KILIMI: Kuna ukweli kuhusu hili?

Mtumishi Mkuu

JF-Expert Member
Mar 31, 2011
259
92
Heshima mbele wakuu.

Ninaomba kwa wale wataalamu, nina mwanangu ana miaka mitatu, siku za hivi karibuni ameanza kukohoa sana haswa anapolala na akila wkt mwingine anatapika. Hospitali tumempeleka akachekiwa tukaambiwa ni hali ya hewa tu maana hana ht homa.

Kuna mtu nimemwambia khs hili akadai inaweza kuwa ana kilimi ambacho kinamsababisha akohoe, hivyo atatakiwa kikakatwe. Je, hili laweza kuwa sawa? Ni sahihi kumkata mtoto kilimi? Natanguliza shukrani
 
Inawezekana kuwa mtoto ana allergy fulani mfano vumbi,mayai etc.Option 1 kamuone daktari mmoja pale Namanga kama uko DSM siku ya j'pili amfanyie kipimo cha allergy ili uwe na uhakika zaidi.

Option 2.Chukua na kamua vitunguu saumu 5 na vitungu maji 5.changanya na asali vijiko 3 mpe mtoto teaspoon X3 kwa siku.
 
Am not sure kama najua kuhusu hii, lakini ushauri wangu ni kuwa kama ni kukata kilimi ifanywe na daktari ENT, na ifanyikie hospitali. Kuna mtu alishanisimulia alikurupuka akaenda kkoo kukatwa na vyombo havikuwa sterile wala hakukuwa na ganzi. Alipata infection kidogo imuue!

Japo in the back of my mind, sidhani kama anahitaji kukatwa.
 
Mkuu Mgalatia nashukuru kwa hizo options zako 2. Nipo DSM, na nitajitahidi kwenda kumwona huyo dk maana nimekumbuka kuna mtu alishaagiziwa kwako kipindi fulani kwa ushauri kuwa ni dk mzuri kwa watoto. Hiyo option ya pili nilishaijaribu ikafanya kazi kwa muda then hali imejirudia. thanks again
 
Am not sure kama najua kuhusu hii, lakini ushauri wangu ni kuwa kama ni kukata kilimi ifanywe na daktari ENT, na ifanyikie hospitali. Kuna mtu alishanisimulia alikurupuka akaenda kkoo kukatwa na vyombo havikuwa sterile wala hakukuwa na ganzi. Alipata infection kidogo imuue!

Japo in the back of my mind, sidhani kama anahitaji kukatwa.

Nashukuru kwa ushauri King'asti. Nitajaribu kutafuta specialist wa watoto km nilivyoshauriwa
 
Be carefully with kids, take necessary precaution to any medication. consult people with who are professional. kama ni kilimi go to Muhimbili they are experts in ENT don't go any other places, they my be experts BUT poor in Anesthesia and equipments
 
Thanks for the caution! Will surely give it its due care
 
Mzee mnyime vitu vyote vya baridi hali itaisha.Saa nyingine watoto wanagawana ice cream,hakikisha hatumii vitu vya baridi.
 
Heshima mbele wakuu.
Ninaomba kwa wale wataalamu, nina mwanangu ana miaka mitatu, siku za hivi karibuni ameanza kukohoa sana haswa anapolala na akila wkt mwingine anatapika. Hospitali tumempeleka akachekiwa tukaambiwa ni hali ya hewa tu maana hana ht homa. Kuna mtu nimemwambia khs hili akadai inaweza kuwa ana kilimi ambacho kinamsababisha akohoe, hivyo atatakiwa kikakatwe. Je, hili laweza kuwa sawa? Ni sahihi kumkata mtoto kilimi? Natanguliza shukrani

Kwanza kabisa hakuna ugonjwa unaoitwa KILIMI, ila hiki ni kiungo cha mfumo wa matezi mwilini (Lymphatic System).
Kazi yake kubwa ni kupambana na maambukizi ya aina yeyote yale yaliyotokea mwilini.

Kukohoa kunaweza kusababishwa na maambukizi ya aina yeyote yale yaliyotokea katika mfumo wa upumuaji wa juu au wa chini kutokana na bacteria au virus.

Kazi kubwa ya kilimi ni kuakikisha maambukizi ya aina kama haya hayaleti madhara katika mwili wa binadamu, kitafanya kazi kadri ya uwezo wake wote, kizidiwa kinahitaji msaada wa dawa ili kumaliza maambukizi hayo. (Kilimi kinapopambana na maambukizi mwili, ukitazama utakiona kimevimba, kinauma na kinabadilika rangi na kuwa chekundu)

Mpeleke mtoto hospitali inayoeleweka ili akapate matibabu ya kukohoa yaliyo sahihi.

Husidanganyike na maneno ya mtaani.
 
Asante mkuu. Nadhani ushauri mwingi unanielekeza niende kwa wataalamu hosp. Nitalifanyia kazi hili wkend hii. Thanks to all for your advice
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom