Kilichofanywa na NHIF si Uungwana

Interview ilianza j3,j4,j5 then sku ya j5 makundi yalikuwa mawili kuna ambalo lilianza na kilingine likafata na maswali yale yale huku,lile kundi la pili walikuwa wamesimama mlangoni wanawasubiri watu!!!!!!!!!
Hawa jamaa walitaka kuwadhalilisha wasomi.
 
Karibu miezi miwili iliyopita watu waliitwa kufanya interview pale NHIF,lakini kilichotokea hawakuwaita wale watu wote waliofanya interview ile,badala yake waliamua kuwaita wale watu waliowahi kufanya tempo pale miaka ya nyuma.
Kilichonishangaza ni kwanini waliamua kutangaza nafasi za ajira then kuwaita watu katika usaili ili hali walikuwa na mpango wa kuwaita hao wa zamani,hawakuelewa kwamba kuna watu walitoka mbali(mikoani)kuja kufanya usaili?
Kiukweli inakatisha tamaa kabisa.
Ni hayo tu.

walitimiza wajibu na pia kutengeneza zengwe la posho
 
Jamani hii taarifa ni ya mwaka 2011 si ya mwaka huu 2012,Potezeeni haina dili!
 
Slogans ya ajira kwa bongo now inasema: Who you know and not what you know.

Ushapata jibu sasa?
 


Tatizo lenu kwa wale msio na experience ya kutafuta kazi ni moja tu! nalo ni KUSIKILIZIA!!!! mnapenda sana kusikilizia application na interview mnazozifanya!!! Wenzenu tulio na uzoefu wa kutafuta kazi bila kupata kwa miaka kadhaa sasa huwa hatusikilizii!!! Tunadondosha CV/application mahali halafu tunapotezea kama hakuna tulichofanya!! Inafikia wakati unaitwa mahali Interview, halafu unajiuliza "ni nani alipeleka application yangu kule!!!" coz', baada ya kudondosha application, ukapotezea hadi unasahau kabisa kwamba ulipeleka application!! Hata baada ya interview, wakongwe huwa tunapotezea kwamba kuna mahali umefanya interview! ukipenda kusikiliia haya mambo, mtaugua ugonjwa wa moyo brodaz!! Sana sana, unaweza kusikilizia maximum mwezi mmoja...sasa wana mnasikilizia hata kazi mlizoomba tangu June?!


Uko very right kaka, huo ni ushauri mzuri sana kwa wahusika ukishatuma we endelea na mingo zingine.Mimi niliwahi itwa kwenye interview baada ya hapo nikamfuata SECRETARY aliyenipigia simu kuniarifu kwamba nahitajika nikamuuliza ametoa wapi namba yangu akaniaonyesha VC yangu nilipigwa na butwaa.Mwanzoni nilifikiri kanyaboya nilipopokea simu ila aliponitolea CV nikamwambia Shkamoo.Wewe panda as much as you can iko siku mvua itanyesha ulipopanda wewe kwani Mungu hana hiyana.
 
Back
Top Bottom