Nkobe
JF-Expert Member
- Feb 17, 2013
- 2,162
- 3,162
Wana JF naliongea hili kwa masikitiko makubwa kutokana na hii tabia ya vijana wa Kitanzania. Baadhi ya vijana wa Kitanzania wamegeuka kuwa watafuta maisha kwa njia ambazo haziwezi kuwa na matunda kwa taifa hili wala kwa wao. Vijana wamekuwa wakitaka maisha ya Short cut sana.
Hapa naongelea swala la kilimo. Kumetokea vijana ambao wanakwenda Kenya, wanapata mafunzo ya muda mfupi ya kilimo cha kisasa ikiwemo kilimo cha greenhouse, ufugaji wa samaka wa kisasa nk. Badala ya vijana kujitahidi kuanzisha kilimo cha kisasa wanageuka na kujifanya wataalam "Ukanjanja".
Wakipata mafunzo ya Muda mfupi baada ya hapo ujitangaza kuwa wao ni wataalam wa kilimo cha Greenhouse. Vijana wanageuka kuwa Madalali wa wauza Greenhouse badala ya wao kujikita katika kilimo. Nasema hii baada ya kuona watu wengi wakipata hasara kutokana na kudanganywa juu ya gharama za kujengewa Greenhouse.
Inapotokea hawa vijana wakafanikiwa kukudanganya kuwa wao ni wataalam baadhi ukimbilia Kenya kuleta wajenzi, au wao wenyewe kwa kubahatisha uhamua kukujengea, pia wanakuchaji pesa nyingi sana kupita kiasi, kuna wengine anakwambia kukujengea greenhouse ya ukubwa wa mita 8x30 inabidi uwalipe milioni 3 za ufundi, ambapo hiyo ni kazi ya siku mbili tu, na kama ukienda kwenye makampuni husika unajengewa bure, wewe utawapa chakula mafundi
Nakushauri wewe mkulima, ukitaka kufanya kilimo cha kisasa jitahidi kufanya utafiti kwa njia mbalimbali ikiwemo kwa INTERNET ili upate taarifa sahihi za hicho kilimo. Kwa upande wa greenhouse tafuta makampuni yanayoeleweka, nenda ukapate taarifa sahihi. Pia wenzetu Kenya wako mbele sana katika kilimo hicho, pia waweza kwenda huko ili upate uhalisia.
Jihadharini na vijana wapenda short cut