Kilichoisambaratisha NCCR-Mageuzi ile ya 1995 ni nini?

Wangwe Bangi zilikuwa zinamsumbua na alidanganywa na UWT kupitia wastaafu wa Jeshi kutoka Tarime kuikengeuka CDM. Baada wao kuona wamemshirikisha mambo mengi ambayo yote hayakuzaa matunda walikuwa hawana jinsi maana siri zao bado walitaka ziendelee kuwa siri.

Kwa Tarime asilimia kubwa wanaipata hiyo kitu tena kwa njia ya kiasili kabisa ya kibuyu!! Kwa rasta kama wangwe sishangai.

Hii hapa sijakuelewa: hawana jinsi maana siri zao bado walitaka ziendelee kuwa siri. Una maana hawa ndio waalimmaliza? Wastaafu gani hao? Hivi ukisema ukweli ndani ya CDM unakuwa mkengeufu? Na kweli naona akina Shibuda wanakengeuka kwa kusema ukweli!!
 
Ukweli ni kwamba NCCR ilianzishwa na maofisa wa usalama ili ku-contain opposition, na kuchafua image yote ya upinzani. Baadaye ikajulikana kuwa wananchi wenye nia ya mageuzi wanaburuzwa na wahuni wanaojidai wanamageuzi. kwa sasa inaonekana kuwa baada ya kumaliza kazi yao NCCR wameanza kuingia CHADEMA, the fact is NCCR imekufa, kilichopo ni kuwa ipo kwenye makaratasi na kuthibitisha uwepo hewa wake kwa wabunge wawili watatu iliyo nao.
Hisia zako tu, NCCR ipo na itaendelea kuwepo.
 
Muuliza swali nashawishika kuamini kwamba ulitaka kujua kweli. Kama ni utafiti naomba uzingatie taarifa hizi

1. Vuguvugu la wanamageuzi lilianza miaka ya 80 wakati wasomi wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam walipoanza kuhoji uwepo wa mfumo wa chama kimoja. Ni katika kipindi hicho Ndg. Mabere Nyaucho Marando (Katibu Mkuu wa kwanza wa NCCR) alifanya presentetion hapo chuoni kuhusu suala hilo. (Kama nakala ya presentation yake inaweza kupatikana basi siku moja tutaiweka hapa, kwa ajili ya kuweka kumbukumbu vizuri)
2. Mnamo mwaka 1984, Ndg.James Mapalala (makamu mwenyekiti wa kwanza wa NCCR) alimwandikia Mwalimu Nyerere barua ya wazi akitaka mfumo wa vyama vingi urejeshwe nchini (kumbuka ulikuwepo awali Mwalimu akaufuta)

3.Miaka saba baadaye (1990) Mwalimu akaanza kuelewa (wakati huo alishaacha urais) akaanza kusema si vibaya mfumo wa vyama vingi ukirejeshwa nchini
4. Mnamo mwaka 1991 wasomi wa UDSM, pamoja na wanaharakati wakaianzisha NCCR. Ikawa chini ya Uenyekiti wa Marehemu Chifu Abdallah Fundikira (waziri wa zamani wa Mwalimu), Makamu; Mapalala, Katibu Mkuu; Marando.
5. Mwaka huo huo 91 Rais Ali Hassan Mwinyi akaunda tume ya kukusanya maoni ya wananchi kama vyama vingi viruhusiwe au visiruhusiwe. Watanzania wengi hawakuvitaka, lakini wapo waliosema virudi.
6. Mzee Mwinyi akaheshimu mawazo ya wachache, mwaka 1992 akaruhusu virudishwe.
7. Mwaka huo 1992 (hapa ndipo sura ya sasa ilipotoka) waliokuwemo ndani ya NCCR wakagawanyika. Fundikira Mwenyekiti akaunda chama; UMD (japo kabla hajafa alirejea CCM), Mapalala huyo naye akaunda CCW ambayo kwa kushirikiana na Shaban Mloo wa KAMAHURU ya Zanzibar wakaunda CUF (sasa Mapalala yuko CHAUSTA). Marando akaendelea kuiongoza NCCR kwa kuiboresha na neno Mageuzi (sasa naye yuko CHADEMA), baadhi ya wajumbe wengine wa NCCR wakashiriki kuiunda CHADEMA wakitumia kaulimbiu ya NCCR 'demokrasia na maendeleo'. Na wengine wakaendelea kuunda vingine, matharani hata Mziray wa APPT-Maendeleo anatokea NCCR.

Kwa ufupi NCCR ilisambaa kabla ya ujio wa Mrema. 'ikawa kama maandiko; nitampiga mchungaji wa kondoo, na kondoo wa kundi lake watatawanyika)
8. Ndio sinema ya 1995 ikaanza (Hii sasa usome Kitabu cha Ndimara Tegambwage)
 
Kwa Tarime asilimia kubwa wanaipata hiyo kitu tena kwa njia ya kiasili kabisa ya kibuyu!! Kwa rasta kama wangwe sishangai.

Hii hapa sijakuelewa: hawana jinsi maana siri zao bado walitaka ziendelee kuwa siri. Una maana hawa ndio waalimmaliza? Wastaafu gani hao? Hivi ukisema ukweli ndani ya CDM unakuwa mkengeufu? Na kweli naona akina Shibuda wanakengeuka kwa kusema ukweli!!

Mkuu marehemu alikuwa kama Kabwe hawana tofauti kabisa; kumbuka huyu Jamaa uchaguzi wa mwaka 2005 alishiriki kuiba kura za CDM za urais kama Jamaa alivyoshiri kuiba kura za Urais za CDM kule Kigoma mwaka 2010.

Haya mambo yalipaswa kufanyika kisayansi si kama enzi za nyumba na jembe wakati wa chaguzi za chama kimoja au wakati Mwinyi anagombea Urais na Giza kana kwamba Wakuna watanzania wanaoweza kupambana naye.
 
Muuliza swali nashawishika kuamini kwamba ulitaka kujua kweli. Kama ni utafiti naomba uzingatie taarifa hizi

1. Vuguvugu la wanamageuzi lilianza miaka ya 80 wakati wasomi wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam walipoanza kuhoji uwepo wa mfumo wa chama kimoja. Ni katika kipindi hicho Ndg. Mabere Nyaucho Marando (Katibu Mkuu wa kwanza wa NCCR) alifanya presentetion hapo chuoni kuhusu suala hilo. (Kama nakala ya presentation yake inaweza kupatikana basi siku moja tutaiweka hapa, kwa ajili ya kuweka kumbukumbu vizuri)
2. Mnamo mwaka 1984, Ndg.James Mapalala (makamu mwenyekiti wa kwanza wa NCCR) alimwandikia Mwalimu Nyerere barua ya wazi akitaka mfumo wa vyama vingi urejeshwe nchini (kumbuka ulikuwepo awali Mwalimu akaufuta)

