Kilichomwangusha Sumaye chatajwa

Hasomi alama za nyakati. Akae tu ale pensheni yake. Mwisho wa yote atapata aibu tu
 
tupo kisiasa hapa bwana..jadili kuhusu kupigwa chini kwa sumaye na anavolialia kwamba lowasa ndo reason eti!

Amesema ataitisha mkutano na wanahabari!
Nna hamu ya kumsikia akiropoka.
Nitam under rate akithubutu kuropoka eti amepigwa chini na kambi ya Lowassa
 
SIASA za makundi ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), zimetajwa kuwa chanzo cha kuangushwa kwa Waziri Mkuu Mstaafu Frederick Sumaye katika nafasi ya Ujumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM (Nec), kupitia Wilaya ya Hanang’ Mkoa wa Manyara.

Sumaye ambaye anatajwa kuwa ana nia ya kugombea urais katika Uchaguzi Mkuu ujao, alishindwa na Dk Mary Nagu ambaye ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji na Uwezeshaji).

Katika uchaguzi huo, Sumaye alipata kura 481 dhidi ya Nagu, aliyepata kura 648.

Mbali na Sumaye, wajumbe wengine waliokuwa wakimuunga mkono akiwamo Mwenyekiti wa CCM wa wilaya hiyo, Goma Gwantu, pia walishindwa katika uchaguzi huo.

Dalili za kushindwa kwa Sumaye, ambaye alikuwa akiungwa mkono na wajumbe wa kamati ya siasa ya CCM wa wilaya hiyo, zilianza kuonekana wiki moja kabla ya uchaguzi huo.

Kambi ya Dk Nagu ambayo inatajwa kwamba inaungwa mkono na kambi ya Waziri Mkuu Mstaafu, Edward Lowassa, ilionekana kuwa na “ushawishi” mkubwa katika vikao vya kamati ya siasa ya mkoa na kwenye Kamati Kuu ya CCM.

Hali hiyo, ilitokana na ukweli kuwa Dk Nagu kama taratibu ambazo zilihitajika, hakupewa baraka na kamati ya siasa ya wilaya hiyo, kugombea kwa kile ambacho kilielezwa kukwepa mpasuko wa CCM Hanang' na pia kumpa heshima Sumaye.

Hata hivyo, habari zimeeleza kuwa tofauti na msimamo wa Kamati ya Siasa ya wilaya hiyo, Kamati ya Siasa ya Mkoa wa Manyara, ilionekana kumuunga mkono Dk Nagu hasa kutokana na ukweli kuwa karibu nusu ya wajumbe wa kamati hiyo walikuwa wagombea.

Kikao cha kamati ya siasa ya mkoa, licha ya kurejesha jina la Dk Nagu pia, kilipendekeza kuondolewa majina ya wagombea kadhaa katika wilaya ya Hanang' likiwamo jina la Mwenyekiti wa wilaya hiyo, Goma Gwaltu ambaye alikuwa kambi ya Sumaye.

Taarifa za kupendekezwa kuondolewa majina ya wanaomuunga mkono Sumaye, zilitolewa na baadhi ya wajumbe wa Wilaya ya Hanang’, lakini hata hivyo, Katibu wa CCM Mkoa wa Manyara, Ndeng'aso Ndekubali alizikanusha.

“Kamati ya siasa ya mkoa ni kikao cha siri na nadhani ni mapema mno kulalamikia suala hilo, ni vyema wakasubiri uamuzi wa juu, ” alisema Ndekubali.

Hata baada ya kurejeshwa majina na Nec, ilibainika kuwa wagombea ambao Kamati ya Siasa ya Wilaya hiyo, iliwapa alama za chini, wamerejeshwa katika mchakato wa uchaguzi.

Dalili za kuanguka Sumaye, pia zilijionyesha siku ya kupiga kura, ukumbini na nje ya ukumbi kutokana na wajumbe waliokuwa wanamuunga mkono Dk Nagu kuwa na uhakika mkubwa wa ushindi.

Wakati wa kujieleza ili aombe kura, Sumaye ambaye alionekana kama tayari amebaini nguvu ya Dk Nagu, alieleza kushangazwa na uamuzi wa Dk Nagu kugombea nafasi hiyo, hali ya kuwa ni waziri.

Sumaye, pia alikemea kile alichodai kuwa ni rushwa kwenye chaguzi za CCM na kuahidi kama akichaguliwa, angeshirikiana na viongozi wenzake kuhakikisha anawachukulia hatua kali watoa rushwa.

Awali Dk Nagu katika maelezo yake, alitumia fursa ya kuomba kura kukanusha kuwa anatumiwa na kundi la Lowassa ili kumkwamisha Sumaye.

Dk Nagu alifafanua kuwa yeye kama Mbunge wa Hanang’ na Waziri, kamwe hawezi kutumiwa na kundi fulani kwa masilahi ya makundi kwani hata yeye ana sifa za kuchaguliwa.

Wakati wa maswali, Dk Nagu hakuulizwa wakati Sumaye aliulizwa maswali matatu ambayo aliyajibu kwa ufasaha, lakini hakuchaguliwa.

Mwenyekiti wa CCM aliyeshindwa, Goma Gwaltu, alieleza kupinga mambo kadhaa yaliyokiukwa katika uchaguzi, lakini hata hivyo, alisisitiza kujiandaa kutoa tamko rasmi.

“Nitazungumza siku si nyingi kuelezea uchaguzi huu,” alisema Gwaltu.

Naye Sumaye kwa upande wake, alisema anakusudia kuzungumzia yaliyojiri katika uchaguzi huo hivi karibuni.

“Naomba uwe na subira, nitawaita wanahabari na tutazungumza. Leo (jana) nimepigiwa simu na waandishi kama 50, wote nimewaambia kuwa nitazungumza siku chache zijazo,” alisema Sumaye.

Mbunge wa Viti Maalumu Chadema, Rose Kamili ambaye kwa muda mrefu alikuwa diwani kwa tiketi ya CCM kabla ya kuhamia Chadema, alieleza kuwa Sumaye aliangushwa kwa nguvu ya fedha.

Alisema kuwa kitendo cha Sumaye kutajwa kuwa anataka kuwania urais katika uchaguzi ujao ndiyo sababu ya kutoswa katika uchaguzi huo ili kupunguza ushindani.


Kwa upande wake Gwaltu alisema kilichomwangusha Sumaye ni makundi ya urais katika uchaguzi mkuu ujao.

Alisema kuwa makundi hayo ambayo yameanza kujipanga kwa ajili ya kushinda katika kinyang’anyiro cha kuwania urais, yalifanya kila njia kuhakikisha kuwa Sumaye hapenyi katika hatua hiyo, lengo likiwa ni kufanya upinzani kuwa mdogo 2015.

Kada mkongwe wa chama hicho ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Basotu, Samwel Kawoga alisema kuwa makundi hayo yalianza kuonekana wazi siku chache kabla ya kufanyika kwa uchaguzi huo.

Alisema kuwa makundi hayo ni pamoja na yale yanayoongozwa na makada wa chama hicho wanaoutaka urais na mengine ni yale yanayoibuka kila unapofanyika uchaguzi ndani ya chama hicho.


hivi Don Lowassa anataka kubaki peke yake kwenye chama na vibaraka tu wa ndiyo mzee, ndiyo mzee...na hii itaisaidia vipi CCM na taifa kwa ujumla. Huyu jamaa ni mfano halisi ya ubinafsi uliokirithi kwenye uongozi.
 
Amesema ataitisha mkutano na wanahabari!
Nna hamu ya kumsikia akiropoka.
Nitam under rate akithubutu kuropoka eti amepigwa chini na kambi ya Lowassa
khaa ngoja tumsikilizie
 
Siasa ni kazi ya Makundi na hakika ni kazi ya fitna kwelikweli...sasa Sumaye ni mwanasiasa wa aina gani asiyejua ukweli huu?Hakuna huruma kwenye siasa bana,na wala hakuna kulegealegea eti kura zitakuja tu,EBO!
 
hata mimi najiuliza kama alikuwa waziri mkuu tena 10 years ...anataka kufanya nini cha tofauti tena sasa kwenye position za chini cause hawezi kurudi tena kwenye ile senior position... au anataka akifa mwili wake uagwe mjengoni? maana hicho tu ndo atakosa...aibu sana ndio maana mimi sipendi wanaume wa nchi hii wanafiki wanafiki sana
Smile usimjaji mtu ukawa na jawabu kwa wote wa jinsia hiyo, hapo utakuwa hujatutendea haki !
 
Last edited by a moderator:
Smile siyo uzinzi, uzinzi ni kua kama kuku...mimi mstaraabu, a true gentleman, a quintessential 21st century african man. Napenda tu wanawake for all they are.
 
wakati Sumaye anapewa nafasi ya kuongea harafu akaanza kuwaubili watu kuwa akishinda atapambana na wala rushwa,moja kwa moja nilijua kuwa atashindwa.maana baada ya kutamka maneno hayo nliona watu wanaanza kutazamana kama kuonesha ishara filanlkn kwa haraka sana watu wle nilielewa kuwa walikuwa wakiteta kuwa mtu huyu akiingia ,adarakani si ndo atatubania riziki yethii ni kwa sababu msing wa ccm ili uwe kiongozi ni lazma uwe tayari kuwabeba wala rushwa zaidi ya hapo huwezi kushinda kama misingi yako ni kuzuia rushwaviongozi wengi wa ccm wameingia madarakani kwa njia ya rushwa wala si kwa misingi bora ya siasa za wagombea husikawe ukitaka kuwa kiongozi kupitia cha hiki cha mafisadi inakibidi uwe na katiba yako binafisi ya kuwatetea wala rushwa,hapo kila kitu kitakuwa sawa ktk suala zima la uongozi
 
jamaa kamis u big boss,yalikuwa malengo yake kuwa prezdaa aftr mkapa bt timing haikuwa mwake ashukuru alimaliza miaka kumi wenzie waliangukia pua katikat ya first term chezeya magamba weye ki2 rotten mbaya
 
hivi hizi juhudi za kutaka u-Nec ccm ni za nini wakati chama chenyewe kinakufa rasmi mwaka 2014?
 
Back
Top Bottom