Kilichofanya TSH istabilize Against USD

forex_strategy_trading_outlook_new_year_body_Picture_2.png
Habari ndiyo hiyo wakuu.

Sawa bana,random walk siyoo eh
 
Mambo makubwa matatu yaliyochangia shilingi ya Tanzania kupanda thamani ikilinganishwa na dollar ya Marekani ni benki kuu kuingilia soko na:
1. Kupandisha "Base lending Rate"- Nadhani kwa 100 basis points
2. Kupunguza "Forex Net Open Position" kwa mabenki kutoka 20% mpaka 10%
3. Kuongeza "Statutory Minimum Reserve" kwenye deposits za serikali kutoka 15% to 30%.

Hizi measures zote kwa ujumla zikiwa na lengo la kupunguza fedha nyingi zilizo kwenye mzunguko kwa ajili ya ku-control "inflation" na kupungua kwa shilingi katika mzunguko kumesababisha watu wauze sana dola walizonazo ili kupata shilingi.

Jambo lingine ni kwa serikali kupitia benki kuu kuwauzia dola moja kwa moja waagizaji wakubwa wa mafuta kupitia benki zao .
 
Uwezo wa kuifanya dola inunuliwe ata kwa tsh 100 tunao ila kuna watu wanafaidika na ughali wa dola.
Iweje mauzo yetu ya dhahabu yanafika $ 2.2 billion na bado tunahangaika kustabilize ela yetu.
Tatizo tuna wataalamu wengi wa political economy and not really economists!
 
Jambo lingine ni kwa serikali kupitia benki kuu kuwauzia dola moja kwa moja waagizaji wakubwa wa mafuta kupitia benki zao .

makampuni ya mafuta kununua dola BOT bado ni optional

kwa wafanayakazi wa makampuni hayo wanaotaka % kwenye uagizaji bado wanaenda direct commercial banks ambako kuna BOT compliance zisizokuwa mandatory sana na zaweza kuchezewa linapokuja suala la exchange rate
 
Hili lilichangia sana, maana kila importer mmoja anapotafuta favourable exchange rate kwenye maduka mawili matatu kwa ajili ya kununua labda $200,000, alikuwa ana send false alarm kuwa kuna demand ya $600,000 sokoni, na hivyo kuathiri bei ya kuuzia dola wakati huo...na hata ikitokea amepata, dola haishuki kwa kuwa kuna wengine wanaendeleza circle hii.

Kingine ni lazima to boost exports zetu, otherwise hii haitakuwa strong basis ya kuhold stability ya shilingi yetu.
 
Da. Sisi tunaolipwa mshahara kwa dolllar hii habari si njema kabisa. Huyo atakuwa dr mwamba kaja na mikakati hiyo. Ee mola haribu mipango hiyo ili shillingi iendelee kuporomoka T
 
Kwa mara ya kwanza katika historia ya Tz Tsh. 1850 ilinunua 1 USD, hii ilikuwa mwaka jana tu! Lakini wiki hii Tsh 1598 imenunua 1 USD. Kwa haraka ninaona kwamba Tsh imepata awheni haraka kuliko ilivyotarajiwa na wengi.

Nimepata taarifa zisizo rasmi (heresay) kwamba mabadiriko haya ya haraka yametokana na utafiti uliofanywa na BOT uliogundua kwamba mfumo wa malipo ya import ya mafuta uliokuwepo ndio umechangia kwa kiasi kikubwa. Mfumo uliokuwepo awali ulikuwa ni kwa Commercial banks kutumika kulipia imports za mafuta nao walikuwa waki hike rates ili kujipatia faida kubwa.

Lakini sasa malipo yote yanafanywa kupitia BOT hivyo hakuna tena nafasi ya kufisadi. Inasemakana kwamba tangu kubalishwa kwa mfumo ndio TSH imeendele kufanya vizuri.

Wanaoujua ukweli wa jambo hili bonyezeni botton.


Nina mashaka sana na maana halisi ya maneno katika red hapo juu. Commercial banks nyingi ni private sector operations. Hilo linaweza kuwa lilikuwa shimo la capital flight, na hao wezi watakuwa wamezitafuna kwelikweli hela za nchi yetu. Kwa kweli tunahitaji Paranoics wawili watatu katika mfumo wetu wa management ya uchumi. Tumekaa muda mrefu mno bila kuliona hili. Unaweza ukute pengine rate ya dola inatakiwa hata kuwa 800/-. Tuishukuru BoT, hata hivyo kwa kufukia shimo hilo, japo ni kwa kuchelewa sana, kama hii taarifa ina ukweli.
 
Mambo makubwa matatu yaliyochangia shilingi ya Tanzania kupanda thamani ikilinganishwa na dollar ya Marekani ni benki kuu kuingilia soko na:
1. Kupandisha "Base lending Rate"- Nadhani kwa 100 basis points
2. Kupunguza "Forex Net Open Position" kwa mabenki kutoka 20% mpaka 10%
3. Kuongeza "Statutory Minimum Reserve" kwenye deposits za serikali kutoka 15% to 30%.

Hizi measures zote kwa ujumla zikiwa na lengo la kupunguza fedha nyingi zilizo kwenye mzunguko kwa ajili ya ku-control "inflation" na kupungua kwa shilingi katika mzunguko kumesababisha watu wauze sana dola walizonazo ili kupata shilingi.

Jambo lingine ni kwa serikali kupitia benki kuu kuwauzia dola moja kwa moja waagizaji wakubwa wa mafuta kupitia benki zao .



Thanks for this more scientific explanation. Kwa nini tulichelewa kufanya hili?
 
Shilingi inaweza kuimarika zaidi na zaidi ikiwa BoT itakuwa na utashi wa kukatisha maslahi ya wakubwa. Ikiwa BoT itafanikiwa, pamoja na mambo mengine, kuzuia matumizi holela ya Dola (kwa sasa kuna taasisi za elimu; maduka n.k yanayotoza malipo kwa Dola). Dola haotoweza kushuka thamani ikiwa uhitaji wake ni mkubwa.
 
Matumizi makubwa ya dola kwaajili ya msafara wa rais na kundi kubwa la kumsindikiza muheshimiwa.
Pia exportation of primary raw materials.
 
JUST mnahitaji ujazo wa dola uwe mwingi kwenye soko, kwa kuzalisha zaidi ili mpate forex . Mngeweza kuingia mikataba nizuri ya ubinafusishaji mngeweza kuwa mnzalisha bidhaa nyingi na kuuza, mngeweza kuuza dhahabu na kupata proceed kupitia local banks ambapo mngekua na billions of dollars rtaer kuwa na vijisenti vinavyorudi kulipia matumizi, kilimo mngeimarisha ili kuuza kahawa na nk. Pia kutegemea sana misaada pia ni shida wapunguzapo misaada ina maana kadola hakaji. Even though uchumi wa dunia ni tete, ulaya wanalia lakini kwa ali ya kawaida ilikuwa ndio kipindi cha nchi zenye rasilimali kupaa kiuchumi. Chimbeni dhahabu mbadilishaje na wese, tumieni gesi msinunue mafuta, tumieni makaa ya mawe msinunue mafuta. Waambieni wawekezaji kuwa 50% ya proceeed ya revenue kutoka mali asili ilipwe kupitia benki zilizopo Tz mtaona mabadiliko na pia acheni kutuma pesa nje wekezeni humuhumu.
 
Back
Top Bottom