3.Miaka saba baadaye (1990) Mwalimu akaanza kuelewa (wakati huo alishaacha urais) akaanza kusema si vibaya mfumo wa vyama vingi ukirejeshwa nchini
4. Mnamo mwaka 1991 wasomi wa UDSM, pamoja na wanaharakati wakaianzisha NCCR. Ikawa chini ya Uenyekiti wa Marehemu Chifu Abdallah Fundikira (waziri wa zamani wa Mwalimu), Makamu; Mapalala, Katibu Mkuu; Marando.
5. Mwaka huo huo 91 Rais Ali Hassan Mwinyi akaunda tume ya kukusanya maoni ya wananchi kama vyama vingi viruhusiwe au visiruhusiwe. Watanzania wengi hawakuvitaka, lakini wapo waliosema virudi.
6. Mzee Mwinyi akaheshimu mawazo ya wachache, mwaka 1992 akaruhusu virudishwe.
7. Mwaka huo 1992 (hapa ndipo sura ya sasa ilipotoka) waliokuwemo ndani ya NCCR wakagawanyika. Fundikira Mwenyekiti akaunda chama; UMD (japo kabla hajafa alirejea CCM), Mapalala huyo naye akaunda CCW ambayo kwa kushirikiana na Shaban Mloo wa KAMAHURU ya Zanzibar wakaunda CUF (sasa Mapalala yuko CHAUSTA). Marando akaendelea kuiongoza NCCR kwa kuiboresha na neno Mageuzi (sasa naye yuko CHADEMA), baadhi ya wajumbe wengine wa NCCR wakashiriki kuiunda CHADEMA wakitumia kaulimbiu ya NCCR 'demokrasia na maendeleo'. Na wengine wakaendelea kuunda vingine, matharani hata Mziray wa APPT-Maendeleo anatokea NCCR.

Kwa ufupi NCCR ilisambaa kabla ya ujio wa Mrema. 'ikawa kama maandiko; nitampiga mchungaji wa kondoo, na kondoo wa kundi lake watatawanyika)
8. Ndio sinema ya 1995 ikaanza (Hii sasa usome Kitabu cha Ndimara Tegambwage)
Mkuu tafadhali.. unajua uongo ukizungumzwa sana hugeuka na kuwa ukweli hasa kwa wale wasiofahamu. NCCR hakikuwa chama bali kundi la watu waliounda umoja ktk kongamano la vyama vingi(Demokrasia) kama hivi leo tunavyozungumzia Katiba mpya, kujumuika kwa kina Profesa Shevji, Kitila, Zitto, Kafulila na wengineo hakuwapi unachama wa chama cha kisiasa.

NCCR kama chama ndicho tunachozungumzia hapa..Tatizo la vyama vya siasa na hasa NCCR na CUF vinapoteza umaarufu wao na hata kuonekana vimekufa ni kwa sababu ya UONGOZI MBAYA wakigombania maslahi binafsi. Vyama hivi vinaweza kuwa na malengo mazuri sana (itikadi) lakini viongozi wake ni wachumia tumbo walojificha nyuma ya itikadi, hawa wasomi wetu ni opportunist na hata ukitazama chimbuko la vyama vingi walikuwa pamoja pale viliporuhusiwa tu wakajikata umoja wao na kutumia fursa hiyo kwa sababu wote hawa walikubaliana umuhimu wa kuwepo kwa vyama vingi lakini hawakuwa na mtazamo wa kitikadi sawa.

Kitu kimoja tunachowaomba nyie wanasiasa wa Kitanzania uwe msomi hata kufikia darini (Phd) kama hutaweza kuishi maisha sawa na wale unaowatetea huwezi kuwadanganya wananchi wakati wote kwa kutumia elimu. Leo hii hakuna mjamaa ktk viongozi wetu, hakuna mkweli katika kutetea haki za wanyonge kwa sababu maisha yake mwenyewe yanamuumbua. Maadam adui yetu mkubwa ni Umaskini, Ujinga na maradhi basi vita hii isiishie kwenye makaratasi.

Na labda niseme tu kwamba kesho akitokea Mjamaa wa kweli mwenye kuyajua machungu ya umaskini na akawa na maskini ktk majonzi yao na kuyatetea. Huyu mtu atachukua nchi kirahisi kabisa akipata wafuasi bora nyuma yake. Lakini NCCR kama chama, sijui CUF au Chadema nina mashaka sana kudumu kwa vyama hivi kwa sababu maneno mengi wakati CCM ikiendelea kufanya maovu ambayo mnayatazama kwa kupitia PC zenu kwa sababu nyie wenyewe mnafanya mitikasi kwa kwenda mbele.

