Kilicho nyuma ya madaktari kuomba radhi ni maagizo toka juu

Hawa jamaa wameonyesha udhaifu mkubwa sana ni bora wangekaa kimya kuliko kuja kuanza kuongea hizo pumba zao. Kwa maana hii wanatudhihirishiakuwa walichokuwa wanadai ni uongo mtupu hayakua madai ya ukweli hata kidogo.
 
Subirini muone matukio ya madaktari kupigwa yatakavyoibuka.
Wakitoa huduma chini ya kiwango, ni mangumi kwa kwenda mbele.
Tuliwaunga mkono kwenye madai yao ili hatimaye huduma ziboreshwe.
Tuta-solve problems kwa kadri zitakavyojitokeza.
 
Mimihili naliona ni hatari sana kwa nchi. Niwakumbushe kuwa kipindi cha nyuma (70s) ulitokea mgomo wa wanafunzi chuo kikuu. Serikali ikawalazimisha tena kwa vitisho, mgomo ukaisha. Lakini wakaapa kuwa wataenda kutumikia nchi miili tu sio roho zao. Kwa tathmini yangu hiyo batch ya wanafunzi hatimaye ndio waliokuwa madarakani kuanzia kipindi cha Mzee rukhsa (Mwinyi). Nadhani mtakubaliana nami kuwa walifanya kazi kwa miili tu roho zao (uzalendo) ilikuwa ni ziro.
Hawa madaktari wameona ngoja yaishe kwa sababu kila mtu ana malengo yake. Lakini kama watakuja kufanya kazi kwa uadilifu, kujituma n.k. ni ndoto.
Watanzania tunaotegemea local government hospital kututibu ni balaa lililopo mbele yetu.
 
where is steven ulimboka?????? No body ask such an important question????!!!!!!!!
huwezi kulipata jibu hapo hadi hapo utakapojua au kupata mawasiliano ya Uli na wale jamaa kabla ya kutekwa.
Kwa nini Uli alifanya majadilano ya kikazi at those odd hours na katika sehemu za mapombe?
Zaidi ya kuwatetea wenzio dhamira yangu inatuma kuwa Uli alikuwa na personal gain katika hili hasa monetary na bargain ilimponza.
 
Njaa ni mbaya sana....!!!

Sio njaa tu, ukosefu wa elimu. Kuna maneno niliwahi kusema hapa jamvini nikimwambia zuzu mmoja aliyekuwa akisema kwa nini kwenye sensa wamepewa nafasi watu wa sekondari ilhali yeye graduate ameachwa. Sikusita kumwambia kuwa madarasa hayabadili hadhi ya mtu, yanachoweza kufanya ni kukufundisha namna ya kufikiri lkn utachofikiri kinatokana na uwezo wako binafsi wa kiakili..

Hawa madaktari ni mfano wa wasomi wasio na elimu.
Elimu ingekuwepo ndani yao wasingejidhalilisha namna hii. Wana mavyeti tu kichwani hamna kitu.
 
Habari toka Ikulu zinasema kuwa mara baada ya tume ya usuluhishi kwenda kutafuta muafaka wa mgomo wa madaktari na namna ya kutekeleza kama ilivyo amuliwa na mahakama ya kazi. Mh Jk alitoa dukuduku lake la moyoni na akawaambia yafuatayo kama wanaipenda kazi na nchi kwa ujumla.

1. Warudi kwa namna ileile walivyotangaza mgomo warudi na waombe radhi kwa kutumia njia ile ile waliotumia kutangaza mgomo.

2. Katika kutangaza kutojihusisha na mgomo wawataje walio watuma kufanya mgomo. ( Mpaka leo CHADEMA ndo wanajulikana ndio walio sababisha mgomo.

