Butola
JF-Expert Member
- Jan 19, 2010
- 2,290
- 756
- Huenda Dr Slaa hapati muda mwingi wa kutafuta taarifa zenye kuwagusa watu walio mbele yake kumsikiliza. Kuwa watu wengi walijazana pale Mwembetogwa jana kwa mtazamo wangu kunachangiwa pia na namna CCM ilivyoboronga katika kumpata mgombea ubunge jimbo la Iringa Mjini. Miongoni mwa waliomsikiliza Dr Slaa jana pale Mwembetogwa ni wanachama na wapenzi wengi wa CCM. Na ajabu kubwa kabisa; Dr Slaa tangu mwanzo hadi mwisho wa hotuba yake hakutamka jina la " Mama Monica Mbega". Mgombea Ubunge wa CCM, Iringa Mjini. Hata mgombea wa CHADEMA Mchungaji Msigwa alipopewa dakika tatu na Slaa aongee, naye hakutamka jina la " Monica Mbega" na kwanini wana Iringa Mjini wasimchague Monica Mbega.
Hili linapaswa kufanyiwa kazi, hii ilikuwa ni fursa nzuri ya kuwaeleza WanaIringa umuhimu wa wao kumchagua Mchungaji Msigwa badala ya Mama Mbega.