Kili Music Awards 2011

Who is Cpwaa? The dude kept sending text msgs ili tumpigie kura, I think that the hard work aliyokuwa akisemea iliyomsaidia kushinda

Ndio tatizo hilo,yaani kampeni walizokuwa waikipiga hawa jamaa hata za uchaguzi mkuu zina nafuu,kila sehemu unawakuta wanapiga mikampeni yao: sms,facebook,twitter,radio stations,Tv stations n.k......Cha msingi wangewaacha watanzania wawachague kwa ubora wa muziki wao badala ya kufanya campaigns.........Fikiria kuna wengine wanadiriki hata kuwanunulia watu VOCHA za simu ili wawapigie kura kwa kutumia sms nyingi...............INABOA ile mbaya
 
JCB oyeee! Umejitahid sana kufika hapo, 'hawajaskia paaa' itakuwa imewapata hyo... Shukrani kwa taarifa wakuu wengine tuko huku pembezoni mwa nchi gesti hazina tv. Big up JF!
 
Ndio tatizo hilo,yaani kampeni walizokuwa waikipiga hawa jamaa hata za uchaguzi mkuu zina nafuu,kila sehemu unawakuta wanapiga mikampeni yao: sms,facebook,twitter,radio stations,Tv stations n.k......Cha msingi wangewaacha watanzania wawachague kwa ubora wa muziki wao badala ya kufanya campaigns.........Fikiria kuna wengine wanadiriki hata kuwanunulia watu VOCHA za simu ili wawapigie kura kwa kutumia sms nyingi...............INABOA ile mbaya
Mwishowe mtu anashinda kutokana na idadi za kura na sio ubora wa kazi yake!!
 
Huu wimbo wa USIJARIBU na HABARI wa AY tumeuchoka kusika kila mwaka kweny tuzo za kili na vodacom mis Tz kila mwaka
 
yaani BSS final ilikuwa way much better na ilikuwa na mwanga wa kutosha, kampuni gani ndio imepamba
 
Hivi hii Kili music awards ina EVENT ORGANIZER? Ni kinyaa kitupu kwenye stage jamani. Watu hawawezi kujieleza, wanashukuru ukoo mzima, marafiki, maproduzer puh! Wengine wanagombea kupokea tuzo. Hao watoaji tuzo wenyewe wana maneno mengi, wewe umepewa kazi ya kumpa mwanamuziki tuzo unaleta story za nini? Mwishowe wanajiumauma na kuchemka kama Nsajigwa katia aibu alipokuwa anamtangaza mshindi.

Napendekeza kuwe na REHESAL kwa wanaowania tuzo wote, wagawa tuzo, na ma MC. Ikiwezekana umeze kabisa utakachosema ukifika pale stejini, na jinsi ya kuipoke tuzo yako. Loh! Halafu nani kasema huyo Milard Ayo anafaa ushereheshaji? Huyo ni presenter mzuri sana kwenye TV na radio but si MSHEREHESHAJI jamani! Anachemka kinoma. Mpoki amejitahidi, hajaongea utumbo, Mzee small na Bi Chau wamefurahisha, C Pwaa yuko presentable hata kwenye kupokea tuzo amejitahidi. Watu hawako serious, hawako presentable ni kichefuchefu.

Huyo Lina nae sijui kavaa nini, wacheza shoo wake wadada wamependeza kama nini na vigauni vyao vya silver , yeye hata sijuui kavaa nini. Duh! Bado tuko nyuma sana. Naona hata aibu jamani. Hivi huwa hawatizami Grammy, Emmy na tuzo zingine?
 
Bi mkubwa upo makini, hadi hilo umeligundua...

Katavi, yaani nili notice kwa kweli wanawake wote wamebaki kubeba tuzo sasa sijui walishindwa kutafuta walimbwende wa kuzibeba maana wanakuja wawili kumtangaza mshindi kwa nini mmoja afanywe picha?

Tegete na mgosi ndio wamenifurahisha. Teget kasalimia na kuanza kibwagizo cha mshindi ni halafu kampokea mwenzie tuzo ili afungue bahasha na kumtangaza mshindi. Niliipenda hiyo!
 
Sitak kuamin kama ni Watz ndio wamemchagua mwimbaji bora wa nyimbo za asilia kuwa ni Mpoki na kibao chake cha Shangazi katika kinyanganyiro cha tuzo hiyo iliyowashirikisha wasanii wengine kama Mrisho mpoto na kibao chake Adela lkn kura za watz zilimwangukia Mpoki.Ikiwa kama watz wa leo tunachagua nyimbo zenye mashairi ya SHANGAZ UNA NYETI KULIKO HIZI TUNAZO, NYOKA HANA KIUNO NDO MANA HAVAI SHANGA kama anavyoimba mpoki na kuacha nyimbo zenye mashairi ya kutufundisha na kuonya basi tumekwisha.
ILA KAMA MAF
 
Guys! Msiombe kuangalia red carpet za kibongo. Yaani sijui kama watu huwa wanatazama award showa za wenzao majuu.
Wanaume wengine wanavaa utafikiri wanaenda kuwinda. Yaani wameva ki-walmart mpaka boots, eti swagga. Wanawake utafikiri wanaenda spring bash za miami. Yaani you do not see due respect kwa tuzo hizi. Sijui waambiwe ni formal dress code? Yaani I do not know!
 
Back
Top Bottom