sijui nini
JF-Expert Member
- Sep 29, 2010
- 2,553
- 1,285
mambo yote oct31 tu!!
zakwako zenye mvuto na zilizo ndani ya uwezo wako ziko wapi tuzisome? uchambuzi wako wa kisayansi na kisomi uko wapi ndugu nikazisome? labda mwenzetu unauwezo wa kuchanganua mambo na labda makala zako ni more analogy!!! tafadhali naomba nisome makala zako ili niweze kuzilinganisha na za Majjid kwani unaonesha wewe ni mahiri zaidi ili tunufaike na uchambuzi wako!! usiandike kwa mate na hali wino upo!!!
Duu nyie watu, mmedata:
Chai Na Chapati Ya Maji Nyumbani Kwa Kaka Michuzi
Leo nilipata heshima ya kukaribishwa nyumbani kwa ndugu yangu Muhidin Issa Michuzi. Hapo nikakaribishwa chai ya nguvu iliyowekwa viungo na kitafunwa cha chapati ya maji. Mchana ukaingia, ikawekwa pilau ya nyama mezani na vyote vyenye kuendana nayo. Basi, nikiwa na Michuzi huwa tuna mengi ya kuongea, kukumbushana na kucheka pia. Nikirudi Iringa nitajitahidi nipike chapati ya maji!
Na wewe mtani wangu kwani ni lazima ujibu kila kitu?
Wewe kama mwandishi uwe unaandika tu unayoyaona yanafaa kuandika.
Sisi kama Wasomaji tutasoma na kuamua kama kweli wewe ni MWAANDISHI kweli au na wewe ni Chambio la Mafisadi.
Jisikie huru kuandika unachotaka na sisi tuache tuwe HURU kukutafutia kundi unalostahili kuwa.
Acha kuandika na baadaye kuja hapa KUTETEA maelezo yako. Hata uandike kumsifu Slaa, wengine bado watakushambulia.
Nafuatilia sana makala zako. Mwenye akili anakuelewa na asiye na akili basi kazi kwake. Kuna wengine wanataka kutafuniwa kila kitu ila ujumbe wako wa kijibwa cha Manzese, ulisema yote.
Mbona hatukaribishani kwenye Ulanzi sasa? Mie ngoja nisema, karibu basi Sikonge, maembe yataanza hivi karibuni.
Wapenda chapati wewe!!! eeeh!
Haya bana! Ina maana JK anweza kuwapa shavu la U-DC watu kama hawa!!! Wapendao chai na pilau, siju nn!!!
Kazi ataikamilishaje??
Huyu Mjengwa ni mmoja kati ya wale waliodandia field ya uandishi bila ya kupata mafunzo ya kina. Huyu si muandishi bali ni mbabaishaji tu. Asiwaumize vichwa kabisa.
Kiuhalisia CCM hawana jipya na hilo halina ubishi. Ahadi hizi ni zile zile miaka nenda rudi kama wanavyofanya katika Bunge la bajeti. Lakini strategy za kuwaong'oa nazo bado ni loose. Inahitajika organisation ya kueleweka yenye kuweka wanafiki kando, wabaguzi wa kidini au kikabila pembeni, maslahi ya nchi mbele, ubabaishaji na udikteta mbele na maadili yaliyotukuka hapo ndio nchi yetu itakombolewa kwa sasa ni blah blah yu ndio zinaendelea.
Mjengwa mbona hukutuambia ulichokiona uwanja wa Sanora alipotembelea JK na pia kutoa uchambuzi wa strengths na weaknesses zake. Bado inaonekana unaogelea kwenye dimbwi la kutaka kutuaminisha CCM na JK are perfect na wengine ni wakulinganishwa.