Kilimo cha matikiti maji (watermelon): Ushauri na Masoko

Ndiyo zipo zinakua na uwezo Wa kuhimili mikikimikiki ya masika.hizi nyingine zinaoza.mi mwenyewe ninampango Wa kulima tikiti la masika kwsbb linalipa.kuna jamaa ni mzoefu zaidi Wa mambo haya ndiye aliyeniwekea oda kiwandani.km utapenda nitakutumia no.yake

Mkuu nami naomba uni inbox hiyo samba
 
Thanks Edmund for this useful information.

Pengine labda utusaidie hatua moja mbele watu kama mm wenye interest ya kilimo. Labda ni wapi unakolima ambako sugar baby inalimwa mara nne kwa mwaka?

Na je maeneo gani mengine ambako kuna sifa kama za huko unakolima? Looks like unahitaji irrigation system ili iweze kulima mara 4 kwa mwaka, je unaweza kutupa some more details kwenye hili pia kwa kesi ya gharama na mambo kama hayo?

Natanguliza shukrani za dhati.

Noimesikia Balton Tanzania
LTD pia wako vizuri kwenye mbegu na ushauri. Labda ungewapitia uje issue za irrigation system
 
Last edited by a moderator:
Za kwako mkuu?vipi umeshapata ile no ya mtu anayejua mbegu bora ya matikiti kipindi cha masika.Naomba unitumie na mm nataka kulima kipindi hiki cha masika.
 
Habari zenu wadau.

Wakuu mimi nataka kujaribu kulima tikiti maji kipindi hiki cha masika. Nitafanya kilimo cha kisasa. Mbegu ni Sukari F1 hybrid.
Tatizo nimekuwa nikipata ushauri tofauti kuhusu kipindi hiki ambacho masika inakaribia kuanza (Takribani mwezi mmoja baadaye) Wengine wanasema Matikiti hayapendi mvua nyingi, wengine wanasema kama nitayahudumia kwa madawa hakutakuwa na tatizo.

Wakuu naombeni mawazo yenu, je inawezekana nikafanikiwa kuvuna kipindi hiki cha masika?

Natanguliza Shukrani.

yaani unataka kujaribu??? bora ukaacha tu mkuu.
 
Ndiyo zipo zinakua na uwezo Wa kuhimili mikikimikiki ya masika.hizi nyingine zinaoza.mi mwenyewe ninampango Wa kulima tikiti la masika kwsbb linalipa.kuna jamaa ni mzoefu zaidi Wa mambo haya ndiye aliyeniwekea oda kiwandani.km utapenda nitakutumia no.yake

Utalaam na ushauri ni muhimu sana ktk kilimo kwa ujumla wake, angalia soko pia. Leo nimepita Ruaha Mbuyuni, matikiti maji yametandazwa barabarani hayana soko kabisa, maskini wakulima wale.

Ila tikiti la masika linalipa sana mkuu, lakini livunwe kabla ya may.
 
Mkuu Malila,hv tikiti la masika unalozungumzia ni la mwezi march to may au hata ili lla la kupandwa kuanzia november to february?
 
Mimi nalima aina ya Sugar baby inachukua siku 60 tu kuvuna tangu plus siku 3-5 za kukaa ardhini, kwa hiyo kwa mwaka nalima mara 4 tu nina ekari 5 na kila eka napata kuanzia 2M-3M.

Spacing ni 2mx2m na kila shimo naweka mbegu 2 ambazo zinazaa matunda 2-3 kwa maana kila shimo napata matunda 4-6 ( wastani matunda 5).

Hivyo kwa spacing hiyo napata mashimo 1000-1200

Idadi ya matunda: Mashimo x Matunda kwa shimo x ekari [1,000 x 5 x 5 = 25,000]

Mapato: wastani wa shilingi 500 kwa tikiti x idadi ya matikiti kwa eneo la ekari 5 [25,000 x 500 = 12,500,000]

Mapato kwa mwaka: 12,500,000 x 4= 50,000,000

Gharama za uendeshaji wa shamba ni Tsh 25,000,000

Faida Kuu ni Tshs 25,000,000 M.

Tujenge taifa letu kwa kilimo

mkuu unalimia wapi??
 
Nikitaka kulima hizi aina za matktk maji, kuna yeyote mwenye idea? ImageUploadedByJamiiForums1413697006.713155.jpg ImageUploadedByJamiiForums1413697017.121066.jpg
 
Sishauri ulime kipindi cha masika ni hatari kumudu changamoto za zao husika.

Kawaida tikiti linapenda joto, ardhi isiyotuamisha maji na kiujumla linapenda liwe exposed kwenye jua muda usiopungua masaa8 kwa siku. Pia kipindi cha utoaji maua maji yanatakiwa kidogo sana na inabidi yasiguse kabisa majani na unashauriwa umwagilie maji asubuhi ili ikitokea kama maji yamelowanisha majani basi yatakaushwa haraka na jua.

Kadharika wakati tunda likiwa changa, likinyeshewa maji kupita kiasi chake lazima lioze.

Kipindi cha kuelekea kukomaa pia napo kuna changamoto kuhusu tikiti maji yakiwa in excess linapasuka.

Nakushauri kama upo mikoa ya ukanda wa pwani unaweza kulima tikiti hata November hii ni Msimu mzuri kwake coz soko la Jan&Feb ni zuri.
 
Sishauri ulime kipindi cha masika ni hatari kumudu changamoto za zao husika.
Kawaida tikiti linapenda joto, ardhi isiyotuamisha maji na kiujumla linapenda liwe exposed kwenye jua muda usiopungua masaa8 kwa siku. Pia kipindi cha utoaji maua maji yanatakiwa kidogo sana na inabidi yasiguse kabisa majani na unashauriwa umwagilie maji asubuhi ili ikitokea kama maji yamelowanisha majani basi yatakaushwa haraka na jua. Kadharika wakati tunda likiwa changa, likinyeshewa maji kupita kiasi chake lazima lioze.
Kipindi cha kuelekea kukomaa pia napo kuna changamoto kuhusu tikiti maji yakiwa in excess linapasuka.
Nakushauri kama upo mikoa ya ukanda wa pwani unaweza kulima tikiti hata November hii ni Msimu mzuri kwake coz soko la Jan&Feb ni zuri.

Mkuu asante sana!haya maelezo naona yametushibisha wengi!
 
Wadau mimi labda naruka mada!naopmba kuuliza,je kwa heka moja ya tikiti maji makadirio ya chini kwa faida ukitoa na majumuisho ya gharama zote unaweza pata hata laki tano kweli kama faida?
 
Wadau mimi labda naruka mada!naopmba kuuliza,je kwa heka moja ya tikiti maji makadirio ya chini kwa faida ukitoa na majumuisho ya gharama zote unaweza pata hata laki tano kweli kama faida?

Mkuu wangu kilimo cha bustani ni changamoto! Faida ipo tena nzuri ya kuridhisha kabisa.

Binafsi nina uzoefu wa kutosha juu ya kilimo cha tikiti maji. Mathalani unataka kulima ekari1 ya tikiti, huu ni mchanganuo mfupi kabisa;

kawaida ekari1=sqm4000
Kwa spacing ya 1m shimo hadi shimo na 2m mstari kwa mstari na kila shimo huwa naacha miche 2 na kuruhusu matunda3.

Na kama utapata mbegu ya hybrid itakuwa vizuri zaidi maana MATUNDA yake yanajiuza yenyewe, shambani ni sh1500.

So ukishusha hesabu hapo juu:
Jumla ya mashina ktk ekari1 ni
Sqm4000÷(1m×2m)×2=4000
Idadi ya MATUNDA =(4000×3)=12000
Mauzo shambani ni 12000×1500=Tshs18,000,000/=
Tatizo ni usimamizi, ila kilimo hiki kinalipa sana!
 
Mkuu wangu kilimo cha bustani ni changamoto! Faida ipo tena nzuri ya kuridhisha kabisa.
Binafsi nina uzoefu wa kutosha juu ya kilimo cha tikiti maji.
Mathalani unataka kulima ekari1 ya tikiti, huu ni mchanganuo mfupi kabisa;
kawaida ekari1=sqm4000
Kwa spacing ya 1m shimo hadi shimo na 2m mstari kwa mstari na kila shimo huwa naacha miche 2 na kuruhusu matunda3.
Na kama utapata mbegu ya hybrid itakuwa vizuri zaidi maana MATUNDA yake yanajiuza yenyewe, shambani ni sh1500.
So ukishusha hesabu hapo juu:
Jumla ya mashina ktk ekari1 ni
Sqm4000÷(1m×2m)×2=4000
Idadi ya MATUNDA =(4000×3)=12000
Mauzo shambani ni 12000×1500=Tshs18,000,000/=
Tatizo ni usimamizi, ila kilimo hiki kinalipa sana!

Mkuu asante sana,hamasa ninayopata ni kubwa sana,naomba namba yakop ya simu tafadhali kama haotojali ndugu yangu,nina mengi ya kujifunza zaidi toka kwako
 
Mkuu Malila,hv tikiti la masika unalozungumzia ni la mwezi march to may au hata ili lla la kupandwa kuanzia november to february?

March to may ndio masika kwa ukanda wa Pwani,nyanda za juu kusini masika huanza november mwishoni mpaka may. Kwa hiyo utaona kwamba,november mpaka february kwa ukanda wa pwani si masika. sasa tikiti maji lenye soko la kufa mtu ni hili la january,february, tikiti la kuanzia may mpaka july huwa ni majanga sababu wakulima wengi huwa wanamudu changamoto za maji mashambani.
 
Asante sana mkuu!nataka nifanye kwa november pale Dar es salaam,sasa sijajua kama kamtaji kangu ka 1 million katatosha au lah!!maana ndio naanza kulima kwa mara ya kwanza ili zao!!na je soko la tikiti la november likoje pale livunwapo january??again thanks mkuu na samahani kwa usumbufu!!
 
Daaaaaaah! !!!!!!!!,menifumbua macho ninalo eneo mkuranga nahisi sijachelewa au vipi wakuu? .
 
Popote tu mkuu alimradi usiwe udongo wa mfinyanzi. Huo ukanda wa Pwani tikiti linastawi tu vizuri ila usilime wakati wa mvua, matikiti hayapatani na mvua, inabidi iwe wakati wa kiangazi na iwe Kwa kumwagilia.

Dah! Eneo ninalo msakuzi mbezi ila ni mfinyanzi. So nisijihangaishe kabisa
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom