Kilimo Biashara na kampuni ya Namaingo Business Agency

Hao jamaa ni matapeli kupita kiasi, mara sijui kijiji biashara eti ili mtimie kundi kisha hiyo mikopo ianze mnatakiwa mfikie 1500!! Kwa mazingira haya mshawishiane mpaka mfikie 1500 ni lini? Ukitaka kujua hawa jamaa ni matapeli huoni huyu aliyeanzisha uzi mpaka hajatoa ufafanuzi mpaka leo. ukifanikiwa kuwapigia cm wanakuuliza uko wapi kisha wanakupa maelezo ya mradi wanaotaka kufanya.eneo hilo. Ila utapewa namba mara wasiliana na huyu, mara yule, full utapeli.
 
Namaingo business agency ACHENI UTAPELI, MUNGU ANAWAONA JAMANI
Threads zote hapo juu watu wanaonyesha LIVE mmewapiga...
 
huu ni ulaghai kama utapeli mwingine wowote unaoendelea hapa bongo. Hawa wanaitwa wakulima wa keyboards au kwa jina lingine wauza maneno. watakuambia utoe 100000 tsh ya form wanapiga bla bla nyingi hakuna jipya. wao interest yao no hiyo laki moja ya kingilio. wao wapo ukonga mombasa. jiulize huko kuna Mashamba? Waambie wakuonyeshe Mashamba yao yako wapi ili ukajifunze huko. wakikuonyesha natembea uchi toka kariakoo hadi mbezi. Mtu anaambiwa eleza vizuri anasema piga simu. kueleza si rahisi kwa kuandika hapa kuliko watu elfu moja kupiga simu? Watu wengi wamedanganyika na hawa wauza maneno. Huwezi kuwaongoza watu kwenye kitu ambacho wewe mwenyewe ufanyi. wanakuambia tutakuanzishia shamba. jiulize kwanini wao wasianzishe ya kwao? Hawa na Amsha ni ndugu moja. Wanaongea kama wahubiri wa kilokole waulize maswali sasa ndiyo utachoka. Mimi sina mengi ni hayo tu.
Kwel mkuu usemacho nkuunga mono huy jamaa cjmpt vzr ila anaonekn mfisidi na mchoyo wa material
 
Jamaa hawa nliwah hudhuria semina yao tarh 22/10/2016 mjin iringa ktk ukumbi uliopo chuo kikuu cha Ruaha yaan RUCU. Alikuwepo mama NAMAINGO,Mkuu wa mkoa,mkuu wa chuo na NSSF. Waliongea meengi na maigizo ambayo sikuelewa hata kidogo nkaona labda yale malecture rooms yamenipa stress ndo maana sikuelewa ngoja niwafuate ofisin kwao.
Jamaa hawa ni MATAPELI wakubwa: waliniuzia vipeperush vyao kwa sh 2000,Eeeh nkahoji nan anatakiwa kulipwa ni mimi ninaewatangaza au wao wanaotangazwa?,ooh hyo ni hela ya maji ya ofisi khaa-PUMBAVU!. Ok mnafanyaje sasa shughuli zenu,.
Tunaanzisha kijiji cha KILIMO BIASHARA,ntarudi
 
Hallo, si kweli kama unavofikiria naombeni kuandika Maelezo kama ifuatavyo
Ninyi kweli ni matapeli haya ona alivyokimbia, leta hayo maelezo ya kitapeli hapa ambayo unayatunga huko sasa hivi. No wonder umeshindwa hata kuleta hayo maelezo.
 
Tunaanzisha kijiji cha kilimo biashara yaan sisi namaingo tunaomba eneo wilayan mfano ekari 500 then tunawamilikisha wanachama wetu,halafu tunaingia ubia na JKT wao watayasafisha mashamba hayo na kujenga mabanda wakishirikiana na wataalam wa kilimo.
ok mfano mi npo mafinga na mashamba mmepata kilolo itakuaje?,
jibu: Hiyo isikupe shida wewe utakuwa unakuja shamba mara moja moja tu maana kutakuwa na waangaliz wa kutosha tu...HAPA NAPO PALINIFIKIRISHA HLO SHAMBA NI LANGU KWEL?.
OK mtaji wa yote mi sina inakuaje?.
jibu: ww ni kuchagua moja kati ya mazao au mifugo elekez then NAMAINGO itakudhamin upate
 
NB: Hvi mkuu wa mkoa alifanya utafiti vzur mpaka ku2ma wawakilishi wake pale?,je tukitapeliwa yeye RC hawez kuwa amefacilitate maana uwepo wake pale unawaaminisha watu kuwa ni jambo jema maana hata kiongoz wetu yupo. MI UKWELI NATAKA KWENDA KWA RC aniambie uhakika wa hawa jamaa NAMAINGO kuna 12000 yangu tayar wamechukua kwaajili ya form

Ukiingia tu ofisin kwao hapa IRINGA unahisi utapeli maana ni ndugu tupu...baba ndo meneja,mtoto mkubwa ni mratibu,anaefuata ni mhasibu,wa chini ni secretary yaan wote ni ndugu wa baba na mama mmoja kama
 
Jamaa hawa nliwah hudhuria semina yao tarh 22/10/2016 mjin iringa ktk ukumbi uliopo chuo kikuu cha Ruaha yaan RUCU. Alikuwepo mama NAMAINGO,Mkuu wa mkoa,mkuu wa chuo na NSSF. Waliongea meengi na maigizo ambayo sikuelewa hata kidogo nkaona labda yale malecture rooms yamenipa stress ndo maana sikuelewa ngoja niwafuate ofisin kwao.
Jamaa hawa ni MATAPELI wakubwa: waliniuzia vipeperush vyao kwa sh 2000,Eeeh nkahoji nan anatakiwa kulipwa ni mimi ninaewatangaza au wao wanaotangazwa?,ooh hyo ni hela ya maji ya ofisi khaa-PUMBAVU!. Ok mnafanyaje sasa shughuli zenu,.
Tunaanzisha kijiji cha KILIMO BIASHARA,ntarudi
Duuu!!! Vipeperushi havilipiwi aisee
 
Aise hata mimi kidogo ningeshawishika kuingia huko ila nilipowapigia nikaambiwa talalile za hapa na pale kweli SERIKALI yetu haina UCHUNGU na wananchi wake nakumbuka DECI serikali ilikuwa inajua fika lakini iliiacha DECI ili waje kuchua hela za wananchi.
 
Back
Top Bottom