Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kilimo bora cha nyanya

Discussion in 'Kilimo, Ufugaji na Uvuvi' started by AMARIDONG, Jun 8, 2011.

 1. AMARIDONG

  AMARIDONG JF-Expert Member

  #1
  Jun 8, 2011
  Joined: Jun 24, 2010
  Messages: 2,508
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 0
  Kilimo Bora cha Nyanya
  (Lycopersicum esculentum)
  Utangulizi:
  • Nyanya ni zao la mboga ambalo hulimwa sehemu nyingi duniani
  kwa ajili ya matumizi ya nyumbani na pia kama zao la biashara.
  Asili:
  Inahisiwa kuwa asili ya nyanya ni nchi ya Peru/Equador huko Amerika
  ya Kusini. Mmea huu ulianza kuzalishwa kama zao katika nchi ya
  Mexico na baadaye kusambaa katika nchi nyingine za ulimwengu.
  • Nchi zinazolima nyanya kwa wingi duniani ni pamoja na USA,
  Italia na Mexico. Kwa upande wa Africa nchi zinazo lima ni kama;
  Malawi, Zambia na Botswana.
  Zao hili hulimwa pia katika nchi za Africa Mashariki, ikiwemo
  Kenya, uganda na Tanzania. Kwa upande wa Tanzania mikoa
  inayolima nyanya kwa wingi hasa kwa ajili ya matumizi ya nyumbani
  na biashara ni pamoja na Mkoa wa Kilimanjaro (Hai, Moshi na
  Rombo), Arusha (Arumeru), Morogoro (Mgeta), Tanga (Lushoto),
  Mbeya (Mbeya vijijini) na Singida. (Tazama jedwali namba:1 uk. 36)
  Mazingira
  • Hali ya Hewa:
  Nyanya hustawi vizuri zaidi kwenye mazingira ya joto la wastani
  kuanzia nyuzi joto 18-27 sentigreti. Mvua nyingi husababisha
  mlipuko wa magonjwa ya ukungu kama vile Baka jani chelewa
  n.k.)
  • Udongo:
  Nyanya hustawi kwenye aina zote za udongo kuanzia udongo wa
  6 TANZANIAN-GERMAN IPM PROJECT
  kichanga, mweupe wa tifutifu hadi udongo wa mfinyanzi, ili mradi
  uwe na mboji ya kutosha na usiosimamisha/tuamisha maji. Pia uwe
  na uchachu wa wastani yaani pH 6.0 - 7.0.
  • Mwinuko:
  Nyanya hustawi vizuri kutoka sehemu za mwambao hadi kwenye
  mwinuko wa mita 400-1500 kutoka usawa wa bahari; yaani
  nyanda za chini kati hadi za juu kutoka usawa wa bahari. Nyanya
  zinazopandwa nyanda za juu sana hukumbwa na mvua za mara
  kwa mara ambazo huambatana na magonjwa ya jamii ya ukungu;
  kama Bakajani chelewa (Late Blight)
  Aina za Nyanya
  Kuna aina kuu tatu za nyanya:
  • aina ndefu (tall variety or intermediate) kwa mfano Marglobe
  (M2009 )n.k.
  • aina fupi (dwarf variety) kwa mfano; Roma VF (nyanya
  mshumaa) na Tanya
  • aina chotara, kwa mfano Tengeru’97 n.k.
  Bila kuzingatia maumbile aina nyingine zinazolimwa Tanzania ni
  pamoja na Money maker, Roma n.k.
  • Katika karne hii ya 21, nyanya zinazopendelewa kulimwa zaidi na
  wakulima, ni zile zinazoweza kuvumilia magonjwa, zinazo zaa sana,
  na zenye ganda gumu ili kufanikisha usafirishaji, na kuhifadhika
  kwa siku nyingi bila kuharibika mapema.
  Nyanya zinazoonyesha kuwa na sifa hiyo ni kama:
  a) Tengeru’97 ambayo ina sifa vifuatazo:
  – Huzaa sana kutokana na wingi wa matunda na muda mrefu
  wa kuvuna, ambao hufikia michumo mikubwa kati ya 6-7
  KILIMO BORA CHA NYANYA 7
  kuanzia kuvuna hadi mwisho wa mavuno.
  – Aina hii ina sifa ya kuwa na ganda gumu, hivyo haziharibiki
  haraka wakati wa kusafirisha au kuhifadhi (wastani wa siku
  20)
  – Zina sifa ya kuvumilia baadhi ya magonjwa kama vile ugonjwa
  wa kunyauka
  – Tengeru’97 hustahimili mashambulizi ya minyoo fundo (Root
  knot nematodes)
  b) Tanya
  – Sifa kubwa ya Tanya ni kwamba nayo huzaa sana
  – Huwa na ganda/ngozi ngumu ambayo inazuia kuoza au
  kuharibika kwa urahisi wakati wa kusafirisha au wakati wa
  kuhifadhi kwa muda mrefu.
  – Tanya nayo ina ladha nzuri inayopendelewa na walaji wengi
  NB: Tatizo la Tanya na T97 ni kwamba si kubwa sana kama marglobe
  2009. Lakini ukubwa ni karibu unge karibiana, haujapishana sana.
  Kwa ujumla, ukubwa na wingi wa mazao hutegemea sana matunzo,
  udongo, hali ya hewa na mazingira kwa ujumla.
  1. Kuandaa Kitalu cha Nyanya
  Mambo muhimu ya kuzingatia:
  • Kitalu kiwe karibu na maji ya kutosha na ya kudumu
  • Kiwe sehemu iliyowazi na yenye udongo ulio na rutuba ya kutosha
  • Eneo la kitalu kama ni kubwa liwe tambarare au na mwiinuko kidogo
  ili kuepuka maji yasituame kwenye kitalu, mtelemko ukiwa mkali sana
  nao sio mzuri kwani husababisha mmomonyoko wa udongo.
  • Kitalu kiwe sehemu ambayo haikuwa na zao la nyanya au viazi
  8 TANZANIAN-GERMAN IPM PROJECT
  mviringo (au mazao ya jamii ya nyanya k.m. mnavu, biringanya n.k.)
  • Kiwe sehemu ambayo ni rahisi kupata huduma zote muhimu
  kwa urahisi, ikiwa ni pamoja na uhamishaji wa miche kwenda
  sehemu nyingine. Pia kurahisisha usambazaji wa miche kwenda
  sehemu nyingine.
  2. Kuandaa Matuta ya Kusia Mbegu za Nyanya
  Aina ya matuta:
  – matuta ya makingo (sunken seed bed)
  – matuta ya kunyanyulia udongo (raised seed bed)
  – matuta ya kawaida (flat seed beds)
  • Mbegu zinaweza pia kusiwa kwenye vyombo mbali mbali au sehemu
  nyingine mbali na matuta, kwa mfano; kwenye vikasha vya mifuko
  ya nailoni, masago ya migomba, vijisanduku vidogo vilivyo jazwa
  udongo n.k.
  – Wakati wa kujaza udongo kwenye vyombo hivyo sharti
  udongo huo uwe na rutuba ya kutosha.
  – Udongo mzuri ni ule ulio changanywa vizuri na samadi,
  mbolea vunde au mboji ya kutosha.
  3. Mambo Muhimu ya Kuzingatia wakati wa
  Kuandaa Matuta
  • Tuta liwe na upana kati ya sentimita 90-120, na urefu wowote, [ili
  mradi muhudumu anaweza kutoa huduma nyingine zote kitaluni
  bila kukanyaga miche].
  • Kwatua/lima kina kirefu cha kutosha kiasi cha sentimita 15-20 ili
  mizizi iweze kusambaa vizuri ardhini.
  • Choma takataka juu ya kitalu, au funika tuta kwa nailoni, majuma
  KILIMO BORA CHA NYANYA 9
  4-8 ili kuua vimelea vya magonjwa na wadudu.
  • Wakati wa kuandaa, kitalu, ongeza mbolea aina ya samadi/vunde
  au mboji kwenye udongo kisha kwatua ili ichanganyike vizuri
  na udongo.
  • Changanya kiasi cha debe 1 hadi 2 kila baada ya mita moja (hatua
  moja) mraba.
  • Tuta lisiwe na mabonde mabonde au mawe mawe ambayo yanaweza
  kuzuia usambaaji mzuri wa mbegu kwenye tuta, lisawazishwe vizuri
  ili kuhakikisha usambazaji mzuri wa mbegu na kuepuka mbegu
  kufukiwa chini mno kiasi ambacho hazitaota.
  4. Faida na Hasara za Matuta yaliyotajwa hapo juu
  Matuta ya kunyanyulia udongo (raised seed beds);
  – matuta ya namna hii huruhusu maji, hewa na mizizi kupenya
  kwenye udongo kwa urahisi zaidi.
  – Mazao ya mizizi hupata nafasi ya kutosha kutanuka haraka
  zaidi
  – Matuta haya hayatuamishi maji kama mengine, hivyo
  hutumika zaidi kwenye maeneo yanayokuwa na mvua mara
  kwa mara.
  Hasara:
  Matuta ya namna hii yana sababisha sana mmomonyoko wa udongo
  kama hayakutengenezwa vizuri.
  Matuta ya makingo (sunken seed beds):
  Faida:
  1. matuta haya ni rahisi kutengeneza
  2. hutumika wakati wa kiangazi ili kuhifadhi maji na unyevu
  10 TANZANIAN-GERMAN IPM PROJECT
  nyevu mdogo unaopatikana ardhini
  3. ni rahisi kumwagilia kwa kutumia maji ya mfereji au bomba
  4. huhifadhi unyevu nyevu kwenye ardhi kwa muda mrefu
  5. huzuia mmomonyoka wa ardhi
  Hasara:
  Matuta ya aina hii hayawezi kutumika kwenye maeneo yenye
  mvua nyingi.
  Matuta ya kawaida (flat seed beds):
  Faida:
  – ni rahisi sana kutengeneza kwani udongo ukisha kwatuliwa
  na kusambazwa mbegu huoteshwa
  – ni rahisi kutumia eneo kubwa kuotesha mbegu
  5. Kusia Mbegu
  • Hakikisha ubora na uotaji wa mbegu kabla ya kuzipanda kitaluni
  (germination test)
  • Weka mistari kwenye tuta kulingana na ukubwa wa tuta, lakini
  mistari isiwe chini au zaidi ya sentimita 15-20 toka mstari hadi
  mstari
  • Kina cha mistari kisiwe cha kutisha bali kiwe kati ya sentimita 1-2
  • Matuta yapate maji ya kutosha siku moja kabla ya kusia mbegu. Ni
  vizuri kutumia chombo cha kumwagilia (watering can).
  • Mbegu ziatikwe kwenye mistari na zisambazwe vizuri ili kufanikisha
  usambaaji mzuri wa mbegu kwenye tuta. Changanya mchanga
  laini na mbegu kisha sambaza kwenye mistari iliyoandaliwa
  kwenye tuta.
  KILIMO BORA CHA NYANYA 11
  Mbegu zinaweza pia kuatikwa kwenye tuta bila mistari, lakini
  zisambazwe kwa uwiano mzuri kwenye tuta ili kupunguza msongamano.
  Msongamano husabisha magonjwa ya ukungu (Damping off).
  • Weka matandazo kiasi cha kutosha ambacho hakitazuia kuota
  kwa mbegu.
  • Mara baada ya kuatika mbegu, mwagilia maji kiasi cha kutosha
  kulingana na unyevu nyevu ulioko ardhini
  6. Mambo ya Kuzingatia baada ya kusia mbegu
  pamoja na Matunzo Kitaluni
  • Mwagilia maji kwenye kitalu baada ya kuotesha kulingana na
  unyevu nyevu uliopo kwenye udongo.
  • Miche yote ikisha ota, ondoa matandazo, kisha weka chanja
  ili kupunguza mionzi ya jua ambayo inaweza kuunguza miche
  michanga. (kipindi cha baridi si muhimu sana)
  • Punguzia miche (thinning) ili ibakie kwenye nafasi ya kutosha.
  Hivyo miche ibakie kwenye umbali wa sentimita 2.5 - 4. Hii
  itapunguza magonjwa ya ulemavu na mnyauko, pia itasaidia kupata
  miche bora na yenye nguvu.
  12 TANZANIAN-GERMAN IPM PROJECT
  • Weka matandazo kati ya mistari ya miche ili kupunguza magugu