Nitakupa mfano mdogo sana, kesho Dr.Slaa au Zitto akifungua chama chake (tukiite CCJ) na wakamtangaza Generali Ulimwengu kama mgombea Urais, kesho utaona mmomonyoko wa viongozi kutoka vyama vyote wakikimbilia CCJ kwa sababu bado kabisa Chadema haija secure nafasi waliyoikamata na kuonyesha wamesimama wapi. Hadi leo wananchi bado hawajapa mtetezi wa haki zao isipokuwa siasa na uongo unaokubalika kwa sababu ukitazama migogoro yote inayotokea leo nchini ni ya kisiasa zaidi. Viongozi kwa viongozi kutokubaliana ktk ulinzi wa maslahi yao wananchi wametupwa kapuni. Naipenda sana Chadema kwa sababu ilikuwa na lengo moja tu kuiangusha CCM, lakini maadam wanashindwa na kupwaya kutokana na nguvu kubwa ya CCM, sidhani kama tutadumu kufikia mwaka 2015.

Pengine njia ilobakia ni kurudi kwenye basic.. Ushauri wetu wa awali ulikuwa vyama vyote vya Upinzani kuungana kama tulivyosema toka awali na utetezi wenu mkubwa uwe kwa wananchi (thumbs up kwa Dr.Slaa na Zitto) lakini mkiendelea kuchumia tumbo, ni swala la wakati tu mtakuwa historia ya nchi mlikuwepo na sasa hampo tena. Kugombania uenyekiti ni kuonyesha jinsi mlivyochini sana kifikra kwa sababu mwenyekiti sii lazima awe mgombea Urais na wala hatakiwi kuwa na mamlaka makubwa kama mnavyowapa viongozi wa vyama vya Tanzania. Mbatia leo anatafutwa kwa kila hali wakati tatizo sii yeye bali katiba ilompa mamlaka makubwa kama tunavyokosea kumpa rais mamlaka makubwa.

- Nawakilisha
 
Pengine njia ilobakia ni kurudi kwenye basic.. Ushauri wetu wa awali ulikuwa vyama vyote vya Upinzani kuungana kama tulivyosema toka awali na utetezi wenu mkubwa uwe kwa wananchi (thumbs up kwa Dr.Slaa na Zitto) lakini mkiendelea kuchumia tumbo, ni swala la wakati tu mtakuwa historia ya nchi mlikuwepo na sasa hampo tena. Kugombania uenyekiti ni kuonyesha jinsi mlivyochini sana kifikra kwa sababu mwenyekiti sii lazima awe mgombea Urais na wala hatakiwi kuwa na mamlaka makubwa kama mnavyowapa viongozi wa vyama vya Tanzania

- Nawakilisha

Umemaliza mkuu..salute!
 
Mkuu marehemu alikuwa kama Kabwe hawana tofauti kabisa; kumbuka huyu Jamaa uchaguzi wa mwaka 2005 alishiriki kuiba kura za CDM za urais kama Jamaa alivyoshiri kuiba kura za Urais za CDM kule Kigoma mwaka 2010.

Haya mambo yalipaswa kufanyika kisayansi si kama enzi za nyumba na jembe wakati wa chaguzi za chama kimoja au wakati Mwinyi anagombea Urais na Giza kana kwamba Wakuna watanzania wanaoweza kupambana naye.

Unavyozungumza kwa kujiamini!..
 
Mkuu tafadhali.. unajua uongo ukizungumzwa sana hugeuka na kuwa ukweli hasa kwa wale wasiofahamu. NCCR hakikuwa chama bali kundi la watu waliounda umoja ktk kongamano la vyama vingi(Demokrasia) kama hivi leo tunavyozungumzia Katiba mpya, kujumuika kwa kina Profesa Shevji, Kitila, Zitto, Kafulila na wengineo hakuwapi unachama wa chama cha kisiasa.