3. Wakiri kuwa wao ndo wakosefu na sio serikali kama walivyokuwa wanadai

Kila mwananchi kwa akili zake changanya na tukio zima la mgomo na tafakari


Kuna msemo wa Kihaya unasema hivi "enkende kushekerera ekibira nikihya". Kuna Watanzania mmojammoja na wengine kupitia taasisi kama magazeti yanayomilikiwa na seriakli na la CCM habari ya madaktari wameifurahia mithili ya nyani anayechelekea kuona msitu unaungua kumbe kajisahau kuwa msitu ndio habitat yake ambamo anakulia na kuzaliana. Hivi ndivyo wanaoshangilia kuomba radhi kwa madaktari wanafunzi. Na no afadhali sababu za kurudi kwao zingekuwa na mashiko na kusheheni mantiki. Lakini ukiziangalia zinachefua moja eti 'tulidanganywa" Hivi mtu unasoma kuanzia chekechea mpaka ngazi ya shahada na stashahda na elimu inayotokana na kukua kwa teknolojia ya computer na internet unadiriki kusema ulidanganywa. Hili neno 'kudanganywa' sasa linakosa maanrais anadanganywa kwani kila mtu siku hizi akivulunda anasakizia kudanganywa. Tujikumbushe Zakia Megji na kashfa ya EPA, rais na kashfa zote ambapo watetezi wake wanasema rais anadanganywa. Sasa turudi kwenye mada ya mgomo wa madaktari. Waliorodhesha mambo mengi mengine yanawahusu wao na mengi yalihusu ubovu wa huduma na vitendea kazi katika hospitali zetuza umma. Hata kabla wao hawajasema hospitali zote za serikali zilikuwa na bado ziko katika pathetic condition. Muhimbili hospitali kuu ya taifa wagongwa wanalala watatu mpaka wanne ktk kitanda kimoja kilichotengenezwa kwa ajili ya mtu mmoja na kumbuka hawa wanaugua magonjwa tofauti, hakuna huduma ya X-Ray, TC-Scan, hakuna madawa na mazingira ni machafu kupita maelelzo. Kama hospitali kuu ya Taifa iko hivyo je zingine na vituo vya afya vikoje? Je kuomba msamaha kutafanya hali iboreshwe. Morari ya madaktari itarudi baada ya kuomba msamaha. Ni aibu na fedheha kwa taaluma na elimu katik ujumla wake kama unakuwa na wasomi wasiopenda kusema ukweli, wasiokuwa critical and critique minded. Maamuzi kama haya yalipaswa yafanywe na watu ambao hawajaona kuta za madarsa. Lakini kwa watu kama wanaosomea udaktari kuwa na usaliti wa aina hii ni ahatari ya mwaka. Najua si wao peke yao ambao wana unafiki na upuuzi ukianza kuataja litania ni ndefu-Vodocom NA Nokia Siemens kunafukuta kwanini? Ni kwa sababu ya unafiki wa Watanzania wachache waliojinufaisha baada ya kupata vyeo wakawasahau wale wasiokuwa na vyeo na mambo yalipogeuk kuashiria kukosa kazi au kukosa marupurupu sasa wanatumia mwavuli wa uzalendo ili kuwavuta wote ili ionekane kuna ubaguzi wa rangi. Kweli? Uzalendo sasa hivi? Mbona mlikuwa mnaendesha magari kwa fujo na mnayyacha kwenye start mode nyie mkiwa nje mnakula vinono eti yasipate joto ndani. Ufujaji wa rasilimali wakati wafanyakakzi wengine hata uwezo wa baiskeli hawana. Hamkuonyesha uzalendo ili kuondoa salary disparities. Hayo tuliyaona Tanesco walivyoigomea Net Group Solutions lakini walivyopewa marupurupu basi wote walinywea. Hayo tunayaona katika taasisi za elimu kuanzia utoaji wa mikopo na elimu isiyo na quality. Hatuoni solidarity hata kidogo bali usaliti. Lakini hiyo haiwaondolei hawa vijana lawama kwa usaliti wao kwa wananchi maskini ambao mbali na kuteseka waliwavumilia vijana hawa wakiwa wana imani mgomo wao ungeleta mabadiliko ktk sekta ya afya ya umma
 
Hivi cha kujiuliza ina maana wanaomba msamaha kuwa madai yao si yakweli? Na kama siyakweli kwa nini waligoma?

Hapa ndio utajua wanajaribu kucheza na akili za babu zao.

Kweli hata maboresho ya huduma mahospitalini na yo madai yalikuwa yakupikwa? Nini maana ya kuomba msamaha?

Kumbe hata CT-SCAN zilikuwepo za kutosha na zilikuwa nzima kabisa?

Kumbe walijiunga kwenye mgomo bila kujua walikuwa wanadai nini?

Kumbe walilazimishwa kuingia kwenye mgomo na kama walilazimishwa kwa nini hawakusema jana?

Hivi huruma yao kwa watanzani na wafiwa wameiona tareh 17/9?
 
Wanataka kutuaminisha kuwa walifanya mgomo kwa bahati mbaya, je, waliyokuwa wanayadai yalikuwa ya uongo? je, ni kweli huduma za afya kwenye vituo vya serikali imekuwa nzuri?

Waende zao, kujibembeleza kwa Jk kumewashushia heshima, walikuwa mfano katika kutetea haki zao lakini wamejishusha chini, bado inakuwa hakuna aliyevunja rekodi ya TANESCO kipindi hicho ilitaka kubinafsishwa.
mimi nilikuwa siku za karibuni najaribu kuamini kuwa Watanzania tunaweza kujikomboa kifikra katika angalau miaka 10 ijayo lakini kwa matukio kama haya nathubutu kusogeza huo muda kwa miaka 30 mbele hivyo inaweza kufika hata miaka 40 ijayo! Sijui Wakenya watakuwa wapi wakati huo Mungu wangu!!!!

 
Mimi hili naliona ni hatari sana kwa nchi. Niwakumbushe kuwa kipindi cha nyuma (70s) ulitokea mgomo wa wanafunzi chuo kikuu. Serikali ikawalazimisha tena kwa vitisho, mgomo ukaisha. Lakini wakaapa kuwa wataenda kutumikia nchi miili tu sio roho zao. Kwa tathmini yangu hiyo batch ya wanafunzi hatimaye ndio waliokuwa madarakani kuanzia kipindi cha Mzee rukhsa (Mwinyi). Nadhani mtakubaliana nami kuwa walifanya kazi kwa miili tu roho zao (uzalendo) ilikuwa ni ziro.
Hawa madaktari wameona ngoja yaishe kwa sababu kila mtu ana malengo yake. Lakini kama watakuja kufanya kazi kwa uadilifu, kujituma n.k. ni ndoto.
Watanzania tunaotegemea local government hospital kututibu ni balaa lililopo mbele yetu.