  na kuzuia kasi ya matone ya mvua pamoja na kuboresha/rutubisha
  udongo.
  • Endelea kumwagilia hadi miche ifikie kimo kinachofaa kuhamishia
  shambani.
  • Punguza kiwango cha umwagiliaji maji, siku chache kabla ya
  kuhamishia miche shambani, yaani siku 7-10.
  7. Kanuni na Mbinu za kuhamisha miche toka
  Kitaluni kwenda shambani (Transplanting
  Rules)
  • Mwagilia miche masaa machache kabla ya kuhamishia miche
  shambani ili wakati wa kung’oa miche mizizi ishikamane vizuri
  na udongo.
  • Kabla ya kuhamisha miche, mashimo yawe yamekwisha andaliwa
  katika nafasi zinazo stahili huko shambani.
  • Miche ihamishwe wakati wa jioni ili kuepuka madhara yanayoweza
  kusababishwa na jua.
  • Kwa ujumla karibu mazao yote ya mboga mboga huwa tayari
  kuhamishiwa shambani yakiwa na majani kamili kati ya 2-6 pamoja
  na mizizi mingi iliyostawi vizuri.
  • Mche lazima uwe na afya nzuri, uwe umenyooka vizuri, hivyo
  miche yote iliyonyongea au myembamba kupita kiasi isichukuliwe
  wakati wa kupeleka shambani.
  • Ng’oa miche kwa uangalifu hasa pamoja na udongo wake kwa
  kutumia vifaa husika ili mizizi isidhurike.
  • Miche ihamishiwe shambani mapema mara baada ya kung’olewa
  toka kitaluni.
  • Wakati wa kuhamisha miche, uangalifu mkubwa utumike ili
  kutoharibu miche/mizizi.
  KILIMO BORA CHA NYANYA 13
  • Punguza mizizi mirefu pamoja na ile iliyopinda kwa kutumia kisu au
  kifaa kilicho na makali ya kutosha (mkasi). Majani nayo yanaweza
  kupunguzwa ili kuongeza kasi ya mizizi kukua na kupunguza upoteaji
  wa maji unaosababishwa na mionzi ya jua.
  • Panda miche shambani kimo kile kile ambacho mche ulikuwa
  kitaluni
  • Wakati wa kupanda miche, hakikisha mche na mizizi imenyooka
  vizuri, mizizi isipinde kuelekea juu
  • Miche ihamishiwe shambani wakati wa jioni ili kupunguza athari
  zinaoweza kusababishwa na mionzi ya jua
  • Wakati wa kuhamishia miche shambani, chagua ile yenye afya tu
  • Mara baada ya kupanda mwagilia miche vizuri maji ya kutosha
  • Mimea itakayo salia bustanini iunguzwe moto au ifukiwe chini ili
  kuepuka kuenea kwa wadudu na magonjwa:
  – magonjwa na wadudu wanaoweza kujitokeza kitaluni na
  shambani ni pamoja na ugonjwa wa kusinyaa/kunyauka
  (Bacterial wilt/damping off), sota, utitiri mwekundu, na
  ukungu/bakajani. (Tazama picha na.1, 2, 3, 4 uk. 39.)
  14 TANZANIAN-GERMAN IPM PROJECT
  Maandalizi ya Shamba la Nyanya
  Shamba la nyanya liandaliwe mwezi 1-2 kabla ya kupanda miche.
  • Mara baada ya kulima choma nyasi juu ya udongo au ondoa magugu
  yote yanayoweza kuhifadhi wadudu na magonjwa ya nyanya.
  • Siku moja au mbili kabla ya kuhamishia nyanya shambani, mwagilia
  sehemu iliyoandaliwa kwa ajili ya kuhamishia nyanya.
  • Andaa mashimo ya nyanya kutegemeana na idadi ya miche
  uliyonayo, nafasi na aina ya nyanya.
  • Nafasi kati ya mche hadi mche ni wastani wa sentimita (50-60)
  x (50-75) kutegemeana na aina au zao litakalo changanywa na
  nyanya.
  Jinsi
   
