Kilichonikera/kunifurahisha kuhusu Maadhimisho ya Miaka 50 ya Uhuru

Sioni chochote kilicho fanywa cha maana,ni hela nyingi zimeisha bure bila
kuacha Symbol yoyote ili watakao kuwepo kwenye sherehe za miaka 100 waje kuona
tulipopata uhuru kulikua na hiki,tulipo fikisha miaka 50 kilifanyika hiki,....etc

Kwa mfano,kama individual,mbowe katika maadhimisho ya
miaka yake 50 kapanda miti mingi kweli huko kwao,....hapo hata miaka 30 ijayo kila mtu
huko hai atajua hii miti ilipandwa na mbowe alipokuwa 50.

At 100 kizazi hicho kitasimulia utumbuaji wa mali waliokua nao mababu zao
 
kilichonikera mimi ni kuchukua watoto wa zanzibar na kuwaleta huku tanganyika eti watoe shoo ya halaiki,nimeshindwa kujua kama walikosa watto huku kwetu? pili gwaride la jwtz limenikera,maana sikutegemea kama wanatumia vifaa vya zamani kiasi kile,SAMs + fighter jet bado ni za zaman sana.hii ni aibu kwa nchi then kumuweka rais wa zenji just beside mkuu wa kaya-kaniudhi-he was just like other invited guests,alitakiwa akae sehem nyingine
 
kutimiza miaka hamsini kwa kitu chochote au jambo lolote is a milestone achievement.

kero yangu kubwa ni kwa hii milestone kufikiwa huku nchi ikiwa na ombwe la uongozi ambalo halijawahi pata kutokea.
so, si jambo la kushangaza nikufahamisha kuwa kero yangu hii si ya jana wala juzi but it's dating back to 2005 baada ya jina la ccm presidential candidate kujulikana.
Looks like self disgust.
 
Rafiki yangu mwanakijiji,
Kwangu mimi sioni kama kulikuwa na umuhimu wa kutumia karibu bil 70 kusherehekea. Hivi tunapongezana nini? Nini tofauti kati ya wakoloni tuliowafukuza na viongozi waliopo madarakani? Wanaishi ktk nyumba zile zile za wakoloni na kuendeleza sheria zile zile.
Nitataja mifano michache.
Wakoloni walikuwa wanajenga hospitali, bara bara, shule kiduchu ukilinganisha na mapato wanayovuna nchini kwetu, tulilalamika tukawatimua. Leo vipi? Kodi inayokusanywa inaendana (Proportional ) na tunachokivuna - yaani huduma ya hosp, bara bara na ubora wa elimu. My response is NO.
Wakoloni walivuna mengi wakapeleka kwao kwa faida yote. Tukawafukuza. Vipi leo? Madini, wanyama hai wanabebwa mchana kweupe? Tunasherehekea nini ?
Wakoloni walikusanya kodi ambayo haikuwasaidia watz,tukawafukza. Leo kila kitu kinatozwa kodi hadi marehemu analipa kodi kwa kuwa hata jeneza inalipiwa kodi- VAT. Tunasherehehekea nini?
Nyerere alipaochia ngazi, 80% wanajua kusoma na kuandika( KKK), Leo ni 63- 65% watz wanajua kkk ( takwimu za UN) Tunarudi nyuma halafu tusherekee tena au tuomboleze?
Miaka 50 baada ya uhuru wanakufa akina mama wajawazito 24 hadi 36 kwa siku wakati wa kujifungua kutokana na huduma mbovu. Tunasherekea vifo vya wamama na shangazi zetu AU tuomboeleze?
2011 tumeambiwa Tz ni nchi ya KWANZA Afrika na ya 3 duniani kupokea misaada. Misaada inayoishia mifukoni mwa wajanja. Tunasherekea umatonya wa kimataifa?
Serikali inajisifia takwimu za kuongezeka kwa idadi ya vyuo vikuu, lakini hawatoi takwimu ya tija inayotokana na wanafunzi hao wa vyuo vikuu?
Rais katuambia 30% ya mapato ya serikali yanapotea kifisadi. Hii ni zaidi ya bil 4 ukilinganisha na tril 13 ya bajeti ya mwaka huu? Ni pesa nyingi sana. Je, tusherekee jinsi tunavyoibiana?
Mkuu mimi naomboleza, sisherehekei. Sina cha kusherehekea. Kinachonikera ni watu kusherehekea msibani.
we kule kwenu umbuluni ni wangapi wenye elimu? Nani kakuambia kuwa ukijua kusoma na kuandika tayari umefuta ujinga (au ndo umeedelea)? Basi kama ndo hivyo shule za msingi tu zilikuwa zinatutosha. kuna haja gani ya kuwa na sekondari na vyuo? Hili ndo tatizo la upeo mdogo wakufikiria.
Na mbaya zaidi ni kuwa hujijui kuwa upeo wako ni mdogo.
 
Looks like self disgust.

self disgust = a painful emotion resulting from an awareness of inadequacy or guilt = yes guilt in the context that we (me included) have put so much trust in these useless fnckiug politicians!
 
Najua wapo waliokerwa hasa na dhana kuwa miaka "hamsini" haihusiani na "Tanzania" wala "Tanzania Bara" bali yanahusiana na "Tanganyika". Hawa walipenda maadhimisho yaitwe kwa haki kabisa kuwa ni ya uhuru wa "Tanganyika". Tukiondoa hilo ambalo ni dhahiri kwa baadhi ya watu kuna vitu vingine vimekera sana kiasi kwamba unatamani hata siku kuu nzima ingeahirishwa hadi tuweze kuipatia.

Umeona toka Januari - Rais alipotangaza maadhimisho haya makubwa - taasisi zikifanya maonesho, matangazo ya kiile kinachoitwa "mafanikio ya miaka hamsini". Lakini kilele cha yote ni maadhimisho makubwa yaliyofanyika Alhamisi usiku (sijui mikoani walifanya nini siku hiyo) na yale ya Uwanja wa Uhuru. Na kati ya hapo pote kuna mengi yamefanyika.

a. Je umefurahia kuwa maadhimisho yameenda kama ulivyotarajia?
b. Je, kuna vitu ambavyo ulidhani vitafanywa lakini havikufanyika?
c. Je vile vilivyofanyika vimefanyika kwa uzito unaoonekana.
d. Taarifa za sasa kwamba tumetumia karibu bilioni 70 kufanikisha maadhimisho haya unaamini yameendana na hela zilizotumika au ni fedha kidogo sana au nyingi sana?


Kama unaona hakuna kilichokukera bila ya shaka kipo kilichokufurahisha sana na unatamani yakifanyika ya Muungano basi yafanane na haya.


Binafsi sioni tunasherekea uhuru upi? maana bora tungeendelea na ukoloni wa wazungu kuliko huu wa CCM, kwa makada wa CCM ni sawa kusherekea lakini kwa waTZ wa kawaida huu ni upuuzi na kupotezeana muda,

Miaka 50 ya uhuru, shule nyingi Dar watoto wanakaa chini?
Miaka 50 ya uhuru, wahindi, wazungu na wachina ndio wanamiliki uchumi?
Miaka 50 ya uhuru, hadi wakenya na waganda wanatutawala?

Uhuru wa kweli utapatikana siku CCM ikitoka madarakani tu.
 
Mkuu kilichonikera mimi ni unafiki wetu sisi wenyewe Watanzania. Unafiki huu utatumaliza kabisa maana watu wanatukana matusi yote lakini wao ndio washiriki wakubwa wa mipango ya kufuja fedha. Kuna mtu namfahamua ambaye amelaani sana matumizi mabaya ya fedha ktk sherehe hizi lakini yeye alikuwa mmoja wa watu walioomba tenda za kufanya kazi fulani (supply) na hakuipata. Laana yake ni kukosa channel hiyo na sii kuchukia matumizi mabaya ya fedha.

Na kweli mkuu wangu habari za mjini zinasema watu wametengeneza mifedha, yaani wametoka sii mchezo! na kibaya zaidi ya yote walipeana hizi deal za kutengeneza fedha na siii kuadhimisha, hivyo wanaziita sherehe kwa sababu walitengeneza faida ya mwaka mzima kwa kazi moja.

Sasa kama wewe kweli unalaani sherehe hizi uliomba tenda ya nini?..Pili, inasikitisha zaidi kwamba bado tunaendelea na mila za Kikoloni na Kikomunist kuadhimisha siku kwa kufuata ratiba na mfumo wao ambao serikali ndiye mtumizi mkubwa wa mfuko wa pato la taifa kwa vitu vya kipuuzi kama hivi. Hivi kweli tunashindwa kufanya maandamano (Parade) ya ngoma zetu za asili juu ya magari (Semi -Trailer trucks) ya kukodisha tuseme kutoka Mjini hadi viwanja vya Mnazimmoja ambako kama sikosei ndipo sherehe za kwanza zilifanyika - Na tuliujenga mnara pale kama kumbukumbu ya Uhuru au nakosea?.

Serikali yetu imekuwa na matumizi mabaya sana na sielewi kwa nini tunapenda sana kusifia vitu vilivyopendeza na sii kutazama matumizi yake kama yalikuwa muhimu. Nadivyo alivyosema jamaa yangu hapo nyuma kwamba tunapenda sana matumizi yasiyokuwa ya msingi - Mahari kubwa, Kitchen Party, Send off, na Reception sherehe za siku zisizopungua 7, wakati mume na mke hawana kazi ama hata sehemu ya kuishi. Halafu basi sii kwamba ndoa imemwondoa mume?mke kwa wazazi wao - hapana!. Mume/Mke bado anahesabu familia yake ya kwanza ni Baba, Mama na ndugu zake. Kuolewa sii hoja kesho unaweza kuachika ukarudi kwenu...sasa sherehe kubwa zote za nini ikiwa huamini ndoa hiyo ama niseme bado tumetawaliwa.

Ni mila kama hii inayotufanya hata Uzalendo ni mgumu sana kupatikana kwa sababu Utaifa ni kitu cha pili, Utaifa hautupi fikra za kuwa familia moja isipokuwa tumeunganishwa kama chanya za chungwa kila mmoja wetu anajitegemea kivywake na kila mmoja maslahi yake yako kwenye chimbuko la FAMILIA YAKE (Ukabila), Utaifa ni familia ya pili. Kuondoa Ufisadi ni dhana ambayo haiwezi kutekelezeka bila kwanza kujitazama sisi wenyewe na kuyakubali makosa yetu.
 
Kwa mliokuwa uwanjani na mlioanngalia TVz, Je, kulikuwa na a minute of ukimya kuwakumbuka mashujaa wetu wapigania uhuru waliotangulia mbele za haki?????????????????????????????????????? Hakuna hata mahali palipojengwa artificial chemichemi kuonyesha ishara ya mafanikio yasiyo na ukomo???????? UHAI wa wapigania UHURU unaodumu kwa ishara milele yote? Uwiiiiiii
 
Ingawa naamini Maendeleo ni hatua lakini nafikiri sisi tunapiga hatua kwenda nyuma badala ya kwenda mbele.

Mbaya zaidi ni kwamba hatujakubali kwamba tunapiga hatua kwenda nyuma. Kwa minajiri hii hatuwezi kujirekebisha.

Ni vizuri kusherehekea hatua zako hasa Kama unaenda mbele. Na si vibaya kuomboleza na kupanga mikakati Upya Kama unasonga kwenda nyuma.


Kwa ushauri wangu tulistahili kuomboleza na kujipanga Upya zaidi ya kusherehekea . Nawakilisha
 
Kauli mbiu ambayo haina uwiano halisia,kujikweza tu

Pamoja na fedha kibao zilizotumika hakuna mradi wowote wa kumbukumbu kuonyesha dira ya huko tunakotaka kwenda
 
Back
Top Bottom