NCCR kama chama ndicho tunachozungumzia hapa..Tatizo la vyama vya siasa na hasa NCCR na CUF vinapoteza umaarufu wao na hata kuonekana vimekufa ni kwa sababu ya UONGOZI MBAYA wakigombania maslahi binafsi. Vyama hivi vinaweza kuwa na malengo mazuri sana (itikadi) lakini viongozi wake ni wachumia tumbo walojificha nyuma ya itikadi, hawa wasomi wetu ni opportunist na hata ukitazama chimbuko la vyama vingi walikuwa pamoja pale viliporuhusiwa tu wakajikata umoja wao na kutumia fursa hiyo kwa sababu wote hawa walikubaliana umuhimu wa kuwepo kwa vyama vingi lakini hawakuwa na mtazamo wa kitikadi sawa.

Kitu kimoja tunachowaomba nyie wanasiasa wa Kitanzania uwe msomi hata kufikia darini (Phd) kama hutaweza kuishi maisha sawa na wale unaowatetea huwezi kuwadanganya wananchi wakati wote kwa kutumia elimu. Leo hii hakuna mjamaa ktk viongozi wetu, hakuna mkweli katika kutetea haki za wanyonge kwa sababu maisha yake mwenyewe yanamuumbua. Maadam adui yetu mkubwa ni Umaskini, Ujinga na maradhi basi vita hii isiishie kwenye makaratasi.

Na labda niseme tu kwamba kesho akitokea Mjamaa wa kweli mwenye kuyajua machungu ya umaskini na akawa na maskini ktk majonzi yao na kuyatetea. Huyu mtu atachukua nchi kirahisi kabisa akipata wafuasi bora nyuma yake. Lakini NCCR kama chama, sijui CUF au Chadema nina mashaka sana kudumu kwa vyama hivi kwa sababu maneno mengi wakati CCM ikiendelea kufanya maovu ambayo mnayatazama kwa kupitia PC zenu kwa sababu nyie wenyewe mnafanya mitikasi kwa kwenda mbele.

Nitakupa mfano mdogo sana, kesho Dr.Slaa au Zitto akifungua chama chake (tukiite CCJ) na wakamtangaza Generali Ulimwengu kama mgombea Urais, kesho utaona mmomonyoko wa viongozi kutoka vyama vyote wakikimbilia CCJ kwa sababu bado kabisa Chadema haija secure nafasi waliyoikamata na kuonyesha wamesimama wapi. Hadi leo wananchi bado hawajapa mtetezi wa haki zao isipokuwa siasa na uongo unaokubalika kwa sababu ukitazama migogoro yote inayotokea leo nchini ni ya kisiasa zaidi. Viongozi kwa viongozi kutokubaliana ktk ulinzi wa maslahi yao wananchi wametupwa kapuni. Naipenda sana Chadema kwa sababu ilikuwa na lengo moja tu kuiangusha CCM, lakini maadam wanashindwa na kupwaya kutokana na nguvu kubwa ya CCM, sidhani kama tutadumu kufikia mwaka 2015.

Pengine njia ilobakia ni kurudi kwenye basic.. Ushauri wetu wa awali ulikuwa vyama vyote vya Upinzani kuungana kama tulivyosema toka awali na utetezi wenu mkubwa uwe kwa wananchi (thumbs up kwa Dr.Slaa na Zitto) lakini mkiendelea kuchumia tumbo, ni swala la wakati tu mtakuwa historia ya nchi mlikuwepo na sasa hampo tena. Kugombania uenyekiti ni kuonyesha jinsi mlivyochini sana kifikra kwa sababu mwenyekiti sii lazima awe mgombea Urais na wala hatakiwi kuwa na mamlaka makubwa kama mnavyowapa viongozi wa vyama vya Tanzania. Mbatia leo anatafutwa kwa kila hali wakati tatizo sii yeye bali katiba ilompa mamlaka makubwa kama tunavyokosea kumpa rais mamlaka makubwa.

- Nawakilisha
Naam, uongozi mbaya, hata mimi ndivyo nilivyomalizia maelezo yangu; akikengeuka mchungaji kondoo hawako salama. Vyama kama taasisi zinahitaji uongozi bora/mzuri, hali kadhalika nchi na taasisi nyinginezo. Ni jukumu langu na wewe kuhakikisha uongozi bora unapatikana.
 
Hii issue inabidi tuwekane sawa.

Nakumbuka kulikuwa na mjadala na binafsi nilkuwa nikimlaumu Marando kwa kusambaratika kwa NCCR,kwasababu tu alitaka ulaji zaidi.

Zitto alibisha na akasema mwenye tatizo alikuwa ni Mrema,akasema nifuatilie vyema.

Ila hadi sasa hakuna aliyekuja na jibu convincing.

Muda haukupita Marando akajiunga na CDM,tena kabla ya hapo nili anzisha thread kuhusu hilo ngoja niitafute.
 
Ndugu Mushi, kila uliyemtaja hapo alihusika kivyake (walikuwepo pia wahusika wadogo). Wakati Marando na wenzake walimwona Mrema (baada ya uchaguzi wa 1995) kuwa mtu asiyeshaurika na mfujaji (kama unajua kisa cha kontena la mali za chama toka Afrika Kusini), yeye Mrema aliwaona akina Marando kama watu wasiokuwa watiifu tena, alijihesabu yeye ndio NCCR na NCCR ndio yeye (hasa baada ya kuitikisa CCM vilivyo) kila amri aliyotoa ilitakiwa kufuatwa kama ilivyo. Kwa ufupi ulitokea msigishano wa mitazamo na maslahi, ukachagizwa na dua la kunguru dhidi ya panzi. Msigishano ulipozidi ... Mrema akatoka
 
Sasa haya ndio matatizo ya vyama vyetu> Na sii swala la mimi mwananchi kumtafuta kiongozi bora bali vyama vyetu vya kisiasa ndivyo vyenye jukumu hilo.

Labda niseme tu ya kwamba mfumo mzima wa vyama nchi Tanzania ni makosa matupu kwa sababu tumeiga kila kitu aidha kutoka CCM ama utawala wowote wa Kidikteta..Mwenyekiti anapewa madaraka makubwa kiasi kwamba huanza kufikiria yeye ndiye Chama. hayakuwa makosa ya Mrema wala Marando kila mmoja wao ali play part yake kuwaonyesheni mapungufu ya muundo wa chama lakini bado vyama hamjaipata kabisa. tazama vyama vingine nchi za magharibi utaona Mwenyekiti hana mamlaka ya kitaifa nje ya ujenzi wa chama. Mara chache sana huingilia matatizo nje ya chama nan kiosha muida huo ataupata wapi ikiwa kazi yake ni kukijenga chama..

Sisi waigaji tuloiga toka dini hadi tamaduni za nje, leo tumeuvamia mkenge wa CCM chama ambacho Udikteta ni lazima uwepo ili wapate kuendelea kuongoza nchi. Na nitakuhakikishia kwamba Demokrasia haiwezi kufanya kazi kukiondoa CCM madarakani ikiwa vyama vya Upinzani havitavuka hatua hii ndani ya vyama kwa sababu hamjashika dola. CCM wao wamechukua nchi toka toka Uhuru ni a syndicate, wanajuana na wale wote wanapewa nafasi ya uongozi ndani ya serikali,bunge na mahakama ni watu walioitumikia CCM kwa miaka ama baba zao, wajoimba na kadhalika sasa nyie mnaokuja na ushirika wa watu toka kona zote za nchi ambao hamna lolote in common zaidi ya kupingana na utawala dhalimu mtaweza vipi kuwa na mawazo sawa..

Amini maneno yangu vyama vya Upinzani vyote hakuna Itikadi kwa sababu hatuna utamaduni huo. Nimewahi kuuliza watu hapa Ukiwa wewe Liberal unakuwa against WHAT? maanake wenzetu wameanza na mila zao wakatokea watu kupingana na baadhi ya mila na tamaduni ambazo zilitangfulia ktk ujenzi wa katiba yao. Sisi hapa tunalinda mila na tamaduni zipi? - Conservative wa nini kama sii kwa tafsiri ya Uhafidhina kama ndio Ubepari..

Leo hii watu wote tunapingana kuhusu Katiba na kwa maslahi ya vyama kweli tutafika. Kila kinachotakiwa kubadilishwa ndani ya katika ni against maslahi ya CCM unafikiri wao watakubali kirahisi. Ni sawa na swala la Posho za vikao, yaani tulitegemea kweli wale wanaopokea posho hizo ndio watoe uamuzi wa kukatiwa posho?.. Mimi sijaona kitu hii maishani kwa sababu hata nilipokuwa nimeajiliwa nikiambia kuna makato ya kuchelewa kazini nilikuwa namwona mhasibu mchawi mkubwa ingawa kuna ukweli na haki ya kukatwa..

Hii ndio Tanzania yetu CCM wataongoza hadi wachoke wenyewe. Katiba mpya hakuna, vyama vya Upinzani vitaweza tu kujiweka katika nafasi nzuri ikiwa katiba mpya itaundwa na trust me ktk hali waliyokuwepo CCM leo mahtuti ati mnataka kuondoa life support yao kwa ajili ya nini? Hawatakubali kabisa! Piga ua...
Pelekeni swala hili kwa wananchi msitake kulimaliza bungeni kwa sababu halitawezekana, hata mimi ningekuwa CCM nisingekubali madaraka matamu jamani msisahau hayo!
 
Kuna kosa kubwa sana la kimkakati ambalo vyama vyetu vimekuwa vikilifanya kila siku. Utakuta ma-opportunist kama huyu Komu kila wanapokwenda wanapewa nafasi za haja, hivi hakuna wanachama waaminifu wakuweza kushika nafasi hizo kuliko hawa wapima upepo? Hata hivyo kilichoiua NCCR ni ile tabia ya Mrema kuamini kwamba yeye ndiye alikuwa kila kitu. Hata hiyo ruzuku alitaka yote iwe mikononi mwake kwa kuamini kuwa ilipatikana kwa ubavu wake. Kumbuka kauli yake wakati akienda TLP kuwa alikuwa na mtaji (wanachama wa kuhama nao). Leo hii yuko wapi na mtaji wake huo? Hili laweza kuwa funzo kwa makamanda wetu wa leo.
Ulichosema miaka saba iliyopita ndio yanatokea. Hawa wanazi akili zao huwa zimefungwa au kupigwa ganzi
 
Mkuu Waberoya nimeuleta upya huu uzi ili kuwakumbusha vijana wenzetu kuwa hizi sarakasi wasifikiri zimeanza juzi.

Wasipopiga kelele sasa na Chadema tutaijadili hivi hivi
Inaonekana wazi kwa Mbowe mmekwama ndio maana mmesubilo sana lakini hamna kitu mmeishia kwenye biashara ya utumwa tu kununuwa binadamu.

Kama jaribio la Kitila Mkumbo, Zitto Kabwe na MMM zao walishindwa ndio basi tena, watu wote wenye nguvu na ushawishi ndani ya Chadema wanamuunga mkono chairman wao Mbowe, nadhani hii ndio habari mbaya sana kwa maccm na ni tofauti kabisa ilivyokuwa NCCR na Chadema leo hii.
 
Mkuu mkiendelea kuamini tatizo la Chadema ni kununuliwa watu wao basi hesabu ni jioni kama waswahili wanavyosema.
 
Hao anaowaita wenye ushawishi ndani ya chadema ya leo asisahau kwamba wakati kina Zitto wanahangaika kuijenga chadema wao walikuwa NCCR.
 
Back
Top Bottom