 2. m

  mchafukuoga Member

  #2
  Jun 8, 2011
  Joined: Apr 17, 2011
  Messages: 26
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  hongera kwa makala mr patric
  hebu tujuze kuhusu root knod nematodes hapa ndio pana mziki .
  nilishawahi kulima nyanya kule mbagala lakini hawa nematodes wanasumbua
  nilitumia furadan na mocup lakini bado hebu tujuze kama una mpya kuhusu hawa nematodes.
   
 3. Zuia Sayayi

  Zuia Sayayi JF-Expert Member

  #3
  Sep 16, 2012
  Joined: Mar 28, 2011
  Messages: 817
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Asante kwa somo zuri mkuu
   
 4. t

  tajirisana Member

  #4
  Sep 17, 2012
  Joined: Sep 29, 2010
  Messages: 83
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 15
  asante kwa somo zuri
   
 5. The dirt paka

  The dirt paka JF-Expert Member

  #5
  Oct 2, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 371
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  ahsante mwezi huu nina project ya kulima nyanya. Umenipa maarifa
   
 6. K

  Kajole JF-Expert Member

  #6
  Sep 17, 2016
  Joined: Apr 12, 2011
  Messages: 390
  Likes Received: 128
  Trophy Points: 60
  [quote uid=8624 name="Malila" post=1489345]Asante dada,<br /> <br />Kiasi ninachofahamu ni kidogo sana,ila njaa ndio imenifanya niyatafute na kuyajua haya mambo,ukiachia mbali kuwa elimu ya kilimo nilipata kidogo kwa vitendo. Pili huku ktk kilimo ushindani sio mkubwa kama ktk biashara nyingine. karibu.[/QUOTE]<br />habar jaman?,<br />hvi sasa npo shamba nachimba mashimo kwaajili ya kupandikiza miche ya NYANYA aina ya TANYA. Naomba mnisaidie kwa ekari moja natakiwa kupata MASHIMO MANGAPI ya kupanda miche?<br />je nikiweka mbolea ya mbuzi kidogo na DAP kwa kila shimo kuna tatizo?,pia yeyote mwenye ushaur zaid anisaidie. Eneo lenyewe lipo Iringa ktk wilaya ya Kilolo hvyo kuna baridi(Malila unalifaham eneo hili ni kijiji cha Masege jiran na kihesa mgagao)<br />pia kuna eneo limebaki la ukubwa wa 20*100 nafikiria kulima bamia je zitakubali kwa hali hii ya hewa?, sina shaka na soko nimeshatafiti hvyo nmepata<br />asanten sana
   
 7. trem

  trem JF-Expert Member

  #7
  Sep 17, 2016
  Joined: Sep 19, 2014
  Messages: 264
  Likes Received: 98
  Trophy Points: 45
  safi sana
   
Loading...