Kilimo cha matikiti maji (watermelon): Ushauri na Masoko

miche yangu inapukutisha matunda Mara tu yanapotoka.napiga dawa ya ukungu na ya kuuawa wadudu kula baada ya wiki tatizo haliishi.nifanye nini?Niko mbeya
 
Wakuu habari za jioni,

Naomba kama mzoefu wa kilimo hiki anisaidie, nataka kuwa na quotation za gharama za kulima tikiti maji kwa ekari moja katika mazingira yafuatayo.
  • Maji ni ya kisima cha kuchimba (nitatumia generator kusukuma maji)
  • Nitatumia drip irrigation, lakini kwa kuanzia sitaweza gharama za green house, kwa hiyo nitatumia mabomba tuu.
So far nina gharama za kuchimba kisima na kuweka simtank pamoja na gharama za labour charges.

Nahitaji kujua gharama za vitu kama mbolea, drip pipes, mbegu, mafuta ya generator kwa siku, etc. kwa ekari moja,
Mimi sina uzoefu naogopa nisije kuweka inflated budget au ya chini sana nikaumia baadaye.

I am humbled
 
Nahitaji kujua Aina ya Mbegu nzuri za matikiti zenye ubora Na Madawa kwa gharama na kwa majina yake naomba msaada wakuu sijawai kulima matikiti ila kwa kufuatilia humu JF na kujifunza naanza kulima, tayari nimeshapata shamba tayari.

Msaada wakuu
 
Sababu kuu za hayo matatizo ni 3

1. Kuna uwezekano dawa za wadudu unazotumia zinaufito wa njano, daraja la 2 kwa ukali, hivyo lazima maua yapukutike. Tumia dawa za wadudu zenye ufito wa rangi ya kijani, kama vile Actara, au dudu all, au Nimbecidine etc

2. Miche ina water stress, hivyo mmea ni wa moto maua yatatondoka, weka maji mengi kwa siku mche lazima upate angalau 500 mls za maji, kama ni mimea ya maisha ya siku 21-90

3. Mimea yako inaupungufu wa Zinc na Boron, Weka maji , kisha tafuta foliar fertilizer (Booster) kama vile Omex, au Multi K, au Wuxal macro mix, mix mls 80 kwa maji lita 15, na spray kila baada ya siku 14

miche yangu inapukutisha matunda Mara tu yanapotoka.napiga dawa ya ukungu na ya kuuawa wadudu kula baada ya wiki tatizo haliishi.nifanye nini?Niko mbeya
 
Hakuna kukata tamaa Mimi nimepanda Jana Bagamoyo kwa Mara ya kwanza 1.5 hekari nimepanda f 1 sukari East African seed, sina uzoefu sana lkn Nina idea kidogo.

Nahitaji msaada Wa ushauri na Masoko.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom