo sm 60 x 60 na nafasi ya shimo panda miche kwenye mashi

Iliki Huchukua miaka 3 tangia kupandwa mpaka kuzaa na kuvuna pale unapopanda miche midogo, ukipanda mbegu huchukua miaka 4-5 mpaka kuvuna. matunda huvunwa hasa mwezi march na aprilmatundwa huvunwa na kukaushwa kwenye jua

na kipanda kunauwezekana wa kuvuna 112-300 kwa heka na 45-120kg kwa eka ikiwa imekaushwa

Matumizi ya iliki husaidia sana kuipa uwezo mzuri figo wa kuondoa taka mwili ndani ya mwili, huku ikisaidia sana kuweka sawa mfumo wa umeng’enyaji chakula tumboni, kuondoa kiungulia, gesi tumboni pamoja na kuwasaidia wale wenye shida ya kukosa choo kwa muda mrefu.

Pia iliki inauwezo mzuri sana wa kutibu matatizo ya maambukizi kwenye njia ya mkojo, matatizo ya figo na kibofu cha mkojo, sambamba na kupambana na magonjwa mbalimbali.
Iliki pia inauwezo wa kukabilina na hali ya mambukizi ya mafua sambamba na kikohozi, huku isifika kwa kuwa na uwezo wa kuimairsha mfumo wa mmengenyo wa chakula pamuja na kuondoa maumivu ya viungo mwilini.

Wadau wanaotaka kujua kuhusu zao hili la iliki

Habari zenu wana Jf nilikua nahitaji msaada jinsi ya kulima iliki pamoja namaeneo inapostawi vizuri pamoja na gharama za kilimo hicho.

Nitanguliza shukrani zangu kwenu wadau.
-----
Wadau, salam!
Ningependa kujua juu ya soko la hiliki.

Mwenye taarifa kamili, tafadhal tujuzane.

Michango ya wadau
Samahani wakuu !
Kweli sijaleta mrejesho kwa mda mrefu tangu niahidi. Nilijisahau!
Kwa kifupi nilikatishwa tamaa na zoezi la uchunguzi nililofanya huko Turiani. Baada ya kufika turiani mjini pale migombani nilichunguza watu kadhaa kuwa ni wapi/maeneo gani kunalimwa pilipili manga. Wengi walinielekeza niende huko milimani kupitia chuo cha ualimu. Nilikodi bodaboda (30,000 kwenda na kurudi) Nikiwa njiani kuelekea huko mlimani nikawa pia nauliza watu kuwa ni nani mkulima mkubwa wa pilipili manga maeneo ya huko. Nilipewa jina la mkulima na nikaelekezwa kwake. Tulikipita chuo cha ualimu tukaenda juu zaidi (kuna baridi kiasi)

Nilipofika kwa huyo mkulima niliogiziwa, kwa bahati mbaya hakuwepo home bali mkewe alikuwepo. Nilimweleza mkewe kisa cha ujio wangu na nikamwomba anionyeshe shamba lao la pilipili manga na pia anipe maelezo juu ya kilimo hicho.

Alinionyesha mashina sita (6) ya pilipili manga yaliozunguka nyumba yao. Nikamuulizaa je kuna mkulima mwingine anaelima zao hilo kwa wingi zaidi akasema wao ndio waanzilishi na wengine huja tu kuomba mbegu bado hawajawafikia kwa wingi wa miche/mshina.
Nimuliza miche walipata wapi akasema mumewe aliipata huko Matombo kutoka taasisi iliyokuwa inahamasisha kilimo hicho.
Kwa mwaka wanapata kilo ngapi toka hiyo mashina sita akasema hawajawahi pata zaidi ya kilo 2.
Kuhusu bei ya kuuza na ni wapi wanauzia alisema mumewe ndio anashugulika yeye hajui

Kwa jinsi nilivyo uona ule mmea hata ukiwa na eka 2 huwezi pata zaidi ya kilo 20 kwa msimu. Ni zao ambalo ni labour intensive. japo linatoa maua mfilulizo na kuvuna ni mara 2 au 3 kwa mwaka kutegemea na hali ya hewa, hizo punje zake ambazo kila shina linazaa chache, kuzivuna,uzianike, utwage, upepete hadi upate kilo moja ni kazi pevu na ndio maana bei yake iko juu sana maana supply ni ndogo siku zote.

Wadau mimi sikuwa encouraged baada ya kuona na kupewa maelezo maana niligundua large scale production ya zao hilo sio jambo rahisi kwangu. Naona niendelee kulima mpunga huko Kilosa kwa sasa! Ila wanaoweza kufuatilia zaidi na kujaribu kulima zao hilo, bei kubwa ipo siku zote.

Asanteni.
 
Wadau, salam!
Ningependa kujua juu ya soko la hiliki.

Mwenye taarifa kamili, tafadhal tujuzane.
 
Inaitwa ILIKI na sio IRIKI,(au Cardamon kwa Ki English)

Halafu maelelezo yako hayajajitosheleza
Je unahitaji kujua soko la kuuza au kununua?
 
Upo Mkoa gani na bei ipoje kwa kilo.
Wewe ni mkulima au shanta

Mkuu, kuna ndugu kanigusia km ana hiyo biashara. Sijaongea nae bei bado. Nilitaka nijue kwanza bei ya mimi kuiuza sokoni ndipo nimsikize na yeye.
Mimi nipo dar bt mzigo ni kutoka ileje.
 
Mkuu haukurudi tena jamvini!

Samahani wakuu !
Kweli sijaleta mrejesho kwa mda mrefu tangu niahidi. Nilijisahau!
Kwa kifupi nilikatishwa tamaa na zoezi la uchunguzi nililofanya huko Turiani. Baada ya kufika turiani mjini pale migombani nilichunguza watu kadhaa kuwa ni wapi/maeneo gani kunalimwa pilipili manga. Wengi walinielekeza niende huko milimani kupitia chuo cha ualimu. Nilikodi bodaboda (30,000 kwenda na kurudi) Nikiwa njiani kuelekea huko mlimani nikawa pia nauliza watu kuwa ni nani mkulima mkubwa wa pilipili manga maeneo ya huko. Nilipewa jina la mkulima na nikaelekezwa kwake. Tulikipita chuo cha ualimu tukaenda juu zaidi (kuna baridi kiasi)

Nilipofika kwa huyo mkulima niliogiziwa, kwa bahati mbaya hakuwepo home bali mkewe alikuwepo. Nilimweleza mkewe kisa cha ujio wangu na nikamwomba anionyeshe shamba lao la pilipili manga na pia anipe maelezo juu ya kilimo hicho.

Alinionyesha mashina sita (6) ya pilipili manga yaliozunguka nyumba yao. Nikamuulizaa je kuna mkulima mwingine anaelima zao hilo kwa wingi zaidi akasema wao ndio waanzilishi na wengine huja tu kuomba mbegu bado hawajawafikia kwa wingi wa miche/mshina.
Nimuliza miche walipata wapi akasema mumewe aliipata huko Matombo kutoka taasisi iliyokuwa inahamasisha kilimo hicho.
Kwa mwaka wanapata kilo ngapi toka hiyo mashina sita akasema hawajawahi pata zaidi ya kilo 2.
Kuhusu bei ya kuuza na ni wapi wanauzia alisema mumewe ndio anashugulika yeye hajui

Kwa jinsi nilivyo uona ule mmea hata ukiwa na eka 2 huwezi pata zaidi ya kilo 20 kwa msimu. Ni zao ambalo ni labour intensive. japo linatoa maua mfilulizo na kuvuna ni mara 2 au 3 kwa mwaka kutegemea na hali ya hewa, hizo punje zake ambazo kila shina linazaa chache, kuzivuna,uzianike, utwage, upepete hadi upate kilo moja ni kazi pevu na ndio maana bei yake iko juu sana maana supply ni ndogo siku zote.

Wadau mimi sikuwa encouraged baada ya kuona na kupewa maelezo maana niligundua large scale production ya zao hilo sio jambo rahisi kwangu. Naona niendelee kulima mpunga huko Kilosa kwa sasa! Ila wanaoweza kufuatilia zaidi na kujaribu kulima zao hilo, bei kubwa ipo siku zote.

Asanteni.
 
Kwanza kabisa ni mshukuru Mungu kwa kutujalia uzima (mimi na wewe).

Lengo la kuandika hii tread ni kwamba natafuta bosi ambaye ananunua iliki, hii ni baada ya kuuza hili zao kwa bei ya chini sana kwa madarali.

Hivyo naitaji tajiri wa uhakika ili tuweke bond na kumuuzia izi mbegu, moja kwa moja badala ya kutegemea madarali.

Na kama wewe unaye soma hii thread sio Tajiri, lakini kuna mtu unamfaham (mnunuzi) itakuwa powa ukanipa contacts zake kwaajiri ya mawasiliano.

Kuusu bei na jinsi ya kuupata mzigo, tupia namba inbox kwaajiri ya mawasiliano.

Tafadhali usipuuze sio Kiki, pia utani na lugha za kuudhi sio mahala pake.
 
Iliki au hiliki/hiriki, sio mbobezi ngoja waje ila ungeweka kichwa cha habari vizuri
 
Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom