Kutoka Makao Makuu CHADEMA: M/kiti Mbowe aahirisha maandamano ya UKUTA ya Oktoba Mosi

Ben Saanane

JF-Expert Member
Jan 18, 2007
14,581
18,123
Nitawaletea Dondoo za Hotuba hii.Nakala ya Hotuba Nzima watapewa waandishi wa Habari baada ya Hotuba kwa faida ya sanaa ya Habari ili Vyombo vya Habari viripoti kwa Weledi na ufasaha

-Tayari Waandishi wa Habari wameketi
-Viongozi wakuu Wakiongozwa na Mhe.Freeman Mbowe wanaingia Ukumbini

Hotuba kwa Taifa itaanza hivi Punde

Saa 12:15 baada ya İtifaki kuzingatiwa, Mwenyekiti Taifa anaanza kuhutubia
Anawapa pongezi wanahabari kwa kufika kwa wingi .Anasema

- Jana kamati ndogo ya kamati kuu imekutana tena ili kufanya marejeo kuhusu yalipofika majadiliano ya Viongozi wa Dini na Rais baada ya kukiomba Chama kisitishe Operesheni UKUTA

-Hadi jana na hadi sasa viongozi wa Dini hawajaleta Taarifa yoyote kuhusu kama waliweza kukutana na Rais

-Sisi kama Chama Cha Siasa tumetekeleza wajibu wetu
-Tunawaheshimu viongozi wa Dini na Tutaendelea kuwaheshim
-Sasa kama chama cha Siasa tutaendelea sasa kutekeleza wajibu wetu

-Kazi ya siasa sio kazi ya siku moja.Tutaifanya kazi hii endelevu ya kupambana na Utawala kandamizi unaowaumiza wananchi kwa kukanyaga sheria na katiba na pia utawala unaokwepa wajibu wake lakini hautaki kukosolewa.

Maisha magumu kwa Watanzani lakini Mtawala asiye na Mbinu mbadala hataki wananchi wapaze sauti

-UKUTA ni Fikra. Yaani fikra za kupambana na ukandamizaji wa haki na demokrasia.Mapambano haya hayahusishi CHADEMA pekee.

Kwa muktadha huu tuna wajibu wa kufanya siasa ndani ya wigo uliowekwa nchini na pia kimataifa

-Tanzania sio kisiwa.Ndio maana chama kiliona Umuhimu wa kutuma ujumbe Mzito kwenye ziara maalumu nchi za Ulaya .Nchi za Ujerumani na Denmark kuendelea kuujulisha Ulimwengu juu ya ukandamizaji mkubwa wa haki za binadamu na Demokrasia kinyume na jinsi ambavyo serikali imekua ikijipamba kuwa ya amani na Utulivu

Hiyo ilikua ziara ya awamu ya kwanza
Bado Ujumbe Mwingine utatumwa kwenye nchi nyingine kama Uingereza,Marekani,Canada , Malaysia,Japan na hata ndani ya Umoja wa Afrika na kwenye mtangamano wa kikanda kama SADC na EAC

Tunataka utawala ujue mipaka yetu haiishii Namanga na Tunduma
Tutatumia Taasisi za kimataifa
Kurugenzi yetu ya Sheria inaendelea na kazi nzuri ya kutumia Mahakama za ndani na za kimataifa kupeleka mashauri yetu

-Viongozi wetu mbalimbali wanakabiliwa na kesi mbalimbali zinazoitwa kesi za Uchochezi

-Tumesikia Juzi polisi katika kujihalalishia uovu wao walipojua CCM sasa wanakaribia kuanza vikao vya ndani wanatangaza kuruhusu Mikutano ya ndani

-Sisi tunaandaa mikutano ya kisiasa nchi nzima
-Ukuta wa Oktoba Mosi utasogezwa mbele kwa Tarehe Maalumu
-Rais anatumia jeshi kupambana na Sisi lakini hakuweza kuwatumia kwenye Tetemeko Kagera na kuwaacha raia wetu wakiteseka
-Leo anatumia jeshi kuumiza Raia na vituko vingine eti kufagia na wengine kupanda Miti

-Rais aliyekwepa mikutano ya kimataifa kwa kisingizio cha Tetemeko la Ardhi Kagera hakufika,Hakupeleka jeshi ila alikaa İkulu akisubiri Ripoti

MİGOGORO İNAYOPANDİKİZWA
-Prof.Lipumba amekituhumu CHADEMA kuhusika na migogoro ndani ya CUF
Sikusudii kumjadili Lipumba.Maana sitaki kumpa nafasi na umuhimu aliokuwa nao zamani
He's politically İrrelevant.

CHADEMA kitashirikiana na chama chochote chenye dhamira ya dhati
CUF tunaheshimu maamuzi yao ya vikao halali

-Natoa Rai kwa Wanachama wa CHADEMA nchi Nzima kupuuza kauli za Prof.Lipumba na tuache kumpa ushirikiano wowote kwa kuwa ni msaliti wa mageuzi anayetafuta kuangamiza Upinzani

MSAJİLİ WA VYAMA VYA SİASA



-Jaji Mutungi amechochea mgogoro CUF na hatuna sababu za kumuheshimu
-Atambue kuwa tutasimama na CUF na ajue yeye sio Msajili wa kwanza.

Mbinu zake na Watawala zitashindwa
-Serikali inatumia nguvu kubwa sana na taasisi nyingine kununuliwa

-Kwa mfano TWAWEZA .Upo ushahidi kuwa walipewa pesa na serikali kupika Utafiti siku moja kabla ya UKUTA kwa bahati mbaya hawakupika kwa kiwango cha kuifanya ripoti ionekane kuwa na sifa za kiutafiti

-Kwa hiyo ndugu wanahabari sisi kama Chama tumebadilisha Tarehe ya kuanza Kufanya maandamano na mikutano

Sasa wale walojiandaa kushambulia na kuua watu wasubiri
Sisi tunabadili mbinu tukihusisha mbinu za kimapambano na kidiplomasia

-Mmeona matokeo ya Mbinu hizi sasa Jumuiya ya Kimataifa imeanza kuona ukandamizaji wa Demokrasia nchini na Udikteta Uchwara ulioshamiri

Tulipowapa Muda viongozi wa Dini wao watawala walidhani tumelala kumbe tumevuka mipaka na kuingia anga za kimataifa

-Sasa serikali inahaha na kutapatapa baada ya kushitakiwa kwenye Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa
Sasa tutaendelea kufanya vikao vya kimkakati nchi nzima na pia mikutano
Tutaendelea kuhabarishana kadiri tunavyopiga hatua katika maandalizi na Mikakati yetu ambayo haitawapa fursa watawala kujipanga

Asanteni


Mwisho:Sasa Mwenyekiti Taifa na Viongozi wakuu anaongea na Baadhi ya Vyombo vya Habari vya Kimataifa kisha ataelekea kwenye kikao nyeti cha Ndani,Kikao cha Kimkakati


Aluta Continua,Victory Ascerta

Ben Saanane
 
UKUTA hautakuwepo, azungumzie mengine.

Mzee Tupatupa
14463311_10154572965094339_432469204327422221_n.jpg
 
Hivi issue ya UKUTA bado ipo kwelii maana sasa hivi macho ya watanzania katika siasa HABARI INAYOPAMBA MOTO NI LIPUMBA NA CUF

Haswa macho ya watanzania wanataka kufahamu nini kitajiri chadema off course kipindi hiki imeanza kusahaulika,

Sasa hivi habali ya mjini inayosikika ni cuf , maalim seif, mtatiro na lipumba kuhusu ukuta watu washaanza kusahau taratibuuu hahaa

Kaka yangu ben sanane ni utani tuu huu lakini kweli
 
38 Reactions
Reply
Back
Top Bottom