Kilimo cha Mitiki: Utaalamu na biashara yenyewe

hivi mbegu kama hizi (pines, eucalyptus saligna etc) hatuwezi kuziagiza Kenya au nchi nyingine na kuzipata? maana naona hapa TZ panazidi longo longo sana!!

Kuna uzembe mkubwa sana hapa Tz kila idara. Zipo mbegu za kutoka Zimbabwe ( pines za miaka 8 etc),lakini mpaka hapo mkulima mdogo atakuwa ameumia,yaani nusu kilo ya mlingoti itoke nje,wakati kituo kipo,si sawa. Ikibidi tutafanya hivyo.
 
Mbona kuna miche mingi tu hapa Dar along Old Bagamoyo rd kama pale bondeni karibu na kwa mh Komba na pale Tegeta,nijuavyo mitiki huhitaji maji mengi,
 
Mbona kuna miche mingi tu hapa Dar along Old Bagamoyo rd kama pale bondeni karibu na kwa mh Komba na pale Tegeta,nijuavyo mitiki huhitaji maji mengi,
Ni kweli kabisa,hata njia ya Morogoro baada ya kupita kwa Msuguri ipo mingi. Hawa wanaojadiliana hapa ni wale wa scale ya kati,kwa anayehitaji miche kama mia hivi au zaidi kidogo ni bora kuchukua huko,lakini kama unataka miche kuanzia 10,000 na zaidi, ni bora kuwa na kitalu chako,kwa sababu ya gharama.
 
Mbona kuna miche mingi tu hapa Dar along Old Bagamoyo rd kama pale bondeni karibu na kwa mh Komba na pale Tegeta,nijuavyo mitiki huhitaji maji mengi,

mfianchi, nilikuwa naulizia mbegu si miche ambayo tayari ipo kwenye kitalu....
Malila nimekupata.. wakati wa maonyesho ya sabasaba niliona watu furani toka Kenya walikuwa wanauza mbegu.... bahati mbaya nimepoteza kipeperushi chao na nimesahau jina lao...
 
hawa wakenya wajanja ile mbaya,wamejua kuwa wakala wa serikali ya Tz kalala ndio maana wao wamechukua nafasi,hata wanaopanda miti ya nguzo za umeme ndani ya nchi yetu kwa wingi ni wakenya lakini mbegu wanachukua ktk vituo vyetu. Inauma sana. Iweje Wakenya wauze mbegu halafu washikaji wamekaa tu? Tunahitaji mabadiliko makubwa hasa vijana. Kulalamika haisaidii kabisa.
 
Walikuja wathaminini shambani kwangu

Wakasema mchungwa, Mpera, Mdimu, Mwembe shs 5,000/=

Mnazi 22,000/=

Mpingo 56,000/=

Wakasema mti wenye thamani zaidi ni MTIKI Lakini bei hawakuniambia

Walikuwa na chati ambayo hawakutaka kamwe mtu yeyeto aitie machoni mwake.

NB: Mchongoma - 100/= (shilingi mia moja tu)
 
Mzee ngoja tukufanyie utafiti halafu tutarudi. Na mimi ni mdau
 
Nafikiria kupanda mitiki kwenye shamba langu lililoko wilayani Kisarawe. Wenye uzoefu na miti hiyo naomba mnishauri, je Kisarawe kunafaa kuotesha mitiki, na soko lake sasa hivi likoje, najua kuwa mitiki inakuwa tayari kuvunwa baada ya miaka 10, lakini sio vibaya kujua soko lake kwa sasa likoje. Wenye data tafadhali naomba mnisaidie
 
mitiki ni zao zuri sana...ila kuvuna ni baada ya 10 to 20 years. kwa mikoa ya pwani, zao hilo ni zuri. hata mimi nina mpango nikapande kule kimbiji, umbali kidogo kutoka kigamboni, dsm. big up man. mche mmoja ni kiasi gani?
 
nakushauri soma threads/links hizi hii utaona article

UOTESHAJI

Mbegu za mitiki zioteshwe kwa mistari zifukiwe kiasi cha kama sentimeta moja chini ya udongo, hakikisha kwamba mbegu haziwi chini sana ya udongo hii itasaidia katika uchipuaji wa mbegu zako. Nafasi kati ya msitari na msitari ni sentimeta kumi (10).

Uotaji wa mbegu huchukua muda kiasi cha siku 30 - 45, wakati wote huu kabla na baada ya kuota kitalu inabidi kimwagiwe maji ya kutosha angalau mara moja kila siku, maji yamwagiwe taratibu kwa kutumia vyombo vya kuwagilia (watering can) ili kuzuia kuzifukua mbegu zilizopo ardhini. Mara baada ya mbegu kuota ziendelee kumwagiwa maji ya kutosha.

Maara baada ya miche kufikia uefu wa sentimea 8- 10, mbolea za kukuzia zinaweza kuwekwa ili kuhahkikisha miti inakuwa na nguvu, wkati huu unaweza kupunguza kiasi cha maji ya kumwagilia ili kuzuia mbolea kuchkuliwa na maji.

UTUNZAJI

Muda wote hakikisha magugu yanang'olewa ili yasinyang'a nyane chakula na miche yako, hakikisha pia kingo za tuna zinanyanyuliwa muda wote kuzuia upotevu wa maji. Huna haja ya kutandaza nyasi juu ya tutalako kwa ajili ya kuzuia upotevu wa maji, kumbuka mbegu za mitiki zinahitaji mwanga wa kutosha na hewa ili ziweze kuchipua.

Kama utagundua kuna wadudu wanaoshambulia kitalu chako, omba ushauri kwa mabwana shamba dawa gani utumie ingawa ni nadra sana mitiki kushambuliwa na wadudu.

Kwa wale watakaouza miche hii au wanategemea kuisafirisha umbali mrefu, basi itawalazimu kuiweka kwenye vifuko, hii iatahisisha usafirishaji mpaka shambani, ingawa kitaalamu miche ya kwenye vifuko huwa inakufa mingi zaidi na huwa inapindapinda wakati wa ukuaji. Uhamishaji wa miche kwenye vifuko hufanyka wakati miche ina urefu wa sentimeta za wastani 2

MITIKI -KILIMO KWANZA: KITALU CHA MITIKI

https://www.jamiiforums.com/busines...-kilimo-pamoja-na-hesabu-kilimo-nanasi-2.html - nenda kipenngele cha MAZAO then click katika namba 3

utapata maelezo unayohitaji

mbegu zinapatikana kwa wakala wa mbegu wapo morogoro njia ya kwenda dodoma baada ya msamvu. kilo moja ya mbegu za mitiki ni Tsh 7000 (katika kilo moja zinakuwepo mbegu takribani 1000).
 
Nafikiria kupanda mitiki kwenye shamba langu lililoko wilayani Kisarawe. Wenye uzoefu na miti hiyo naomba mnishauri, je Kisarawe kunafaa kuotesha mitiki, na soko lake sasa hivi likoje, najua kuwa mitiki inakuwa tayari kuvunwa baada ya miaka 10, lakini sio vibaya kujua soko lake kwa sasa likoje. Wenye data tafadhali naomba mnisaidie

Kwanza tupe ukubwa wa shamba lako, na je shamba lako lina udongo wa aina gani? sehemu kubwa ya Kisarawe ni kame fulani hivi, ktk ardhi kavu mitiki haikui haraka kama ktk ardhi yenye unyevu kiasi.

Kwa sasa, soko la uhakika ni nje ya nchi zaidi, kiwanda cha kusindika mazao ya mitiki kinajengwa huko Kilombero. Kwa hiyo kwa mtu wa small scale ni kasheshe kupata soko la ndani, lakini kama unaweza kuuza kama nguzo za umeme,hilo linawezekana.
 
mitiki ni zao zuri sana...ila kuvuna ni baada ya 10 to 20 years. kwa mikoa ya pwani, zao hilo ni zuri. hata mimi nina mpango nikapande kule kimbiji, umbali kidogo kutoka kigamboni, dsm. big up man. mche mmoja ni kiasi gani?

Bei ya mche mmoja wa mtiki inatofautiana kutoka kitalu kimoja hadi kingine, na aina ya uoteshaji wa mche. Bei ya juu kwa sasa kwa vijiwe vingi vya dar ni Tsh 1,500/ kwa mche na bei ya chini ni Tsh 500/ pale mbagala mwisho. Kwa pale Mbagala mwisho nina hadi simu yao ukitaka. Lakini kama utapata miche toka ktk vitalu vya serikali ni bora zaidi, hasa Handeni, pale kuna kitalu bomba.
 
Kwanza tupe ukubwa wa shamba lako, na je shamba lako lina udongo wa aina gani? sehemu kubwa ya Kisarawe ni kame fulani hivi, ktk ardhi kavu mitiki haikui haraka kama ktk ardhi yenye unyevu kiasi.

Kwa sasa, soko la uhakika ni nje ya nchi zaidi, kiwanda cha kusindika mazao ya mitiki kinajengwa huko Kilombero. Kwa hiyo kwa mtu wa small scale ni kasheshe kupata soko la ndani, lakini kama unaweza kuuza kama nguzo za umeme,hilo linawezekana.

Sasa hivi nina ekari nne, lakini nitakuwa naongeza taratibu. Sehemu yenyewe ni kutoka Masaki kwa kupitia njia ya Chanika. Maeneo hayo mihogo inastawi vizuri sana
 
asante sana
Mbegu za mitiki zinapatikana Tanzania Tree Seed Agency wako Msamvu Morogoro.Kilo moja ya mbegu za mitiki inatosha kuotesha kwenye shamba la hekta moja, ambayo ni wastani wa miti 1500

Matayarisho:

  • Ganda la nje la mbengu ya mtiki ni gumu sana na lina sumu mbaya.Unatakiwa uloweke mbegu ya mitiki kwa masaa 72, na kila baada ya masaa 12 unatakiwa ubadilishe maji kwa kumwaga maji ya zamani na kuweka maji mapya.
  • Baada ya masaa 72 anika mbegu zako juani kwa masaa 12.
  • Tengeneza kitalu, weka mbolea ya wanyama au mboji, kisha panda mbegu zako kwenye kitalu.
  • Mwangilia maji kila siku asubuhi na jioni, mbegu zitaanza kuota baada ya siku 10 hadi 20.
  • Miche ikifikia urefu wa futi moja, unaweza sasa kuiotesha kwenye shamba lako ulilotayarisha kwa ajili ya kuotesha miti.
  • Kabla ya kung’oa miche hakikisha unamwaga maji mengi, ili mizizi isikatike sana, kisha chukua kisu chenye makali ya kutosha na kata ncha ya juu ya mti na ondoa majani, hii inasaidia mti kuchipuka upya hasa eneo ambalo halina maji mengi.
  • Otesha miti futi 6x6 mitiki inaposongamana, hurefuka haraka ikikimbilia jua angani, hivyo kwa vipimo hivyo miti yako itakuwa mirefu sana na iliyonyooka, baadaye unaweza kuipunguza na kuuza fito za kujengea.
  • Ili upate mbao bora hakikisha unaondoa matawi yanayochipuka pembeni hadi mti ufike zaidi ya futi 10 kwani ndiyo yanafanya mbao kuwa na mabaka (vidonda)
 
Sehemu nyingi inastawi.......ila zaidi kwenye mvua za kutosha, joto la wastani na udongo wenye kina kirefu. Mashamba makubwa ya Teak yapo Tanga (Longuza), Morogoro (Turiani, Ifakara etc). Kazi kwako.....ukipata kijitabu cha mbegu cha Tanzania Tree Seed Agency kimeorodhesha maeneo kwa ufasaha zaidi.

maeneo ya kibaha Mlandizi vp?
 
Wadau naomba kupata ukweli juu ya hii miti ya mitiki,kuna mengi yanasemwa juu ya miti hii,kifupi mimi naomba kujua,je ni 1: kweli kua miti hii ni ghali sana kidunia? 2: ni kweli kua zipo baadhi ya banks hapa nchini zinatoa mikopo ukiwa na miti hii?kama ni kweli je ni bank gani hizo? 3:je mitiki uwa inachukua muda gani kuanza kukua mpaka kufikia hatua ya kuingizwa sokoni?kuna mtu aligusia kua kuna aina tofauti tofauti za miteak na ukuaji wake,ila nae hana uhakika sana juu ya ilo
 
Nami niko hapa pembeni kungoja majibu ya wanaojua vzr.
Ukitoka Segera kama unakwenda Korogwe kn shamba kubwa sana la Mitiki.
 
Wadau naomba kupata ukweli juu ya hii miti ya mitiki,kuna mengi yanasemwa juu ya miti hii,kifupi mimi naomba kujua,je ni 1: kweli kua miti hii ni ghali sana kidunia? 2: ni kweli kua zipo baadhi ya banks hapa nchini zinatoa mikopo ukiwa na miti hii?kama ni kweli je ni bank gani hizo? 3:je mitiki uwa inachukua muda gani kuanza kukua mpaka kufikia hatua ya kuingizwa sokoni?kuna mtu aligusia kua kuna aina tofauti tofauti za miteak na ukuaji wake,ila nae hana uhakika sana juu ya ilo

Hata mimi nilishawahi sikia tetesi juu ya uyaongeleayo mkuu,ngoja waje wadau kama kina Malila watatoa elimu ya uhakika hapa
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom