Kilimo cha Mihogo (Cassava): Mbinu, Ushauri, Changamoto na Masoko yake

Tazama mzigo wa muhogo tunaohitaji kwa siku upate picha hapa..
 
Attachments

  • Kiwanda cha starch Thailand.JPG
    Kiwanda cha starch Thailand.JPG
    168.7 KB · Views: 347
  • Kiwandani 2.JPG
    Kiwandani 2.JPG
    138.3 KB · Views: 307
  • Muhogo na starch.JPG
    Muhogo na starch.JPG
    210.3 KB · Views: 315
Si lazima uwe umesajiliwa ila ni muhimu kwa mafanikio zaidi angalia hapo juu tumesema "interested parties, farmers, AMCOS, Cooperative Unions, companies involved in agriculture and farm groups"

Roughly maximum unaweza kutumia Sh 200,000 kwa eka kufyeka na kung'oa visiki, kulima ni Sh 45,000, kupalilia ni sh 45,000, kuvuna sh 50,000, zote ni kwa eka.. kununua mbegu ni kama sh 3000 hivi kwa eka

Eka 1 inaweza kutoa kati ya tani 10 - 15 za muhogo mbichi so kwa eka 100 unaweza kupata tani 1000 hadi 1500.

Bei tutakayoanza nayo ni $50 kwa tani ambayo ukiwa na tani hizo una uhakika wa kupata $50,000 hadi $75,000

So kwa kifupi unaweza kupata kati ya sh 79,000,000 hadi 120,000,000 kwa mwaka kwa eka 100..

Haya karibuni hizo ndiyo projections kwa sasa
Mkuu Mzuzu,maelezo mazuri, na je inachukua muda gani kwa muhogo kuanzia kupanda hadi kuvuna?
 
Mkuu Mzuzu,maelezo mazuri,na je inachukua muda gani kwa muhogo kuanzia kupanda hadi kuvuna?
Tangu kupanda hadi kuvuna ni kuanzia miezi 7 ila unavyoacha shambani ukomae zaidi unakuwa na uzito mkubwa zaidi na ndio unapata fedha zaidi. Hakuna mbolea wala madawa inayohitajika kwa kilimo cha muhogo Rufiji hadi sasa kwa mujibu wa tafiti zilizopo.Tutakuwa na trekta za kulima, buldozers za kufyeka (tutakodi caterpillar na watakaopenda tutachanga tungeze muda zaidi) , mashine ya kupanda na kuvuna ambazo zote tutafanya makubaliano ya kutumia hizo kwa kukodi na baadaye tutakata kwenye malipo.Tunataka kazi nyingi zifanywe na mashine zaidi
 
Naona kama picha za Thailand hizo!

Yes ni Thailand nimeweka kama sample wadau wapate picha ya amount tunayotaka kwa kuwa kiwanda tunachojenga ni cha aina hiyohiyo. Hapa Tz hamna production ya aina hiyo.. Thanks
 
Tangu kupanda hadi kuvuna ni kuanzia miezi 7 ila unavyoacha shambani ukomae zaidi unakuwa na uzito mkubwa zaidi na ndio unapata fedha zaidi. Hakuna mbolea wala madawa inayohitajika kwa kilimo cha muhogo Rufiji hadi sasa kwa mujibu wa tafiti zilizopo.Tutakuwa na trekta za kulima, buldozers za kufyeka (tutakodi caterpillar na watakaopenda tutachanga tungeze muda zaidi) , mashine ya kupanda na kuvuna ambazo zote tutafanya makubaliano ya kutumia hizo kwa kukodi na baadaye tutakata kwenye malipo.Tunataka kazi nyingi zifanywe na mashine zaidi

That's very professional Mkuu May God bless you and May He take care of this Project ninavyoiona itawatoa watu wengi sana kama tutitumia vizuri hii fursa
 
Sawa Mkuu Sabayi, lakini si wanasema mchuzi wa mbwa huliwa wa moto?
Wengine tunafikiria kuanza kaunti dauni ya kuachana na utumwa mambo leo pindi tukiowa na miradi ya uhakika.
The early the better mkuu hapo hata ukipata ekari 50 tu zinakutoa tayari Mkuu Mzuzu ameshasema sio lazima uwe na kampuni iliyokuwa registered go for it brother usisubiri next time kama kuna uwezekano wa kufanya sasa hivi.
 
Yes ni kweli sir japo wa mwanzo wako likely kufaidi zaidi kuliko wanaokuja baadaye...

Kwanini unasema wa mwanzo ndo watafaidi zaidi mkuu? unamaanisha kuwa baadaye mtashusha bei au kuweka masharti magumu?
 
Si lazima uwe umesajiliwa ila ni muhimu kwa mafanikio zaidi angalia hapo juu tumesema "interested parties, farmers, AMCOS, Cooperative Unions, companies involved in agriculture and farm groups"

Roughly maximum unaweza kutumia Sh 200,000 kwa eka kufyeka na kung'oa visiki, kulima ni Sh 45,000, kupalilia ni sh 45,000, kuvuna sh 50,000, zote ni kwa eka.. kununua mbegu ni kama sh 3000 hivi kwa eka

Eka 1 inaweza kutoa kati ya tani 10 - 15 za muhogo mbichi so kwa eka 100 unaweza kupata tani 1000 hadi 1500.

Bei tutakayoanza nayo ni $50 kwa tani ambayo ukiwa na tani hizo una uhakika wa kupata $50,000 hadi $75,000

So kwa kifupi unaweza kupata kati ya sh 79,000,000 hadi 120,000,000 kwa mwaka kwa eka 100..

Haya karibuni hizo ndiyo projections kwa sasa

Ukiwa na Tractor lako mwenyewe hizi gharama si zitashuka sana?
 
Tukimaanisha tunaweza kabisa kufika juu ya mlima Kilimanjaro.
Ni jambo njema tukaunganisha nguvu tutafika, siyo mlima kilimanjaro tuu hadi juu kabisa.

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
 
Kama trector hilo utaliendesha mwenyewe, gharama lazima zishuke, na pili linakuwa lorry wakati wa mavuno kwako na kwa wenzako.
Ni kweli mkuu hii inaanza kunipa moyo kuwa na mimi naweza kusonga front kulima Mihogo.
 
Tangu kupanda hadi kuvuna ni kuanzia miezi 7 ila unavyoacha shambani ukomae zaidi unakuwa na uzito mkubwa zaidi na ndio unapata fedha zaidi. Hakuna mbolea wala madawa inayohitajika kwa kilimo cha muhogo Rufiji hadi sasa kwa mujibu wa tafiti zilizopo.Tutakuwa na trekta za kulima, buldozers za kufyeka (tutakodi caterpillar na watakaopenda tutachanga tungeze muda zaidi) , mashine ya kupanda na kuvuna ambazo zote tutafanya makubaliano ya kutumia hizo kwa kukodi na baadaye tutakata kwenye malipo.Tunataka kazi nyingi zifanywe na mashine zaidi
Kwa hiyo mkuu inawezekana mkamkodisha mtu vifaa (bulldozer) vya kusafishia shamba na tractor ya kulimia then mkamkata kwenye malipo? That's a kind of a soft loan kama ni hivyo huo mpango mtauanza sasa hivi au awamu nyingine? Nijibu tafadhali hii itasaidia sana interested wakulima hasa wadogo kumake decision kuanza na awamu ipi
 
Mkuu Mzuzu

Naomba kujua kuhusu output product yaani starch ya muhogo huu mnaotarajia ku-process. Je, wajasiriamali wadogo wadogo wanaweza kuitumiaje starch ya muhogo mtakaotengeneza kama raw material na kuweza kuprocess by products gani zitakazotumika locally?
 
Last edited by a moderator:
Mkuu Mzuzu, aksante sana kwa maelezo ambayo kimsingi yalikuwa ndiyo maswali yangu. Nimemaliza kupiga hesabu za magazijuto hapa na kugundua mkiunga nguvu watu kumi na kuchukuwa ekari 50, kwa gharama ulizotaja at most kila memba atachangia T shs. 1,750,000/= INAWEZEKANA.

Tatizo langu linabaki kwenye bei ya kununulia naona ipo chini au inajadilika?
 
UZOEFU WANGU KUHUSU KILIMO HIKI

Tuwe wakweli ndugu hayo mahesabu uliopiga hapo hayawezekani, mimi nina udhoefu na kilimo cha muhogo, isitoshe mimi mwenyewe nina shamba hukohuko Bungu.

Kusafisha shamba kwasasa ni 50,000 kwa heka, kumbuka shamba ppri lina hatua tatu za kusafisha 1. Kuvunja msitu, 2. Kukusanya mara ya kwanza, kukusanya mara ya pili baada ya kuchoma moto.

3. Kungoa visiki alafu na kuchoma moto tena au kutolewa nje ya shamba, mwisho ndio kulima.

Jambo jingine ni kuhusu mbegu ya muhogo kweli fungu ni 3000 lakini heka moja inaweza kuchukua mafungu hata zaidi ya kumi.

Ghalama nyingine za ziada ni kudhibiti panya na nguruwe huku swala hili limekuwa tatizo kubwa sana maana labda uweke wigo au mfanye ulinzi nyakati za usiku, fikiria muhogo unaotakiwa uwe mzito zaidi utakaa shambani kwa muda gani?

Mwisho wa yote bei iliokuwa inatolewa hapa ni 50 -100 @ kilo na wanataka upeleke muhogo uliomenywa baganda na bado gharama ya kuusafirisha kupeleka kiwandani.

hapo sijataja gharama za palizi kwahuku palizi kwa msimu mmoja tunafanya hata mara nne kutokana na nyasi na rutuba ya udongo, bado gharama za watu watakaovuna pia.

But kila lakheri.
 
Wapo humu, kwa sasa tunapitia MoU yetu, wakati huo huo shamba mojawapo limeanza na tunaendelea na upanuzi. Tukikamilisha usajiri, break ya kwanza ni Rufiji kwa Mzuzu.

Imitulia hiyo kaka mkubwa.. ulipita kipindi flani sikubahatika kukupata mkuu.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom