Kingdom_man
JF-Expert Member
- May 19, 2010
- 405
- 456
Jipange msimu ujao wa kilimo
Najipanga. Ndio maana nafanya tafiti. Wataamu mnipe mwelekeo!.
Asante
Jipange msimu ujao wa kilimo
Asante mdau. Kwahiyo nikikomaa na kilimo cha mpunga naweza pata pesa ya ya kujikimu sio?
Zaidi ya pwani mkoa gani mwingine naweza pata kwamba la kukodi kwa being raisi.
Asante sana!
.Ndugu yangu Robbinhood Kilimo cha mpunga kitakachokuinua ni kile cha kwenye maeneo yenye umwagiliaji. Huko ukishamailiza kupandikiza mpunga wako hesabu hiyo ni hela au ni chakula tayari! Achana na kilimo cha kutegemea mvua utalia siku zote! Mkoa wa Morogoro kuna maeneo kupanda na kuvuna ni. mwaka mzima, hakuna eti umechelewa msimu, watu wanapanda tu mwaka mzima. Wanaoongelea kuchelewa msimu ni kwa kilimo cha kutegemea mvua. Mashamba ya kukodi ni mengi na bei ni nzuri tu. Kuna maeneo si utani, bei ya kukodi na ya kununua hakuna tofauti, tembea ujionee!
Mkuu japo suala la bei na risk siwezi kuongele chochote ila maeneo mazuri kwa kilimo cha mpunga ni IFAKARA ukiwa unaelekea wilaya ya MAHENGE ukishavuka tu mto kilombero kuna eneo wenyeji wanaliita mashambani.
Ni eneo zuri sana kwa mpunga na linakubali mpunga kweli kweli, pia kuna ardhi ya kutosha na maji ya kutosha pia, kwa suala la soko la bidhaa ni rahisi sana kusafirisha kuja DAR ES SALAAM....
Ni kaz ya miez 7 (januar to july ) na hapo una uhakika wa kupata gunia ishirini mpaka ishirin na tano(20-25) zenye thaman ya 2000. Hvyo chukua hzo 2,000,000 toa 761,000 unapata 1,239,000/ekari,.. karibuni
Hilo eneo lako ukubwa gani?
Mi nina uzoefu kwa iringa...gharama zote (kwa ekali)mpaka kufikisha mpunga store ni kama ifuatavyo:
Vipi kilimo kinaendaje?
Tumemaliza kung'olea, na zinaendelea mvua vizuri