Kilichofanya TSH istabilize Against USD

Lawkeys

JF-Expert Member
Nov 16, 2009
1,118
287
Kwa mara ya kwanza katika historia ya Tz Tsh. 1850 ilinunua 1 USD, hii ilikuwa mwaka jana tu! Lakini wiki hii Tsh 1598 imenunua 1 USD. Kwa haraka ninaona kwamba Tsh imepata awheni haraka kuliko ilivyotarajiwa na wengi.

Nimepata taarifa zisizo rasmi (heresay) kwamba mabadiriko haya ya haraka yametokana na utafiti uliofanywa na BOT uliogundua kwamba mfumo wa malipo ya import ya mafuta uliokuwepo ndio umechangia kwa kiasi kikubwa. Mfumo uliokuwepo awali ulikuwa ni kwa Commercial banks kutumika kulipia imports za mafuta nao walikuwa waki hike rates ili kujipatia faida kubwa.

Lakini sasa malipo yote yanafanywa kupitia BOT hivyo hakuna tena nafasi ya kufisadi. Inasemakana kwamba tangu kubalishwa kwa mfumo ndio TSH imeendele kufanya vizuri.

Wanaoujua ukweli wa jambo hili bonyezeni botton.
 
Selikali hii haiaminiki, hata linalofanywa vizuri jua kuwa limefanywa kwa bahati mbaya hivyo ni rahisi kurudi kwenye makosa bila kujijua. Kesho ukikuta dola 1 ni sh. 2000 usishangae, au ikashuka hata tsh 500. usishange maana ktk vululu vululu za nao wana shangaa hali hizo zinazojitokeza.
 
Kwa mara ya kwanza katika historia ya Tz Tsh. 1850 ilinunua 1 USD, hii ilikuwa mwaka jana tu! Lakini wiki hii Tsh 1598 imenunua 1 USD. Kwa haraka ninaona kwamba Tsh imepata awheni haraka kuliko ilivyotarajiwa na wengi.

Nimepata taarifa zisizo rasmi (heresay) kwamba mabadiriko haya ya haraka yametokana na utafiti uliofanywa na BOT uliogundua kwamba mfumo wa malipo ya import ya mafuta uliokuwepo ndio umechangia kwa kiasi kikubwa. Mfumo uliokuwepo awali ulikuwa ni kwa Commercial banks kutumika kulipia imports za mafuta nao walikuwa waki hike rates ili kujipatia faida kubwa.

Lakini sasa malipo yote yanafanywa kupitia BOT hivyo hakuna tena nafasi ya kufisadi. Inasemakana kwamba tangu kubalishwa kwa mfumo ndio TSH imeendele kufanya vizuri.

Wanaoujua ukweli wa jambo hili bonyezeni botton.
Lawkeys umepotea sana ndugu yangu.. nafikiri hilo japo sio rasmi lakini lina harufu ya ukweli maana mabenki yetu bwana ni tatizo tu, wako kibiashara zaidi na sio kuisaidia nchi kuimarika kiuchumi.
 
Mkuu unajua kuna watu wanalipwa bonus mpaka 90million mwisho wa mwaka kwenye mabenki? hawa watu wanao-handle forex na kufanya makeke ya kuipatia bank faida........ndio mchezo wenyewe.
 
Imports huwa zinapungua wiki au siku chache kuelekea mwisho wa mwaka (kama inavyotokea karibia na bajeti ya serikali). Kwa maana hiyo demand ya US Dollars inapungua kulinganisha na supply yake na hivyo exchange rate kuwa favourable kwa local currency.
 
Sidhani kama hiyo ni sababu maana kilichofanyika hakijawahi kutokea Tanzania eti shilingi kutengamaa kwa zaidi ya sh 200 dhidi ya dollar..! hilo usemalo wewe ni zile fluctuations za 20-50 shillings
 
Kwa hiyo tuexpect kua haitorudiiliko kua? Kwa sisi ambao tunaweka hakiba in Tsh, kuna faida gani?
 
Imports huwa zinapungua wiki au siku chache kuelekea mwisho wa mwaka (kama inavyotokea karibia na bajeti ya serikali). Kwa maana hiyo demand ya US Dollars inapungua kulinganisha na supply yake na hivyo exchange rate kuwa favourable kwa local currency.
...Hii inaweza kuwa sababu ya maana zaidi -kuelezea kwanini thamani imepanda baada ya kushuka kwa kasi- kwani siku zote mafuta yalikuwa yakiagizwa na hatukuona trend ile ya mwishoni mwa mwaka. Uwezekano wa speculation -hasa pale ilipotoka 1800 hadi 2000- ni mkubwa zaidi.

...Mwanzo wa mwaka sitegemei kuona thamani ya shillingi inashuka, kutokana na uchumi kufubaa -serikali ikikabiliwa na ukata mkubwa- ikizingatiwa kwamba sekta ya umma ina nafasi kubwa katika kuuchangamsha uchumi wetu, kimatumizi. Hivyo uagizaji bidhaa kwa ujumla, utapungua na kupunguza mahitaji ya dollari.
 
huku kwa wachumi....
sisi watumiaji tunachenji tuuu hata ikipaaje.
 
Tanzania ilibidi ijikwamue kwa kuuza akiba ya dhahabu zake benki ya dunia baada ya kuona hali ni ya hatari, kisiasa na kiuchumi, hilo la imports kupungua mwisho wa mwaka ilikuwa zamani kwa sasa huongezeka maana migodi haifungwi mkaburu hana likizo, waenda china, dubai kama kawaida tena wanabebana na bidhaa huwa nyingi kipindi hicho. Nawasilisha
 
forex_strategy_trading_outlook_new_year_body_Picture_2.png
Habari ndiyo hiyo wakuu.
 
Benki kuu iliongeza base interest rate, hii inasababisha mikopo kuwa gharama zaidi hivyo mzunguko wa fedha unapungua, nadhani hii ndo iliyostabilize shillingi.
 
Hii imetokana na kupanda na kushuka kwa thamani ya dollar per se kama inavyoonyeshs kwenye kielelezo hapo juu. Angalieni trend yake arround september to november halafu fananisheni na trend ya shs against $ kwenye miezi hiyo.Halafu angalieni ilivyoshuka towards the end of 2011.

Ukiangalia kwa undani zaidi, Shilingi ilitakiwa ishuke kutoka 1800 mpaka 1300 hivi. Kwa hiyo, 1600 wala siyo habari nzuri... inaonyesha Shilingi bado ni very weak against the dollar. Kwa sababu trend yake bado hailingani na trend ya dollar kwenye soko la dunia 100%. That is to say, the Shilling is not really stable.
 
Nilipenda sana niwe mchumi, ila du Dr. Kalamage alinifanya nikimbie!
 
Tanzania ilibidi ijikwamue kwa kuuza akiba ya dhahabu zake benki ya dunia baada ya kuona hali ni ya hatari, kisiasa na kiuchumi, hilo la imports kupungua mwisho wa mwaka ilikuwa zamani kwa sasa huongezeka maana migodi haifungwi mkaburu hana likizo, waenda china, dubai kama kawaida tena wanabebana na bidhaa huwa nyingi kipindi hicho. Nawasilisha
Mkuu uko nyuma kidogo,Ndullu alishasema mwaka juzi hatuna akiba ya dhahabu=(wajanja kushauza) na sasa tunaweka akiba in euro na dolari,hili lilizua tafrani bungeni wakitaka kujua dhahabu yote iliyonunuliwa na BOT late 80 early 90's zilienda wapi ??
 
The shilling is up for a real battle, come April. Please, keep your HCs. Gov expenditure is still going up, exports down, gas export is still several years away.
 
Vile vitu vilivyopanda bei kwa kisingizo kwamba Tshs ipo weak kwa sasa vimepunguzwa bei? - kwangu mimi sioni tofauti. Actually mabadiliko haya yananiumiza sana. Kwa sasa natumia pesa nyingi zaidi kwa huduma zile zile kuliko miezi michache hapo nyuma (wakati dollar ipo juu)
 
Mfumuko wa bei unakuua[ inflation] ambayo BOT wanajaribu kuithibiti kwa kutumia monetary instruments wakati source kubwa ya mfumuko wa bei ni structural!! Remember the increase in interest rates has an adverse effect on the growth of the economy.
 
Vile vitu vilivyopanda bei kwa kisingizo kwamba Tshs ipo weak kwa sasa vimepunguzwa bei? - kwangu mimi sioni tofauti. Actually mabadiliko haya yananiumiza sana. Kwa sasa natumia pesa nyingi zaidi kwa huduma zile zile kuliko miezi michache hapo nyuma (wakati dollar ipo juu)
mi'naona kama hamna kilicho wahi pungua bei hapa tz toka kipande
 
Back
Top Bottom