Kwa hili kwamba walitumiwa na CHADEMA, mimi siamini kabisa. Kwanza niseme kuwa mimi si mwanachama wa chama chochote cha siasa.
Ninalikumbuka mimi ni kuwa madai ya madaktari yalianza baada ya kuona kuwa Wabunge wao wanapanga kujiongezea maslahi kuwa makubwa mno kupindukia wakati madaktari kama kada ya muhimu haifikiriwi.
Huu ndi ukweli wabunge wasingetaka kujiongezea mshiko madaktari bado wangeendelea kuvumilia.

My take: Ni ukweli kuwa wafanyakazi wa Umma (madaktari wakiwemo) wanalipwa kidogo mno. Utatuzi ni kuona ukweli huu na kutatua maana rasilimali zipo za kutosha. Ni kujipanga tu.
 
Nadhani huu ni uamuzi wa 'liwalo na liwe' wameona Ulimboka kanyamazishwa hawana kiongozi tena watawala ndiyo hao akili mgando ikabidi wawasikilize wanataka nini.

Hawa akili mgando(J. K n' co.) wanaona ni sawa na wanafurahi madaktari wakiomba msamaha kwa sababu uelewa wao ni MGANDO(zero brain) Dr. na professional yake aje akuombe msamaha wewe usiyekuwa na professional hata nukta! (?) Tujiulize sawasawa.

Tutakaoumia ni sisi wananchi, tujiandae kwa hongo mahosiptali ya serikali, wagonjwa kulala chini, Dr. atakuwa anajiamulia anavyotaka, madawa ni kununua pharmacy za madokta, unaweza ukatibiwa au usitibiwe, tiba ni vyovyote vile atakavyoona Dokta yaani yote ya yote ni Liwalo na Liwe.
 
mimi nilikuwa siku za karibuni najaribu kuamini kuwa Watanzania tunaweza kujikomboa kifikra katika angalau miaka 10 ijayo lakini kwa matukio kama haya nathubutu kusogeza huo muda kwa miaka 30 mbele hivyo inaweza kufika hata miaka 40 ijayo! Sijui Wakenya watakuwa wapi wakati huo Mungu wangu!!!!


Umenifurahisha
 
Sio njaa tu, ukosefu wa elimu. Kuna maneno niliwahi kusema hapa jamvini nikimwambia zuzu mmoja aliyekuwa akisema kwa nini kwenye sensa wamepewa nafasi watu wa sekondari ilhali yeye graduate ameachwa. Sikusita kumwambia kuwa madarasa hayabadili hadhi ya mtu, yanachoweza kufanya ni kukufundisha namna ya kufikiri lkn utachofikiri kinatokana na uwezo wako binafsi wa kiakili..

Hawa madaktari ni mfano wa wasomi wasio na elimu.
Elimu ingekuwepo ndani yao wasingejidhalilisha namna hii. Wana mavyeti tu kichwani hamna kitu.

Mkuu Las Mas Bobos, you are probably right..
 
Humu humu ndani mlisema na kutoa orodha ya madaktari eti wamepata kazi nje ya nchi na mambo kibao oohoo mara sijui nini kumbe bado wapo hapa hapa bongo mmmh.Na anae sema JK ni mbabe huyo ni mzushi na muongo mkubwa kama angekuwa hivyo sidhani hata wewe ungejua kusema hayo unayo yasema na kuropoka ovyo kwa kutumia mitandao ukudhani huonekani kwa taarifa yako hata ungetumia njia gani serikari ikikuhitaji utapatikana sana,Hakuna rais aliyeruhusu uhuru wa watu kutoa maoni mpaka wengine wanatukana ovyo na kuhujumu nchi lakini bado wapo tuu,kila lenye mwanzo linamwisho.
 
Hivi cha kujiuliza ina maana wanaomba msamaha kuwa madai yao si yakweli? Na kama siyakweli kwa nini waligoma?

Hapa ndio utajua wanajaribu kucheza na akili za babu zao.

Kweli hata maboresho ya huduma mahospitalini na yo madai yalikuwa yakupikwa? Nini maana ya kuomba msamaha?

Kumbe hata CT-SCAN zilikuwepo za kutosha na zilikuwa nzima kabisa?

Kumbe walijiunga kwenye mgomo bila kujua walikuwa wanadai nini?

Kumbe walilazimishwa kuingia kwenye mgomo na kama walilazimishwa kwa nini hawakusema jana?

Hivi huruma yao kwa watanzani na wafiwa wameiona tareh 17/9?

We acha tu! Ni kichefuchefu kitupu!
 
Back
Top Bottom